Mwanza: RC Chalamila anapotosha au amepotoshwa?

MenukaJr

Member
Apr 24, 2021
50
150
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila ametangaza ziara ya Rais wa JMT katika Mko wa Mwanza itakayofanyika kuanzia tarehe 13 hadi 15, Mkoani Mwanza. Katika ziara hiyo, RC Chalamila amesema Rais Samia Suluhu pamoja na mambo mengine atatembelea na kufungua kiwanda cha usafishaji (uchenjuaji) dhahabu kilichojengwa kwa thamani ya bilion 10.4, mali ya mtu binafsi (Sekta binafsi). Pitia hapa kutazama na kusikiliza taarifa ya RC Chalamila;

Baada ya taarifa hiyo ya RC Chalamila, kwa sababu nilipata kusikia taarifa kidogo kutoka kwa JPM kuhusu mtambo huo wa uchenjuaji madini (dhahabu) uliojengwa Mwanza, ikanibidi kuchukua muda kujiridhisha ikiwa ni mradi wa mtu binafsi (Sekta binafsi) kama RC Chalamila alivyoeleza au ni ubia kati ya Sekta binafsi na Serikali (PPP).

Taarifa ya kwanza niliyopitia inapatikana katika Tovuti ya Mkoa wa Mwanza (Website). Taarifa hii iliwekwa 18.05.2020, wakati Naibu Waziri wa Madini wa wakati huo Stanslaus Nyongo alipotembelea mradi wa ujenzi wa Kiwanda hicho. Kwa maelezo ya Naibu Waziri wa Madini, kiwanda hicho kilikua kinasimaiwa na STAMICO (shirika la madini la Taifa) na kwamba gharama yake ni billion 133.4. Mkuu wa Mkoa wa wakati huo, John Mongela alisema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho ulikua unatimiza ndoto za Rais Magufuli. Pitia hapa kusoma taarifa hii; Kiwanda cha kuchakata madini chajengwa Mwanza

Taarifa nyingine niliyopitia inapatikana katika tovuti ya #Fullshangweblog iliyowekwa tarehe 21. 04.2021 (mwezi mmoja baada ya kifo cha JPM). Taarifa hii inakieleza kiwanda hicho cha uchenjuaji kwa jina la Mwanza Precious Metals Rifinery (MPMR) kuwa kama kiwanda kikubwa cha kusafisha dhahabu Afrika Mashariki. Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance Mwasse inasema kuwa chimbuko la kiwanda hicho ni matokeo ya mabadiliko ya sheria ya Madini yaliyofanyika mwaka 2017.

Taarifa inaeleza kuwa kiwanda cha Mwanza Precious Metal Refinery (MPMR) kinamilikiwa kwa ubia wa kampuni tatu. Kampuni ya kwanza ni STAMICO kwa niaba ya Serikali ya JMT ambapo inamiliki 25%. Kampuni zingine ni Rozella General Trading LLC ya Dubai na Umoja wa Kiarabu (UAE) pamoja na Kampuni ya ACME Consultant Engeneers PTE LTD ya Singapore ambapo zote zinamiliki 75%. Pitia njia hii kusoma taarira hiyo; KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU MWANZA CHAANZA UZALISHAJI RASMI | Full Shangwe Blog

Baada ya taarifa hizo zote pamoja na ile ya RC Chalamila ya ziara, maswali ya msingi ya kujiuliza yanaweza kuwa;

1. Je, RC Chalamila amepotoshwa kuhusu umiliki wa kiwanda cha kuchenjua madini Mwanza (MPMR) au ni yeye amekusudia kupotosha umma?
Kama RC amepotoshwa na kukubali kupotoka kwa urahisi namna hiyo, bila kupitia taarifa zaidi kujiridhisha ni kwa namna gani anaweza kuendelea kuaminika katika nafasi hiyo.

2. Kama RC Chalamila amekubali kupotoshwa katika jambo lenye maslahi makubwa kwa umma namna hii, Je atakua amepotoshwa katika mambo mangapi na nchi itakua imepata hasara kiasi gani kwa kupotoshwa kwake. Fikiria, hadi sasa Dunia inatambua kuwa Rais anakwenda kufungua kiwanda cha mtu binafsi ilahali Serikali imewekeza mamilioni ya pesa zake. Kwa maelezo ya Chalamila nafasi katika umiliki imekufa.

