Uzi wa kuweka mikasa ya utapeli wa mali, pesa kwa njia mitandao

Sanyambila

JF-Expert Member
Jan 24, 2018
339
457
Wajumbe wa kikao aka mkutano, habari zenu na poleni na majukumu.

Leo nimekuja na agenda hiyo juu kuhusu utapeli wa kimtandao na wa rejareja wakati maisha yakiwa magumu huku kuna watanzania wenzetu wanapiga hela kwa wenzao kwa kutumia uongo uliokaribu na ukweli. Kuna utapeli wa wa aina nyingi tusaidiane kuweka wazi ili tuwaokoe wenzetu hasa wa vijijini.

Mfano 1.Tapeli: "Mtoto wako amezidiwa akiwaa shuleni Mimi ni mwalimu sasa tumekodi Tax na huduma za hospitali gharama ni sh.100,000/= tuna haraka kwa namba hii...

2. Tapeli anajifanya ni Customer Care wa Vodacom M-PESA: "Kuna mteja katuma pesa kimakosa" ukisasema hujaionna wanatuma pale pale ukikata asimu unaiona Meseji ya ku-forward ikikuambia umepokea kiasi. Hapo hakupi muda mrefu wa kutafakari anakupigia anakwambia nenda kwa wakala katume, ukienda umepigwa. Msala wa kwako na Wakala.


Tuma hiyo hela kwa namba hii haraka n.k

Toa shuhuda ilikuwaje. Ulitapeliwa au ulipata kuona kwa jirani, rafiki. Je, hatua gani zichukuliwe ili kudhibiti janga hili? Kwa ufahamu nahisi mitandao, yaani wafanyakazi wa mitandao wanahusika (Vodacom, Airtel, Tigo, Halotel nk.) maana ukipiga simu wanaishia kusikitika tu wakati wana uwezo wa kuifunga laini mapema. Sasa laini moja inatapeli watu 10, kama so wahusika ni nini?

TCRA NDO WAMECHEMKA

Sasa tuwaumbue matapeli tuweke mbinu zao hapa na namba zao. Ukitapeliwa njoo weka mkasa fasta ili wengine washituke. Weka mbinu za matapeli hapa na namba wanazotumia, mkasa, shuhuda za utapeli n.k.

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom