SACO
JF-Expert Member
- Jul 25, 2011
- 2,902
- 3,829
Amehitimu form four mwaka jana kwa msaada wa mfadhili ambae kwa bahati mbaya alifariki akiwa katikati ya masomo, hivyo kafanikiwa kumaliza kidato cha nne kwa kuungaunga tu lakini alifanikiwa kupata division one na kachaguliwa kwenda kusoma kidato cha tano Arusha. Ana mama yake ambaye hana uwezo kabisa kuweza kumlipia gharama za masomo na hana ndugu mwenye uwezo. Nimeingiwa na huruma kutokana na uwezo alionao kimasomo na ndoto zake kuvunjika kabisa.
Mimi nilitamani kumchangia lakini nimeshindwa kutokana na mimi mwenyewe kusomesha ndugu na watoto hivyo nimeona mzigo sitauwezo. Hivyo kwa yeyote mwenye uwezo naomba amsaidie kwani shule zimeshafunguka, binti yupo Mbeya hata nauli tu ya kumfikisha Arusha ni shida