Rostam Aziz: Sekta Binafsi ilishakubalika na Serikali kwamba Jukumu la Kufanya Biashara ni la Sekta Binafsi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,984
142,002
Shujaa Magufuli alishatoa angalizo kwamba Vita ya Uchumi ni mbaya sana

Nimemsikia Bilionea Rostam Aziz akisema Sekta Binafsi ilishakubalika na Serikali kwamba Jukumu la Kufanya Biashara ni la Sekta Binafsi na Jukumu la Serikali ni Kukusanya kodi na kutoa Huduma

Sasa kama tayari kuna makubaliano hayo Bunge letu halitaweza kufanya au kuzuia chochote kwa sababu Wabunge na Mawaziri wakiwa mmoja mmoja wote ni Wafanyabiashara siyo kama enzi za CCM ya " Jembe na Nyundo"

Aziz ameongea Ukweli mchungu!

Mungu wa mbinguni awabariki!
 
Sawa uchumi kuendeshwa na sekta binafsi na Serikali iwawekee mazingira rafiki, lakini si sahihi kupora haki hiyo wakapewa wawekezaji kutoka nje. Wazawa wawezeshwe na wageni waingie ubia nao na si vingenevyo.

Ni hatari Serikali kuingia mikataba na sekta binafsi za kigeni, km DPW kupitia mgongo wa nchi yake badala ya mkataba kati ya DPW na TPA. Kufanya hivyo kunanyima fursa ya kukua kwa Sekta binafsi nchini. Ni dhahiri kunakuwa na harufu ya ufisadi
 
Back
Top Bottom