Kwako Kaka William Malecela

Kwako Kaka William Malecela

CCM sasa imepata makamanda wa kupambana na kelele za Dr. Slaa. Hawa watu walizoea wao kupiga makombora na akina Makamba kutulia, siku hizi tz mambo mswano, Dr. Slaa akitoa kashfa kuhusu ufisadi wa CCM, Nape anajibu na vielelezo wa UFISADI wa Dr. Slaa.

siasa sio malumbano
 
Ahsante sana Mkuu Masa,

Naona kama JF ya enzi zile inataka kurudi,

Nitapita baadaye kuchungulia nondo.

Ila huu usanii wa CCM ni zaidi ya leukemia!!

Mzee DC
 
Mchungaji na William naomba ni wakatishe kidogo!

Natumaini hamjambo na mnaendelea vyema na kutafakari mstakabali wa Tanzania kama siyo Tanganyika kwa nia njema kabisa! Wakuu nahitaji sana kuchangi hii topic lakini nawaomba sahamani sana kabla ya kuchangia mnisaidie maswali yafuatayo:
  1. Ni kwanini sisi waafrika Mtu babaye akiwa Mkristo na yeye anakuwa Mkristo! hata kama haendi kanisani ukimuuliza we dini gani atakutajia ya Baba na mama yake! ni kwanini? akiwa Muislam hata kama nikiwa kijiweni ukiniuliza Arafat we dini gani? haraka nitajibu Muislam! hata kama sijui mlango wa Mskiti! Ukiusema Uislam vibaya tutapamba hapo hapo maana dini ya baba yangu ndio yangu! nitaitetea milele?
  2. Ni wakati gani kwa kumbukumbu zenu utokea kijana wa kiafrika akawa na dini tofauti kabisa na ya wazazi wake?
  3. Sahamani sana hili la tatu halihusiki lakini pia mnaweza kulijibu siyo muhimu sana hili, Je ni kijana yupi Katika Tanzania ambaye babae/***** yupo katika list ya key figures za CCM (Naomba mtu hasiniulize key figures za CCM ni watu gani?) amewai kuwa chama cha upinzani?
  4. Kama mtakuwa mmeamua kujibu hilo swali ambalo halihusiki, Na.3 basi hamna budu mjibu na hili la nne, Je vijana ambao ni watoto wa key figures za CCM hawaoni kuwa kuendelea kutokuona maovu ya wazazi yao yataleta tabaka la ubaguzi huko mbeleni? na hasa hii tabia ya toa Mwinyi weka Mwinyi, kafariki Kawawa weka Kawawa mwingine, nk nk sahamani majina kawawa na mwinyi ni majina Fictitious (Kubuni) hayana uhusiano na Mtu yoyote yule haliyeopo au aliyewai kuwepo hapa Duniani.
Naomba Msaada wenu Tafadhali ili nami niweze kuendelea nanyi katika huu mjadala kabambe.
 
Arafat!

1. Nadhani ni mapokeo na makuzi, ukizaliwa kwa wakristo basi utaaminishwa kuwa hiyo ni dini bora, kama itakavyokuwa kwa waislam wazazi. Makuzi yetu haya mfanyi mtoto achague kile anachokiona bora. Wazazi watamwelekeza mtoto kuamini na kufuata kama wazazi wake.

2. Kwa ufahamu wangu watoto huweza kubadili dini wanapokuwa wakubwa na kujitegemea wanapoacha kuishi na wazazi ama walezi, mfano mtoto anapofikia kuowa basi anaweza amua kubadili dini kufata ya mwenza wake wazazi huweza kupinga kama kijana anamisimamo basi hufata dini mpya.

3. Namkumbuka makongoro Nyerere alikuwa NCCR na mbunge wa Arusha wakati baba yake ndiye muasisi wa chama cha Magamba (CCM) baada ya kushindwa mahakamani na ubunge kutenguliwa na kupigika mtaani basi akaamua kurudisha majeshi CCM na sasa ni mwenyekiti wa Magamba kule mkoani Mara.

