DOKEZO Sheria/Utaratibu Mpya ulivyowakosesha Wanafunzi wa UDOM Haki yao…

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
SHERIA MPYA ILIVYOWAKOSESHA WANAFUNZI WA UDOM HAKI YAO.


Chuo kikuu dodoma,UDOM.

25/11/2022 uongozi wa chuo kikuu cha dodoma( UDOM) katika ndaki ya TIBA ulitoa sheria mpya kwamba mwanafunzi yeyote aliyepata carry over(Yani kufeli somo ambalo hujafikisha coursework) katika somo lolote hatakiwi kuendelea mwaka wa masomo 2022/2023 mpaka hapo atakaposahihisha somo hilo husika katika semister husika.

Sheria hii mpya iliumiza wengi hasa wanafunzi wa mwaka wa kwanza (ambao walitakiwa wawe mwaka wa pili kama wasingerudia) kwani haikuwepo kabla bali ilikuwepo kwa wanafunzi wa mwaka wa pili na wa tatu ambao walitakiwa kwenda wodini kwa ajili ya mafunzo ya vitendo( clinical rotation).

Wanafunzi wengi walilalamikia sana hii sheria mpya kwa sababu haikuwepo kabla na ilivyoanzishwa imewaathiri wale waliopata carry over kabla ya sheria hii mpya yaani mfano sheria ya nchi iseme kwamba mtu akiiba kuku adhabu yake ni miezi sita halafu wewe ukaiba kuku na ukahukumiwa hiyo miezi sita wakati unatumikia miezi yako sita sheria inabadilishwa inasema kwamba ukiiba kuku adhabu yake ni mwaka mmoja na hiyo sheria inawahusu na ambao tayari wanatumikia adhabu zao kwa sasa kitu ambacho sio haki kimsingi.

Sheria hii inasema kwamba ukipata carry over(course work chini ya 25/50) katika mwaka wowote wa masomo huruusiwi kuendelea na masomo mpaka usahihishe carry hiyo katika semister husika ndio utaendelea.Sheria hii ipo ndani ya tiba tu hapa UDOM na haipo katika ndaki (college) zingine.

Wanafunzi walikubaliana na sheria hii mpya iliyokubaliwa na baadhi ya wakuu wa idara na wakaendelea na masomo japo kuna baadhi waliacha chuo na wengine walifanya majaribio ya kujiua

Wanafunzi waliopata Carry Over walitakiwa kwenda katika ofisi za wakuu wa idara kwenda kuchukua barua kisha kuzipeleka kwa mhasibu ili wabadilishiwe.

Wale wenye carry za semister ya kwanza walitakiwa kubaki chuo na wale wenye carry za semister ya pili walitakiwa kurudi nyumbani kisha waje semister ya pili kufanya usajili na kusoma masomo waliyofeli.

Katika wale walio carry wengi wao walikuwa ni wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu inayitolewa na HESLB yaani wanalipiwa pesa ya chakula na malazi (Meals and accomodation) pamoja na peda ya ada (school fees).

Wanafunzi wenye carry over hasa za semister ya pili walipoanza kufanya usajili baada ya chuo kufunguliwa mwez wa 4 walikutana na changamoto kubwa.

Yaani kila wakiingia kwenye account zao za chuo (sr2) kwa ajili ya kufanya usajili system ilikuwa inasumbua usajili ukawa unagoma hivyo wengi wao walichelewa kufanya usajili.

Waliowahi kufanya usajili walisaini ada zao lakini hazikutakiwa kutumika katika mwaka wa masomo 2022/2023 na waliambiwa watazitumia katika mwaka wa masomo 2023/2024.

Wale waliochelewa kufanya usajili kutokana na changamoto zilizopo kwenye mfumo wa chuo hawakusaini ada zao mpaka muda huu na wala karatasi za kusaini hazijaja.

Hawa wanafunzi wanadai walihangaika sana kufanya usajili mpaka kufika utawala mkuu lakini tatizo hili halikutatuliwa mapema.

Mbaya zaidi wanasema wakuu wao wa idara hawawasaidia.Wanadai hasa mkuu wa idara ya Public Health,Mr Katalambula ndiyo jipu kabisa kwanza ofisi hakai na simu hapokei hivyo ukiwa na shida ni ngumu kukusaidia.

Kuna wanafunzi wa Udom-Tiba wameniambia waliwahi kwenda kwa mhasibu kwa ajili ya kufatilia kusaini ada zao lakini mhasibu aliwafokea sana kuonekana wao ndiyo wazembe ilihali uzembe ulikuwa ni wa chuo lakini kauli ya mwisho alisema watawaombea bodi ya mikopo ili wasaini ada zao (ni haki yao).

Ipo voice ambayo mhasibu wa UDOM-TIBA alirekodiwa bila kujua.

Mpaka sasa mwaka wa masomo 2023/2024 umekaribia kuanza wanafunzi hao hawajasaini hizo ada ambazo ni haki yao na hata viongozi wao hawawapi majibu ya kueleweka.

Wanafunzi walichelewa kujisajili kutokana na mifumo mibovu ya chuo na chuo hakikuwaombea ada zao bodi ya mikopo mpaka sasa.

Upande mwingine wa chuo cha UDOM ni kwamba ukiwa unadaiwa hata Tsh 100 huwezi kufanya mtihani wa mwisho wala kujisajili lakini wao ikitokea ukawa unawadai na ukazihitaji pesa zao utazungushwa sana mpaka utakata tamaa.

Pia suala lingine ni kuhusu ada ya kukaa hostel,chuo chenyewe kilisema kwamba wa wenye carry over wanatakiwa kubaki chuo kwa semister aliyo carry baada ya hapo arudi nyumbani lakini wanawalazimisha wanafunzi walio carry lazima walipe gharama za mwaka mzima za hostel ilihali wamekuwepo chuo kwa nusu mwaka.

Nimewasilisha kama nilivyoelezwa na hawa wanafunzi na wanaomba muwapazie sauti sauti.
 
Inafikirisha Sana kukomoana Sana hasa chuo Cha kata Kama Udom kufanya hivyo nikunyima haki za wanafunzi
 
Inafikirisha Sana kukomoana Sana hasa chuo Cha kata Kama Udom kufanya hivyo nikunyima haki za wanafunzi
Chuo cha kata na una carry 😂😂😂😂

Kikubwa wasome, na uongozi uache mapuuza, uwasaidie madogo wapate haki yao, huyo katarambula kweli ni jipu sanaaa, ikibidi atolewe, ana maringo sana
 
Chuo cha kata na una carry 😂😂😂😂

Kikubwa wasome, na uongozi uache mapuuza, uwasaidie madogo wapate haki yao, huyo katarambula kweli ni jipu sanaaa, ikibidi atolewe, ana maringo sana
Kweli vijana wapige Kitabu maana huyo katarambula huna huruma yeye Wala Hana habari na mtu
 
Back
Top Bottom