Kwako Kaka William Malecela

Kwako Kaka William Malecela

- Ndugu yangu sana Bob, sikusema Mbowe ajiuzulu, no way bado Chadema inamuhitaji sana na bado ana miaka mingi zaidi ya siasa, isipokuwa Dr. Slaa huu ni wakati muafaka kwake kuanza kufikiria kukaa pembeni na awaachie wengine watafute agenda mpya ya Chadema kwa taifa, maana ya ufisadi imesiha nguvu tayari!

- Nitakupigia weekend maana last week ulikuwa hupatikani kwenye simu! Na sasa naomba kutoka kidogo baaadaye wakuu wote!

William @ NYC, USA.
Duh mbona mapema mkuu wangu unaondoka hali bado twakupenda?..
Hata hivyo ukirudi utayakuta haya..Dr.Slaa akae pembeni kwa sababu gani?..

Issue ya Ufisadi haiwezi kwisha ikiwa CCM wanacheza ngoma ya Dr.Slaa utafikiri wazungu wanavyocheza kiduku..Na wala sii swala la kisiasa tu Ufisadi ni lazima upigwe vita juu chini hadi imani ya watu irudi sio tu kwa CCM na viongozi wake bali kwa Taifa zima. Hvi vita sio vya Dr.Slaa hata kidogo, tazama mabillioni ya JK yalivyoyeyuka, Zana za kilimo kwanza zinavyopotea yaani wee acha tu. Ufisadi ni kwa kwenda mbele. Pengine unahitaji kutembea Bongo hata iwe kwa week tu utaipata fresh.

Hakuna sababu za kimsingi kwa Dr.Slaa kukaa pembeni wakati moto ndio umekolea, isipokuwa kuna watu pembeni ambao mimi nina mashaka na dhamira yao kwa sababu wanatumia sana jina lake lakini hawapo Chadema ati wao ni NEUTRAL na wanaunda kundi la kisiasa pasipo mrengo..Kwa maneno yao wanafuata mtu sio chama, hii kusema kweli inanipa shida sana kuelewa...
 
Arafat!

1. Nadhani ni mapokeo na makuzi, ukizaliwa kwa wakristo basi utaaminishwa kuwa hiyo ni dini bora, kama itakavyokuwa kwa waislam wazazi. Makuzi yetu haya mfanyi mtoto achague kile anachokiona bora. Wazazi watamwelekeza mtoto kuamini na kufuata kama wazazi wake.

2. Kwa ufahamu wangu watoto huweza kubadili dini wanapokuwa wakubwa na kujitegemea wanapoacha kuishi na wazazi ama walezi, mfano mtoto anapofikia kuowa basi anaweza amua kubadili dini kufata ya mwenza wake wazazi huweza kupinga kama kijana anamisimamo basi hufata dini mpya.

3. Namkumbuka makongoro Nyerere alikuwa NCCR na mbunge wa Arusha wakati baba yake ndiye muasisi wa chama cha Magamba (CCM) baada ya kushindwa mahakamani na ubunge kutenguliwa na kupigika mtaani basi akaamua kurudisha majeshi CCM na sasa ni mwenyekiti wa Magamba kule mkoani Mara.

4. Nadhani wazazi ambao ni key figures kwenye chama cha magamba, wanajitahidi kuweka watoto wao ili waweze kuwalindia maslahi yao iwapo wao hawatakuwa madarakani. Mfano wa kina Kawawa, Mzindakaya, Makamba, Kikwete na wengine wengi. Ila sijui kama Gamba Kingunge naye anafanya hilo maana mtoto wake Kinjeketile yeye anafaidi ufisadi wa baba bila yeye kuwa kwenye active siasa. Ni uwoga wa kujiwekea wigo mambo yasiende hadharani na watawale milele

