Kwa mtizamo wangu kuna "perfect age for mates"...inatakiwa Mwanaume awe na kati ya miaka 3-5 zaidi ya mwanamke.
Ikiwa zaidi ya hapo itafika wakati mwanaume utakua unaona kama unaishi na mdogo wako (unamlea).
Ikiwa chini ya hapo, kuna tatizo ya "superiority complex" kwa pande zote mbili. Hata kama kuna vitu mnatofautiana basi mmoja wapo kati yenu atachukulia kwamba anauwezo zaidi yako. Kitu kigumu katika mahusiano ni kujiona wote sawa na kitu kimoja.
Kuna "factors" zingine wazungu wanaita "outliers"...kuna watu wana maarifa na busara(akili ya maisha) zaidi ya wastani wa miaka yao. Mfano mwanamke au mwanaume mwenye miaka 20 lakini akili yake inao uwezo sawa na mtu wa miaka 30. Hii inatengeneza matabaka ya watu wa rika lao kwasababu wanawaona kwa kiasi fulani wana akili za kitoto. Wengi wao hupendelea kutembea na wapenzi walio wazidi umri.
Ni vigumu kutumia kigezo cha umri kwa matakwa ya ndoa (unless for biological reasons)
Mahusiano (ndoa) ni suala la kisaikolojia zaidi kuliko baiolojia, mira na desturi zimeweka miiko na mifumo ambayo inafunga watu ambao sio wa kawaida (average people)...
Ikiwa unahitaji mahusiano na ndoa yenye mafanikio ni vigumu lakini inawezekana (inahitajika bahati pia). Umri sio kigezo kuna "physiology" pia, mchunguze mwenzio kama ana chembechembe za "dwarfism" au "giantism". Ingawa katika hayo mawili kuna mapungufu yanayo jitokeza, "early boomers" na "late boomers" ambapo huchangiwa sana na vyakula mnavyotumia kila siku.
"Ego and honesty" hichi ni kigezo kikubwa katika mahusiano kuliko vyote, kama mtaweza kutengeneza mshababiano mzuri basi mtafika mbali.