Ndoa za makaburi janga kwa wanawake, watoto mkoani Mara

Kikwajuni One

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
13,150
6,982
Kwa jamii ya Wakurya wanaoishi katika Wilaya za Tarime, Butiama, Rorya na Serengeti ni jambo la kawaida kuona familia ikichumbia na kuoa binti kwa ajili ya kijana wake wa kiume alifariki dunia kabla ya ndoa, lakini akiwa amefikia umri wa kuoa lakini.

Ndoa za aina hiyo hujulikana kama ndoa ya makaburi, zikimaanisha binti anayechumbiwa huolewa na mwanaume ambaye tayari amefariki dunia na kuzikwa.

Lengo la ndoa za aina hii, wenyeji wanasema ni kuendeleza jina na ukoo wa kijana aliyefariki kabla ya kuoa, kwa kuwa watoto wote wanaozaliwa na mwanamke aliyeolewa kwenye ndoa ya makaburi, huitwa kwa jina la marehemu licha ya ukweli kwamba amewazaa na mwanamume wengine.

Kwa mila na desturi za Wakurya, anayetoa mahari ndiye mwenye haki ya watoto watakaopatikana na wote huitwa jina lake hata kama hajawazaa.

Hii ndiyo maana watoto wanaozaliwa na mwanaume mwingine kwa mwanamke wa Kikurya aliyeolewa kwa kulipiwa mahari na akaachika bila mahari ya mume wa kwanza kurejeshwa, wote uhesabika wa mume wa kwanza aliyetoa mahari.

Kutokana na mila hiyo, mwanamke aliyeolewa katika ndoa ya makaburi yuko huru kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na kuzaa na mwanaume yeyote ampendaye ili kupata watoto wa kuendeleza jina na ukoo wa kijana ‘aliyemuoa’, yaani aliyefariki kabla ya kuoa wala kupata watoto.

Ndoa za aina hii zinakaribia kufanana na ile ya “nyumba nthobu” inayopatikani pia katika jamii ya Wakurya, ambayo mwanamke ambaye hakujaaliwa kupata watoto lakini ana mali, anaweza kumtolea mahari mwanamke mwingine na “kumuoa” kisha watoto wote atakaowazaa muolewaji wanakuwa wa mwanamke aliyemlipia mahari .

Upweke na ukatili
Licha ya ndoa za makaburi kuonekana kama aina ya ukatili na unyanyasaji kijinsia dhidi ya wanawake kutokana na wahusika wengi kuolewa bila ridhaa yao baada ya wazazi kupokea mahari, vilevilewengi wanaoolewa na makaburi hujikuta katika hali ya upweke, masononeko na umasikini.

Upweke na hata sonona kwa waolewaji hao hutokana na kukosa wanaume wa kudumu wa kuishi nao kwa sababu wengi wanaoingia nao kwenye mahusiano huwa ni tayari ama wana familia zao au baadaye huoa wanawake wengine na kuachana na wale wa makaburi.

Kutokana na kutokuwa na waume, wanawake wanaoolewa na makaburi huzaa watoto na wanaume tofauti na kujikuta wakilazimika kujitagutia riziki zao wenyewe na watoto wao.
Hii wakati mwingine husababisha familia kuishi katika umaskini.

Mila imesahaulika
Ni mara chache unaweza kusikia kuhusu ndoa za makaburi na hata watetezi wa haki za binadamu, hususan haki za wanawake, ni kama wameshau kama kuna jambo hili ambalo linadaiwa ni moja ya ukatili kwa wanawake unaotekelezwa kwa usiri mkubwa kwa kigezo cha mila.

Mwanaharakati wa haki za wanawake katika Kijiji cha Mwibagi wilayani Butiama, Adi Semberya anasema katika kijiji hicho kuna zaidi ya wanawake 20 ambao wameolewa katika ndoa hizo.

"Hii mila bado ipo na inatekelezwa sana. Hapa kuna binti ameolewa tu majuzi na ndiyo kwanza amezaa mtoto mmoja na hii inaonyesha kuwa jamii bado inaendeleza mila hii, ingawa haya mambo hayapigiwi kelele kama ukatili mwingine," anasema.

Mwanaharakati mwingine wa haki wanawake katika kijiji cha Masurura, wilayani Butiama, Yustina Marwa anasema umefika wakati wadau waungane kwa pamoja ili kupiga vita mila hii.

"Kama suala ni kuendeleza jina, mbona msichana akifa hakuna kinachofanyika kuendeleza jina lake, hii mila ipo kwa ajili ya kumkandamiza mwanamke na haina faida yoyote," anasema.

