Kwa hili, namsaidiaje binti yangu?

Kwa hili, namsaidiaje binti yangu?

Yalinikuta kwa nwanangu wa kuzaa sikumnyonyesha sana alipofika miezi kumi alinyonyeshwa na mwingine nilikuwa nikienda likizo kumsalimia kwa mara ya kwanza alinikataa kabisa alikuwa bado mdogo sana ili anikubali walimtambulisha kwamba mimi ni dada alikubali tu kwamba dada ni mpika uji likizo ikiisha narudi kazini nifupishe nilipoanza kuishi naye hakuwa na mapenzi na mimi kabisa nilichofanys ni kijipendekeza kwake na mara kwa mara kuwa karibu naye kwa sasa ananipenda sana sana japo simfikii aliyemnyonyesha, mwambie mzazi mwenzio ajiweke karibu naye hata kama mtoto haonyeshi mapenzi kwa mama yake, yeye asijali akipata senti amnunulie vizawadi na ampe mwenyewe likizo aende kwa mama japo wiki au siku tatu hutoamini atampenda tu akikosa amshauri asimgombeze itachukua muda mrefu ila yataisha
Unahisia za kisaliti sana.. Nisamehe

Unawezaje kuwa mgeni kwa mwanao uliemzaa.!

Na ukaona sawa.!?
 
Sijamalizana na wewe leo naomba uniambie wakielewana utapata faida gani? Au huyo mke wako wa talaka hali kwa sababu ya mtoto? Kuna huruma zingne ni kutupilia mbali ili mengne yaendelee. Unamuonea huruma mtu aliyekubali talaka na tayar ana bwanake huko bro alikulisha nini? Umesema vodka sasa ngoja akili ya nyago itatue hili.
Ndio ni mzazi mwenzako sawa, lakin kumbuka neno talaka, ndugu yangu mtoto usijekumlazimisha unayoyataka wewe kama huyo x wako halali usingzi ngoja asilale maisha yake yote. Bwana huruma nakwambia ukijaribu kulazimisha huyo mtoto huo utopolo utakuja kujilaumu mwenyewe. Hapo we la kufanya mpe mto haki yake ya msingi akija kujitambua ukubwani yeye ataamua la kufanya na sio wewe kujifanya unamuonea mzazi mwenzako huruma.
 
Binti yupo shule ya "kulala"? Okay.Binti hana mapenzi na mamaye yawezekana sababu ni umbali/kutokuishi pamoja,mazoea au dokezo hasi kuhusu huyo mama kutoka kwa mtu mwingine.Unahitaji kumpanga kwa akili nyingi ili uwaunganishe wapatane.Au,tumia wataalamu wa saikolojia wamuweke relini.
ANGALIZO;Usilazimishe upendo umuingie mtoto kama roho mtakatifu na vilevile chunga usiharibu ndoa ya mzazi mwenzio kwa kung'ang'aniza upendo kwa binti yenu.
Hama kwenu na wewe nenda kajitemee

Kazi kula ugali wa mama tu
 
Yalinikuta kwa nwanangu wa kuzaa sikumnyonyesha sana alipofika miezi kumi alinyonyeshwa na mwingine nilikuwa nikienda likizo kumsalimia kwa mara ya kwanza alinikataa kabisa alikuwa bado mdogo sana ili anikubali walimtambulisha kwamba mimi ni dada alikubali tu kwamba dada ni mpika uji likizo ikiisha narudi kazini nifupishe nilipoanza kuishi naye hakuwa na mapenzi na mimi kabisa nilichofanys ni kijipendekeza kwake na mara kwa mara kuwa karibu naye kwa sasa ananipenda sana sana japo simfikii aliyemnyonyesha, mwambie mzazi mwenzio ajiweke karibu naye hata kama mtoto haonyeshi mapenzi kwa mama yake, yeye asijali akipata senti amnunulie vizawadi na ampe mwenyewe likizo aende kwa mama japo wiki au siku tatu hutoamini atampenda tu akikosa amshauri asimgombeze itachukua muda mrefu ila yataisha
hii yako ni tofauti na ya huyu mtu tena mbali sana na kwanza yako sio kesi hata kidogo ni majukumu yalikufanya ukapitia hiyo hali. Lakn ya huyu bwana huruma hafai.
 
Niseme tu mimi ni single father wa binti mmoja , japo nilisha sema nawakiume mkubwa ila ni stori ndefu mpaka kufanya maamuzi ya kubaki na binti yangu tu.