Mtizamo wangu tu huu

Nashukuru sana Mchungaji! Bado nasubiri majibu ya Wlliam; Mchungaji kutokana na majibu yako unadhani kijana aliyekulia ndani ya CCM na ambaye uovu na magamba unayoyasema ndio yaliyomkuza, kumsomesha, na kumlea anaweza kushindwa kufa na haya Magamba?Kumbuka kuwa tofauti na wewe na mimi tunaokula kula vumbi hapa na kusubiri mgao wa Umeme William kupitia Magamba ya CCM uenda hakawa toka kuzaliwa hajawai hata kula mihogo! (sahamani sana Wliliam Naomba husichukulie kuwa nakuongea wewe so direct, ila nakutumia kama jukwaa kufika ujumbe)

Ndio umetoa mfano wa Makongoro, ni Challenge ya aina yake alitoa tena nakumbuka kipindi kile tukizunguka na Mwalimu kupiga kampeni za Ben yeye alikuwa anazunguka na Mrema pia kupiga kampeni nchni nzima, tena ubunge wa Arusha aliupata bila hata kufanya kampeni kwasababu yeye alikuwa Bizi na kampeni za Mrema!

Mchungaji inaweekana kama ulivyotoa mfano wa dini, lakini umesema mpaka kijana akuwe, labda niongeze pia Mpaka akomae kifikra na pia mpaka ajue kuwa siasa siyo dini hivyo siyo swala la imani ni itikadi tu!

Rev kama una mfano mwingine ndani ya EA unaweza kuutoa, maana hata wakina Uhuru walikulia USA hawakuwa wanaijua hata kenya inafafana vipi lakini ilipofikia Moi kustaafu alimwita Uhuru arudu home kuwa Rais wa Kenya! Ajabu sana.
 
mtanzania sina dini tofauti na ya wazazi wangu ambao ni wakatoliki tena wamekulia mission; wazazi wangu wako kwenye key figure za CCM tangu kaunzishwa TANU wakarithisha na mwingine ambaye amekuwepo for more than 15 years lakini mm ni CHADEMA damu [...]so mpaka hapo naamini wako wengi kama mm hapa. By the way hiyo ni inferiority complex walizonazo watu wengi kama wewe kiasi kwamba they want to mask individuals with other people's identity [...] Mawazo yako yanawakilisha vijana wengi wasiojiamini ndiyo maana CCM inaendelea kuwepo

Umeandika mambo mengi sana uenda ikawa kuna hoja ndani yake yakini yamefunikwa na magugu! Unaweza kuthibitisha hayo maneno hapo juu maana ndio yanawakilisha akili na upeo wako katika kujaribu kujibu maswali marahisi kabisa ambayo yalikuwa yanajieleza yenyewe sijui hata kama shule ulifaulu vyema wewe! Maana kama ni mtihani wa kiswahili wewe uneigia na majibu ya kukariri ukafanya mtihani wa hesabu, alafu hesabu zenyewe huzijui kweli wasahishaji wa mitihani wana kazi kweli kweli!
 
nadhani jumbe ameupata mkuu maaaana ni mzito na una mantiki...............
 
- Mkuu nenda uteme mate chini kwanza na umuombe Mungu wako akusamehe kwani sio siri kwamba hujui ulisemalo, jaribu kumjua mtu kwanza kabla hujatoa comment kama hii, kwa kweli hii imenidhi sana watu wanaolala macho kulisaidia hili taifa wanavyoweza kupachikwa anything, kwa sababu ni siasa tu! Jaribu kumjua the man na siku moja utakumbuka maneno yangu kwako kwamba muombe Mungu akusamehe na haya maneno!

William @ NYC, USA.

Kaka hata mimi nisiyejua siasa kwa kiasi kikubwa, ila kama kuna watu naawakubali nawapo nyuma ya pazia tangu jambo forums na jamii forums, mwanakijiji ni namba moja katika real fighters katika jamii/kizazi chetu hiki. Msamehe bure hajui alilosema.