3. Kama RC Chalamila hakupotoshwa ila amekusudia mwenyewe kupotosha umma kwa maahi yake au aliyemtuma nini madhara ya upotoshaji wake katika nchi. Je, Kampuni za RGT na ACME wakiamua kutumia kauli ya RC Chalamila kuondoa umiliki wa 25% wa Serikali (STAMICO), nchi inaweza kuingia hasara kiasi gani. Tukumbuke, njia kama hii ilitumiwa na watu wachache kuondoa umiliki wa Serikali katika kampuni ya mawasiliano ya Airtel (Celtel wakati huo) hadi ziliporudishwa na Rais JPM mwaka 2019. Tujifunze!!

Mwisho: RC Chalamila atoke tena hadharani abadilishe statement yake kuhusu eneo hilo. Anaweza kuomba radhi kwamba alipotoshwa kwa bahati mbaya katika taarifa yake ya awali. Ni lazima umiliki wa Serikali (STAMICO) utambulike katika kiwanda hicho cha uchenjuaji wa dhahabu kwa sababu faida yake itakwenda Serikalini. Pesa zilizotumika katika uwekezaji huo pamoja na wabia wengine ni za wananchi wa Tanzania lazima zitambulike.

Hatuwezi kuvutia sekta binafsi kwa kuua nafasi ya Serikali katika uwekezaji. Au la, RC Chalamila awaeleze Watanzania kuwa umiliki wao katika kiwanda hicho umefutwa, haupo tena. Dalili hizi ni mbaya, pesa nyingi za nchi hii zimeibiwa kwa njia hii huko nyuma. Tukiendelea hivi kesho tunaweza kuambiwa kuwa TPDC haina umiliki katika kampuni ya EACOP yenye kujenga bomba la mafuta la Hoima-Tanga. Tuliambiwa nchi inaliwa sana hii, tujichunge.

#TutakukumbukaDaimaJPM.

MenukaJr,

Da'slam-Tanzania.
 
SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,520
2,000

RC yupo sawa tu, hasa kama 75% ya kiwanda hicho inamilikiwa na private entities (kwa mujibu wa maelezo yako).

Kwenye corporate governance, decision making inafanywa na majority shareholders kupitia uwezo wao kwa kuweka/kuiondoa board ya wakurugenzi wa kampuni husika.
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
10,466
2,000
Lengo la mleta mada ni kutaka mwendazake amwagiwe sifa.

Kiwanda siyo cha serikali, ni mali ya mtu binafsi. RC Chalamila siyo mjinga, na waliompa taarifa siyo wajinga.

Hizo taarifa zako zote za nyuma ulizopitia zilipikwa ili mwendazake apate sifa. Rejea uwongo wa mwendazake kwamba ATCL imepata faida na kutoa gawio.

Mwendazake acha aende zake na mambo yake yapigwe teke yaanguke kama kelele zake..
 
blogger

JF-Expert Member
Mar 13, 2012
5,334

Hawa akina Veronika Musiba...wana matatizo sana
 
Moisemusajiografii

JF-Expert Member
Nov 3, 2013
15,987
2,000
RC yupo sawa tu, hasa kama 75% ya kiwanda hicho inamilikiwa na private entities (kwa mujibu wa maelezo yako).

Kwenye corporate governance, decision making inafanywa na majority shareholders kupitia uwezo wao kwa kuweka/kuiondoa board ya wakurugenzi wa kampuni husika.
Kazi ipo hapo.Who is who?
 
lebabu11

JF-Expert Member
Mar 27, 2010
2,185
2,000
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila ametangaza ziara ya Rais wa JMT katika Mko wa Mwanza itakayofanyika kuanzia tarehe 13 hadi 15, Mkoani Mwanza. Katika ziara hiyo, RC Chalamila amesema Rais Samia Suluhu pamoja na mambo mengine atatembelea na kufungua kiwanda cha usafishaji (uchenjuaji) dhahabu kilichojengwa kwa thamani ya bilion 10.4, mali ya mtu binafsi (Sekta binafsi). Pitia hapa kutazama na kusikiliza taarifa ya RC Chalamila;
Baada ya taarifa hiyo ya RC Chalamila, kwa sababu nilipata kusikia taarifa kidogo kutoka kwa JPM kuhusu mtambo huo wa uchenjuaji madini (dhahabu) uliojengwa Mwanza, ikanibidi kuchukua muda kujiridhisha ikiwa ni mradi wa mtu binafsi (Sekta binafsi) kama RC Chalamila alivyoeleza au ni ubia kati ya Sekta binafsi na Serikali (PPP).

