Kwa hili, namsaidiaje binti yangu?

Kwa hili, namsaidiaje binti yangu?

Niseme tu mimi ni single father wa binti mmoja , japo nilisha sema nawakiume mkubwa ila ni stori ndefu mpaka kufanya maamuzi ya kubaki na binti yangu tu.

Binti yangu nilianza kukaa nae alipo timiza miaka miwili baada ya kuvutana na mama yake mno.

Ila mama yake alipo pata mtu mwingine wa kumuoa ndoa kabisa, baada ya mimi kupeana nae talaka , ikawa rahisi sana kunipa binti yangu .

Nilimlea binafsi , alipo kua alienda kwa bibi yake na sasa yupo shule ya kulala anaendelea vyema.

Shida inakuja , baada ya binti ya kuwa mkubwa kiasi , naona kama hana bond na mama yake , wala hana hisia nae kabisa 🥲 , sikupenda hii hali ijitokeze kabisa , yani hata ukimwambia wewe unafanana na mama yako vitu fulani analia kabisa 🤔

Wakionana hauwezi fikiri ni mtu na mtoto wake , hii hali siipendi kwa sababu sijawahi kumsaigia kunguni mama watoto wangu kwa mwanae kabisa , tunaelewana kama wazazi na hata yeye ana shiriki matunzo ya mwenetu.

Hii hali imekaaje wadau , na nina weza fanya vipi nikaweka ukaribu wa binti yangu na mama yake 🤔.

Kuna wanawake ni wachawi, wakishindwa kuwasukumia mabinti zao uchawi wao na Roho zao Mbaya, watoto kwa sababu ya wema wao Kuna namna wanawachukia sana Mama zao, sio Jambo la kawaida, advice : Take it positive and move on, Wacha iwe hivyo hivyo, Kama alikuwa mbaya kwako bila sababu, ni Mbaya pia kwa Binti yako, usiweke uadui, ila uadui kati yao unapokuja naturally, Mshukuru Mungu.
 
Ipe muda hii hali.

Ila kwa sasa Mama mtoto ashiriki kwa ukaribu (hata akiwa mbali) kwenye mambo/shughuli zinazomuhusu binti yenu ambazo zinaonekana mko sambamba mfano ( birthdays, kula Christmas pamoja, kwenda visiting day ww na Mama mtoto, pia Mama mtoto ampigie Binti kumuelekeza mambo ya Hedhi nk).

Binti huwa ni kipenz cha Baba.
Ila malezi mazuri anapata kwa Mama.
Binti yangu akiwa na miaka 3 wakati wa likizo alipokuja kwangu aliniambia out of blue, "halafu mama huwa anasema umekufa", nikamuuliza wewe huwa unasemaje? Akajibu, huwa nasema hujafa, si hivi nakuona. Mimi nilisikitika kwa kuona jinsi mama yake anavyojitengenezea chuki na huyu binti yetu, baadae atakuja mchukia sana mama yake kwa kauli za kijinga kama hizo. Inaonekana dogo, hiyo kauli ya kifo ilikuwa inamkereketa sana..

Nilichojifunza min -me watoto wa kike huwa wanaona wivu na hasira kuwa mama zao waliwadhulumu furaha baba zao. Wanawafanya washua wao kuwa victim
 
Kuna wanawake ni wachawi, wakiahindwa kuwasukumia mabinti zao uchawi wao na Roho zao Mbaya, watoto kwa sababu ya wema wao Kuna namna wanawachukia sana Mama zao, sio Jambo la kawaida, advice : Take it positive and move on, Wacha iwe hivyo hivyo, Kama alikuwa mbaya kwako bila sababu, ni Mbaya pia kwa Binti yako, usiweke uadui, ila uadui kati yao unapokuja natural, Mshukuru Mungu.
Umeongea point kubwa sana mkuu.
 
-Mtoto ni wa kwenu.
-Mmeachana
-mtoto hajabond na mama na wewe siyo kikwazo na mama mtoto hajali sana hali hiyo.
-HUU UZI NILITARAJIA ULETWE NA MAMA MTOTO, AU AMEKUTUMA?.
X wako yupo nje ya udhibiti/ ushawishi wako kwa sasa kwani kaolewa.
Kama x wako hajakutuma, kinachokusumbuwa ni huruma kwa bintiyo.

Itoshe kusema kuwa x wako ni imara sana ki hisia kukuliko. Vinginevyo wewe ndo uliyemmisi x wako.
 
OA Ndugu yangu.

Ni namna unatakiwa uliweke hili sawa kwenye fikra zake.

Alaf hawa Watoto wa sikuhizi hata kama hawakuambii ila wanajua kabisa hata kama hujaoa basi kuna sehem unahemea.

Sasa kuliko kujua Baba yao ni mzinzi.
Mvalishe pete Seran na umuoe.

Au uache alaf aje akupekenyue JF miaka 10 mbele ajue umemchezea msukuma wa watu kama ulivyomchezea mama ake.