"Unaendelezaje jina la mtu ambaye amekufa na hakuacha mtoto hata mmoja? Kuna uhusiano gani kati ya watoto wanaozaliwa wakati mlengwa tayari amefariki," anahoji. Rhobi Samuel, mwanaharakati wa haki za wanawake na watoto anasema ndoa za makaburi ni mojawapo ya vichocheo vya kuwepo watoto wa mitaani kwa kuwa wengi hukosa malezi ya pamoja.

Wengi hudanganywa
Wanawake walioolewa katika ndoa ya makaburi wanafichua kuwa wengi wao huingia katika ndoa hizo bila kufahamu kutokana na mila na desturi inayowapa wazazi haki ya kujadiliana kuhusu ndoa na kupokea mahari bila anayeolewa kuhusishwa wala kumfahamu anayemuoa.

"Kwa mfano, mimi nililipiwa mahari na kuchukuliwa kwenda kwa mume bila hata kuonana na mwanaume mwenyewe. Kufika huko ndiko nikagundua kumbe nimeolewa kwa ajili ya mwanaume aliyekwishafariki," anasimulia Magreth Chacha (49), mkazi wa Kijiji cha Mwibagi.

Magreth, mama wa watoto watano, anasema maisha yake yemekuwa ni magumu kutokana na kulazimika kutafuta mahitaji kwa ajili ya familia bila msaada wa mtu yeyote.

"Mimi ndiye mama na ndiye baba; watoto wangu wananitegemea kwa kila kitu kuanzia makazi, mavazi, chakula na gharama zote za maisha," anasema Magreth.

Mama huyo aliingia kwenye ndoa ya makaburi akiwa na umri wa miaka 16 baada wazazi wake kupokea mahari ya ng'ombe 16.

Anasema licha ya yeye kufichwa ukweli, wazazi wake walifahamu kuwa anaolewa kwenye ndoa ya kaburi kwani mwanzoni alikabidhiwa kwa mwanaume akitambulishwa kuwa ndiye mumewe kabla ya kubaini ukweli baadaye.

"Niliishi na mwanaume yule kwa miaka miwili kama mume na mke. Lakini cha ajabu hakuwa akiwajibika kwa mahitaji yangu. Nilipoanza kuhoji ndipo nikabaini ukweli baada ya kuonyeshwa kaburi nikiambiwa mume wangu amelala humo. Niliumia lakini sikuwa na la kufanya," anasema Magreth.

Maryciana Mgosi (41), mkazi wa Kijiji cha Mwibagi naye alijikuta kwenye ulaghai wa aina hiyo baada ya wazazi wake kupokea mahari ya ng'ombe sita na kumuoza kwa sherehe huku alikabidhiwa kwa mwanaume akitambulishwa kuwa ndiye mumewe kumbe ilikuwa hadaa.

"Baada ya miezi mitatu ya kuishi na yule mume na nikiwa tayari nimepata ujauzito, ndipo nikabaini kumbe hakuwa mume wangu, bali ilikuwa ni ulaghai ili nisihtuke kwamba nimeolewa ndoa ya kaburi kwa ajili ya mtu aliyefariki," anasema Maryciana.

Anasema aliporejea nyumbani kwao kueleza alichokibaini, wazazi wake walimtaka kurudi kwenye ndoa yake maana hiyo ni mila na desturi ya jamii yao.

Lucia Chacha (56), mkazi wa Kijiji cha Masurura Wilaya ya Butiama ni muathirika mwingine wa ndoa ya makaburi anayeamini hali ya umaskini wa kipato aliyonayo ni matokeo ya mila hiyo iliyomfanya kugeuka mama na baba kwa watoto wake.

Kauli ya kulaani ndoa ya makaburi imetolewa pia na Bhoke Mwita (43) anayesema mila hiyo si tu huwaathiri wanawake, bali pia watoto wanaozaliwa na kukua bila malezi na huduma za baba.

"Katibu wa Muungano wa Koo 12 za Wakurya, Mwita Sibora anasema mila hiyo ni muhimu kwa kuwa endapo familia haitatekeleza mila hiyo kwa kijana wao aliyefariki basi kuna uwezekano wa familia hiyo kukumbwa na mabalaa na hata kutoweka kabisa.

"Marehemu anayetafutiwa mke ni yule aliyefikisha miaka 18 na tayari alifanyiwa tohara, sasa ikitokea familia ikapuuza kuna uwezekano wa vifo vya ghafla na ajabu huku watu wa familia wakikumbwa na ndoto za ajabu ajabu," anasema Nyasibora.