Heshima mbele
 
Nashukuru sana Mchungaji! Bado nasubiri majibu ya Wlliam; Mchungaji kutokana na majibu yako unadhani kijana aliyekulia ndani ya CCM na ambaye uovu na magamba unayoyasema ndio yaliyomkuza, kumsomesha, na kumlea anaweza kushindwa kufa na haya Magamba?Kumbuka kuwa tofauti na wewe na mimi tunaokula kula vumbi hapa na kusubiri mgao wa Umeme William kupitia Magamba ya CCM uenda hakawa toka kuzaliwa hajawai hata kula mihogo! (sahamani sana Wliliam Naomba husichukulie kuwa nakuongea wewe so direct, ila nakutumia kama jukwaa kufika ujumbe)

Ndio umetoa mfano wa Makongoro, ni Challenge ya aina yake alitoa tena nakumbuka kipindi kile tukizunguka na Mwalimu kupiga kampeni za Ben yeye alikuwa anazunguka na Mrema pia kupiga kampeni nchni nzima, tena ubunge wa Arusha aliupata bila hata kufanya kampeni kwasababu yeye alikuwa Bizi na kampeni za Mrema!

Mchungaji inaweekana kama ulivyotoa mfano wa dini, lakini umesema mpaka kijana akuwe, labda niongeze pia Mpaka akomae kifikra na pia mpaka ajue kuwa siasa siyo dini hivyo siyo swala la imani ni itikadi tu!

Rev kama una mfano mwingine ndani ya EA unaweza kuutoa, maana hata wakina Uhuru walikulia USA hawakuwa wanaijua hata kenya inafafana vipi lakini ilipofikia Moi kustaafu alimwita Uhuru arudu home kuwa Rais wa Kenya! Ajabu sana.

Unalosema ni jambo la msingi. Kwa Tanzania na labda nchi nyingi za Afrika, siasa inakuwa ni kama vile mali ya ukoo. Na kwa vile dola bado ni chanzo cha uchumi wa watu wanaohangaikia matumbo (bila kujali legacy yao wenyewe), inakuwa vigumu kwa vijana kujitenga na wazazi wao. Na kama alivyosema Rev. Masa....vijana wameingizwa mkenge kujiona ni warithi na watetezi wa mali za jinai wanazojilimbikizia wazazi wao. Hili ni jambo la hatari kwa sababu sisi tulioko pembeni ambao tunachukia na kukemea vitendo vya watawala wetu na vibaraka wao (wengi wao wakiwa ni ndugu wa karibu na wanafamilia) tunaonekana kama maadui wakubwa (enemies of the state for their status quo). Ndio maana ujumbe wa UVCCM wa mkoa wa Pwani uko wazi...Kwamba uongozi Tanzania (na labda Afrika nzima) ni kujaza matumbo!!
 
Kaka hata mimi nisiyejua siasa kwa kiasi kikubwa, ila kama kuna watu naawakubali nawapo nyuma ya pazia tangu jambo forums na jamii forums, mwanakijiji ni namba moja katika real fighters katika jamii/kizazi chetu hiki. Msamehe bure hajui alilosema.

Heshima mbele

- Sawa sawa mkuu hapo tupo ukurasa mmoja saana.

William @ NYC, USA.
 
Umeandika mambo mengi sana uenda ikawa kuna hoja ndani yake yakini yamefunikwa na magugu! Unaweza kuthibitisha hayo maneno hapo juu maana ndio yanawakilisha akili na upeo wako katika kujaribu kujibu maswali marahisi kabisa ambayo yalikuwa yanajieleza yenyewe sijui hata kama shule ulifaulu vyema wewe! Maana kama ni mtihani wa kiswahili wewe uneigia na majibu ya kukariri ukafanya mtihani wa hesabu, alafu hesabu zenyewe huzijui kweli wasahishaji wa mitihani wana kazi kweli kweli!

