Kwako Kaka William Malecela

Kwako Kaka William Malecela

Ndugu William kwani huyo anayechaguliwa kushika nafasi zote mbili ana miaka 300? Alijifunza wapi kuw Rais na mwenyekiti wa chama kwa pamoja? Na huko alikojifunzia alikuwa peke yake?. In maana Tanzania hatuna uwezo sasa hivi wa kutengeza utaratibu ili kila mtu awe na area of focus badala ya huu mfumo wa kachumbari? Kenya wamepata Uhuru baada ya sisi na tayari wako mbele ki-mfumo, pamoja na matatizo ya baadhi lakini you can see these guys are on the move. Sisi tumebaki na huu umbilikimo wa mawazo -wachanga hili wachanga lile. Nakataa hoja.

- Well, siasa za vyama vinaongozwa na katiba ya vyama hata huko Kenya wanaongozwa na katiba ya chama kwa hiyo kiongozi anayechaguliwa hahitaji kuseoma anything zaidi tu ya kusoma katiba, Kenya walianza na itikadi za kibepari sisi tulianza na itikadi za kijamaa, ambazo zilishindwa kwenye vita na za kibepari, sasa ya Kenya kwua mbele yasikushangaze sana, ingawa it can be debated of what hasa wako mbele yetu!

- Kwa maoni yangu bado CCM tunahitaji Mwenyekiti kuwa mgombea u-Rais.

William @ NYC, USA.
 
- Well, Nape amesema mafisadi wataondolewa CCM, Nape ni my loongtime friend tunatoka mbaali sana na huu mchezo wa siasa and I trust him kwa sababu at one time in 2005 mimi na yeye we were offered big rewards kama tungejiunga na kundi flani la siasa tukakataa kwa kauli moja, nimeongea naye na ninamuamini 100%, kama sio hivyo Nape asingekubali kuchukua hii nafasi ya CCM!

- Mtatizo ya umasikini yapo hata huku ndugu yangu, ndio maana mimi ninajali sana tunakokwenda sio tulikotoka!

William @ NYC, USA.

William, Matatizo ya wenzetu ni afadhali haya ya kwetu yamepita kiasi. Fikiria umeme unakatika usiku mzima na joto hili la dar na maji ya kuoga hakuna dumu mojaTsh 250 tena maji ya chumvi, hapo kaka mshahara sh 85,000 kwa mwezi? Mchele kilo 1600, Unga 1000 bado matumizi mengine... Mafuta ya Petrol na ya Taa ni zaidi ya dola moja na ushee kwa lita... yaani hakuna pa kujikuna hali ni mbaya sana.

hali ni mbaya mbaya vibaya, niamini mimi bila marekebisho katika uongozi wa nchi hii nakwambia hatufiki 2015, watu wa hali ya chini itafikia hatua watashindwa uvumilivu. na dalili ya tunakokwenda kwa mtazamo wangu ni GIZA kabisa, sioni mwanga kabisa kama hata elimu tunailetea maloloso (utani) yaani tunajiua wenyewe.

Ni maoni tu, sina jingine ndugu yangu, sina uhakika ulikuwa unaongelea CCM inakotoka na inakokwenda au Taifa kwa ujumla.
 
Bwana WM usikate tamaa na hizo porojo. CCM sasa imepata makamanda wa kupambana na kelele za Dr. Slaa. Hawa watu walizoea wao kupiga makombora na akina Makamba kutulia, siku hizi tz mambo mswano, Dr. Slaa akitoa kashfa kuhusu ufisadi wa CCM, Nape anajibu na vielelezo wa UFISADI wa Dr. Slaa.

Hao CDM kesho wana mkutano Songea, leo CCM ina mkutano Songea; KUMEKUCHA!!!!

Umeshaambiwa Tanzania ni yetu wote hata sisi tusiokuwa na vyama. Hizo ngonjera za Nape na Slaa hazitoisaidia Tanzania. Ni matendo.
NDIO MAANA TUNAOMBA KATIBA IBADILISHWE ILI TUWE NA WAGOMBEA HURUUUUUUUUU, hapo ndio mtaona vifo vya wanasiasa wa ngonjera na vifo vya vyama
 
Bwana WM usikate tamaa na hizo porojo. CCM sasa imepata makamanda wa kupambana na kelele za Dr. Slaa. Hawa watu walizoea wao kupiga makombora na akina Makamba kutulia, siku hizi tz mambo mswano, Dr. Slaa akitoa kashfa kuhusu ufisadi wa CCM, Nape anajibu na vielelezo wa UFISADI wa Dr. Slaa.

Hao CDM kesho wana mkutano Songea, leo CCM ina mkutano Songea; KUMEKUCHA!!!!

Samahani sana ndugu yangu nakuomba tafakari na tambua kuwa hatushindani na hata hayo makombora sio kufurahisha watanzania, Sisi hatuitaji makombora tunaitaji kuona KODI zetu zina tunufaishi sisi watanzania na sio nyie viongozi, nakuomba jua kuwa Gharama hizi za maisha aziwezi kupungua kwa kujibu kashfaa kwa kashfaa bali kashfaa kwa vitendo, au wewe unaishi Tanzania ipi?
 
Mkuu inabidi wengine waendele au tuendele na majina haya haya ili jf iwe na michango iliyoendela shule.

Wengine wakijivua "magamba ya majina" watabaki kuwa wanafiki sababu ya nafasi zao au ajira zao au tender zao au familia zao. Hivi tulivyo na haya magamba we can call a spade a spade bila kuuma uma maneno inagwa nasi au wazee wetu wako huko huko kwenye magamba original wakila keki ya taifa teh teh teh .

Inawezekana tofauti yako na sisi wenye majina feki ni kuwa wewe unauma uma maneno sisi wenye majina yenye magamba ni straight to the point. but sote lengo letu ni moja......

Huwa naona post zako na Idea zako sometine na zetu hazitofautiani .Tofauti na kikwazo kwako ni hiyo screen name inakufanya kuzunguka kama treni.

Nilikutumiga issue fulani sijui mwaka juzi mpakaleo kimyaaaaa

Tuko pamoja teh teh teh

What is 7.5???????? unaona nyingi sana??????? dr slaaa anatakiwa kupata mshahara kama au zaidi ya anaopata mbunge sababu lile jimbo aliloaacha kule ni kama lake. May be sema mbunge wa bunge linaloongozwa chini ya serikali ya CCM anapata shilingi ngapi kwa mwezi?

- Mkuu heshima yako sana, umenivunja mbaavu sana well, ninasema hivi sio wote lazima wajitoe na sio kwamba ukijitoa basi huwezi kuendelea kujificha ficha pia, lakini ninasema hivi Dr. Kitila mbona alijitoa na mpaka leo anaendeela tena kwa juu sana kulisaidia taifa letu, au nayeye ana jina la baba? I mean I am shocked na jinsi hili taifa linavyohitaji msaada wa mawazo, I mean kujitoa sio ya wote, lakini kamainawezekana please, ingawa una hoja nzito sana kwamba bila kujificha JF itakosa chumvi yake ya asili.

- HOWEVER: sasa hivi JF we have a National platform na infact we have a mandate from the people, sasa ni lazima tuendelee kuitumia kuwaamsha wananchi, na sio siri tunaiweza hiyo kazi zaidi tunapokuwa tumejificha ya kukosoa ubovu katika taifa, sawa sawa ndugu yangu
!

William @ NYC, USA.
 
