Kuweni makini na vibanda vya huduma ya pesa kwa njia ya simu, wengi hutoa hela mbovu

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,121
27,128
Ni kama vile huwa wanaambiana au wanapeana semina.

Hii imenitokea mara nyingi mpaka nilipo anza kuchukua tahadhari. Hii inawahusu zaidi wanao toa kuanzia laki 2, 3 na kuendelea lakini pia hata wanao toa chini ya hapo inawahusu pia. Ni hivi ukienda kutoa hela kuanzia lets say laki 2 au 3 nakuendelea, lazima utamiksiwa kama sh elfu 20 hivi mpaka 30 ambazo ni mbovu.

Utakuja kustukia wakati unafanya manunuzi unatoa hela mbovu muuzaji anakwambi ni hela mbovu. So unabaki unajiuliza hii hela mbovu nimeitolea wapi bila majibu.

Kuna siku iliwahi kunitokea nimetoa kama laki nne na ushee naamka asubuhi nagundua kama sh. Elfu arobaini hivi ni mbovu. Siku hiyo nilikuwa na mishe town nikaenda town asubuhi nikarudi jioni nikamwambia mwenye kibanda anibadilishie hiyo 40 n.a. alibadilisha bila hata ku complain kwa sababu alikuwa anajua alicho kifanya.

Mimi nahisi huwa wananunuaga hela mbovu halafu wanawapiga watu mabomu kwa staili hiyo.

Ukienda kutoa hela kwenye kibanda cha huduma ya pesa kwa njia ya simu hakikisha unazihesabu na kuzihakiki kwanza usije kupigwa bomu.
 
Naona labda utakua umechukulia tofauti mkuu ila kupewa pesa mbovu/chakavu sio kosa hasa kwa hivi vibanda vya huduma za kifedha.

Kwenye bandiko lako ungekua umesemea official branch za kibank, Mawakal wakubwa au bank kwenyewe basi ningeungana na wewe ila kwa vibanda vya mpesa wala sio kosa kutokana na mazingira.

Hua kuna semina za mawakala hupewa hasa wale wakubwa, kua hawapaswi kukataa pesa chakavu iliyo kwenye sifa za uhalali, wao wanapozipokea hutakiwa kuzitenga na uziwakilisha kwa wakala wakuu na mwisho hurudi bank kuu ambapo hubadilishwa kwa thamani ile ile na hurudishwa kupitia mabank zikiwa mpya.

Kimsingi hupaswi kukataa pesa as long as ni halali maana pesa ni mali ya serikali kwaiyo sisi jukumu letu nikutumia itapofika kwenye system za wahusika zitakua eliminated automatic.
 
Hela mbovu ni ile isiyo na namba za usajiri tu.

Kama zipo hiyo ni hela halali kwa malipo,kuchafuka ama kuchanika hakuiondolei pesa thamani yake,usijejaribu kukataa malipo kwa kigezo cha hela chafu au imelegea.
 
Mangi haelewi hizo mkuu
 
Naona labda utakua umechukulia tofauti mkuu ila kupewa pesa mbovu/chakavu sio kosa hasa kwa hivi vibanda vya huduma za kifedha.

Kwenye bandiko lako ungekua umesemea official branch za kibank, Mawakal wakubwa au bank kwenyewe basi ningeungana na wewe ila kwa vibanda vya mpesa wala sio kosa kutokana na mazingira.

Hua kuna semina za mawakala hupewa hasa wale wakubwa, kua hawapaswi kukataa pesa chakavu iliyo kwenye sifa za uhalali, wao wanapozipokea hutakiwa kuzitenga na uziwakilisha kwa wakala wakuu na mwisho hurudi bank kuu ambapo hubadilishwa kwa thamani ile ile na hurudishwa kupitia mabank zikiwa mpya.

Kimsingi hupaswi kukataa pesa as long as ni halali maana pesa ni mali ya serikali kwaiyo sisi jukumu letu nikutumia itapofika kwenye system za wahusika zitakua eliminated automatic.
Kuna taarifa muhimu za kwenye noti ambazo zikikosekana hata benki wanakataa hizo noti.

Kuna namba za noti na baadhi ya alama za utambulisho kama hazipo hakuna mahali hiyo noti itakubalika.

Mathalan, iwapo kama noti haina namba, huwezi kuipeleka hata Benki Kuu kwa sababu haijulikani ni noti namba ngapi imeharibika ili iweze kufyatuliwa mpya.

Mimi ni mdau wa kukusanya mapato. Kwa hiyo noti zinapita sana mikononi mwangu.
 
Back
Top Bottom