4. Nadhani wazazi ambao ni key figures kwenye chama cha magamba, wanajitahidi kuweka watoto wao ili waweze kuwalindia maslahi yao iwapo wao hawatakuwa madarakani. Mfano wa kina Kawawa, Mzindakaya, Makamba, Kikwete na wengine wengi. Ila sijui kama Gamba Kingunge naye anafanya hilo maana mtoto wake Kinjeketile yeye anafaidi ufisadi wa baba bila yeye kuwa kwenye active siasa. Ni uwoga wa kujiwekea wigo mambo yasiende hadharani na watawale milele

Mtizamo wangu tu huu
 
Mchungaji na William naomba ni wakatishe kidogo!

Natumaini hamjambo na mnaendelea vyema na kutafakari mstakabali wa Tanzania kama siyo Tanganyika kwa nia njema kabisa! Wakuu nahitaji sana kuchangi hii topic lakini nawaomba sahamani sana kabla ya kuchangia mnisaidie maswali yafuatayo:
  1. Ni kwanini sisi waafrika Mtu babaye akiwa Mkristo na yeye anakuwa Mkristo! hata kama haendi kanisani ukimuuliza we dini gani atakutajia ya Baba na mama yake! ni kwanini? akiwa Muislam hata kama nikiwa kijiweni ukiniuliza Arafat we dini gani? haraka nitajibu Muislam! hata kama sijui mlango wa Mskiti! Ukiusema Uislam vibaya tutapamba hapo hapo maana dini ya baba yangu ndio yangu! nitaitetea milele?
  2. Ni wakati gani kwa kumbukumbu zenu utokea kijana wa kiafrika akawa na dini tofauti kabisa na ya wazazi wake?
  3. Sahamani sana hili la tatu halihusiki lakini pia mnaweza kulijibu siyo muhimu sana hili, Je ni kijana yupi Katika Tanzania ambaye babae/***** yupo katika list ya key figures za CCM (Naomba mtu hasiniulize key figures za CCM ni watu gani?) amewai kuwa chama cha upinzani?
  4. Kama mtakuwa mmeamua kujibu hilo swali ambalo halihusiki, Na.3 basi hamna budu mjibu na hili la nne, Je vijana ambao ni watoto wa key figures za CCM hawaoni kuwa kuendelea kutokuona maovu ya wazazi yao yataleta tabaka la ubaguzi huko mbeleni? na hasa hii tabia ya toa Mwinyi weka Mwinyi, kafariki Kawawa weka Kawawa mwingine, nk nk sahamani majina kawawa na mwinyi ni majina Fictitious (Kubuni) hayana uhusiano na Mtu yoyote yule haliyeopo au aliyewai kuwepo hapa Duniani.
Naomba Msaada wenu Tafadhali ili nami niweze kuendelea nanyi katika huu mjadala kabambe.

Usipende ku generalise issues! Mm ni mwafrica mtanzania sina dini, tofauti na wazazi wangu ambao ni wakatoliki tena wamekulia mission; wazazi wangu wako kwenye key figure za CCM tangu kaunzishwa TANU wakarithisha na mwingine ambaye amekuwepo for more than 15 years lakini mm ni CHADEMA damu so mpaka hapo naamini wako wengi kama mm hapa. Kwahiyo hiyo ni hisia yako tu ambazo hazina ukweli wowote. By the way hiyo ni inferiority complex walizonazo watu wengi kama wewe kiasi kwamba they want to mask individuals with other people's identity hata pale hao watu wanapoonyesha kuwa they are not a copy of somebody. Mfano mzuri ni Willium amekuwa mfano mzuri tu wa kulitetea taifa lake kwa vitendo lakini wengi wenu mlipoona jina lake tu mkaanza kumwekea sura ya Malecela senior. Bila shaka kama Willium anatumia jina lingine basi huenda yeye ndiye mwanakijiji naninyi mnapa thanks kibao humu kisa tu cover yake haim distract bali inatoa picha halisi ya yeye ni nani.

Mawazo yako yanawakilisha vijana wengi wasiojiamini ndiyo maana CCM inaendelea kuwepo hata kama haistahili kwani mna kosa ujasiri wa kuikabili na kuiambia no stop this is not the direction we want to go. Na mkimaanisha hawana njia watasalimu amri tatizo je mnathubutu? Mpaka Slaa awape ka ujasiri kidogo ndiyo hao mnatokeza nyuma yake na makelele mengi bila action zozote. Action si lazima ziwe violent bali zinazoonyesha kweli hapa mimi na simama ili nihesabiwe.
 