☺☺☺☺
Khaa shemeji kwanini anioe mimi jamani! Mabinti wote hawa akaanze kusota na mshangazi mimi😆
 
Kuna Ile likizo nenda kwa mama halafu kuna ILe mtoto anaumwa unamwita mama yake anakuja anampa faraja kuna sikukuu aende kwa mama akale sikukuu hiyo ulimnyima no connection yoyote
Kwa mtu aliyeolewa na watoto wengine wawili, hiyo option inaweza kuwa ngumu sana. Huyo mama ameshapoteza emotional touch na mtoto baada ya kuzaa tena.
 
Kwa mtu aliyeolewa na watoto wengine wawili, hiyo option inaweza kuwa ngumu sana. Huyo mama ameshapoteza emotional touch na mtoto baada ya kuzaa tena.
Nakataaa kabisaaaa hata kwenye mahusiano kama hakuna mawasiliano Mazur basi ujue hakuna Mapenzi ndo yaliyomkuta huyo bint na mama yake no communication na baba ndiye chanzo
 
Hahaha uoga wake ndio umasikini wake😅
Hafu we mzee bana, mimi sio binti excuse me!😁
Nashangaa sana ujue, vijana wanapofeli sielewi ni wapi. Huna ushangazi wewe, utakuwa shangazi kwa vijana wa 20s labda, ila min anaanza kuwa mwanaume...wewe nsio size yake kabisa! Kabla libido yake haijaharibiwa na Jack Daniels 😅
 
Min ana aina zake, pia mimi ni dada yake babu, hebu acha kumoresharaiz kijana wa watu hajaamua kusettle bado..
 
Bond Kati ya mtoto na mama inajengwa taratibu kadili mtoto anavyokua akiwa na mama yake

Kutokana na binti kuanza kujitambua akakuta yuko kwenye mikono ya watu wengine imemfanya asijenge bond na mama yake.

Hapa panahitajika ushirikiano kati yako wewe na mzazi mwenzio ili kurudisha ukaribu wa mama na mtoto

Huyo mama ajenge mazoea ya kumtembelea mwanae kumletea zawadi ili kurudisha ukaribu na mwanae hii ni suala kuliendea taratibu,ikiwezekana hata wakati wa likizo mpekeleke akakae naye kwa muda
Angalizo,Kuwa makini usijekuonekana unammendea wife wako wa zamani ikaleta vurugu kwa mumewe
 
Min ana aina zake, pia mimi ni dada yake babu, hebu acha kumoresharaiz kijana wa watu hajaamua kusettle bado..
Msukuma na mchagga wanaweza kuwa kaka na dada toka lini? Unaweza kumfanya mwanaume akasettle vizuri tu, lqbda kama na wewehutaki..

CC: min -me
I'm just a messenger 😅😅
 
Nakataaa kabisaaaa hata kwenye mahusiano kama hakuna mawasiliano Mazur basi ujue hakuna Mapenzi ndo yaliyomkuta huyo bint na mama yake no communication na baba ndiye chanzo
Sawa mkuu,
Ila kama una uzoefu tuliopìtia, mama aliyeolewa anapoteza connection na watoto wa mwanzo ambao hakai nao. Haijalishi mazingira...
 
Niseme tu mimi ni single father wa binti mmoja , japo nilisha sema nawakiume mkubwa ila ni stori ndefu mpaka kufanya maamuzi ya kubaki na binti yangu tu.

Binti yangu nilianza kukaa nae alipo timiza miaka miwili baada ya kuvutana na mama yake mno.

Ila mama yake alipo pata mtu mwingine wa kumuoa ndoa kabisa, baada ya mimi kupeana nae talaka , ikawa rahisi sana kunipa binti yangu .

Nilimlea binafsi , alipo kua alienda kwa bibi yake na sasa yupo shule ya kulala anaendelea vyema.

Shida inakuja , baada ya binti ya kuwa mkubwa kiasi , naona kama hana bond na mama yake , wala hana hisia nae kabisa 🥲 , sikupenda hii hali ijitokeze kabisa , yani hata ukimwambia wewe unafanana na mama yako vitu fulani analia kabisa 🤔

Wakionana hauwezi fikiri ni mtu na mtoto wake , hii hali siipendi kwa sababu sijawahi kumsaigia kunguni mama watoto wangu kwa mwanae kabisa , tunaelewana kama wazazi na hata yeye ana shiriki matunzo ya mwenetu.

Hii hali imekaaje wadau , na nina weza fanya vipi nikaweka ukaribu wa binti yangu na mama yake 🤔.
Mkuu kwanza pole ila pia usiumize kichwa kwa vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wako,kwa kifupi anaetakiwa kujenga ni mama yake sio wewe hapo ni sawa sawa na kulazimisha maji kupanda mlima, upendo hauitaji msaada toka kwa third part ni kitu cha baina ya watu wawili period, sasa kama mama mtu hawezi kujenga huo upendo asitegeme mtoto kuujenga
 
Back
Top Bottom