Binti yangu nilianza kukaa nae alipo timiza miaka miwili baada ya kuvutana na mama yake mno.

Ila mama yake alipo pata mtu mwingine wa kumuoa ndoa kabisa, baada ya mimi kupeana nae talaka , ikawa rahisi sana kunipa binti yangu .

Nilimlea binafsi , alipo kua alienda kwa bibi yake na sasa yupo shule ya kulala anaendelea vyema.

Shida inakuja , baada ya binti ya kuwa mkubwa kiasi , naona kama hana bond na mama yake , wala hana hisia nae kabisa 🥲 , sikupenda hii hali ijitokeze kabisa , yani hata ukimwambia wewe unafanana na mama yako vitu fulani analia kabisa 🤔

Wakionana hauwezi fikiri ni mtu na mtoto wake , hii hali siipendi kwa sababu sijawahi kumsaigia kunguni mama watoto wangu kwa mwanae kabisa , tunaelewana kama wazazi na hata yeye ana shiriki matunzo ya mwenetu.

Hii hali imekaaje wadau , na nina weza fanya vipi nikaweka ukaribu wa binti yangu na mama yake 🤔.
Mpe muda awe anaenda kukaa kwa mama yake mara kwa mara
 
Mshauri mama yake aendelee kujenga ukaribu nae, na Kama ninyi ni waislam, mpeleke huyo binti madrasa akajifunze thamni ya wazazi na namna ya kuamiliana nao hata kama walikutelekeza, huko atjifunza pia thaman ya mama na nafasi yake. Mwisho kwenye swala zako kithirisha maombi ya kuwafanya wapatane.
Naomba kuwasilisha.
 
Wazazi inaonekana kuna maisha mnayapata yana raha yake ya kupasha viporo ambapo sisi ambao hatuna wazazi wenza tunayakosa.

Mama yangu akiwa anaongea na mzee kwenye simu huwa anamwambia "Mpenzi wangu wa zamani.."
Kwa hiyo kumbe wale watoto 6 walikuwa ni wa kuchemsha?
 
Kwanza kabisa nikupe pole ndugu min -me pamoja na utani wa hapa na pale.. Ila kwenye hili tambua kwanza hapo kuna kitu mwanao tayari amesha kuwa affected by trauma...(najua na sound intense ila ukweli) She has learned over time that she's not worthy of mom's care... Why? Kwasababu huko asomako kuna wenzake pia...

Wenzake mashuleni wana wazazi wote na huenda kwenye family meetings day, wanakuja pamoja as a couple... Huenda ni kweli mnashirikiana, ila ukishaona mwanao hampendi mzazi mmoja jua kuna complex issue baina yake na mzazi..

Sasa, hapo concerns zako nimezielewa kabisa... You feel sorry for her...na Nimesoma mpaka unataka mama ake arudi aishi nyumbani but she's already gone.. Anafamilia ambayo hawezi kuacha just because of that..

Sasa mkuu hapo inabidi ufanye maongezi magumu, it is now or never..

Mwanao anamaumivu ya kutokuwa ma mother's love, kumbuka hakuna kama mama. I lost mine at a very young age, na I had to pay the price for almost 2 decades kujua I was worth of her love.. (regrets are worse than discomfort)

Kaa Meza moja na huyo mwenza na mme wake... Ajue kabisa what's going on... Anzisha namna kila baada ya muda unawaweka karibu, do some parties and stuff, wafanye both wawe na furaha.. Mfanye mtoto ajue mama yake anampenda. Do it now,

tupilia mbali ego yako ya ulevi ndugu😂

Kuna watu kama Icebreaker wa nakwambia uiachie nature iamue broo acha kabisa, huyo dogo atakuja kuishi maisha mabaya... Atakuja kuwa anaongea vitu vichafu na atakosa kujipenda.. Ila the only cure is love. Kaeni muongee namna ya kumsaidia dogo... Nasisitiza DO IT NOW

Cc binti kiziwi
 
Mama yake anashiriki kila kitu hata leo kanitumia rangi ya gauni la mtoto kwa birthday yake mwezi wa tisa, ila kuna bond ya mama nahisi anaikosa, kwenye familia ya mtu kuweka hii bond kwa mtoto ambae yupo na bond na mimi naona ni ngumu sana 🤔
bond ya mtoto kwa mama ni natural. huwa sio ya kutengenezwa, ila hapo kwako there is something big wrong!
 
Back
Top Bottom