Waweza anza biashara ya samaki,unaenda zako feri/mwaloni unachukua wabichi,ukirudi unawakaanga,kisha unauza,wallah utarudi kuniambia,Kikubwa,wenzio huwa wanawakaanga kwa kuwatia chumvi tu,wewe unaweza kuwaroga wateja kwa kuongezea ndimu/limao,vitunguu saumu na tangawizi ,ladha haitakuwa kama ya competitors wako.
Kama uko sehemu yenye joto kama Dar funga Ice cream,Barafu za Ubuyu weka kwenye Deli peleka shuleni,hasa shule za msingi,utashangaa,huwa zinatoa faida double,kikubwa ziwe laini ubuyu ukolee,mpaka watu wazima watakufata nyumbani(Hii nna Experience Nayo)
Waweza uza vinywaji Baridi kama Soda,Maji na Juice....
Kila la Kheri Mkuu