Mkuu Mkandara
Kwanza, naungana na
JokaKuu kuhusu watoa tuhuma.
Mfano, J.Selasini aliyeshirikiana na Msajili kuhujumu NCCR ndiye mtoa tuhuma.
Ukimsikliza anataka maridhiano kwa maana kwamba kuna kikwazo, HECHE
Yupo Lembrus Mchome aliyekodiwa apartment na Msajili kuhujumu CHADEMA, huyu naye unamsikiliza
Yupo Katibu wa UVCCM naye katoa tuhuma kama CHADEMA, naye unamsikiliza
Wapo wa mikoani, wote wanatoa tuhuma hakuna anayetueleza ushahidi upo wapi. Kwamba kuna pesa zimeliwa, hawaelezi wapi na kiasi gani
G. Msigwa wa CCM msemaji wa serikali anapokerwa na tuhuma za CHADEMA kuliko uhuni wa kujiteua uliofanyika pale Dodoma. Naye umamsikiliza kama mtu makini.
Msigwa anakerwa na tone tone lakini hakerwi na Trilioni moja ya Bajeti ya kachori, maandazi na vitumbua! Hakerwi na Wanawake kujifungua juu ya matenga. Huyu unamsikiliza kwa dhati kabisa!!!
Pili, Katibu mkuu kaeleza wazi taratibu za fedha . Kwamba, yeye ndiye anayehusika. Kwanini watu wanamtuhumu HECHE badala ya kuanza na mwenye dhamana?
Tatu, kuna taratibu za Chama chao kuhusu madai. Je wamezifikisha huko? CHADEMA ni taasisi siyo genge la watu. CCM walimwita Kolimba wakamalizana naye. CCM husema kuna taratibu za chama hata Wabunge wao kama caucus hawawezi kuisema serikali yao. Leo unaona utaratibu wa kuzungumza hovyo ni mzuri tu kwasababu ni CHADEMA
Mkuu utaruhusu uholela katika chama hiyo siyo taasisi. Kesho litaibuka kundi linalompinga Mnyika, utachunguza. Keshokutwa Sugu, utachunguza, siku nyingine Lema utachunguza. Yaani huoni kabisa kwamba kuna uhuni hapo !
Kinachotakiwa hapa si pesa za tone tone, ni kumuondoa HECHE aliyekuwa na LISSU katika mazungumzo yaliyofeli.
CCM na Serikali wanataka mtu laini kama MBOWE watakayeweza kupiga naye picha na kukaa vikao miaka 2 bila matokeo. CCM wanawaita akina HECHE Hardliners wanataka waondoke wapachike watu wao kama MBOWE.