YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,908
- 51,904
Kilio cha wadau cha kutaka kurahishwe njia za kupokea pesa zimeanza kusikilizwa
Sasa hivi Mteja wa vodacom mwenye Mpesa Sasa waweza pokea pesa toka nchi za nje kwenye simu yako ukitumiwa kwa njia ya World Remit,Money Gram na Juba express.
Kama una mtu nje na una namba ya vodacom yenye Mpesa mwambie akutumie kwenye namba yako ya simu pesa zitaingia kwa hela za Tanzania na zitakufikia kwenye simu yako popote ulipo hata porini kijijini na utazitoa kwa wakala kwa wakati wako au ukitaka ku zi deposit kwenye akaunti yako ni wewe tu Pesa inakuwa kiganjani mwako
Tunashukuru kwa hatua hii kubwa
Tunaomba pia serikali iruhusu watu kupokea pesa kupitia Paypal kwa sababu:
Tanzania kumekuwa na tatizo kubwa la ajira. Njia moja ya kuondoa hilo tatizo ni kwa watu kutafuta kazi za kufanya online, yaani mitandaoni. Kazi zipo nyingi. Mfano, waweza pata kazi ya kutafsiri website ya kampuni au mtu kwa Kiswahili au kutafsiri kitabu. Unafanya online malipo yanakuwa kwa njia ya PayPal hata kwenye simu yako ya mkononi, hata mwajiri au mnunuzi awe Ulaya au Marekani
Pia, mtu waweza chora hata katuni, ramani za nyumba n.k ukauza online. Au, ukajitungia wimbo wako wa kienyeji binafsi nyumbani kwako bila hata kwenda studio, ukauweka kwa mfumo wa video au audio ukauuza online kwenye maduka kibao ya online.
Tatizo kwa Tanzania haijaruhusu matumizi ya kupokea pesa kwa njia ya PayPal ambapo mtu aki-click tu kununua bidhaa yako, pesa yako inaingia chapchap kwenye PayPal account yako.
Kenya walisharuhusu; vijana wengi hushinda mitandaoni wakitengeneza pesa wakiuza bidhaa zao, viwe vichekesho, michezo ya kuigiza n.k ambavyo huviuza online. Wanaweka clip zao kwenye maduka ya online mtu ananunua anamlipa online kupitia Paypal.
Kuna shughuli nyingi za ujasiliamali online. Kikwazo kwa nchi yetu ni upataji wa pesa wa kazi yako au mauzo yako online. Bado tuko enzi za mawe tukiamini minjia ya kizamani ya kupokea hela. Na hivyo kuifanya nchi yetu kuwa ni ya kulipa zaidi pesa za kigeni na si ya kupokea pesa za kigeni.
Serikali ikiruhusu upokeaji pesa kupitia PayPal itafanya vijana wengi waingie mitandaoni kutafuta pesa
Biashara za online zaweza kufungua Watanzania wengi kupata pesa toka nje, sababu ni juhudi ya mtu binafs na ubunifu wake tu auze nini. Waweza kujirekodi unarukaruka kama ngedere ukiimba hovyohovyo tu bila hata vyombo halafu ukaita wimbo Crazy Monkey Song ukauweka online na ukauza. Wapo watu wana pesa wanapenda vituko wananunua.
Taasisi za elimu nazo ziweke kwenye mitaala ujasiliamali wa online wasibakie tu kufundisha ujasiriamali wa kuzurura tu juani wa kimachinga