Ndio kutofaa kwake kuliko hapa. Kama bungeni wanaweka sheria ili ziiweke serikali ktk mathubuti sasa na siku zote yy kimya. Akijua yy atataka kuiongoza hiyo serikali anakaa kimya. Wakulima na mazao yao yy kimya. Mishahara kimya. Pensheni ya wazee wa zamani kimya. Wastaafu wa EAC yy kimya. Wamachinga yy kimya. Wasukuma kula mapanki yy kimya. Wanyamwezi na nyumba 'ubavu wa mbwa' yy kimya. Singida wanakula mlo mmoja kwa siku yy kimya. Kila Mtz kipato duni lakini nchi deni kubwa yy kimya. Hajawahi kukemea walau kusemea ufisadi, rushwa, wizi na ubadhirifu wa mali za umma. Wanahamisha na kuua maliasili yy kimya. Elimu bora kwa wao na mbovu kwa akina Karumanzila yy kimya. Polisi, TISS na Jeshi vinatumiwa kinyume yy kimya. Mizengwe ktk Katiba Mpya yy kimya! Kama haya yote anayanyamazia huku ktk mfumo wa kuongoza yanakaa visivyo yy anataraji aje na staili ipi ya kuyarekebisha? Huyu Bwana ni mdhaifu sana, sana tena sana. Uongozi anautaka lakini hautengenezi bali kuendekeza rushwa Kanisani, Miskitini na Bodaboda.