Let me know if you need any financial assistance on establishing the new CCM branch in NYC area.
Be blessed!

If you are not an opportunist i hope you would extent your financial assistance to the Tanzanians who are perpetually dying of maralia. The new CCM branch in NYC is not as important to common Tanzanians as the treatment of maralia or books for 'Kata' secondary schools.
 
nikalikupongeza lkn mdini mkubwa. utashauri kwa faida ya kanisa tu

Asante Sheikh ila unaonaje kama ukipisha watu wenye hoja.....naona unataka kuelekea kwenye anga zako ....Kila laherina kwa heri
 
If you are not an opportunist i hope you would extent your financial assistance to the Tanzanians who are perpetually dying of maralia. The new CCM branch in NYC is not as important to common Tanzanians as the treatment of maralia or books for 'Kata' secondary schools.

The ministry of Health will take care of the Malaria problem. I'm not an opportunist as you claim but rather deeply and selflessly dedicated to assist CCM-the party of the people, by the people, and for the people!!!
Long live CCM
 
Nakataa kabisa, Mwanakijiji mjanja mjanja sana, atatuuza...Dr Kitila hapana kabisa, ni aina ya wasomi wanaoamini wanajua kila kitu!!!!

- Mkuu nenda uteme mate chini kwanza na umuombe Mungu wako akusamehe kwani sio siri kwamba hujui ulisemalo, jaribu kumjua mtu kwanza kabla hujatoa comment kama hii, kwa kweli hii imenidhi sana watu wanaolala macho kulisaidia hili taifa wanavyoweza kupachikwa anything, kwa sababu ni siasa tu! Jaribu kumjua the man na siku moja utakumbuka maneno yangu kwako kwamba muombe Mungu akusamehe na haya maneno!

William @ NYC, USA.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Rev Masa
Kwanza ahsante sana kwa ushauri kwa kijana mwenzio.
Katikati ya mjadala humu, kuna mawazo yametokea hoja ni kujilaumu sisi watz kwamba tunaendekeza sana siasa kuliko utendaji.
Hii imekuwa maranyingi sana, watu kuponda siasa na wengine mkianza kujadili siasa tu hataki kusikia kitu kama hicho.
Binafsi napata shida kuelewa hivi vitu/hawa watu, labda niwekwe sawa lakini ninavyoelewa ni kwamba kupitia mfumo husika wa siasa ndimo mnamofuma aina ya jamii. Na kutokea hapo ndio uratibu wa mambo yote ya jamii husika yanapita, hivyo ipo wazi sana kwamba bila mfumo bora wa siasa ni ngumu sana kupiga hatua yoyote ya kimaendeleo, kwamba hata hizo nchi za ulimwengu wa kwanza zimefika hapo kwa matokeo ya mfumo bora (kwa mazingira yao) wa siasa.
Ni muhimu ikaeleweka kuwa matatizo yetu yote ya kijamii na kiuchumi mzizi wake mkuu ni siasa mbovu. Sijui ni vipi tunaweza kurekebisha eneo lolote katika jamii yetu chini ya mfumo wa kisiasa uliokandamizi na nyonyaji ambao umeshindwa kwa miaka 50 ya "uhuru" wa taifa hili.
Ni kujidanganya tu.
 
Mkuu wangu hapo ndio utaona tofauti yetu na hawa jjamaa. Obama anazirudi baada ya Ushindi wakati jamaa yetu yupo ktk Kampeni na hakika utamaduni wa mwafirika unaanza na ngoma. Hivyo kisiasa jamaa kapiga bao..

Nikirudi ktk siasa za Bongo, umezungumza kuhusu Dr.Slaa na Mbowe wajiuzuru nadhani haya ni mawazo ya KiCCM wakitaka force kubwa ya chama iondoke wakati hawa watu hawana hesabu kubwa bungeni kuwakilisha wananchi. Mbowe na Dr.Slaa wataondoka ktk nafasi zao ikiwa chama kinapoteza mwelekeo au kinapoteza umaarufu lakini huwezi kuondoa chama kubwa pasipo sababu ili mradi kupisha vijana wengine. Ila sema ni kweli ndani ya Chadema wapo watu au niseme viongozi ambao hata mimi nina mashaka nao sana.. kuna Unafiki wa kiana ambao unanipa wasiwasi sana kama vile wapo watu wanajiunga na Chadema kwa maslhai fulani..