Vichwa vyote vizuri vikiwekwa chama kimoja hatutafika kokote. Tutafute tu chama mbadala. Tuwaache wengine wabaki bila vyama wala watu wao. Sasa tuna watu wa Dr Slaa sio CHADEMA. Tuna watu wa JK sio CCM. Tutake tusitake tunao. Wapo pia wanaoangalia kiongozi mkuu wa chama ni KABILA au DINI gani. Tunao. Na hiyo ndio Tanzania ya sasa. Tunatakiwa tugawanyike kwa staili ya Simba na Yanga ndipo tutasonga mbele kama nchi.
 
CCM mnajikanganya, hakuna msimamo wa taarifa, huyu akisema A mwingine anasema Z. Oneni wenzenu wa Chadema walivyo smart, hata kwenye kampeni 2010 walikuwa smart katika kujibu maswali utafikiri walipewa kwanza somo. Tatizo sijaweza kuona tofauti ya comrade Makamba na Nape na huyo Mukama. Wote kushoto kulia tu. Hakuna cha kujivua gamba wala nini? Nyoka ni yule yule tu, tena kwa kawaida nyoka akijivua gamba ndo anakuwa mkali zaid, kwa mantiki hiyo mambo ni mabaya zaidi kwa Chama chetu hicho. Kuna zaidi ya kubadili viongozi, chama kimeshapasuka makundi matatu, CCM Asili, CCM Mamboleo na CCM Chumia tumbo.
 
- Mkuu heshima yako sana, umenivunja mbaavu sana well, ninasema hivi sio wote lazima wajitoe na sio kwamba ukijitoa basi huwezi kuendelea kujificha ficha pia, lakini ninasema hivi Dr. Kitila mbona alijitoa na mpaka leo anaendeela tena kwa juu sana kulisaidia taifa letu, au nayeye ana jina la baba? I mean I am shocked na jinsi hili taifa linavyohitaji msaada wa mawazo, I mean kujitoa sio ya wote, lakini kamainawezekana please, ingawa una hoja nzito sana kwamba bila kujificha JF itakosa chumvi yake ya asili.

- HOWEVER: sasa hivi JF we have a National platform na infact we have a mandate from the people, sasa ni lazima tuendelee kuitumia kuwaamsha wananchi, na sio siri tunaiweza hiyo kazi zaidi tunapokuwa tumejificha ya kukosoa ubovu katika taifa, sawa sawa ndugu yangu!

William @ NYC, USA.

Naona mheshimiwa unatimiza maelekezo ya Msekwa kuzima fikra chanya za JF. Woga umewaingia wengi wa CCM sasa mnataka kuwatisha watu ili wasiweze kutoa mawazo huru. Haya tu majina watu wanatafutwa wanataka kutolewa roho. Je kweli wote wakivua nguo hapa si hao usalama wa mafisadi utapata kazi rahisi kutungua mmoja baada ya mwingine kama kitorondo.

Hakuna haki ya kidemokrasia Tanzania ya kutoa mawazo, haki zote zimo mikononi mwa wachache, usijali siku tukiwa huru kama ninyi wenye mibuyu tutatoka nje tuna kenua. Ila leo mnatakiwa mtusikie tu wakati tuna sogea kwenye haki.

JF inafanya kazi yake vizuri, ni chanzo kikubwa cha habari kwani kuna sources mpaka ikulu. sasa sio rahisi kutaka kumjua informer Msekwa asubiri na kikosi kazi chake.

Ila anayeona ni sawa hasa kwa wenye mamlaka wanaweza kuja live. Swala la jina gani kila mtu apime uzito na kama ataweza kuendelea kuwa huru kuchangia na kutuletea habari maridhawa.
 
Vichwa vyote vizuri vikiwekwa chama kimoja hatutafika kokote. Tutafute tu chama mbadala. Tuwaache wengine wabaki bila vyama wala watu wao. Sasa tuna watu wa Dr Slaa sio CHADEMA. Tuna watu wa JK sio CCM. Tutake tusitake tunao. Wapo pia wanaoangalia kiongozi mkuu wa chama ni KABILA au DINI gani. Tunao. Na hiyo ndio Tanzania ya sasa. Tunatakiwa tugawanyike kwa staili ya Simba na Yanga ndipo tutasonga mbele kama nchi.