Taarifa ya kwanza niliyopitia inapatikana katika Tovuti ya Mkoa wa Mwanza (Website). Taarifa hii iliwekwa 18.05.2020, wakati Naibu Waziri wa Madini wa wakati huo Stanslaus Nyongo alipotembelea mradi wa ujenzi wa Kiwanda hicho. Kwa maelezo ya Naibu Waziri wa Madini, kiwanda hicho kilikua kinasimaiwa na STAMICO (shirika la madini la Taifa) na kwamba gharama yake ni billion 133.4. Mkuu wa Mkoa wa wakati huo, John Mongela alisema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho ulikua unatimiza ndoto za Rais Magufuli. Pitia hapa kusoma taarifa hii; Kiwanda cha kuchakata madini chajengwa Mwanza

Taarifa nyingine niliyopitia inapatikana katika tovuti ya #Fullshangweblog iliyowekwa tarehe 21. 04.2021 (mwezi mmoja baada ya kifo cha JPM). Taarifa hii inakieleza kiwanda hicho cha uchenjuaji kwa jina la Mwanza Precious Metals Rifinery (MPMR) kuwa kama kiwanda kikubwa cha kusafisha dhahabu Afrika Mashariki. Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance Mwasse inasema kuwa chimbuko la kiwanda hicho ni matokeo ya mabadiliko ya sheria ya Madini yaliyofanyika mwaka 2017.

Taarifa inaeleza kuwa kiwanda cha Mwanza Precious Metal Refinery (MPMR) kinamilikiwa kwa ubia wa kampuni tatu. Kampuni ya kwanza ni STAMICO kwa niaba ya Serikali ya JMT ambapo inamiliki 25%. Kampuni zingine ni Rozella General Trading LLC ya Dubai na Umoja wa Kiarabu (UAE) pamoja na Kampuni ya ACME Consultant Engeneers PTE LTD ya Singapore ambapo zote zinamiliki 75%. Pitia njia hii kusoma taarira hiyo; KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU MWANZA CHAANZA UZALISHAJI RASMI | Full Shangwe Blog

Baada ya taarifa hizo zote pamoja na ile ya RC Chalamila ya ziara, maswali ya msingi ya kujiuliza yanaweza kuwa;

1. Je, RC Chalamila amepotoshwa kuhusu umiliki wa kiwanda cha kuchenjua madini Mwanza (MPMR) au ni yeye amekusudia kupotosha umma?
Kama RC amepotoshwa na kukubali kupotoka kwa urahisi namna hiyo, bila kupitia taarifa zaidi kujiridhisha ni kwa namna gani anaweza kuendelea kuaminika katika nafasi hiyo.

2. Kama RC Chalamila amekubali kupotoshwa katika jambo lenye maslahi makubwa kwa umma namna hii, Je atakua amepotoshwa katika mambo mangapi na nchi itakua imepata hasara kiasi gani kwa kupotoshwa kwake. Fikiria, hadi sasa Dunia inatambua kuwa Rais anakwenda kufungua kiwanda cha mtu binafsi ilahali Serikali imewekeza mamilioni ya pesa zake. Kwa maelezo ya Chalamila nafasi katika umiliki imekufa.

3. Kama RC Chalamila hakupotoshwa ila amekusudia mwenyewe kupotosha umma kwa maahi yake au aliyemtuma nini madhara ya upotoshaji wake katika nchi. Je, Kampuni za RGT na ACME wakiamua kutumia kauli ya RC Chalamila kuondoa umiliki wa 25% wa Serikali (STAMICO), nchi inaweza kuingia hasara kiasi gani. Tukumbuke, njia kama hii ilitumiwa na watu wachache kuondoa umiliki wa Serikali katika kampuni ya mawasiliano ya Airtel (Celtel wakati huo) hadi ziliporudishwa na Rais JPM mwaka 2019. Tujifunze!!

