Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,815
- 4,565
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Bukoba Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, amesema itakuwa ni jambo la ajabu kwa Tanzania kutochangamkia fursa ya kumpata mwekezaji mwingine katika bandari ili kuleta ufanisi wa utendaji na mapato.
Karamagi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kagera, ameyabainisha kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kanda ya Ziwa hivi karibuni na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Daniel Chongolo.
"Mimi ni Karamagi ambaye ni mwasisi wa kampuni ya TICTS ambayo wameizungumzia sana. Serikali zetu zote hazijafanya makosa katika uwekezaji ili Taifa letu linufaike. TICTS ilifanya kazi vizuri, ingawa kwa sasa tulipofikia Serikali imesema basi hebu tujaribu na wengine, jambo ambalo si baya,” amesema.
Amesisitiza umuhimu wa Tanzania kuchangamkia fursa ya mwekezaji mwingine atayakeboresha utendaji kazi na ufanisi wa bandari hiyo, huku ikitumika kimkakati kuongeza mapato ya nchi.
“TICTS wakati inaingia, bandari yetu ilikuwa na shehena ya makontena 70,000 kwa mwaka. Sasa hivi ni 700,000 kwa mwaka. Lakini tulipofika hapa, mkataba wetu ukafika mwisho. Sisi hatuna matatizo na hilo…nchi kwanza. Kwa sababu kuna mkakati mkubwa tunaweza kuwekeza sehemu nyingine,” amesema.
Akizungumza falsafa ya biashara, Karamagi amesema: “Serikali imewekeza zaidi ya Sh1 trililioni kwenye uboreshaji wa bandari gati 0 mpaka namba saba, mpaka leo hii, eneo hili linachangia kwa asilimia 15 ya makontena yote yanayotoka bandari ya Dar es Salaam.”
“Kwa mkopo mkubwa kama huu na watu binafsi wapo, ambao wana uwezo wa kuwekeza, kutulipa kodi na mafao mengine, tukalipa deni hilo, alafu tukapata faida ya kuendeleza maeneo mengine, tutakuwa wajinga wa mwisho kama hilo hatutalichukua.”
Karamagi anayeamini katika falsafa ya biashara, alisema Tanzania inahitaji uwekezaji wenye manufaa utakaosaidia nchi kuitumia bandari kimkakati kuwa mojawapo ya vyanzo vitakavyoongeza mapato.