DOKEZO Serikali, elezeni ukweli kuwa watoto chini ya miaka 5 wanalipia huduma, kama sivyo kituo cha afya Kimara wawajibishwe kwa kutoza pesa na huduma mbovu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mawele

Member
Jul 25, 2023
30
116
Leo nilifika kituo cha afya Kimara baada ya ndugu yangu kuniita nikalipie gharama ili mtoto wake apatiwe matibabu baada ya kuanguka na kuumia mguu.

Picha linaanza kuingia kwa daktari, mama wa mtoto anaeleza mwanaye kaumia baada ya kuaguka wakati anacheza, dk bila hata kumgusa wala kumwangalia mtoto akatoa jibu, NENDA KAMCHUE NA UMPE NA DAWA YA MAUMIVU!

Mama wa mtoto akamwambia dk nishampa dawa ya maumivu na kumchua ila hakuna matokeo mazuri, dk akasisitiza aende, ikabidi mama wa mtoto alazimishe kuomba dk aandike akapigwe X-ray, cha ajabu dk. anakubali ila anamuuliza mama wa mtoto unataka apigwe picha wapi, mama akamwambia mkague ili uone ni eneo gani hasa maana alipoumia mguu ulivimba na hataki kuguswa, dk akarudia tena we sema apigwe wapi mama wa mtoto ikabidi ajibu apigwe picha mguu mzima.

Daktari akaandika kwenda kwenye picha(X-ray), kufika huko mama wa mtoto akiwa na kadi ya kliniki akijua huduma ni bure, anaambiwa anatakiwa kulipia 15000 kwa ajili ya kupata huduma hiyo na hakuwa na hela hapo maana Serikali kutwa inaimba huduma ya matibabu chini ya miaka 5 ni bure, huku wananchi wanatozwa pesa.

Nikaenda nikapewa namba nikalipia japo mwanzo hawakutaka nilipie kwa namba ya malipo walitaka niwape pesa taslimu nikakataa, ili kuonesha ni malipo halali ya serikali hivyo sina shaka kuwa serikali inawadanganya wananchi kuwa huduma za matibabu chini ya miaka 5 ni bure na huku wanalipa na hii ni risiti halali ya malipo.

Risiti.jpg

Baada kupiga picha kurudisha majibu kwa Dk, akasema kavujika mguu kwenye paja, na apewe 50000 ili mtoto afungwe PoP, nikasema hiyo hela ni ya nini? akajibu ni ya kununua vifaa na gharama ya kufungia, nikasema nipewe namba ya malipo nilipe, dk akakunja sura mara mbili zaidi maana tangu mwanzo alishaonesha chuki.

Dk akasema hapa hakuna vifaa ni vya kununua na gharama yake ni 32,000 nikamwambia niandikie nikanunue mwenyewe, akaandika huku anasema kwa hiyo umeamua kwenda kununua mwenyewe sawa kanunue.

Nikafika duka la dawa nikapata vifaa kwa gharama ya 11500, nikapata hisia huenda alikuwa kashapiga hesabu zake juu ya hela ya kunuua vifaa ndio maana sura ilibadilika na kuuliza kama nimeamua kwenda kununua mwenyewe.

Niliporudi kwa Dk. akasema nikalipie gharama ya huduma ya kufunga, nikaenda mapokezi kulipia nao vilevile wakataka niwape pesa taslimu nikagoma ndipo wakanipa namba ya kulipia nikalipa sh, 20,000.

Risiti 3.jpg
Je, Serikali kwa nini mnadanganya matibu bure kwa watoto chini ya miaka 5? Kama si kweli hamdanganyi ni kwa nini kituo cha Kimara watoze pesa ambazo zinakuja Serikalini?

Wafatilieni watoa huduma wa Kimara, wana lugha mbaya na wanatoa huduma mbovu, na hawako makini kabisa maana wakati nipo pale kuna mama mmoja alikuwa karudia kupiga picha mara ya pili baada ya mwanzo kupigwa uti wa mgongo na wakati yeye anasumbuliwa na kichwa!

Pia wanataka walipwe pesa wao na si kwenye mfumo wa malipo.
 
Nchi imejaa uhuni hii. Ccm wanaongea mambo mazuri sana majukwaani kuwahadaa wananchi. Maana wanayoyaongea hayana baraka za kisheria, kannuni na waraka. Ili jambo lifanyiwe kazi ni lazima yatungiwe sheria na kanuni kisha waraka utumwe kwenye taasisi na ofisi zote.
 
Welldone mtoa hoja hii,nimefurahishwa mno na push back yako, hujaja humu kulalama kama wengine, umetuonyesha kuwa wewe sio mtu wa ndio ndio, it's sad yanayotokea kwa poor of the poorest, wao kitenzi dume kidogo wanakimbilia USA (kwa mabeberu, wanaogopa kufa pale, Frelimo hospital)
 
Nchi imejaa uhuni hii. Ccm wanaongea mambo mazuri sana majukwaani kuwahadaa wananchi. Maana wanayoyaongea hayana baraka za kisheria, kannuni na waraka. Ili jambo lifanyiwe kazi ni lazima yatungiwe sheria na kanuni kisha waraka utumwe kwenye taasisi na ofisi zote.
Umeanzaje kuiamini serikali ya ccm ?
Shida yenu kila kitu mnaleta siasa.. namsifu mtoa mada ameonyesha mfano kufichua maovu badala ya kulalamika pembeni
 