Kwenye kutokujua luga hapo umenena kweli tupu maana ndiyo hasa tatizo langu! Ila mengine kwakua wewe unatawaliwa na hisia labda nikuulize swali unataka ni kwambie ukweli ama nikwambie kile moyo wako unataka kusikia ili kutimiza haja ya moyo wako? (kujifariji). Vijana wengi sana wakitanzania wako huru kimawazo hasa wale ambao wazazi wao walikuwa in practice Nyerere's followers sasa wewe kwa sample yako ndogo ya akina Riz1 and the cores unataka ku generalize wote ni kosa kubwa sana. After all angalia mawazo ya wachangiaji hapa ambapo ukiyasoma tuu wanaamini sana katika haya hata bila uhalisia. Hapa watu wakijibu hoja za Wilium unaona kabisa hazilengi katika hoja bali cheo cha baba yake na wengine wanaamini kabisa he is in a better position to bring significant change kama atakuwa in their favours. Hawamcchukulii Wilium kama one of their ranks he is given a special position hata bila yeye kujiweka hapo. Hapo niambie ni tatizo la nani? Wilium ama wale ambao wameji classify na kujiposition kwenye nafasi za kutoweza kumchallenge na wanaishia kumtukana na wengine kulaani ishara ya defeat!

To me Wilium is just like any other kijana wakitanzania kama ameshindwa kuleta gud welfare inamaana na mimi nikishindwa basi sote hatuna tofauti. Lakini kwakua naamini yeye to some extent ameweza kwa nafasi yake kwa mfano kuja na wazo la JF kama magazeti yanasema ukweli this is very independent from Malecela's ideas and shows the diference between. Sasa yeye kaweza huko inamaana mimi naweza kivyangu maana na talent zangu ambazo yeye hana. Na mimi hili likiingia vizuri kwenye ubongo wangu sita angalia viongozi wa CCM walioamua kuwaweka watoto kwenye madaraka kama threat bali ni weak agents ambao I can easly technically defeat them maana mimi ni kama siko kwenye hiyo kubebwa maanake nimekutana na challenge nyingi sana ambazo zinanipa opportunity ya kuwa out compete. Ndiyo maana huwezi mlinganisha Lisu, Kitila, Mnyika, Zitto etc na mtoto yeyote wa kibosile aliyebebwa na kupachikwa kwenye position wasimame kwa hoja na ionekane kawa defeated ndiyo maana walijiamini wakaenda upinzani. Lakini usisahau kuna Makongoro Nyerere aliye onyesha anaweza; vincent Nyerere and many other ambao wako under ground. Nilichotaka kukuonyesha nikuwa sample yako ni ndogo kuja na general conclusion. Na ku spot Africa tu ni kuionea mbona huzungumzii akina Bush; Hilary Clinton etc ambao wazazi/waume wao walikua kwenye vyama walivyovitumia kupigania madaraka? Wengi wa challengers wakubwa hapa JF na amini ni hao hao unaowalaumu nahisi waki reveal ID zao utashangaa kuona na utabadili kauli yako haraka sana!
 
Kwenye kutokujua luga hapo umenena kweli tupu maana ndiyo hasa tatizo langu! Ila mengine kwakua wewe unatawaliwa na hisia labda nikuulize swali unataka ni kwambie ukweli ama nikwambie kile moyo wako unataka kusikia ili kutimiza haja ya moyo wako? (kujifariji). Vijana wengi sana wakitanzania wako huru kimawazo hasa wale ambao wazazi wao walikuwa in practice Nyerere's followers sasa wewe kwa sample yako ndogo ya akina Riz1 and the cores unataka ku generalize wote ni kosa kubwa sana. After all angalia mawazo ya wachangiaji hapa ambapo ukiyasoma tuu wanaamini sana katika haya hata bila uhalisia. Hapa watu wakijibu hoja za Wilium unaona kabisa hazilengi katika hoja bali cheo cha baba yake na wengine wanaamini kabisa he is in a better position to bring significant change kama atakuwa in their favours. Hawamcchukulii Wilium kama one of their ranks he is given a special position hata bila yeye kujiweka hapo. Hapo niambie ni tatizo la nani? Wilium ama wale ambao wameji classify na kujiposition kwenye nafasi za kutoweza kumchallenge na wanaishia kumtukana na wengine kulaani ishara ya defeat!

