Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Nadhan hapo ujaribu kuwa mbunifu. Angalia kiwango cha pesa ulichokuwa nacho na muda ulikuwa nao vinaendana? Pia kwenye chaguzi za biashara au mradi huwa tunaangalia fursa zilizopo au ulizoziona eneo husika. Siwez kukushauri ufuge kuku wakati kumbe mtaa unaokaa kuna watu zaidi ya 10 wanafuga kuku pia. Tafakari changamoto wanazopata wakazi wa hapo, Kama ni shida ya vipodozi, saloon ya kike, vifaa vya umeme, huduma za vinywaji, mbogamboga, matunda, nafaka au hata huduma za kiusafiri...
Baada ya kugundua changamoto ndipo unapokaa na kuitafutia suluhu, ww ukiitazama Kama fursa...
Hili wazo la kuangalia changamoto wanayokumbana nayo wakaazi wa mtaani kwake nimelipenda,binafsi mtaani kwangu kuna shida sana ya maji,nimewaza kuchimba kisima nivute maji kwa mota niwe matank ya lt 5000 mawili nianze biashara ya kuuza maji.

Mdau afanyie kazi ushauri wako.
 
Nafanya biashara ya mchele kutoa mbeya kuleta dar kama upo tayar kuinvest while ukiwa unaendelea na kazi yako unakaribishwa
Ahsante mkuu. Ni wazo zuri!

Unaweza kunipa japo mcahnganuo kidogo wa biashara hiyo unavyoendesha! Kule mbeya unanunua kilo au gunia kwa bei gani? Na gharama za usafirishaji zikoje kutoka Mbeya hadi Dar? Vipi hapa Dar unapofikisha unawateja wako ambao pengine unawauzia jumla jumla kwa maana unawauzia mzigo mkubwa au unaweka mzigo unaanza kuuza kidogo kidogo mwenyewe?
 
Tafuta biashara ya kufanya ambayo kila mwisho wa mwezi utakua unaweka hyo pesa humo kwa maana ya kununua mzigo,kwa mfano chukulia ukafungua duka la kurefil gas na kuuza vifaa vyake,ni vitu visivyooza na vina hakika ya kununuliwa,unakua na Gas point ambayo utaianzisha kama kwa Tsh 3,000,000/=tu hv.then kila mwezi unaendelea kuongeza hiyo laki tano yako kwa kuongeza mitungi ya gas na bidhaa zake.mpaka unakuja kutoka kazini au baada ya miaka 7-10 hv utakua si Gas point tena.utakua ni super dialer mwenye magari ya kusambazia mzigo na mitungi ya gas ya kutosha.jaribu ila fanya kitu unachojisikia unapenda na unaweza,na si kwa kufata mkumbo.
HIS IMPERIAL MAJESTY EMPEROR HAILE SELLASIE I.
JAH BLESS YOU
Ahsante sana kwa ushauri mzuri!
 
Nadhan hapo ujaribu kuwa mbunifu. Angalia kiwango cha pesa ulichokuwa nacho na muda ulikuwa nao vinaendana? Pia kwenye chaguzi za biashara au mradi huwa tunaangalia fursa zilizopo au ulizoziona eneo husika. Siwez kukushauri ufuge kuku wakati kumbe mtaa unaokaa kuna watu zaidi ya 10 wanafuga kuku pia. Tafakari changamoto wanazopata wakazi wa hapo, Kama ni shida ya vipodozi, saloon ya kike, vifaa vya umeme, huduma za vinywaji, mbogamboga, matunda, nafaka au hata huduma za kiusafiri...
Baada ya kugundua changamoto ndipo unapokaa na kuitafutia suluhu, ww ukiitazama Kama fursa...
Ahasante kwa ushauri wako mkuu!
 
Nina Pesa TSh. 500,000/= (Laki tano) Nina taka Nifanye biashara Nipo mkoani (Mazingira ya mjini) ila sijajua Nifanye biashara gani Maana si mzoefu kabisa wa biashara na Hali bado ni Ngumu Ninaona kitu cha msingi ni bora kujichanganya na Pesa hii hii Ndogo niliyo Nayo.

Shukrani kwa usikivu Nasubiri maoni yenu.
 
Kwanza Weka Aibu Pembeni Maana Itakurudisha Nyuma. Angalia kama Upo Jirani na Shule, Vyuo au Njia Ambazo watu huwa wanapita au kukusanyika kwa Wingi. Fanya Mpango uwe Freelancer wa Mitandao yote ya cm, uwe una kazi ya kusajili line, kutengeneza special number, ku renew line, kuuza vocha n.k.

fight upate mwamvuli mf wa voda, chonga meza ya mbao ya kishkaji na kiti cha mbao, au kama vipo home vifanye viwe vya ofisi .

Ongea na Muuza magazeti jirani na wewe, akufanyie mpango nawe uwe wakala, tengeneza stand ya wavu ya chuma ambayo kwa ubavuni na juu kidogo utaweza kutenga eneo la kuweka pipi, biskuits, karanga, hankerchiefs, pen n.k

Tafuta Deli, tengeneza Maji na Juice za kupima, weka na barafu uwe unafaya biashara zako eidha jiran na maeneo ya njia panda, karibu na shule/vyuo, jirani na maeneo ya sokoni au kwenye mikusanyiko ya watu. Pia waweza omba nafasi mbele ya duka mfano la nguo ukaweka biashara yako huku ukawa unamlipa 500-1000 mwenye frem kila siku.

hapo nimekadiria upo home, friji lipo, blender, kiti meza pia unaweza vitoa home. otherwise gharama za mtaji zinaweza fika hata laki 2 au 3.