Hata hivyo, Askofu Daniel Ouma wa Kanisa la Newlife Gospel Community, anasema: "Kibiblia mila kama hii hazikubaliki na kanisa, tunafanya kila jitihada kushirikiana na wadau wengine kukabilia nayo kwa sababu si tu ni kinyume cha mafundisho mema ya kiimani, bali pia ni kinyume cha sheria na zinachangia hali duni kimaisha katika jamii," anasema Askofu Ouma.

Wakuu wa Wilaya za Butiama, Moses Kaegele anasema japo hajawahi kupata uthibitisho wa kuwepo kwa ndoa za aina hiyo, ofisi yake itafuatilia na kuchukua hatua ikianza kwa kutoa elimu kwa umma kuhusu mila na desturi zinazotweza utu wa mwanamke.

Kauli kama hiyo pia imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka akisema; "Ndiyo kwanza nafahamu hilo kutoka kwako, pengine ni kutokana na uchache wa watu wa jamii ya Kikurya wilayani Rorya; nitafuatilia na kwa kweli ofisi yangu itachukua hatua ikibaini uwepo wa ndoa za aina hiyo."
 
Wadau hamjamboni nyote?

He unafahami ndoa za makaburi wilayani tarime rieya nacserengeti mkoani Mara?

Kwa jamii ya Wakurya wanaoishi katika Wilaya za Tarime, Butiama, Rorya na Serengeti ni jambo la kawaida kuona familia ikichumbia na kuoa binti kwa ajili ya kijana wake wa kiume alifariki dunia kabla ya ndoa, lakini akiwa amefikia umri wa kuoa lakin...
Duhi Wakurya wako nyuma sana kwa mambo mengi!
 
Sipati picha ushubwada huu ungekuwa unatendeka huko Lindi au Mtwara; watu wote wa kutoka huko wangezomewa, wangezodolewa, wangetukanwa, wangepewa kila aina ya majina kama vile washamba, hawajaendelea, hawajaelimika, wapo nyuma ya wakati, hawajielewi n.k
 
Hahaha nani adhubutu kutukana wanamme hajipendi . watu wanaangalia sura za kutukana wanajua madume ya kanda hiyo yakinyanyua panga au sime au silaha yoyote hairudi chini bila kuwa na tone la damu. Ile ni nchi nyingine ujue. Tuliowahi kufika huko tunalijua hili
 
Kwa jamii ya Wakurya wanaoishi katika Wilaya za Tarime, Butiama, Rorya na Serengeti ni jambo la kawaida kuona familia ikichumbia na kuoa binti kwa ajili ya kijana wake wa kiume alifariki dunia kabla ya ndoa, lakini akiwa amefikia umri wa kuoa lakini.

Ndoa za aina hiyo hujulikana kama ndoa ya makaburi, zikimaanisha binti anayechumbiwa huolewa na mwanaume ambaye tayari amefariki dunia na kuzikwa.

Lengo la ndoa za aina hii, wenyeji wanasema ni kuendeleza jina na ukoo wa kijana aliyefariki kabla ya kuoa, kwa kuwa watoto wote wanaozaliwa na mwanamke aliyeolewa kwenye ndoa ya makaburi, huitwa kwa jina la marehemu licha ya ukweli kwamba amewazaa na mwanamume wengine.

Kwa mila na desturi za Wakurya, anayetoa mahari ndiye mwenye haki ya watoto watakaopatikana na wote huitwa jina lake hata kama hajawazaa.

Hii ndiyo maana watoto wanaozaliwa na mwanaume mwingine kwa mwanamke wa Kikurya aliyeolewa kwa kulipiwa mahari na akaachika bila mahari ya mume wa kwanza kurejeshwa, wote uhesabika wa mume wa kwanza aliyetoa mahari.

Kutokana na mila hiyo, mwanamke aliyeolewa katika ndoa ya makaburi yuko huru kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na kuzaa na mwanaume yeyote ampendaye ili kupata watoto wa kuendeleza jina na ukoo wa kijana ‘aliyemuoa’, yaani aliyefariki kabla ya kuoa wala kupata watoto.

Ndoa za aina hii zinakaribia kufanana na ile ya “nyumba nthobu” inayopatikani pia katika jamii ya Wakurya, ambayo mwanamke ambaye hakujaaliwa kupata watoto lakini ana mali, anaweza kumtolea mahari mwanamke mwingine na “kumuoa” kisha watoto wote atakaowazaa muolewaji wanakuwa wa mwanamke aliyemlipia mahari .

Upweke na ukatili
Licha ya ndoa za makaburi kuonekana kama aina ya ukatili na unyanyasaji kijinsia dhidi ya wanawake kutokana na wahusika wengi kuolewa bila ridhaa yao baada ya wazazi kupokea mahari, vilevilewengi wanaoolewa na makaburi hujikuta katika hali ya upweke, masononeko na umasikini.

