Kwako Kaka William Malecela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwako Kaka William Malecela

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Masanilo, May 12, 2011.

 1. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kaka William Malecela

  Bila shaka uko salama na unaendelea na majukumu ya kila siku ya kimaisha. Nimeona leo nikuandikie waraka wa kirafiki kuhusiana na hali ya kisiasa na maisha yetu huku Tanzania. Nilikusoma siku chache zilizopita ukifahamisha umma jitihada zako za kuanzisha tawi la CCM huko uliko. Wengi walikupongeza na wengine kama kawaida walikubeza na kwenda mbali zaidi. Nakumbuka kwenye lile bandiko uliweka kauli mbiu ya kuvua magamba na CCM mpya. Nadhani Kaka Wiliam unajua sasa zile zilikuwa ni sanaa tu, Mukama na Nape wamekuwa wakitofautiana na muafaka na nani na lini hatua zitachukuliwa zidi ya wale waliokiweka chama chenu hapo kilipo. Mukama alienda mbali zaidi kudai hakuna listi ya watakao vuliwa magamba. Kumbuka huyu ndiye mtendaji mkuu wa shughuli za kila siku za chama na sekretariat nzima.

  Bila shaka hakuna anachofanya Kikwete bila Rostam, Chenge na Lowassa kujua. Hawa watu wameshiriki kwa karibu sana na Kikwete na kufanikisha CCM-Mtandao Kushika dola. Haikuwa rahisi watu hawa kutengana kirahisi kama wengi tulivyotaka iwe. William ningeweza kukuandikia PM ila nimeona wacha na wanaJF wengine walione na watachangia. CCM na Magamba ilikuwa ni sanaa, kama ambavyo mwenyekiti wenu amekuwa akicheza na jukwaa kufurahisha hadhira. Alianza na semina elekezi Ngurudoto, kwa top govt officials, tunajua kashfa za ngono zilizofanyika kule 2006. Juzi katembelea wizara na kuamsha utendaji wa kazi, sasa amekuja na semina elekezi Dodoma, anarudia yale yale, kwenye formal logic hali inaitwa Tautology, hakuna tija wasiofanya kazi awapige chini, ngonjera zake zina gharama sana kwa wapiga kura. Nina wasi wasi CCM itagawanyka mikononi mwake na Muungano na Zanzibar utavunjika kabla ya 2015.

  Kaka ningekushauri ufunge hilo tawi njoo tuungane kwa mambo yenye maslahi kwa taifa! Tuwe watanzania na si waCCM. Taifa lije mbele kama watanzania shida za umeme zinatokana na ufisadi zinatupata wote.

  Ilikuwa niandike mengi wacha niwahi mazishi kuna kada wa CCM amekufa hapa mtaani

  Respect

  Mdogo wako Mch Masa
   
 2. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  mwenye macho na aone.. mwenye masikio na asikie! asante mkuu
   
 3. M

  MILKYWAY GALAXY JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2011
  Joined: Dec 12, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  ReV,

  Kwanza pole na msiba wa mwenzetu.

  Ombi:
  Utakapo rudi jukwaani naomba umalizie hayo mengi uliyonayo.
  Ni muhimu sana tuelimishane, tuhabarishane na tuelekezane.

  Tanzania (bara na visiwani) ni yetu sote (CCM/CDM/CUF/HIZBU/Yahaya/Mtikila/EL/Mrema/mimi/wewe nk).

  Ni mboni ya jicho letu, likipofu hatuna pa kuponea.
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  May 12, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  !!!!!!! ?????////
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  May 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,383
  Likes Received: 5,670
  Trophy Points: 280

  Mwenye Pua kama yangu na aje Anuse !!
  polen pastor Mungu awape wepesi kama wenzangu wa pemba wasemavyo mmalize salwama
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  May 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,383
  Likes Received: 5,670
  Trophy Points: 280
  Yanatosha Mpwa akimaliza waweza tusikuone tena humu ndani..kuna upuuzi mwingi wa CCM bora ameamua kumtanabaisha ndugu yetu nae asome nyakati ..tatizo la malecela mgomba ulipochimbwa najua aana hamu ya kuingia kule kwenye kisima cha uzima cdm tatizo ndio hilo
  so kwa kuanzia tuanze kuombea ule Mgomba uje kwetu nilifurahi sana maneno yake siku watu walipojivua gamba..yule mzee soon atatoka kule sio mahali pake kabisa natumaini mkianza kwa willy mi wacha nianze maombi kwa Babu Yangu..unajua tunapoelekea kuna uwezakano wa kuoona Mbingu kwa ajili ya CCM kwako Willy
   
 7. wasaimon

  wasaimon R I P

  #7
  May 12, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aisee, ulikuwa wapi siku zote kumwandikia WM barua ya namna hii, sasa maliza mistari yako yote huenda kuna mistari mizuri umeiacha.
   
 8. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #8
  May 12, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,231
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Naam Rev,
  Ni imani yangu William amekusoma...na kama ana kichwa kizuri atakua ameelewa hata yale ambayo hukuandika! Kwa suala la msiba nitoe pole kwa kua aliyefariki ni mwanadamu mwenzetu bila kujali itikadi yake kichama!
   
 9. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #9
  May 12, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Bwana WM usikate tamaa na hizo porojo. CCM sasa imepata makamanda wa kupambana na kelele za Dr. Slaa. Hawa watu walizoea wao kupiga makombora na akina Makamba kutulia, siku hizi tz mambo mswano, Dr. Slaa akitoa kashfa kuhusu ufisadi wa CCM, Nape anajibu na vielelezo wa UFISADI wa Dr. Slaa.

  Hao CDM kesho wana mkutano Songea, leo CCM ina mkutano Songea; KUMEKUCHA!!!!
   
 10. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #10
  May 12, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Aisee huyu kumbe ni gamba pia!
   
 11. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #11
  May 12, 2011
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Sisi tulifikiri mnafikiria jinsi ya kutatua shida za wananchi, kumbe juhudi zote ni kujibu makombora ya Slaa!. Ama kweli kazi tunayo!.
   
 12. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #12
  May 12, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,231
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Mafilili usichojua ni kwamba kila zama ina kitabu chake! itafaa nini km mtu akijikusanyia watu wengi kupindukia wakati wa maziko yake?
   
 13. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #13
  May 12, 2011
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Masa baada ya kugundua jamaa ni share holder unatetemeka! unaogopa ban nini (joke). Huyo mwache abaki huko huko kuna watu wako upande huo ili kutimiza jambo fulani, ni mpango kamili. Hivi unafikiria Mungu anashindwa kumwangamiza shetani aka lucifer? la hasha ila ni kwa sababu Mungu anataka unconditional love!
   
 14. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #14
  May 12, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Well, Mkuu sana Masa heshima yako na ahsante sana kwa ujumbe wako, naomba kusema hivi:-

  1. CCM ni chama kikubwa sana kuliko Mukama na Nape, waliowavua ujumbe wa NEC na CC mafisadi sio Mukama na Nape, isipokuwa ni chama cha CCM collectivelly.

  2. Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye ndiye Rais wa Jamhuri kwa sasa, ndiye mtendaji mkuu wa chama CCM na amesema wazi kabisa kwamba maneno ya Nape ni yake pia, kwenye siasa za taifa hapo ndio mwanzo na mwisho, hakuna mwingine tena hata awe Mukama, Mwenyekiti ndio; FULL STOP WA YOTE!

  3. CCM kujivua magamba, ninaliamini kwa 100% kwanza tayari lilishaanza na sasa ni process tu kwenye kusomga mbele na kujivua na ni kwa speed ya CCM sio ya Chadema au anybody else! na kama kweli Rais wa sasa haamui maamuzi bila hao mapacha, basi wangekuwa bado wapo CC na NEC, na kama kweli Lowassa ana nguvu kama inavyosemekana basi angekua Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, siku aliponyimwa hivyo nafasi ukienda kuanglia records humu JF utaona nilisema wazi kwamba ulikuwa ndio mwisho wake politically, sasa jiulize nani aliymenyima hiyo nafasi?

