Serikali iwaajiri Walimu wahitimu wa mwaka 2015-2018 kwa mkupuo

Kandongu

New Member
Mar 5, 2018
2
2
Serikali kupitia OR TAMISEMI inawajibu wa kuwaajiri walimu hususan wahitimu wa mwaka 2015-2018 kwa mkupuo bila kujali masomo waliosoma.

Walimu hawa wengi wao wapo mitaani wakirandaranda huku na kule ili kuwezesha mikono yao iende kinywani.

KWANINI SERIKALI IWAAJIRI WALIMU HAWA KWA MKUPUO?

1. Ni mfumo uliopelekea walimu hawa wengi kusoma masomo ya arts.

Ukifuatilia kwa kina sana utagundua kuwa walimu hawa ambao hawaajiliki ni wale walioanzisha shule za sekondari za kata katika Miaka ya 2005-2009. Katika shule hizi za kata palikuwa na upungufu mkubwa sana wa vitu vifuatavyo:-

( a) Walimu wa masomo ya sayansi PHYSICS, BASIC MATHEMATICS, CHEMISTRY NA BIOLOGY. Hali hii ilipelekea wanafunzi wengi kutokusoma masomo haya toka kidato cha kwanza mpaka wanaohitimu kidato cha nne.

(b) Shule nyingi kutokuwa na maabara za masomo ya sayansi. Hii ilipelekea wanafunzi wengi kujifunza kwa nadharia na siyo kwa vitendo .

(c) Upungufu mkubwa wa vitabu vya masomo ya sayansi. Kitabu kilikuwa kinamilikiwa na mwalimu tu wanafunzi hawakuweza kupata vitabu vya kujisomea.

Mapungufu haya yalipelekea wanafunzi wengi kujikita kwenye masomo ya SANAA ambayo yalikuwa na walimu wa kutosha,vitabu vya kutosha.

Na ukifuatilia kwa kina sana utagundua walimu hawa walikuwa ni vipanga sana kwa sababu ukizingatia wakati ule ufaulu ulikuwa ni WA wanafunzi 0-5 kwa darasa moja lenye wanafunzi 50-300..

2. Uanzishwaji wa shule mpya za kata. Miaka ya hivi karibuni kumeibuka ongezeko kubwa sana la shule mpya karibia kila halmshauri ina shule mpya 2-5. Hivyo serikali iwaajiri walimu hawa wengi ili waweze kuzifungua shule hizi.

3. Maarifa yanapungua kwa sababu wamekaaa ntaani muda mrefu sana hivyo itachukua muda mrefu sana kwa walimu hawa kuregain momentum..
 
Tangu serikali ya awamu ya 5 ilipojiingiza kwenye ujenzi wa mamiradi makubwa na yasiyoisha; ndipo matatizo ya ajira kwa walimu, kupandisha madaraja/vyeo watumishi kwa wakati, na kuwaongezea mishahara yalipoanza.

Na kwa sababu mrithi wa Rais wa awamu ya 5 naye anaendeleza ile miradi mikubwa ya mtangulizi wake; basi sahau tu kuhusu ajira za hao walimu. Na kama wanaweza, bora wakaamua tu kujiajiri.
 
Hivi ukisomea ualimu inakua lazima kwa serikali kukuajiri ?
 
Ndiyo maana yake. Na huo mpango ulianza enzi za utawala wa JK. Lengo lilikuwa ni kupunguza uhaba wa walimu kwenye shule za serikali, na pia kuhakikisha walimu walioko kwenye hizo shule wanakidhi vigezo.

Ni bahati mbaya sana mpaka sasa huo uhaba bado upo kwenye shule nyingi za serikali, na hasa zile za pembezoni! Huku maelfu ya wahitimu wa hiyo fani ya ualimu wakiendelea kubakia mtaani kwa kushindwa kuajiriwa.

Ni kawaida pia katika hizo shule nyingi za serikali kukuta mwalimu mmoja anafundisha darasa lenye watoto zaidi ya 200, waliogawanywa katika mikondo 4 na kuendelea! Na wakati alitakiwa afundishe walau watoto wasiozidi 50, ili iwe rahisi kwake kuwasimamia vizuri kitaaluma.

Ajabu Kikwete aliweza ndani ya miaka yake 10! Aliweza kuajiri maelfu ya wahitimu wote waliomaliza chuo kila mwaka. Ila Magufuli na Samia, wameshindwa.
 
Ni bahati mbaya sana mpaka sasa huo uhaba bado upo kwenye shule nyingi za serikali, na hasa zile za pembezoni! Huku maelfu ya wahitimu wa hiyo fani ya ualimu wakiendelea kubaia mtaani kwa kushindwa kuajiriwa.

Ni kawaida pia katika hizo shule nyingi za serikali kukuta mwalimu mmoja anafundisha darasa lenye watoto zaidi ya 200, waliogawanywa katika mikondo 4 na kuendelea! Na wakati alitakiwa afundishe walau watoto wasiozidi 50, ili iwe rahisi kwake kuwasimamia vizuri kitaaluma.
Kwa utafiti nilofanya walimu wengi wapo mijini huko vijijini kwenye uhaba wakipangwa wanaenda wanakaa kidogo wanahama.kwaio tatizo linabaki vile vile
Lkn ifike mahala graduatess mliosomea ualimu msione kama ni lazima serikali iwaajiri.Huo utaratibu ulikuwepo lkn imefika wakati ambao graduate wamekua wengi kuliko mahitaji na kuna shule zipo walimu wanagawana topic za kufundisha.kwaio serikali iendelee kuajiri kulingana na mahitaji
 
Ndiyo maana yake. Na huo mpango ulianza enzi za utawala wa JK. Lengo lilikuwa ni kupunguza uhaba wa walimu kwenye shule za serikali, na pia kuhakikisha walimu walioko kwenye hizo shule wanakidhi vigezo.