Upweke na hata sonona kwa waolewaji hao hutokana na kukosa wanaume wa kudumu wa kuishi nao kwa sababu wengi wanaoingia nao kwenye mahusiano huwa ni tayari ama wana familia zao au baadaye huoa wanawake wengine na kuachana na wale wa makaburi.

Kutokana na kutokuwa na waume, wanawake wanaoolewa na makaburi huzaa watoto na wanaume tofauti na kujikuta wakilazimika kujitagutia riziki zao wenyewe na watoto wao.
Hii wakati mwingine husababisha familia kuishi katika umaskini.

Mila imesahaulika
Ni mara chache unaweza kusikia kuhusu ndoa za makaburi na hata watetezi wa haki za binadamu, hususan haki za wanawake, ni kama wameshau kama kuna jambo hili ambalo linadaiwa ni moja ya ukatili kwa wanawake unaotekelezwa kwa usiri mkubwa kwa kigezo cha mila.

Mwanaharakati wa haki za wanawake katika Kijiji cha Mwibagi wilayani Butiama, Adi Semberya anasema katika kijiji hicho kuna zaidi ya wanawake 20 ambao wameolewa katika ndoa hizo.

"Hii mila bado ipo na inatekelezwa sana. Hapa kuna binti ameolewa tu majuzi na ndiyo kwanza amezaa mtoto mmoja na hii inaonyesha kuwa jamii bado inaendeleza mila hii, ingawa haya mambo hayapigiwi kelele kama ukatili mwingine," anasema.

Mwanaharakati mwingine wa haki wanawake katika kijiji cha Masurura, wilayani Butiama, Yustina Marwa anasema umefika wakati wadau waungane kwa pamoja ili kupiga vita mila hii.

"Kama suala ni kuendeleza jina, mbona msichana akifa hakuna kinachofanyika kuendeleza jina lake, hii mila ipo kwa ajili ya kumkandamiza mwanamke na haina faida yoyote," anasema.

"Unaendelezaje jina la mtu ambaye amekufa na hakuacha mtoto hata mmoja? Kuna uhusiano gani kati ya watoto wanaozaliwa wakati mlengwa tayari amefariki," anahoji. Rhobi Samuel, mwanaharakati wa haki za wanawake na watoto anasema ndoa za makaburi ni mojawapo ya vichocheo vya kuwepo watoto wa mitaani kwa kuwa wengi hukosa malezi ya pamoja.

Wengi hudanganywa
Wanawake walioolewa katika ndoa ya makaburi wanafichua kuwa wengi wao huingia katika ndoa hizo bila kufahamu kutokana na mila na desturi inayowapa wazazi haki ya kujadiliana kuhusu ndoa na kupokea mahari bila anayeolewa kuhusishwa wala kumfahamu anayemuoa.

"Kwa mfano, mimi nililipiwa mahari na kuchukuliwa kwenda kwa mume bila hata kuonana na mwanaume mwenyewe. Kufika huko ndiko nikagundua kumbe nimeolewa kwa ajili ya mwanaume aliyekwishafariki," anasimulia Magreth Chacha (49), mkazi wa Kijiji cha Mwibagi.

Magreth, mama wa watoto watano, anasema maisha yake yemekuwa ni magumu kutokana na kulazimika kutafuta mahitaji kwa ajili ya familia bila msaada wa mtu yeyote.

"Mimi ndiye mama na ndiye baba; watoto wangu wananitegemea kwa kila kitu kuanzia makazi, mavazi, chakula na gharama zote za maisha," anasema Magreth.

Mama huyo aliingia kwenye ndoa ya makaburi akiwa na umri wa miaka 16 baada wazazi wake kupokea mahari ya ng'ombe 16.

Anasema licha ya yeye kufichwa ukweli, wazazi wake walifahamu kuwa anaolewa kwenye ndoa ya kaburi kwani mwanzoni alikabidhiwa kwa mwanaume akitambulishwa kuwa ndiye mumewe kabla ya kubaini ukweli baadaye.

"Niliishi na mwanaume yule kwa miaka miwili kama mume na mke. Lakini cha ajabu hakuwa akiwajibika kwa mahitaji yangu. Nilipoanza kuhoji ndipo nikabaini ukweli baada ya kuonyeshwa kaburi nikiambiwa mume wangu amelala humo. Niliumia lakini sikuwa na la kufanya," anasema Magreth.