Hawa ndio type ya washauri wa CCM badala ya kufanya research unabuni mawazo yako kichwani unaanda repoti unampelekea mtu eti JF ni adui wa CCM, mkuu hakuna mshabiki wa Dr Slaa, ila kuna mashabiki wa haki, na alama ya haki inaonekana ni Dr Slaa kwahiyo mwanachama yeyote wa CCM mpenda haki ni lazima alimpikia kura Dr Slaa kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

kumbuka Watanzania wengi si wanachama wa vyama vya kisiasa wao wakati wa uchaguzi wanaangalia mtu huwa hawaangalii chama. mfano hai ni jimbo la Bukoba mjini, wapiga kura ni walewale lakini urais Dr Slaa ameongoza kutoka CHADEMA lakini Lwakatare kutoka CHADEMA hiyohiyo kaanguka kwenye ubunge. kwahiyo usiwa under estimate Watanzania wa sasa ukadhani ni misukule, watu wanajuwa wanachohitaji.

Ushauri kwa William Malecela: Naomba ongea na viongozi wako wa CCM wakifute mara moja kitengo cha propaganda kwani ni matumizi mabovu ya pesa za chama. Hakuna tena Mtu mwenye akili timamu ambaye anaweza kusikiliza propaganda, hiyo ni lugha ya karne nyingi nyuma, badala yake waunde kitengo cha teknohama.
 
Kwa nini kila anayeikosoa CHADEMA au VIONGOZI wake mnamtupa CCM? Tuna vyama vingi sana jamani na vingine vinakuja.
 
- Well, siasa za vyama vinaongozwa na katiba ya vyama hata huko Kenya wanaongozwa na katiba ya chama kwa hiyo kiongozi anayechaguliwa hahitaji kuseoma anything zaidi tu ya kusoma katiba, Kenya walianza na itikadi za kibepari sisi tulianza na itikadi za kijamaa, ambazo zilishindwa kwenye vita na za kibepari, sasa ya Kenya kwua mbele yasikushangaze sana, ingawa it can be debated of what hasa wako mbele yetu!

- Kwa maoni yangu bado CCM tunahitaji Mwenyekiti kuwa mgombea u-Rais.

William @ NYC, USA.

William, kwa kiasi fulani I can understand kwa nini umeshikilia bango hii hoja ya kofia mbili kuvaliwa na mtu mmoja. And you know why I said you know.

Kuhusu mfumo wa ubepari Kenya na Ujamaa Tanzania - siamini hata kwa asilimia 5 kwamba ndio sababu kuu ya kuchanganya mambo. Appriximately, 40% wa watanzani wana umri chini ya miaka 17!!! Azimio la Zanzibar lililozika Ujamaa lilikuwa lini? vijana hawa wanajua mambo/maneno kama ujasiriamali, machinga, google na sasa facebook. kwa maneno mengine hawajakuzwa na huu mfumo wa ujamaa. Na ukienda mbele zaidi more than 60% ni chini ya 30 yrs old. kama Watanzania are old enough kuona mapungufu kwenye mfumo wa kiuongozi inakuwaje mtu aseme ni wachanga kutoa solution? Hivi kuna hasara gani kutenganisha viti hivi viwili? CHADEMA wamefanya hivyo wakati wa campaign walau mwenyekiti amebakia kuwa mwenyekiti na mgombea urais akawa kwenye safu ya Urais. Halikuharibika jambo!
 
The great Mark Twain once said this "I've never killed a man, but I've read many an obituary with a great deal of satisfaction".

That's my sincere belief regarding William's dying party.
 
