Kwanini chuo cha MUST Mbeya kinawafanya wanafunzi warudie mwaka wa masomo kwa sababu mifumo inasumbua. Hasa wa Diploma

Moneyman

New Member
Jan 21, 2021
4
8
Nimeona niulize huku labda naweza pata msaada wa mawazo tofauti kwa watu wanaopitia hii changamoto.

Nna ndugu yangu amesotea Diploma pale MUST Mbeya kwa miaka mitano badala ya mitatu na mpaka sasa hivi bado hajatoboa, na tatizo sio kufeli. Ni mifumo yao.

Wanaambiwa mfumo umebadilika so mwalimu anashindwa kuupload matokeo kwenye mfumo mpya, inabidi mwanafunzi afuatilie mwenyewe, urasimu unakua mkubwa na kuzungushwa kwingi mpaka muda wa kuweka matokeo unaisha, itabidi arudie mwaka.

Hili jambo limeshamtokea mara mbili na sasa anaona kuna dalili litatokea tena.

Miaka 6 kwa diploma ya miaka 3, kisa mfumo mpya hauingiliani na matokeo yao walioanza chuo kabla ya huu mfumo mpya.

Mwanzo tulihisi anafeli tu anaogopa kusema ndo maana anatupanga. Ila tumefuatilia tunaona kuna ukweli wa wanafunzi kulazimika kurudia mwaka wa masomo sababu ya mfumo.

Kama kuna watu waliopitia hili suala mlichomokaje, maana naona familia nzima imeshachoka, hawajui wamuambia aache tu miaka yake mitano iwe imepotea au aendelee kukomaa labda ipo siku mifumo yao itakaa sawa.
 
nyie mmejuaje kwamba hadanganyi, tuanze hapo kwanza

mimi nasoma hapo MUST sijawahi sikia kitu kama hicho, ndio mifumo ni mibovu ila mpaka hali inafika huko hajafikiria kumhusisha hata principal wa chuo?

nina mashaka anadanganya aisee
 
Back
Top Bottom