Mm nimewaza hayo, Mengine utajiongeza mwenyewe depending na mazingira uliopo. Kila la kheri.
Ushaur mzur sana
 
Somo hapo juu lahusika.
Kutokana na ugumu wa maisha ktk suala zima la ajira naomba kuungana na mtu yeyote aliyemuaminifu na mchapa kazi na kuweza kuanzisha kazi au biashara yoyote halali.
Yawezekana ulikuwa na idea juu ya kitu fulani lakini ulishindwa kulifanikisha hilo kutokana na hali halisi ya kifedha uliyonayo hivyo lengo la kuanzisha uzi huu nikuweza kutengeneza fursa ya sisi wenyewe tuweze kujiajiri.
Labda maeneo ya mkoani au kijijini kwenu kuna fursa mbali mbali hivyo kupitia kikundi hiki tunaweza kuitumia fursa hiyo na kufikia malengo.
Faida itatolewa kwa asilimia kulingana na kile kianzio chako,(Mfano umeingia kwa laki3 basi utapata faida kwa asilimia 30 ya fedha yako utapata papo hapo na yule aliyetoa laki 1.5 nae atapata asilimia 30 ya pesa yake.) Nyingine tunaingiza kwenye kukuza mtaji na hata hiyo faida kama mtu atahitaji iendelee kukuza mtaji pia yakubalika.

KUSUDIO:
01. Kujiwezesha vijana kujiajiri na kujiongezea kipato.
02. Kukusanya nguvu mbali mbali kutoka kwa watu wenye kipato kidogo na kuwa katika hali kusudiwa kwa kila mwana kikundi.
03. Kujenga na kukuza ushirikiano na upendo miongoni mwetu.
04. Kujua na kufurahia umuhimu wa mtandao huu wa kijamii kupitia muunganisho huo.

VIGEZO:

01. Kiwango cha juu kabisa cha kipato chako kisizidi milioni moja.
02. Kikundi kiwe na watu wasiozidi kumi.
03. Wanakikundi kufahamiana ktk makazi yako na kumjua at least mtu mmoja ktk familia/ukoo wako ambae ni wa damu ktika kuzaliwa
04. Kujituma na kuwa tayari kupokea maagizo kutoka kwa wanakundi
05. KUJA NA WAZO KUHUSU ULITAKALO TULIFANYE KTK KUNDI KWA FAIDA YA WOTE.
06. Utanzania
07. Jinsia yoyote(walio kamili ktk jinsia hiyo) mashoga na wasagaji hawaruhusiwi.
08. Uwe na tabia njema ktk jamii inayokuzunguka.
09. Upatikane kwa mara ya kwanza ktk kikao kitachowezesha kufahamiana na kuonana.
10. UAMINIFU.

UKIWA UPO TAYARI PIGA SIMU NAMBA:-
0682580560 / 0653273420

Maoni tunapokea kwa nia njema wapi pa kurekebisha au kuongezea kwa nia njema.

.....................................................................
 
Somo hapo juu lahusika.
Kutokana na ugumu wa maisha ktk suala zima la ajira naomba kuungana na mtu yeyote aliyemuaminifu na mchapa kazi na kuweza kuanzisha kazi au biashara yoyote halali.
Yawezekana ulikuwa na idea juu ya kitu fulani lakini ulishindwa kulifanikisha hilo kutokana na hali halisi ya kifedha uliyonayo hivyo lengo la kuanzisha uzi huu nikuweza kutengeneza fursa ya sisi wenyewe tuweze kujiajiri.
Labda maeneo ya mkoani au kijijini kwenu kuna fursa mbali mbali hivyo kupitia kikundi hiki tunaweza kuitumia fursa hiyo na kufikia malengo.

KUSUDIO:
01. Kujiwezesha vijana kujiajiri na kujiongezea kipato.
02. Kukusanya nguvu mbali mbali kutoka kwa watu wenye kipato kidogo na kuwa katika hali kusudiwa kwa kila mwana kikundi.
03. Kujenga na kukuza ushirikiano na upendo miongoni mwetu.
04. Kujua na kufurahia umuhimu wa mtandao huu wa kijamii kupitia muunganisho huo.

VIGEZO:

01. Kiwango cha juu kabisa cha kipato chako kisizidi milioni moja.
02. Kikundi kiwe na watu wasiozidi kumi.
03. Wanakikundi kufahamiana ktk makazi yako na kumjua at least mtu mmoja ktk familia/ukoo wako ambae ni wa damu ktika kuzaliwa
04. Kujituma na kuwa tayari kupokea maagizo kutoka kwa wanakundi
05. KUJA NA WAZO KUHUSU ULITAKALO TULIFANYE KTK KUNDI KWA FAIDA YA WOTE.
06. Utanzania
07. Jinsia yoyote(walio kamili ktk jinsia hiyo) mashoga na wasagaji hawaruhusiwi.
08. Uwe na tabia njema ktk jamii inayokuzunguka.
09. Upatikane kwa mara ya kwanza ktk kikao kitachowezesha kufahamiana na kuonana.
10. UAMINIFU.

UKIWA UPO TAYARI
PIGA SIMU NAMBA 0682580560

Maoni tunapokea kwa nia njema wapi pa kurekebisha au kuongezea kwa nia njema.
Wazo zuri kwa vijana ila sijui kama watajitokeza walioko serious!
 
Back
Top Bottom