Kwa waliotazama tamthilia ya Jumong wataona Rais Samia ana mtazamo ule ule katika kujenga Tanzania yenye nguvu

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,603
Tamthilia ya Jumong inaelezea mengi, magumu kwa mepesi ya kiongozi anayokutana naye anapotaka Kujenga nchi yenye nguvu. Na haya ni baadhi:

I. Atakutana na kukosolewa vikali na kupingwa na hata walio karibu yako. Kwenye Jumong tunaona mtu wa karibu sana wa Jumong, Mfalme Geumwa alipoona nchi ya Goguryeo itakuwa tishio Kwa Buyeo akaanza mipango ya kumpinga lakini hakufanikiwa.

II. Atakutana na kukata tamaa, kwenye Jumong tuliona Jumong akiwa mwenye kukata tamaa lakini nia na dhamira zilimuongoza na kuishinda roho ya kukata tamaa.

III. Atakutana na kutakuwa kufanya maamuzi magumu, Kuna kipindi Jumong alikuwa anafanya maamuzi magumu kama kujitoa kwenda kwenye Kambi ya adui mwenyewe au kupambana hata kwenye hatari na uwezekano wa kushindwa.

Nauona mtazamo wa Rais wetu ni uleule wa Jumong , muasisi wa Taifa la Goguryeo ambaye tumeufahamu kupitia tamthilia ya Jumong.

Kusudi kubwa la Jumong ni kutengeneza Taifa kubwa na lenye nguvu chini ya jua Kwa vizazi vingi, mtazamo ambao unafanana kama alionao Rais Samia
 
Back
Top Bottom