  4. Kuhusu Tawi, kwa kweli kama nilivyoahidi nipo mbioni kulifungua very soon bado some very few touches ninazipitia kabla halijasimama, na mimi binafsi sina nia ya kuongoza tawi hilo, nitaliongoza kwa muda tu kuelekea kusimama na kuwaachia wengine maana in the wake ya habari za ushiriki wangu hapa JF last two weeks, nimeongezekewa sana na shughuli ambazo sasa zinaanza hata kunizidi kimo kwa sababu watu wanahitaji sana msaada wa mawazo! So!

  - Mwisho naomba kutoa ushauri wangu wa bure hapa JF, kwamba wakati umefika kwa baadhi yetu kujitoa nje to the public ili mfahamike na muweze kutumika kulisaidia taifa letu changa, maana hapa kuna watu kama wewe na wengine wengi ambao wana mawazo makubwa sana, lakini wenye shida hawawezi kukutafuta na hili jina, I mean ni ushauri wa bure tu!


  William @ NYC, USA.
   
 15. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #15
  May 12, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Sishangai wana CDM kawaida yenu ni kushangiliwa tu!!! Hamtaki kusikia mawazo ya upande wa pili wa shilingi. Songea ni kipimo chenu cha mapenzi ya wananchi kwenu, CCM Songea siku zote inagalagaza siku wapinzani. Usitumie nafasi ya akina WM kuwa nje ya nchi kuwadanganya badala ya kuwapa hali halisi kuhusu UPEPO wa kisiasa hapa nchini. Daima sitafungana na wale wasiotaka kuambiwa NO.
   
 16. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #16
  May 12, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Mkuu sijui hata unaongea nini! mimi siko chadema nipo CUF kama ukitaka kujua chama changu, Hapa hatuko kwenye kugalagazana mkuu hebu soma mawazo ya Malecela hapo juu ndo maana watoto wa viongozi wa ccm wataendelea kuongoza nchi hii sababu mtu kama wewe hufunguki na mawazo yako ya kitoto ya ushabiki zaidi kuliko UTAIFA!
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  May 12, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Maneno mazito sana haya! Kiasi nakubaliana na wewe ingawa umekuwa mjanja sana umenijibu kisiasa zaidi. Kama mwenyekiti ni tatizo huoni kuwa maamuzi yake yanaweza kuweka CCM pabaya? Kumbuka Raisi huyu aliye madarakani anamaliza muda wake 2015, CCM itaendelea kuwepo na ingependa iendelee kushika dola kwa miongo mingi mbele.

  Nadhani ifike wakati kofia ya Rais itenganishwe na Uenyekiti wa chama kusudi kama raisi anaharibu basi mwenyekiti aweze kuwa anampa mwongozo kwa sera za chama. Kuna Kada mmoja msibani hapa anadai CCM itakuwa imara iwapo Kikwete ataachia uenyekiti na apewe mtu mwingine makini kama Salim A Salim hata Kinana....walisemeaje hili?

  Kuhusu ushauri wako:

  Wengi tutaufanyia kazi ila bado kidogo

  Tupo Pamoja

   
 18. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #18
  May 12, 2011
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  sasa Brother William unaweza ukakubaliana na hali ilivyo ndani ya CCM kuwa kuna kukinzana katika utoaji wa Taarifa???? Au kwa maneno mengine maneno ya MUKAMA sio ya Mwenyekiti????

  Kwa nini zile kauli alizokuwa akizitoa NAPE dhiki ya mapacha watatu kwa sasa hazisikiki??? Kapigwa BITI???

  Further more kwa hali ya Maisha ilivyo hapa Home esp. huku KIGOMA nani wa Kulaumiwa???? Vp kuhusu mgao unaoendelea kulitesa taifa??? na viongozi ni wale wale wenye same old porojo.....

  CHUKUA HATUA BRO'!!!!
   
 19. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #19
  May 12, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  :A S 103::A S 103::A S 103: Umejieleza vizuri toka juu lakin hapo kwenye RED ndo umealibu :pound::pound::pound:
   
 20. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #20
  May 12, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kwa wale ambao mmesoma 'literature', iwe ya Kiswahili au ya Kiingereza, mnaweza kutafsiri ujumbe wa Mafili kwa aina mbili. Je umeweza kubaini tafsiri hizo?
   
Loading...