To me Wilium is just like any other kijana wakitanzania kama ameshindwa kuleta gud welfare inamaana na mimi nikishindwa basi sote hatuna tofauti. Lakini kwakua naamini yeye to some extent ameweza kwa nafasi yake kwa mfano kuja na wazo la JF kama magazeti yanasema ukweli this is very independent from Malecela's ideas and shows the diference between. Sasa yeye kaweza huko inamaana mimi naweza kivyangu maana na talent zangu ambazo yeye hana. Na mimi hili likiingia vizuri kwenye ubongo wangu sita angalia viongozi wa CCM walioamua kuwaweka watoto kwenye madaraka kama threat bali ni weak agents ambao I can easly technically defeat them maana mimi ni kama siko kwenye hiyo kubebwa maanake nimekutana na challenge nyingi sana ambazo zinanipa opportunity ya kuwa out compete. Ndiyo maana huwezi mlinganisha Lisu, Kitila, Mnyika, Zitto etc na mtoto yeyote wa kibosile aliyebebwa na kupachikwa kwenye position wasimame kwa hoja na ionekane kawa defeated ndiyo maana walijiamini wakaenda upinzani. Lakini usisahau kuna Makongoro Nyerere aliye onyesha anaweza; vincent Nyerere and many other ambao wako under ground. Nilichotaka kukuonyesha nikuwa sample yako ni ndogo kuja na general conclusion.

- Strong sana mkuu, nice works!

William @ NYC, USA.
 
William CCM chini ya mwenyekiti wetu imepoteza imani si kwa watanzania tu bali hata sisi wanachama wa kawaida; nilisema na narudia kusema mh. Raisi si msafi yeye ni fisadi na ndiye kiongozi wao; kumteua Mkama kuwa katibu mkuu ni usanii, wapo viongozi wa zamani safi kama mzee Warioba angeweza kutusaidia lakini tatizo mh. Raisi hayupo serious kwenye vita vya ufisadi; nadhani labda kutokana kujuana kwenu bado una imani naye lakini ukweli wa mambo hawezi kuongoza vita dhidi ya mafisadi denial mechanism yako bado ipo juu, Rev. Masanilo ameliharikisha hilo binafsi nilikuwa nasubiri siku 120 nikuulize kuhusu kujivua gamba. Yeye na mafisadi wenzake wametuweka (CCM) kwenye hali ngumu, sijui kama ulikuwepo kwenye uchaguzi ukweli wa mambo hatukushinda, watanzania hawakuipa kura CCM si kwasabu wamekubali sera za Chadema bali matendo machafu ya viongozi wa juu wa CCM, ni aibu kubwa kwetu CCM tunajivunia kuleta demokrasia na leo hii tumegeuka wezi wa demokrasia, historia itatuhukumu.
Chama
Gongo la Mboto DSM.
 
Kaka William Malecela

Bila shaka uko salama na unaendelea na majukumu ya kila siku ya kimaisha. Nimeona leo nikuandikie waraka wa kirafiki kuhusiana na hali ya kisiasa na maisha yetu huku Tanzania. Nilikusoma siku chache zilizopita ukifahamisha umma jitihada zako za kuanzisha tawi la CCM huko uliko. Wengi walikupongeza na wengine kama kawaida walikubeza na kwenda mbali zaidi. Nakumbuka kwenye lile bandiko uliweka kauli mbiu ya kuvua magamba na CCM mpya. Nadhani Kaka Wiliam unajua sasa zile zilikuwa ni sanaa tu, Mukama na Nape wamekuwa wakitofautiana na muafaka na nani na lini hatua zitachukuliwa zidi ya wale waliokiweka chama chenu hapo kilipo. Mukama alienda mbali zaidi kudai hakuna listi ya watakao vuliwa magamba. Kumbuka huyu ndiye mtendaji mkuu wa shughuli za kila siku za chama na sekretariat nzima.

