Lazima ujifunze kusema mimi mume wangu hato toka nje ya ndoa, lazima ujifunze kujinenea mema kila siku katika ndoa yako
Kumbuka kumuombea kila siku huku ukiizunguka picha yake kama hayupo ila kama yupo omba naye
Semesha hiyo picha semesha vyote ambavyo hutaki afanye,
Kwenye kuomba kuna nguvu sana
Kwa Wakristo mzungushie damu ya Yesu huyo mume kila siku, hao makahaba wasimuone hata wakienda kwa waganga wasimuone
Achilia Malaika wamlinde kila siku
Tafuta siku moja ya kufunga kwaajili yake tuu muombee
Ukiona alianza kucheat rudi kwa Mungu uanze na toba ina maana hukusimama katika zamu yako ya ulinzi wa kumuombea kila siku ndio maana adui kapata mwanya
Wanawake wengi wanatumia dawa za kiganga kunasa waume za watu
Usipo omba lazima abebwe
Hivyo kama Mungu alikupa mume mwambie Mungu mume uliye nipa namrudisha kwako nisaidie kumfinyanga omba hadi upendo.wa kwanza urudi. Hata akiona wengine nje aseme nina mke ninaye mpenda mno
Kingine ni hichi jiangalie nyuma je uliwahi tembea na waume za watu?
Kama ndio rud kwa Mungu omba toba vizur kila siku kwa makosa uliyo yatenda na ufute maneno yote uliyo tamkiwa na watu au mke wa huyo mtu sababu apandacho mtu ndicho avunacho
Angalia je wanawake alio waacha kabla hajaja kwako walimnenea nini?
Yapo maneno huwa tunatamka wadada pindi tunapo achwa hakikisha unaingia katika maombi kutubia na kufuta hayo maneno
Na kuanza kukiri maneno mema kila siku
Na ukiona anacheat usiseme ni fungu langu, sema hii sio yangu na kamwe haitokuwa yangu
Rudi kwa Mungu wewe kaa magotini kuomba hakuna kugombana ukiona unaumia lia na Mungu
Haya machozi yana thamani mnooo kwa Mungu usimkatie tamaa ni mume wakwako ni wako hivyo ombaa narudia tena omba,
Kuwa cheated sio fungu langu, ukijinenea hivi utakuwa mlinzi mzuri ktk maombi kwaajil ya mume. Kuna raha kuomba pamoja kuwa na mume wako.
In ua Presence Jesus is where I belong