Kwa utendaji kazi uliotukuka wa Rais Samia naanza kuziona dalili za upinzani kutafuta visingizio vya kumkimbia na kumkwepa katika Uchaguzi Mkuu ujao

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,231
9,668
Ndugu zangu hivyo ndivyo hali halisi ilivyo, kwasasa upinzani umefika hatua hauelewi ushike lipi na uache lipi, uongee nini na usimame na lipi, ubebe lipi na uache lipi, utembee na lipi na usimame na lipi.

Imefika hatua hata kuaminiana wao kwa wao wameacha, maana kila mtu anahisi mwenzie anadalili za kusaliti chama na kwenda kumuunga mkono Mh. Rais wetu mpendwa, hapa unaweza kurejea habari za Mch. Peter Msigwa namna alivyo tukanwa na vitoto vidogo kiumri kisa tu kusimamia mtizamo wake katika kuiunga mkono serikali juu ya suala la Loliondo.

Ndugu zangu kwa sasa hata wenyewe hawaoni wakuweza kushindana na Mh. Rais Samia maana kila waliyemuona awali kuwa ndio kamanda wa kuongoza mapambano, wanakuta amerudi mstari wa nyuma akiunga juhudi za Mh. Rais na hata kama ni kukosoa anakosoa kwa kushauri baadhi ya maeneo kwa heshima na staha, jambo linalozidi kuwa changanya na kuwalaza na viatu vijana wa upinzani.

Hii yote ni kwa kuwa Mh. Rais kafanikiwa kugusa kila eneo kiutendaji, watanzania wana matumaini makubwa sana na Mh. Rais kwa kuwa wanaona juhudi zake katika kujenga nchi yetu, wanaona namna kila mtu, kila kundi na kila eneo linavyoguswa kiutendaji. Hakuna anayeachwa nyuma wala kutengwa au kubaguliwa, wote wanapata huduma sawa.

Kila mtu anapata huduma sawa,kila mtu anasikilizwa, kila mtu anathaminiwa,kila mtu anaona anayo nafasi ya kuchangia ujenzi wa Taifa hili na kila mtu anaona anaweza kutimiza Ndoto na malengo yake katika nchi hii kwa kuwa fursa zipo wazi kwa kila mtu mwenye kuzitaka.

Sasa hapa ndioo mtihani mkubwa walionao upinzani kwa sasa katika kuweza kusimamisha mgombea kiti cha Urais maana hawaelewi watamsimamisha nani? Kwa sera na ajenda zipi, hawaelewi watawashawishi kipi watanzania, maana Mh. Rais amefanya kazi zilizogusa maisha ya watanzania hasa wanyonge wasio na sauti.

Wameona namna Mh. Rais alivyo shapu kuchukua hatua katika kumsaidia mwananchi pale panapojitokeza tatizo la kidhalula kama alivyo fanya kutoa Ruzuku katika kilimo na nishati ya mafuta, kiukweli kasi hii ya Mh. Rais imewaweka pabaya sana kisiasa.

Ushauri wangu kwao ,kwa kuwa wameonyesha kukubali utendaji kazi wa mh Rais Basi hawana budi Kuendelea kumuunga mkono Mh. Rais wetu, waendelee kutoa ushauri watakapoona panafaa kwa lugha ya heshima na staha.

Maana mama ni msikivu na mnyenyekevu anayemjali na kumsikiliza kila mtu, kwa sasa mama amekaa katika mioyo ya watanzania. Watanzania walitaka maendeleo na mtumishi mnyenyekevu atakayewasikiliza, sasa amepatikana Mh. Rais Samia anatekeleza kwa vitendo ndoto za watanzania.

Kazi iendeleee.
 
Magufuli japokuwa alifanya mambo makubwa ikiwemo kuwadhibiti wapinzani lakini kwenye uchaguzi aliomba ardhi ipasuke immeze mzima mzima kwa aibu aliyokuwa anaona Lisu alivyokuwa akisepa na kijiji,pona pona yake aliiba kura na kuharibu uchaguzi!.
Sembuse huyu mzururaji?,labda watumie mitutu ya bunduki lakini kwenye boksi la kura hatoboi!.

Pamoja na kiherehere,kisebengo na kiroho papo chako cha kusifu na kuabudu ukweli unaujua!
 
Back
Top Bottom