Maryciana Mgosi (41), mkazi wa Kijiji cha Mwibagi naye alijikuta kwenye ulaghai wa aina hiyo baada ya wazazi wake kupokea mahari ya ng'ombe sita na kumuoza kwa sherehe huku alikabidhiwa kwa mwanaume akitambulishwa kuwa ndiye mumewe kumbe ilikuwa hadaa.

"Baada ya miezi mitatu ya kuishi na yule mume na nikiwa tayari nimepata ujauzito, ndipo nikabaini kumbe hakuwa mume wangu, bali ilikuwa ni ulaghai ili nisihtuke kwamba nimeolewa ndoa ya kaburi kwa ajili ya mtu aliyefariki," anasema Maryciana.

Anasema aliporejea nyumbani kwao kueleza alichokibaini, wazazi wake walimtaka kurudi kwenye ndoa yake maana hiyo ni mila na desturi ya jamii yao.

Lucia Chacha (56), mkazi wa Kijiji cha Masurura Wilaya ya Butiama ni muathirika mwingine wa ndoa ya makaburi anayeamini hali ya umaskini wa kipato aliyonayo ni matokeo ya mila hiyo iliyomfanya kugeuka mama na baba kwa watoto wake.

Kauli ya kulaani ndoa ya makaburi imetolewa pia na Bhoke Mwita (43) anayesema mila hiyo si tu huwaathiri wanawake, bali pia watoto wanaozaliwa na kukua bila malezi na huduma za baba.

"Katibu wa Muungano wa Koo 12 za Wakurya, Mwita Sibora anasema mila hiyo ni muhimu kwa kuwa endapo familia haitatekeleza mila hiyo kwa kijana wao aliyefariki basi kuna uwezekano wa familia hiyo kukumbwa na mabalaa na hata kutoweka kabisa.

"Marehemu anayetafutiwa mke ni yule aliyefikisha miaka 18 na tayari alifanyiwa tohara, sasa ikitokea familia ikapuuza kuna uwezekano wa vifo vya ghafla na ajabu huku watu wa familia wakikumbwa na ndoto za ajabu ajabu," anasema Nyasibora.

Hata hivyo, Askofu Daniel Ouma wa Kanisa la Newlife Gospel Community, anasema: "Kibiblia mila kama hii hazikubaliki na kanisa, tunafanya kila jitihada kushirikiana na wadau wengine kukabilia nayo kwa sababu si tu ni kinyume cha mafundisho mema ya kiimani, bali pia ni kinyume cha sheria na zinachangia hali duni kimaisha katika jamii," anasema Askofu Ouma.

Wakuu wa Wilaya za Butiama, Moses Kaegele anasema japo hajawahi kupata uthibitisho wa kuwepo kwa ndoa za aina hiyo, ofisi yake itafuatilia na kuchukua hatua ikianza kwa kutoa elimu kwa umma kuhusu mila na desturi zinazotweza utu wa mwanamke.

Kauli kama hiyo pia imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka akisema; "Ndiyo kwanza nafahamu hilo kutoka kwako, pengine ni kutokana na uchache wa watu wa jamii ya Kikurya wilayani Rorya; nitafuatilia na kwa kweli ofisi yangu itachukua hatua ikibaini uwepo wa ndoa za aina hiyo."
Pole yake Magreth hii ni tamaduni chafu , haya ndio maswala ya wote kuungana kupinga hizi mila masheikh na mapadri kwa pamoja nao waseme haifai.

Kikwajuni One hongera kwa mtiririko mzuri wa taarifa
 
"Katibu wa Muungano wa Koo 12 za Wakurya, Mwita Sibora anasema mila hiyo ni muhimu kwa kuwa endapo familia haitatekeleza mila hiyo kwa kijana wao aliyefariki basi kuna uwezekano wa familia hiyo kukumbwa na mabalaa na hata kutoweka kabisa"

Hii kauli ni tatizo
 
Wengi wamesoma lakini hawaja elimika
 
Mila imesahaulika
Ni mara chache unaweza kusikia kuhusu ndoa za makaburi na hata watetezi wa haki za binadamu, hususan haki za wanawake, ni kama wameshau kama kuna jambo hili ambalo linadaiwa ni moja ya ukatili kwa wanawake unaotekelezwa kwa usiri mkubwa kwa kigezo cha mila.
Mila hizo zingekuwepo mikoa ya Pwani au jamii kubwa inazozienzi ingekuwa Muslim hapo ungewasikia wanaharakati wanavyocharuka lakini kwa kuwa hali ipo kinyume chake huwezi kusikia kelele zozote.
 
Ndoa za ki-mizimu hizi....ushirikina mtupu

Mshana Jr
 
Back
Top Bottom