Mwisho: RC Chalamila atoke tena hadharani abadilishe statement yake kuhusu eneo hilo. Anaweza kuomba radhi kwamba alipotoshwa kwa bahati mbaya katika taarifa yake ya awali. Ni lazima umiliki wa Serikali (STAMICO) utambulike katika kiwanda hicho cha uchenjuaji wa dhahabu kwa sababu faida yake itakwenda Serikalini. Pesa zilizotumika katika uwekezaji huo pamoja na wabia wengine ni za wananchi wa Tanzania lazima zitambulike. Hatuwezi kuvutia sekta binafsi kwa kuua nafasi ya Serikali katika uwekezaji. Au la, RC Chalamila awaeleze Watanzania kuwa umiliki wao katika kiwanda hicho umefutwa, haupo tena. Dalili hizi ni mbaya, pesa nyingi za nchi hii zimeibiwa kwa njia hii huko nyuma. Tukiendelea hivi kesho tunaweza kuambiwa kuwa TPDC haina umiliki katika kampuni ya EACOP yenye kujenga bomba la mafuta la Hoima-Tanga. Tuliambiwa nchi inaliwa sana hii, tujichunge.
#TutakukumbukaDaimaJPM.

MenukaJr,

Da'slam-Tanzania.
Maelezo yako yanathibitisha kuwa ni kiwanda cha mtu binafsi.
Shirika au kampuni ya uma serikali humiliki hisa asilimia zaidi ya 50.
 
Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
14,068

Mpaka hapo ulipofikia sijaona kosa la Chalamaila.
 
JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
4,234
2,000
Lengo la mleta mada ni kutaka mwendazake amwagiwe sifa.

Kiwanda siyo cha serikali, ni mali ya mtu binafsi. RC Chalamila siyo mjinga, na waliompa taarifa siyo wajinga.

Hizo taarifa zako zote za nyuma ulizopitia zilipikwa ili mwendazake apate sifa. Rejea uwongo wa mwendazake kwamba ATCL imepata faida na kutoa gawio.

Mwendazake acha aende zake na mambo yake yapigwe teke yaanguke kama kelele zake..
Umeanza kupoteza umakini. Shituka.
 
TASK FORCE

JF-Expert Member
Apr 7, 2017
2,479
2,000
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila ametangaza ziara ya Rais wa JMT katika Mko wa Mwanza itakayofanyika kuanzia tarehe 13 hadi 15, Mkoani Mwanza. Katika ziara hiyo, RC Chalamila amesema Rais Samia Suluhu pamoja na mambo mengine atatembelea na kufungua kiwanda cha usafishaji (uchenjuaji) dhahabu kilichojengwa kwa thamani ya bilion 10.4, mali ya mtu binafsi (Sekta binafsi). Pitia hapa kutazama na kusikiliza taarifa ya RC Chalamila;
Baada ya taarifa hiyo ya RC Chalamila, kwa sababu nilipata kusikia taarifa kidogo kutoka kwa JPM kuhusu mtambo huo wa uchenjuaji madini (dhahabu) uliojengwa Mwanza, ikanibidi kuchukua muda kujiridhisha ikiwa ni mradi wa mtu binafsi (Sekta binafsi) kama RC Chalamila alivyoeleza au ni ubia kati ya Sekta binafsi na Serikali (PPP).

Taarifa ya kwanza niliyopitia inapatikana katika Tovuti ya Mkoa wa Mwanza (Website). Taarifa hii iliwekwa 18.05.2020, wakati Naibu Waziri wa Madini wa wakati huo Stanslaus Nyongo alipotembelea mradi wa ujenzi wa Kiwanda hicho. Kwa maelezo ya Naibu Waziri wa Madini, kiwanda hicho kilikua kinasimaiwa na STAMICO (shirika la madini la Taifa) na kwamba gharama yake ni billion 133.4. Mkuu wa Mkoa wa wakati huo, John Mongela alisema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho ulikua unatimiza ndoto za Rais Magufuli. Pitia hapa kusoma taarifa hii; Kiwanda cha kuchakata madini chajengwa Mwanza

Taarifa nyingine niliyopitia inapatikana katika tovuti ya #Fullshangweblog iliyowekwa tarehe 21. 04.2021 (mwezi mmoja baada ya kifo cha JPM). Taarifa hii inakieleza kiwanda hicho cha uchenjuaji kwa jina la Mwanza Precious Metals Rifinery (MPMR) kuwa kama kiwanda kikubwa cha kusafisha dhahabu Afrika Mashariki. Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance Mwasse inasema kuwa chimbuko la kiwanda hicho ni matokeo ya mabadiliko ya sheria ya Madini yaliyofanyika mwaka 2017.