Yawezekana kuwa ni wakati muafaka kwa CCM kubadilisha utawala wake ndani ya chama lakini nionavyo mimi CCM wamefanya makosa makubwa ktk mageuzi haya ya sectretariet kwa sababu wote walioingia madarakani hawajui siasa za Bongo...Na kusema kweli kama CCM ingeweza kumchagua mzee Malecela au vigogo wa zamani kuwa mwenyekiti au katibu mkuu wa chama nina hakika mngeweza kurudisha nguvu ya chama kwa sababu hawa watu wanaheshimika na wana nguvu ya kauli licha ya kwamba watu kaa Malecela wanazijua mbinu za kisiasa kupata ushindi kuliko malumbano ktk magazeti...Na labda nikwambie tu kwamba kina Nape na viongozi wa CCM waliopo leo wanacheza ngoma ya Chadema kujihusisha na malumbano ya Ufisadi..

Halafu mkuu wangu swala la Mafisadi ndilo linalosababisha matatizo yote ya kiuchumi.. Iwe kukosekana kwa umeme, maji, elimu,kilimo kwanza, afya yote haya yamerudishwa nyuma kwa sababu ya Ufisadi uliopo ngazi zote za utendaji. Hivyo huwezi kupuuza Ufisadi ukataka kujenga sera ambazo zitatumbukia ktk Ufisadi vile vile. JK kajaribu sana kuimarisha policies zetu ngazi za uzalishaji lakini zote zimeshindwa kufanya kazi kwa sababu ya UFISADI..Kibaya zaidi JK hataki kabisa kutazama huko kwa sababu ambazo anazijua mwenyewe - Hapa ndio kifo na mazishi ya CCM..

Na kusema kweli tatizo kubwa la JK ni udhaifu wake ktk kukemea Ufisadi laasivyo nina hakika yapo mengi aloyafanya yangekuwa na matunda makubwa sana..Sasa ikiwa kiongozi wa Taifa ni dhaifu, nashindwa kuelewa mtaweza vipi kukijenga chama wakati kiongozi wenu ni dhaifu ktk maamuzi na utekelezaji. Halafu kibaya zaidi navyosikia JK ana tabia ya wale wanaojua kila kitu hali hawajui na mwenye msimamo wake pekee yaani hatabiriki, haambiliki na hasamehe wala kusahau fadhila au hasidi..Na hizi personal emotional hazifungamani na social development..

- Ndugu yangu sana Bob, sikusema Mbowe ajiuzulu, no way bado Chadema inamuhitaji sana na bado ana miaka mingi zaidi ya siasa, isipokuwa Dr. Slaa huu ni wakati muafaka kwake kuanza kufikiria kukaa pembeni na awaachie wengine watafute agenda mpya ya Chadema kwa taifa, maana ya ufisadi imesiha nguvu tayari!

- Nitakupigia weekend maana last week ulikuwa hupatikani kwenye simu!
Na sasa naomba kutoka kidogo baaadaye wakuu wote!

William @ NYC, USA.
 
The ministry of Health will take care of the Malaria problem. I'm not an opportunist as you claim but rather deeply and selflessly dedicated to assist CCM-the party of the people, by the people, and for the people!!!
Long live CCM

I am sorry if i offended you, i acknowledge your dedication to the party of the people which does not take care of the common people!
 
Kaka ningekushauri ufunge hilo tawi njoo tuungane kwa mambo yenye maslahi kwa taifa! Tuwe watanzania na si waCCM. Taifa lije mbele kama watanzania shida za umeme zinatokana na ufisadi zinatupata wote.

