DOKEZO Kero yangu kuhusu utaratibu wa 'refund' kwa Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Habari!

Napenda kuleta kero yangu ili mnisaidie kufikisha kwa wahusika wa Chuo cha DIT. Kuna kero kubwa hususani kwa wanafunzi waliopata mkopo kupitia Bodi ya mkoppo ya elimu ya juu (HESLB) pale wanapokuwa wanaanza mwaka wa masomo huitajika kulipa ada kwanza kabla ya kufanyika usajili, wanafunzi hao hulipa ada halafu baada ya muda HESLB hupeleka fedha hizo vyuoni.

Inapotokea pesa ya ada imezidi iliyotakiwa kulipwa, kiutaratibu inabidi mwanafunzi husika arudishiwe pesa iliyozidi. Lakini kumekuwa na maelezo kutoka kwa uongozi wa chuo kuwa Mwanafunzi hatorudishiwa pesa hadi pale atakapomaliza masomo yake yaani baada ya miaka minne au itatumika (transferred) kwa mwaka mwingine wa masomo kitu amabacho si sahihi kwa kuwa kila mwaka wa masomo unajitegemea ndio maana kunausajili kila mwaka mpya wa masomo unapoanza.

Je, ni halali Chuo kukaa na pesa ya mwanafunzi kwa muda wa miaka minne? Na ni sababu gani inasababisha baada ya miaka minne ndio pesa iweze kutoka na ishindikane kutoka ndani ya muhula wa masomo aliolipa hiyo pesa? Chuo hakioni kinatakiwa kulipa interest kwa kukaa na pesa za wanafunzi kwa muda mrefu?

Je, Chuo hakioni kinatengeneza mazingira magumu kwa wanafunzi ambao wanahitaji kutumia pesa hiyo kwenye mahitaji yao binafsi?

Je, Chuo hakioni kinatengeneza mazingira ya wanafunzi kuacha pesa kwa kusahau kwa kuwa ni vigumu kukumbuka na kutunza vielelezo vya malipo kwa muda wa miaka minne?

Asante.
 
Huu ni wizi kama wizi mwingine tu, dhuluma ya wazi kwa wanafunzi, kama ni kweli jambo hili halikubaliki@
 
Andika barua ya kuomba pesa iliozidi ilipie mchango fulani mwaka unaofuata kama mwaka husika umesharipia kila kitu.
 
Yaani tatizo bado ni kubwa sana katika vyuo vyetu hasa UDSM na matawi yake,
Udsm main campus walituambia uongozi wa idara ya fedha unashughulikia pesa za refund tar 7 July 2023, kusudi likizo inapoanza tar 24 July basi pesa refund ziwe tayari, lakini mwishowe tunadanganywa kwa kupewa calenda za uwongo hadi sasa hakuna hata mwanafunzi aliyepewa refund yake.

Na hili ni changamoto sana maana kipindi tunafanya usajili tulikataliwa hata tuliokuwa tunadaiwa senti chache mpaka kukamilisha usajili ni tumelipa kila kitu lakini sasa hivi refund yetu ni kutupiga tarehe na Pengine taarifa za uongo kutolewa na uongozi ya kuwa refund zimeanza kutolewa walakini hakuna hata moja aliyepew refund maana kila mwanafunzi analilia hilo.

Tunawaomba jamiiforums iweze kutufikia UDSM tuwaambie mengi mengi sana kuhusu yanayoendelea huku
 
Hivi ni kipi kinakwamisha urejeshwaji hizo pesa za wanafunzi? Maana inamaana wanazitumia kwa mambo ambayo hawakua kwenye mpango na budget yao.
 
Swala hili limeshakuwa jipu karibu vyuo vyote ,wakuu wa vyuo wahojiwe vizuri shida iko wapi ?
 
Hili tatizo na mimi nimekutana nalo, niliambiwa hadi nifike mwaka wa mwisho ndo nianze hatua za ufuatiliaji wa pesa hiyo. Niliandika barua hadi kuambatanisha viambatanisho vyote walivyosema niweke lakini sikuweza kurejeshewa fedha hiyo. Na nina miaka mitatu toka nimalize chuo.
 
Back
Top Bottom