BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,513
- 8,408
“Ukikuta kijana ameingia ndani kwa kuvunja dirisha ujue kuna mambo mawili ameyadhamiria. Jambo la kwanza amedhamiria kuiba na jambo la pili amedhamiria kuua na jambo la tatu amekubali kuuawa. Naomba nisisitize, jambo la tatu amekubali kuuawa, naomba nirudie, jambo la tatu amekubali kuuawa.
“Sioni faida ya kumpa nafasi mtu anayebomoa mlango, anaingia ndani kuiba kitu hata kama ameiba chumvi. Uingiaji wake amekubali mambo matatu, kakubali kuiba, kuua na kuuawa. Na kama amekubali kuuawa mnasubiri nini? Kama amekubali kuuawa mnasubiri nini? Mambo mengine sipendi turembe na wala hatupo katika dunia ya kuremba.
“Kama amekubali kuingia kuuawa mnasubiri nini kupitisha maombi yake? Mnasubiri nini? Askari anayemuwakilisha OCD njoo nikupe maelezo matamu, huko jela tumechoka watu wengi huko.
“Kuanzia leo panga vikosi kazi vifanye operesheni ya kufa mtu kutimiza maombi ya vibaka, ameomba mambo matatu; amekubali kuiba, amekubali kuua na amekubali kuuawa, pitisha ombi la tatu!
“Haya siyo yangu Mkuu wa Mkoa, haya ni anayeiba, amekubali kuingia kwenye nyumba ya mtu bila kujua huyo mtu ana mali gani ndani. Mimi juzi nipo pale Iringa naona kuna kijitu kinabomoa nyumba ili kiingie kwangu. Nilimjibu kwa kumpa ombi aliloliomba! Nilimwambia hunijui na umeingia kwenye nyumba yangu bila kujua nina mali gani.
“Nilipiga shoo tu ya dakika hizi (2), kilichotokea hakuwa mtu tena, na nikabaki kwa kufaraha nikanywa na bia moja.”
Chalamila aliyasema hayo wakati akiwa Mkuu wa Mkoa Mbeya katika ziara yake Mbalizi Road alipowenda kuzungumza na wananchi pamoja na kusikiliza kero zao tarehe 28.08.2019.