Ni bahati mbaya sana mpaka sasa huo uhaba bado upo kwenye shule nyingi za serikali, na hasa zile za pembezoni! Huku maelfu ya wahitimu wa hiyo fani ya ualimu wakiendelea kubakia mtaani kwa kushindwa kuajiriwa.

Ni kawaida pia katika hizo shule nyingi za serikali kukuta mwalimu mmoja anafundisha darasa lenye watoto zaidi ya 200, waliogawanywa katika mikondo 4 na kuendelea! Na wakati alitakiwa afundishe walau watoto wasiozidi 50, ili iwe rahisi kwake kuwasimamia vizuri kitaaluma.

Ajabu Kikwete aliweza ndani ya miaka yake 10! Aliweza kuajiri maelfu ya wahitimu wote waliomaliza chuo kila mwaka. Ila Magufuli na Samia, wameshindwa.
Wahitimu kutoka shule za kata ulianza mwaka gani.
 
Kwa utafiti nilofanya walimu wengi wapo mijini huko vijijini kwenye uhaba wakipangwa wanaenda wanakaa kidogo wanahama.kwaio tatizo linabaki vile vile
Lkn ifike mahala graduatess mliosomea ualimu msione kama ni lazima serikali iwaajiri.Huo utaratibu ulikuwepo lkn imefika wakati ambao graduate wamekua wengi kuliko mahitaji na kuna shule zipo walimu wanagawana topic za kufundisha.kwaio serikali iendelee kuajiri kulingana na mahitaji
Ila kwa kuweka tu kumbukumbu sawa! Mimi siyo mmoja wa hao graduates wanaosubiri ajira.
 
Tangu serikali ya awamu ya 5 ilipojiingiza kwenye ujenzi wa mamiradi makubwa na yasiyoisha; ndipo matatizo ya ajira kwa walimu, kupandisha madaraja/vyeo watumishi kwa wakati, na kuwaongezea mishahara yalipoanza.

Na kwa sababu mrithi wa Rais wa awamu ya 5 naye anaendeleza ile miradi mikubwa ya mtangulizi wake; basi sahau tu kuhusu ajira za hao walimu. Na kama wanaweza, bora wakaamua tu kujiajiri.
kenge hawawezi kukuelewa hapa.... yule marehemu ametuachia msala utakaotutesa mpaka kiama..
 
Ndiyo maana yake. Na huo mpango ulianza enzi za utawala wa JK. Lengo lilikuwa ni kupunguza uhaba wa walimu kwenye shule za serikali, na pia kuhakikisha walimu walioko kwenye hizo shule wanakidhi vigezo.
Hujajibu swali. Umeulizwa kuwa ukisomea ualimu ni lazima serikali ikuajiri? Muuliza anataka kujua kama:-
*uwezi kuajiriwa na shule za binafsi? *Huwezi kujiajiri mwenyewe?
* Huwezi kuajiriwa sekta nyingine tofauti na ualimu?
 
Akikujibu unipigie.
Kuna watu ni ma slow learner mpaka basi. Sasa swali la kitoto kama hilo ndiyo nishindwe kujibu! Kwani huo ualimu inahusiana na usalama wa nchi mpaka ulazimishwe kuajiriwa na serikali?
 
Aisee! Yani jamii forum ni mseto,wengine wanalia wanajuta kufanyakazi ya ualimu,wengine wanalilia Ajira za ualimu,wengine wanataka kuacha kazi ya ualimu wajiajiri😕🥱
 
Nikajua kwa sasa hakuna tena jobless mtaani maana tuliambiwa kwa sasa ajira zinatangazwa zinakosa waombaji wanarudia kutangaza tena nafasi hizohizo bado hola.😁.
 
Mama hawezi ku absorb ma jobless wote wa miaka 5 ya Mwendazake.

Ila amejitahidi sana na watu wengi niliowafahamu wamepata kazi na qanashukuru kweli kweli.
 
Hujajibu swali. Umeulizwa kuwa ukisomea ualimu ni lazima serikali ikuajiri? Muuliza anataka kujua kama:-
*uwezi kuajiriwa na shule za binafsi? *Huwezi kujiajiri mwenyewe?
* Huwezi kuajiriwa sekta nyingine tofauti na ualimu?
haya ni maswali ya kipumbavu unayotakiwa kumuuliza mpumbavu...mtoa mada sio mpumbavu mkuu muombe radhi
 
Tulia mwalimu, kwann ulifeli mpk ukaangukia kusoma ualimu??

Maana moja ya sifa za kusoma ualimu ni kufeli. Hakuna mwenye one kali ya form 6 anaweza kwenda kusoma ualimu.

Na kwa ujinga wenu , maswali fikirishi mnayaona upumbavu.

Kwanza walimu timezivhoka mada za malalamiko yenu hapa JF. Nyambafu!!
 
HKL one kali nisisome ualimu
 
Back
Top Bottom