Kwa hili, namsaidiaje binti yangu?

Kwa hili, namsaidiaje binti yangu?

Niseme tu mimi ni single father wa binti mmoja , japo nilisha sema nawakiume mkubwa ila ni stori ndefu mpaka kufanya maamuzi ya kubaki na binti yangu tu.

Binti yangu nilianza kukaa nae alipo timiza miaka miwili baada ya kuvutana na mama yake mno.

Ila mama yake alipo pata mtu mwingine wa kumuoa ndoa kabisa, baada ya mimi kupeana nae talaka , ikawa rahisi sana kunipa binti yangu .

Nilimlea binafsi , alipo kua alienda kwa bibi yake na sasa yupo shule ya kulala anaendelea vyema.

Shida inakuja , baada ya binti ya kuwa mkubwa kiasi , naona kama hana bond na mama yake , wala hana hisia nae kabisa 🥲 , sikupenda hii hali ijitokeze kabisa , yani hata ukimwambia wewe unafanana na mama yako vitu fulani analia kabisa 🤔

Wakionana hauwezi fikiri ni mtu na mtoto wake , hii hali siipendi kwa sababu sijawahi kumsaigia kunguni mama watoto wangu kwa mwanae kabisa , tunaelewana kama wazazi na hata yeye ana shiriki matunzo ya mwenetu.

Hii hali imekaaje wadau , na nina weza fanya vipi nikaweka ukaribu wa binti yangu na mama yake 🤔.
Huu sio mwandiko wako mkuu!

Mwandiko wako ninaujua!

Nipe code ya game za kesho tunatokaje pale sportybet kamanda?
 
Bwashee kwanza ni ngumu sana kwa Mama wa mtoto kuamini kua wewe hujampa sumu mtoto ili amchukie Mama yake,si ajabu hata huko pembeni anakusema kua umempa maneno mtoto ili amchukie yeye Mama yake,

Just relax,acha nature iamue,Kujenga emotion connection kwa sasa hivi kati ya Mama na mwanae sio kazi rahisi,almost impossible kama mtoto kisha zidi miaka 10 ya umri wake.
Bwashee mama mtoto , mume wake , ni marafiki sana , sijawahi achana kwa ugomvi na tunashirikiana
 
Binti yako ni mdogo, kiumri lkn anajitahidi kuchangua kwanini mama hakai na mimi anakaa na wengine??

zaidi sana inaonekn akienda huko huyo mume wa mzazi mwenzako anaweza kuwa sio rafiki kwake hivyo napo lazima ajiulize mbona huyu mzee naye sio kama baba yangu ??

Hivyo ni kutafuta njia ya kumkutanisha na mama yake pasi kwenda nyumbani kwake inapobidi ili. Pengine uweze kuona anakuwaa huru au la


Yapo mengi mzee min
 
Kiukweli asiwasiliane na mimi. Level yangu ya elimu inaniruhusu kujua situation na kuweza kufikiria solution ila sina elimu ya kunifanya nikideal nayo nione kwamba swala nimedeal nalo.
SitAfanya hivyo
 
Binti yako ana miaka mingapi?


Ila kwa ufupi tu, toka akiwa mdogo alipaswa awe anaenda kwa mama muda likizo.

Na hapaswi kabisa kujua kwamba mliachana na mama ake, mpaka pale akue aje adadavue mambo mwenyewe.
Yn mtoto asijue kama wameachana afu hapo hapo awe anaenda nyumbani kwa baba wa kambo?
Labla mtoto wa darasa la kwanza.
 
Kammiss! Mama akiwa na ukaribu na binti yake lazima atakua na ukaribu na min me.

Sasa huyu bwana inaonekana kamiss kumuona bibie hata kwa video call.
Unanionea ephen
 
Kammiss! Mama akiwa na ukaribu na binti yake lazima atakua na ukaribu na min me.

Sasa huyu bwana inaonekana kamiss kumuona bibie hata kwa video call.
Kama vile naanza kuwaelewa vijana wanaogopa single mothers wanaosema hadi waonyeshwe kaburi la baba mtu ndio wanachukua single mother 😁
 
Ndoa n mtoto, mtoto ndie anayerudisha mapenzi ya wazazi.

Na ndio maana tupo tunaopinga kuwa na mahusiano na single mother huku tukijua pia ambaye hajazaa nae pia amelombwa.
Mama wa mtoto wangu ana mabinti wengine na mume wake
 
Back
Top Bottom