Taarifa inaeleza kuwa kiwanda cha Mwanza Precious Metal Refinery (MPMR) kinamilikiwa kwa ubia wa kampuni tatu. Kampuni ya kwanza ni STAMICO kwa niaba ya Serikali ya JMT ambapo inamiliki 25%. Kampuni zingine ni Rozella General Trading LLC ya Dubai na Umoja wa Kiarabu (UAE) pamoja na Kampuni ya ACME Consultant Engeneers PTE LTD ya Singapore ambapo zote zinamiliki 75%. Pitia njia hii kusoma taarira hiyo; KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU MWANZA CHAANZA UZALISHAJI RASMI | Full Shangwe Blog

Baada ya taarifa hizo zote pamoja na ile ya RC Chalamila ya ziara, maswali ya msingi ya kujiuliza yanaweza kuwa;

1. Je, RC Chalamila amepotoshwa kuhusu umiliki wa kiwanda cha kuchenjua madini Mwanza (MPMR) au ni yeye amekusudia kupotosha umma?
Kama RC amepotoshwa na kukubali kupotoka kwa urahisi namna hiyo, bila kupitia taarifa zaidi kujiridhisha ni kwa namna gani anaweza kuendelea kuaminika katika nafasi hiyo.

2. Kama RC Chalamila amekubali kupotoshwa katika jambo lenye maslahi makubwa kwa umma namna hii, Je atakua amepotoshwa katika mambo mangapi na nchi itakua imepata hasara kiasi gani kwa kupotoshwa kwake. Fikiria, hadi sasa Dunia inatambua kuwa Rais anakwenda kufungua kiwanda cha mtu binafsi ilahali Serikali imewekeza mamilioni ya pesa zake. Kwa maelezo ya Chalamila nafasi katika umiliki imekufa.

3. Kama RC Chalamila hakupotoshwa ila amekusudia mwenyewe kupotosha umma kwa maahi yake au aliyemtuma nini madhara ya upotoshaji wake katika nchi. Je, Kampuni za RGT na ACME wakiamua kutumia kauli ya RC Chalamila kuondoa umiliki wa 25% wa Serikali (STAMICO), nchi inaweza kuingia hasara kiasi gani. Tukumbuke, njia kama hii ilitumiwa na watu wachache kuondoa umiliki wa Serikali katika kampuni ya mawasiliano ya Airtel (Celtel wakati huo) hadi ziliporudishwa na Rais JPM mwaka 2019. Tujifunze!!

Mwisho: RC Chalamila atoke tena hadharani abadilishe statement yake kuhusu eneo hilo. Anaweza kuomba radhi kwamba alipotoshwa kwa bahati mbaya katika taarifa yake ya awali. Ni lazima umiliki wa Serikali (STAMICO) utambulike katika kiwanda hicho cha uchenjuaji wa dhahabu kwa sababu faida yake itakwenda Serikalini. Pesa zilizotumika katika uwekezaji huo pamoja na wabia wengine ni za wananchi wa Tanzania lazima zitambulike. Hatuwezi kuvutia sekta binafsi kwa kuua nafasi ya Serikali katika uwekezaji. Au la, RC Chalamila awaeleze Watanzania kuwa umiliki wao katika kiwanda hicho umefutwa, haupo tena. Dalili hizi ni mbaya, pesa nyingi za nchi hii zimeibiwa kwa njia hii huko nyuma. Tukiendelea hivi kesho tunaweza kuambiwa kuwa TPDC haina umiliki katika kampuni ya EACOP yenye kujenga bomba la mafuta la Hoima-Tanga. Tuliambiwa nchi inaliwa sana hii, tujichunge.
#TutakukumbukaDaimaJPM.

MenukaJr,

Da'slam-Tanzania.
Mpuuzi wewe gazeti lote ilo,ili tu kutetea Legacy ya dikteta mangfool
 
Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,158
2,000
Wakubwa, hiki kiwanda kinachenjua makinikia ili kupata dhahabu au kinanunua dhahabu na kuichakata ili kupata dhahabu safi yenye 99.99 purity??

Vyanzo vingi ni kweli vyaonesha Mwanza Precious Metals inamilikiwa na Kampuni toka za
Dubai ambayo ni Rozella General Trading LLC na
Singapore-based ACME Consultant Engineers PTE Ltd ambazo kwa pamoja zinamiliki 75% ya hisa huku STAMICO (state Mining Corporation) ikiwa na hisa 25%

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom