DOKEZO Chuo Kikuu Iringa hawalipi mishahara kwa wakati na kuna changamoto ya Mifumo ya Malipo, hivyo Watumishi wasio waadilifu wanachezea mifumo ya malipo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Sakata la Chuo Kikuu cha Iringa roho za Watanzania zinateseka katika hicho chuo, kwanza hakilipi mishahara kwa wakati matokeo yake Watumishi wasio waadilifu ikiwepo Ofisi ya Uhasibu wanatengeneza mchezo mchafu wa malipo hewa ili kujipatia fedha.

Ishu hiyo ilipokugundulika chuo bila kuchunguza kikatoa tamko Wanafunzi walipe baada ya muda mchache wakafukuza Wanafunzi wa Mwaka wa Tatu waliokuwa kwenye hilo sakata.

Kwa ufupi wanachangamoto za mifumo ya ada na za kiutendaji ambazo bila kurekebishwa zinapelekea kushuka kwa hadhi ya vyuo vikuu nchini.

================

Updates...

MAJIBU YA CHUO

Afisa Mahusiano na Masoko wa Chuo Kikuu cha Iringa Crispin Nyomoye anafafanua: Kwanza kabisa hakuna changamoto ya malipo, mishahara inatoka kama kawaida, mfano mwezi uliopita watumishi walilipwa Julai 27.

Kuhusu mfumo tulitolea ufafanuzi, hakuna mfanyakazi yeyote ambaye alihusika, kilichofanyika ni taratibu za kawaida ambapo kuna wafanyakazi kadhaa wa Idara husika wakiweka kando kwa muda uchunguzi ukafanyika, baada ya muda ikaonekana hakuna tatizo ndipo wakarejeshwa kazini.

Kuhusu mifumo yetu ya malipo ipo imara japokuwa kuna maboresho ambayo yanafanyika, kwa sasa tuna mfumo mpya ambao tunautumia si kwa sababu uliokuwepo ulichezea bali kwa kuwa tunataka kuwa na kitu bora zaidi ya awali.

Pia soma:
Chuo Kikuu cha Iringa chawafukuza wanafunzi zaidi ya 50 kwa kudukua Mfumo wa Malipo ya Ada
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa wadaiwa kuingilia Mfumo na kuonekana kama Wamelipa Ada
 
Wanajitetea ila ukweli wanaujua
 
Back
Top Bottom