Kinachoelezwa kuwa waraka upo wa upokeaji matibu kwa mama wajawazito na watoto chini miaka 5 upo katika hospital za selikali na zahanati zake Ila selikali haipeleki fedha kwenyw ospital kufudia gharama za mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka 5 bila kujali kuwa kina mama ndio mtaji mkubwa ifikapo wakati kampen za changuzi mbalimbali hupatia ushindi kupitia kwa wake zetu dada, bibi, zetu,waraka umekuwa wa magumashi hata bungeni Kuna mbunge Aliza awali Hilo wizara ya afya kupitia kwa waziri akajibu awali kisiasa tu
 
Walishaambiwa mtazame mzazi wa mtoto je anajiwezaweza? Km anajiweza lipisha. Ukiona hohehahe kabisa usimlipishe. Nimekubia siri
 
Huyo daktari na mphamacia lazima watolewe kafara kwa kufukuzwa au kusimamishwa kazi lakini ukweli ni kwamba ukisikiliza sana wanasisa mgonjwa wako lazima afe….serikali haipeleki hela wala vifaa tiba na madawa ya kutosha kwenye hospitali na vituo vya afya!

Hakuna huduma ya bure kinyume na hapo mginjwa wako anakufa….mtawaonea bure tuu hao
 
Leo nilifika kituo cha afya Kimara baada ya ndugu yangu kuniita nikalipie gharama ili mtoto wake apatiwe matibabu baada ya kuanguka na kuumia mguu.



Pia wanataka walipwe pesa wao na si kwenye mfumo wa malipo.
Tuvumilie tu,tupo chini ya failed state!
 
Hakuna kitu kinaitwa matibabu Bure bila utaratibu.Watanzania tusipende dezo, serikali inanunua dawa,wahudumu na mazingira ya matibabu ni hela.Ukate kiuno huko na kumwagia ndani halafu serikali ikulipie.

Upo utaratibu maalumu wa kupata matibabu bure, kawaone maafisa ustawi wa jamii watakupa utaratibu.Bure ni hewa tu tena kama utakuwa na uwezo wa kuivuta na kuitoa mwenyewe otherwise unalipia.
 
Leo nilifika kituo cha afya Kimara baada ya ndugu yangu kuniita nikalipie gharama ili mtoto wake apatiwe matibabu baada ya kuanguka na kuumia mguu.



Pia wanataka walipwe pesa wao na si kwenye mfumo wa malipo.
Huduma bure kwa under 5 ni kama imekaa kisiasa hivi, in short kiuhalisia haitekelezeki kwa sababu ya gharama za matibabu. Hospitali zinahitaji dawa na vifaa Tiba ili zijiendeshe. Na mara nyingi kwa hizi za ngazi ya chini bajeti wanapanga kupitia mapato yao ya ndani.

Kunakuwa na changamoto kubwa kutoa hiyo " misamaha" ndio maana pia ukifatilia kunakuwa na " Referral case" nyingi za " under five" kupeleka kwenye hospital za rufaa za mkoa ili kukwepa hiyo the so called " exemption/ misamaha " kwa underfive kwa kuwa kiuhalisia zinaleta mizigo.

Kuna hosp fulani ilifuata hiyo sera kwa muda fulani ikajikuta mapato ya mwezi ni m50 ila kati ya hizo m50 , m40 ni misamaha na wameamua kukaza sasa maana inakuw mzigo coz hosp ndio inaumia. Suluhisho la hili ni moja tu BIMA YA AFYA KWA WOTE ili kuondoa haya mambo.

Kama una uwezo wa kulipia huduma ni bora ukalipia tu na ni kweli wengine wapo wapigaji , so unapolipia huduma , hakikisha unadai risiti kama ulivyoomba hapo.
 
Hiyo wizara na Tanesco lao ni moja, unaambiwa umeme vijijini gharama yake ni sh 27,000 nikawauliza hata nikihitaji nguzo 8 ili nifikiwe umeme nitalipa hiyo sh 27,000? Jibu lao ni kuwa sisi tunajua umeme ni sh 27,000 tu.Ajabu ni kwamba hata anayehitaji nguzo 1 hawawezi kumpa umeme kwa sh 27,000 ila akilipa zaidi ya milioni umeme anapata.Hizo wizara 2 ni waongo waongo sijawahi kuona.
 
Leo nilifika kituo cha afya Kimara baada ya ndugu yangu kuniita nikalipie gharama ili mtoto wake apatiwe matibabu baada ya kuanguka na kuumia mguu.

Pa mara ya pili baada ya mwanzo kupigwa uti wa mgongo na wakati yeye anasumbuliwa na kichwa!

Pia wanataka walipwe pesa wao na si kwenye mfumo wa malipo.
Hiyo email iliyopo kwenye risiti ndio ya hospitali au ya mtu binafsi?
 
Hiyo email iliyopo kwenye risiti ndio ya hospitali au ya mtu binafsi?
Hiki ni kituo binafsi, kituo cha Serikali hakiwezi kuwa na E-mail hiyo! Ila si unajua wabongo wanavyopenda kuilalamikia Serikali!
 
Back
Top Bottom