- Mkuu heshima yako sana, umenivunja mbaavu sana well, ninasema hivi sio wote lazima wajitoe na sio kwamba ukijitoa basi huwezi kuendelea kujificha ficha pia, lakini ninasema hivi Dr. Kitila mbona alijitoa na mpaka leo anaendeela tena kwa juu sana kulisaidia taifa letu, au nayeye ana jina la baba? I mean I am shocked na jinsi hili taifa linavyohitaji msaada wa mawazo, I mean kujitoa sio ya wote, lakini kamainawezekana please, ingawa una hoja nzito sana kwamba bila kujificha JF itakosa chumvi yake ya asili.

- HOWEVER: sasa hivi JF we have a National platform na infact we have a mandate from the people, sasa ni lazima tuendelee kuitumia kuwaamsha wananchi, na sio siri tunaiweza hiyo kazi zaidi tunapokuwa tumejificha ya kukosoa ubovu katika taifa, sawa sawa ndugu yangu
!

William @ NYC, USA.

Sijasomea phychologia lakini i can always read from your comments one diff btn me and you ni majina yetu. Nikiandika jina langu hapa michango yangu itakuwa ni kichekesho kwa kweli na itabidi nipingane na ukweli just bcs ................. teh teh teh

Kuhusu mawazo yetu yanaweza kupitia kwa wachache tuliowachangua au walioamua au nyie mliomaua kujitoa mbele ndio mana kuna siku nilikupa wazo fulani hivi. kama umelisahu naweza kukumbusha. teh teh teh teh.

Zaidi ya kukosoa kama ulivyosema tunaweza kutoa idea ambazo labda mkiwshtua wazee huko Iwe ni CCM au CDM au CUF wazifanyie kazi. the poblem is tumejikita kwenye siasa sana. tunaandika hapa tunajua wahusika wanweza kuona na kushtuka na kufanyia kazi lakini wapi.

Mfano niliweka link hii BBC News - Google to amend Rio maps over Brazil favela complaints kwenye post niliyonadika hapa https://www.jamiiforums.com/jamii-i...kufuatia-kifo-cha-osama-google-earth-map.html

Una assume ingawa unatumia jina la magamba meya wa arusha mwanza dar etc wakiona na watu wao wa IT au wizara mbali mbali kama ya utalii wanaweza kujifunza jinsi ya kutumia opportunity na kuanalysse risk za IT sehemu zao za kazi. na to do the needful. Nothing is done mameya wetu tena wengine vijana nao wamekuwa wanasiasa.........

Siasa ndo best career in tannzania. Politics is everything. Hili ni tatizo.
 
Kwa nini kila anayeikosoa CHADEMA au VIONGOZI wake mnamtupa CCM? Tuna vyama vingi sana jamani na vingine vinakuja.

Matendo yako tu yanakutambulisha mkuu, kama kuna vyama vingine mbona hauviongelei wewe kila siku ni anti CHADEMA tu? au nikuwekee ushahidi wa post zako zote hapa sasa hivi?
 
Kaka William Malecela

Bila shaka uko salama na unaendelea na majukumu ya kila siku ya kimaisha. Nimeona leo nikuandikie waraka wa kirafiki kuhusiana na hali ya kisiasa na maisha yetu huku Tanzania. Nilikusoma siku chache zilizopita ukifahamisha umma jitihada zako za kuanzisha tawi la CCM huko uliko. Wengi walikupongeza na wengine kama kawaida walikubeza na kwenda mbali zaidi. Nakumbuka kwenye lile bandiko uliweka kauli mbiu ya kuvua magamba na CCM mpya. Nadhani Kaka Wiliam unajua sasa zile zilikuwa ni sanaa tu, Mukama na Nape wamekuwa wakitofautiana na muafaka na nani na lini hatua zitachukuliwa zidi ya wale waliokiweka chama chenu hapo kilipo. Mukama alienda mbali zaidi kudai hakuna listi ya watakao vuliwa magamba. Kumbuka huyu ndiye mtendaji mkuu wa shughuli za kila siku za chama na sekretariat nzima.

