Tunakwenda na mtazamo na msimamo wa rais dkt. Samia suluhu hassan, katika kanuni yake ya 4R ya kuendesha mambo katika uongozi

Venus Star

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
19,680
59,801
Nimekuwa nikitafakari sana kwa kina kuhusu 4R za Rais Dkt. Samia. Leo nimeona niwezekutoa ufafanuzi.
Hebu ungana nami katika kuelewa jambao hili.

Reconciliation (Maridhiano)​

Rais Dkt. Samia anaamini katika kujenga jamii yenye maridhiano na maelewano. Amesisitiza umuhimu wa kuwa na msimamo usiobadilika kuhusu masuala ya kitaifa na kuwa na uwezo wa kushirikiana na kusuluhisha tofauti.

Rais Dkt. Samia anasisitiza kuwa misimamo ya kisiasa haipaswi kuwa ngumu ya kutokuwa na mabadiliko na kwamba ni muhimu kujenga jamii inayojadiliana na kutatua changamoto kwa Amani.

Resiliency (Ustahamilivu)​

Rais Dkt. Samia anasisitiza umuhimu wa ustahimilivu katika Uongozi wake, hii inamanisha kuwa uongozi unapaswa kuwa na uwezo wa kuvumilia changamoto na kukabiliana na hali ngumu bila kuyumba au kuvunjika moyo.

Kujenga ustahimilivu kunaweza kusaidia Nchi kushinda matatizo na kufikia malengo yake.

Reforms (Mabadiliko)​

Rais Dkt. Samia anatambua umuhimu wa kufanya mabadiliko katika Nchi ili kuboresha na kuleta maendeleo. Anasisitiza kwamba uongozi unapaswa kuchukua hatua za kufanya mabadiliko yanayohitajika katika sekta mbalimbali ili kuboresha maisha ya Wananchi.

Rebuilding (Kujenga Upya)​

Rais Dkt. Samia anataka kuona juhudi za kujenga upya Nchi. Hii inaweza kumaanisha kurejesha miundombinu, kukuza uchumi na kuhakikisha kuwa Nchi inaendelea kusonga mbele baada ya changamoto au matatizo.

#TunzaDemokrasia
#TunzaAmani
#KatibaYaWatu
#KatibaNiMaridhiano
#UchaguziNiMashindano
#MatokeoChanya
#SisiNiTanzania
 
5 Image.jpg
6 Image.jpg
7 Image.jpg
8 Image.jpg
 
Lazima tuwe kama nchi tuweze kukaa pamoja na kujadili wapi tulipojikwaa na kusimama.
 
Back
Top Bottom