THINKINGBEING
JF-Expert Member
- Aug 9, 2010
- 2,779
- 1,304
Hatuwezi kukulaumu.CCM ndio iliyokufikisha hapo.Wakati ikikupatia mkate na siagi wenzio ilituacha tule ugali na upupu.Nafikiri pia hujui kama kwetu upupu umekuwa mboga.- Well, Mkuu sana Masa heshima yako na ahsante sana kwa ujumbe wako, naomba kusema hivi:-
1. CCM ni chama kikubwa sana kuliko Mukama na Nape, waliowavua ujumbe wa NEC na CC mafisadi sio Mukama na Nape, isipokuwa ni chama cha CCM collectivelly.
2. Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye ndiye Rais wa Jamhuri kwa sasa, ndiye mtendaji mkuu wa chama CCM na amesema wazi kabisa kwamba maneno ya Nape ni yake pia, kwenye siasa za taifa hapo ndio mwanzo na mwisho, hakuna mwingine tena hata awe Mukama, Mwenyekiti ndio; FULL STOP WA YOTE!
3. CCM kujivua magamba, ninaliamini kwa 100% kwanza tayari lilishaanza na sasa ni process tu kwenye kusomga mbele na kujivua na ni kwa speed ya CCM sio ya Chadema au anybody else! na kama kweli Rais wa sasa haamui maamuzi bila hao mapacha, basi wangekuwa bado wapo CC na NEC, na kama kweli Lowassa ana nguvu kama inavyosemekana basi angekua Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, siku aliponyimwa hivyo nafasi ukienda kuanglia records humu JF utaona nilisema wazi kwamba ulikuwa ndio mwisho wake politically, sasa jiulize nani aliymenyima hiyo nafasi?
4. Kuhusu Tawi, kwa kweli kama nilivyoahidi nipo mbioni kulifungua very soon bado some very few touches ninazipitia kabla halijasimama, na mimi binafsi sina nia ya kuongoza tawi hilo, nitaliongoza kwa muda tu kuelekea kusimama na kuwaachia wengine maana in the wake ya habari za ushiriki wangu hapa JF last two weeks, nimeongezekewa sana na shughuli ambazo sasa zinaanza hata kunizidi kimo kwa sababu watu wanahitaji sana msaada wa mawazo! So!
- Mwisho naomba kutoa ushauri wangu wa bure hapa JF, kwamba wakati umefika kwa baadhi yetu kujitoa nje to the public ili mfahamike na muweze kutumika kulisaidia taifa letu changa, maana hapa kuna watu kama wewe na wengine wengi ambao wana mawazo makubwa sana, lakini wenye shida hawawezi kukutafuta na hili jina, I mean ni ushauri wa bure tu!
William @ NYC, USA.
Kaka najua kwa hii "political inbreeding" ya tanzania upo kwenye warithi wa ufalme hivyo huwezi kuupinga utawala mbovu wa CCM.
"SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA" bado kitambo kidogo hizo ndoto za ufalme tutazitowesha.