Bila shaka hakuna anachofanya Kikwete bila Rostam, Chenge na Lowassa kujua. Hawa watu wameshiriki kwa karibu sana na Kikwete na kufanikisha CCM-Mtandao Kushika dola. Haikuwa rahisi watu hawa kutengana kirahisi kama wengi tulivyotaka iwe. William ningeweza kukuandikia PM ila nimeona wacha na wanaJF wengine walione na watachangia. CCM na Magamba ilikuwa ni sanaa, kama ambavyo mwenyekiti wenu amekuwa akicheza na jukwaa kufurahisha hadhira. Alianza na semina elekezi Ngurudoto, kwa top govt officials, tunajua kashfa za ngono zilizofanyika kule 2006. Juzi katembelea wizara na kuamsha utendaji wa kazi, sasa amekuja na semina elekezi Dodoma, anarudia yale yale, kwenye formal logic hali inaitwa Tautology, hakuna tija wasiofanya kazi awapige chini, ngonjera zake zina gharama sana kwa wapiga kura. Nina wasi wasi CCM itagawanyka mikononi mwake na Muungano na Zanzibar utavunjika kabla ya 2015.

Kaka ningekushauri ufunge hilo tawi njoo tuungane kwa mambo yenye maslahi kwa taifa! Tuwe watanzania na si waCCM. Taifa lije mbele kama watanzania shida za umeme zinatokana na ufisadi zinatupata wote.

Ilikuwa niandike mengi wacha niwahi mazishi kuna kada wa CCM amekufa hapa mtaani

Respect

Mdogo wako Mch Masa

Rev. Unaishi huko anakoishi huyu kada wa CCM ALIYEGOMBEA UBUNGE KOROGWE NA MAJI MAREFU NINI?
 
Mkuu nadhani kwa kauli za kukinzana za kina MUKAMA na NAPE itabidi tufanye semina elekezi immediately St Gasper(Dodoma) patapokuwa wazi baada ya hii semina elekezi.
 
Ushauri kwa William Malecela: Naomba ongea na viongozi wako wa CCM wakifute mara moja kitengo cha propaganda kwani ni matumizi mabovu ya pesa za chama. Hakuna tena Mtu mwenye akili timamu ambaye anaweza kusikiliza propaganda, hiyo ni lugha ya karne nyingi nyuma, badala yake waunde kitengo cha teknohama.

Matola katika vitu vinavyoniacha nimeduwa ni hiki cha CCM kuendelea kutumia kitengo cha PROPAGANDA ndani ya utawala wake. Kitendo cha kuwa na neno Propaganda peke yake kinaharibu kama si kubatilisha kabisa habari inayotelewa - habari zinahalalishwa kuwa ni PROPAGANDA maana zinatolewa na kitengo cha PROPAGANDA. Na hawa ndio wamekazana kuwa ni chama kikubwa, kikongwe etc. well, inawezekena ni wakongwe kweli kweli ndio maana hawajui ni zama gani wanaishi. Old solution to new challenges.
 
Rev. Unaishi huko anakoishi huyu kada wa CCM ALIYEGOMBEA UBUNGE KOROGWE NA MAJI MAREFU NINI?

Mkuu nitake radhi! Mimi nataambika na hizi adha za mgawo wa umeme! Mvua ikinyesha kidogo tu foleni ya kufa mtu...bila shaka umenisoma.
 
Mkuu nadhani kwa kauli za kukinzana za kina MUKAMA na NAPE itabidi tufanye semina elekezi immediately St Gasper(Dodoma) patapokuwa wazi baada ya hii semina elekezi.

Hapo kwenye RED mkuu mimi sijakuelewa bado, kwani ccm nayo siku hizi ni chama cha kanisa? kwani hawana ukumbi wao wa Chimwaga?
 
Back
Top Bottom