Bila shaka hakuna anachofanya Kikwete bila Rostam, Chenge na Lowassa kujua. Hawa watu wameshiriki kwa karibu sana na Kikwete na kufanikisha CCM-Mtandao Kushika dola. Haikuwa rahisi watu hawa kutengana kirahisi kama wengi tulivyotaka iwe. William ningeweza kukuandikia PM ila nimeona wacha na wanaJF wengine walione na watachangia. CCM na Magamba ilikuwa ni sanaa, kama ambavyo mwenyekiti wenu amekuwa akicheza na jukwaa kufurahisha hadhira. Alianza na semina elekezi Ngurudoto, kwa top govt officials, tunajua kashfa za ngono zilizofanyika kule 2006. Juzi katembelea wizara na kuamsha utendaji wa kazi, sasa amekuja na semina elekezi Dodoma, anarudia yale yale, kwenye formal logic hali inaitwa Tautology, hakuna tija wasiofanya kazi awapige chini, ngonjera zake zina gharama sana kwa wapiga kura. Nina wasi wasi CCM itagawanyka mikononi mwake na Muungano na Zanzibar utavunjika kabla ya 2015.

Kaka ningekushauri ufunge hilo tawi njoo tuungane kwa mambo yenye maslahi kwa taifa! Tuwe watanzania na si waCCM. Taifa lije mbele kama watanzania shida za umeme zinatokana na ufisadi zinatupata wote.

Ilikuwa niandike mengi wacha niwahi mazishi kuna kada wa CCM amekufa hapa mtaani

Respect

Mdogo wako Mch Masa

Heshima mkuu!
Waraka wako umejaa hekima na maneno mazito. Bila shaka, mlengwa atautafakari na kuufanyia kazi.
 
Watz ni kama wamelaaniwa na ccm! Kila saa ccm, ccm, ccm! ivi ni mama yenu? Wacheni ujinga! ccm is no longer a political party! It doesnt act like one nor behave like one! kila siku story mpya mpya tu! Hatuna muda wa kusubiri wakati nchi inaoza. Ondokeni ccm muanzishe chama kipya nyie mnajidai wasafi na wataka mabadiliko! Sijui kwa nini hamuwezi kufikiria namna hiyo! au mnasubiri mfanye kama wale wenzenu wa ccj kabla ya uchaguzi?
 
Mkuu Rev fr Masanilo wewe ndio wastahil pongez, umejivua gamba kwa faida ya wanajf wote, umesema ukweli wako kwa mtu stahili kuujua!nikikulinganisha na bwana wiliam nagundua kuwa huna malengo wala kitu chochote upatacho/utarajiacho zaid ya kutupa/kushare mawazo na sisi! Bwana william anandoto ya kurithishwa Madaraka. Kazi njema kaka!
 
I only see this Brother William....doom for CCM

IMG_4530.jpg
 
Matendo yako tu yanakutambulisha mkuu, kama kuna vyama vingine mbona hauviongelei wewe kila siku ni anti CHADEMA tu? au nikuwekee ushahidi wa post zako zote hapa sasa hivi?
Hivi mwanzilishi wa thread alimwalika Malecela ajiunge naye chama gani? Tukiijadili CCM, CUF, NCCR nitachangia kwa kadri ya uelewa wangu aloonijalia Mwenyezi Mungu. Ukifuatilia vizuri bila chuki posts nimewaweka kwenye kona watu wengi tu.
 
- Mkuu nenda uteme mate chini kwanza na umuombe Mungu wako akusamehe kwani sio siri kwamba hujui ulisemalo, jaribu kumjua mtu kwanza kabla hujatoa comment kama hii, kwa kweli hii imenidhi sana watu wanaolala macho kulisaidia hili taifa wanavyoweza kupachikwa anything, kwa sababu ni siasa tu! Jaribu kumjua the man na siku moja utakumbuka maneno yangu kwako kwamba muombe Mungu akusamehe na haya maneno!

William @ NYC, USA.

Mkuu, dunia ya ajabu sana hii, ndio maana Osama ni sahihi kwa fundamentalists wenzake na Obama ni sahihi kwa Wamarekani wenzake...nikwambie kitu; kila story ina Part II yake,,,wasema haya kwa sababu unaamini katika Part mojawapo ya story, mimi naamini katika Part nyingine...by the way ni mtizamo tu,,,,after critical analysis lakini!!!
 
Back
Top Bottom