Ilikuwa niandike mengi wacha niwahi mazishi kuna kada wa CCM amekufa hapa mtaani

Respect

Mdogo wako Mch Masa

Mch. hiyo hapo kwenye red ndicho hasa wanaccm wanachoshindwa kuwa rational linapokuja suala la kipi kitangulie kati ya hivyo viwili. Naomba maombi yako yawafikie na waelewe tofauti ya hayo mawili na hapo ndipo nchi itasonga mbele
 
........ Sijui ni vipi tunaweza kurekebisha eneo lolote katika jamii yetu chini ya mfumo wa kisiasa uliokandamizi na nyonyaji ambao umeshindwa kwa miaka 50 ya "uhuru" wa taifa hili.[/COLOR]
Ni kujidanganya tu.

Kurekebisha mfumo ni pale wanasiasa wataka potambua kikomo cha wajibu na mdaraka yao na aple watendaji wengine watakapotambua wajibu na majukumu yao kivitendo.

Ni sababu tumejikita kwenye siasa ndio maana kichumi, Kielimu may be kisayansi kwenye makaratasi tunaweza kuwa na sera nzuri kuliko hata kenya ,uganda na Rwanda...... lakini kiutenedaji na iutekelzaji we are worse if not worst

  • Wanasiasa wanahubiri Teknolojia but hawatekelezi wanayohubiri.

  • Wabunge wanasema tununue na tupende bidhaa zetu lakini suti na viatu wananvyoavaa bungeni ni za italy na china. Ukiondoa wanawake my be Hakuna hata moja ameshonesha au kuchongesha japo pair moja ya viatu kwa mafundi wa hapa nchini au majimboni kukuza ajira.
Part ya tatizo ni mfumo wa siasa na part ya tatizo ni watendaji ambao tunasubiri kuagizwa na wanasiasa hatutoi ushauri wala mapendekezo kiofisi.

Mimi narudi kwenye mfano wangu wa elimu. Nenda wizara ya elimu uone kuna miradi mingapi? Je ni mradi gani inawanufaisha wanafunzi na elimu moja kwa moja. Hivi kuchukua walimu wachache na kurekodi video za masomo na kuuza video practical ni sh ngapi? Lakini Pale wizara ya elimukuna wataalam wa ICT wote tunajua kuna uhaba wa maabara na vifaa. Mimi narudia sioni kwa nini shule tena za mjini ziendee kusema hazina maabara au vifaa vywa maabara. kama hakuna maabra tengenza video lab wanafunzi waone. Nikiangalia hizi video naona kabaisa ningeziona kipindi nasoma nisingepata mswaki wa hesabu teh teh teh

  • Je watendaji wa ICT pale hawajawai kufikria jinsi taaluma yao inaweza kusaidia kutatua matatizo ya elimu.
  • Je watendaji wanatoa mapendekezo na ushauri hayafanyiwi kazi au wanasubiri Katibu mkuu na waziri mkuu wa mkoa waagize wao watekeleze.?
So sometine hata sisi wajiriwa vijana hasa walioko serikalini tena wenye elimu nzuri kama unamaliza mwaka mzima bila officialy kutoa na kuandika pendekezo lolote linalo weza kuboresha utendaji wa eneo lako la kazi ujue una kasoro.

Ni kasumba ya Top Down na Boss know it all ndo inaharibu na kuuua creativity , innoviation na new constructive Ideas/ criticism
 
- Mkuu mimi ni member tu kama wengine hapa, lakini sio siri kwamba I have access kwa watawala wa vyama vyote vya siasa, kwamba ninaweza kutatua tatizo lolote hapana, lakini ninaweza kuwafikishia wanaohusika malalamiko. HOWEVER Mama Makinda alipopewa u-Spika nilisema hivi, amepewa kwa ridhaa ya Ikulu, meaning kwamba kwa uwezo wangu wa kusoma siasa, kuna mabadiliko makubwa yanakuja on mafisadi maana huyo sio chaguo lao,

- Matokeo yakawa mafisadi kuondolewa NEC na CC na sasa wako njiani kuondolewa kabisa CCM, ninasema hivi wanaondoka very soon kama hawajaambiwa tayari ni kwamba wataondolewa tu ndio maana wameshaombwa kuingia upinzani na kuna wakati walitishia kuanzisha chama chao, sasa wakati wao ni huu wakaanzishe chama chao maana wataondolewa very soon. So mkuu tunajidiliana na kupena moyo pia kwamba pole pole tutafika!

William @ NYC, USA.

mbona iko dhahiri kwamba mama Makinda ni chaguo la Mafisadi?
Pili nakuomba kaka mshauri mbunge wetu wa same mashariki akumbuke zile barabara zetu kwani Tangia uhuru tunaahidiwa tu zitajengwa kama ngonjera. Kuna ile ya mkomazi- kihurio- ndungu- kisiwani- same. Na kuna ya ndungu- mamba miamba- bwambo- saweni. Na bwambo suji-makanya. nyingine Mamba miamba-gonja- mbaga.

Najua sio rahisi kujenga zote kwa wakati mmoja ila bila hizi barabara maendeleo mitaa hiyo itakuwa ngumu. Nimeandika kwa sababu umesema una access na watawala na viongozi wote wapinzani na CCM. Mpelekee huu ujumbe anayehusika. mwambie kile kiwanda cha iliki ni usanii wa uchaguzi sasa afanye kazi uchaguzi umekwisha. Na mwambie Same imeshika mkia kwenye elimu kwenye ubunge wake. Same ilikuwa ndio kioo cha elimu TZ. Mwambie ni vigumu sana kuvuvuzela na kazi. Wananchi wanataka maendeleo walao kitu kimoja kwa mwaka wa fedha. utaifa mbele siasa nyuma.

Utaifa ukiwa kweli mbele tutaendelea, ila kuna njia panda ya utaifa na uzalendo pale ufunguo wa hazina akikabidhiwa mtu. Ndio maana wengi tunataka katiba mpya itakayotoa maelekezo ya kufikishana segerea kirahisi bila ubaguzi.

Swala la Jina la mwisho au majina ya wakubwa sio dhambi kuwa nayo tatizo kuna wakati watu wali abuse jamii kwa majina hayo, yalikuwa ndio yanaonekana ni watu zaidi ya wengine, jitihada zilikuwa hazihesabiwi kaka. Mfano mpaka leo kijana mwenzetu hajatuambia amepataje ubilionea kirahisi ili nasi tufanye. Hakuna shida kina Nape, na Makamba kupewa vyeo kama wamevifanyia kazi ila ukweli unajulikana ni mbereko ya chuma.

Naona unamategemeo sana na vijana hawa ila ukumbuke kuwa Chenge, Lowassa, Y Makamba, JK, Yona Nk nao walikuwa vijana siku moja tena walianzia umoja wa vijana wa wakati huo. Walipohamia serikalini kwa kofia ya CCM matokeo yake tunayaona.

Lazima chama kilichopo madarakani kikubali kuwa mfumo wa utawala umeshindwa, tunahitaji utawala wa sheria na katiba ifuatwe tena katiba ya wananchi. Matatizo yapo serikali ambapo huko hakuna kuwajibika, uzembe, ufisadi na matumizi mabovu ya mali za taifa. huko ndiko kwenye ngozi za kuchunwa. Mwenyekiti wa CCM analijua hilo ila hataki kufanya kazi. Swala la kufikiri uvuvuzela wa Nape utawapa nafuu CCM sidhani.

Kelele za wananchi ni huduma bora na maisha walioahidiwa hayatokei. Mfano halamshauri ya Ndesa-pesa ndio halmashauri bora kwa sasa usafi, mipango mijini nk. CCM wao wanapita kuuza sura eti kisa mmemwondoa Makamba mkamwingiza makamba. Kwani hizo sura za akina Nape zinawasha Umeme, zinaleta maji au zina jenga barabara? CCM ni wajibu wao kujibu mashambulizi kiutendaji badala ya kivuvuvzela?

Niatawashangaa sana CDM wakiwa madarakani, wananchi wakapiga kelele ufisadi ufisadi, uzembe , rushwa na tip za hao wanapewa na wananchi eti wakaanzisha uvuvuzela wa kutetea mambo yaliyo wazi. Nategemea CDM itamwajibisha mzembe, fisadi, mla rushwa, na mtu yeyote atakayesaidia kuingiza nchi hasara. hiyo ni kazi ya mtawala, sio kutoa ahadi kila asubuhi, ooh tumewafukuza wakati wapo. ooh ngoja muone lini? ooh mafisadi hawapo tena come on !!
 
Back
Top Bottom