Mi ni ME samahani wamama kwa wadada ila nmeona hakuna muafaka na nina wazo la jumla ambalo laweza wasaidia.
Nadhani wote tunajua hakuna kitu kinazidi nguvu ya upendo hapa duniani. Naimani hamna mtu asiependa kuona kwamba ana thamani mbele ya mpenzi wake.
Labda tu kwa kuweka sawa, wanawake inabidi mjitathmini jinsi mnavyoishi na waume zenu hasa kwa kuzingatia upendo, msitukere waume zenu kwa kauli za hovyo, muache viburi na muwe wepesi kusamehe na pia kutoa ushauri wa kutujenga zaidi, naamini ukiwa karibu na mumeo ukamfanya kuwa rafiki yako wa pekee mna share everything bila ubinafsi, inapendeza na muda mwingi hatotaka akukose na hata kusameheana inakuwa rahisi endapo mtapishana.
Wanawake wengi siku hizi wanafeli sehemu ndogo mno ambayo ni ubinafsi mwingi, kutokuwa romantic na kuwa na gubu la mara kwa mara, yani inakuwa kama routine..mwanamke hajui kusema samahani wala asante zaidi ukimsema atajinunisha bila sababu, siku za mke kumnunia mume ni nyingi kuliko wanazocheka...Haya huwa yanatokeaga baada ya mwanamke kupata ndoa tu ambapo anaona hana haja ya kukip effort tena. Siku kidume unastimu unaomba gemu unapewa ilimradi tu, mtu atikisiki au anakwambia nmechoka bhana ntakupa kesho.
Hamjui tu ila men like to be appreciated sana na pia kupewa treatment special pia. Sio unarudi salamu hakuna, hupokelewi yani ni unaanza pewa stori za matatizo tu...Stress mtindo mmoja, mwanamke kang'ang'ania umpe hela hajali tupo nyakati gani yani sio muelewa! Apo kashakuharibia siku hamna stori tena ye yupo busy na simu full time hataki jua umeshindaje yan kero tu.
Hapa ndipo michepuko wanapowin waume zenu, utakuta mchepuko anamfanyia vyote ambavyo we hufanyi. Anamkirimu mume vyema na pia anampa utamu kwa staili ya kipekee bila kuchoka huku akimlevya na maneno matamu. Mchepuko hana gubu yeye ni kutumia ulimi vyema tu mpaka anajikuta kajengewa nyumba kabisa. Anacho offer ni kitu kidogo ila kina thamani kubwa sana kwa mwanaume.
Nadhani wanawake wengi mkizingatia jinsi ya ku handle wanaume zenu itasaidia mno.