Kuwa introvert ni tabu sana!

Kuwa introvert ni tabu sana!

Ukubwani huku my introvency naona ndo inazidi
Mimi ni maua, pets , kupika na social media
Naweza kumaliza likizo ya siku 28 nikiwa nimetoka nje mara 4 tu, nazo ni kanisani paap(napo nitatafuta kona nitakayokaa mostly mwenyewe.
Sipendi kwenda harusini wala kwenye watu wengi popote.
Nikifika vituoni, sokoni kuna namna nasikia kubanwa pumzi.
The only place ninajiona niko happy, full and peace ni nyumbani kwangu.
Inanipa peace ya kutizama mimea yangu, wanyama ninaofuga, nachora sometimes, nafuma occasionally yani kwa ujumla mimi najiona kabisa Ulimwengu unajikamilisha ndani ya nyumba.
Kipindi cha working from home was my best working moment.
Watu tuongee ila muwe huko huko mliko like this, sending email, kuchat(sipendi pia simu , iwe kupiga na kupigiwa)
Sipendi video calls(kama wewe sio mwenzi wangu usinipigie video call, sitaki kukuona sitaki unione while talking, just send a text nitakujibu, maana sipendi hata mlio wa simu. Hata yeye anajua sipendi video calls, na simu ni vile tu ndiyo mawasiliano.
Ninaweza kuwasiliana kwa maandishi zaidi(nina uwezo wa kuchat hata na watu 10 kwa muda mmoja na hakuna atakayefeel siko makini nae!)

Weird i know, but with my age sijioni nikibadilika.
Sina opportunity yoyote ninakosa, links zangu zinajikamilisha kunifanya niishi , as sina tu ndoto ya utajiri, ninataka tu kumudu maisha yangu binafsi na ya familia, which nimeweza hizo zingine sioni ni my cup if tea.
 
Unaweza kushinda ndani kama jini nani sijui!, Halafu ukitoka nje dakika mbili tu unatamani tena kurudi ndani.. mbaya mbovu introvert tunaujinga huu.

Naweza nikawa nataka kutoka na wewe umekaa sehemu nayotaka kupita naweza nikasubiri mpaka utoke ndo namimi nipite!, mitabia myengine sijui ya wapi tu!..

Huku mitandaoni tumejazana maana ndo sehemu tunaweza hata kumtishia mtu kumdunda!, ila huku ana kwa ana hata kutukana tu ni kasheshe!.

Ndo viumbe pekee vinakaa mji fulani ila vinajua mitaa michache sana maana kutembeatembea sio pendeleo sana kwao!.

Mzazi mwenye mtoto wa aina hii usimsokote sana mwanao kumlazimisha achanganyikane na watu!, wakati wake ukifika atachanganyika na atachagua wakuchanganyika nao!.

Pili mfatilie ila usimfatilie sana mpaka ukaziba uhuru wake ambao ni amani yake!, utamkosesha kujiamini hata akiwa peke yako atakuwa anaona kama unamuangalia 24/7.
Usiruhusu mtu mwengine ambae hazijui hulka za mwanao amsumbue hovyohovyo bila sababu za msingi.

Jua vitu anavyovipenda ukiweza mpatie kadri uwezavyo kwa vipimo vya wastani, usimzidishie.
Introvert wengi wana hulka ya uoga na akikuwa hiyo hulka ikakomaa ndo inamvaa na kumsababishia "anxiety".

Hivyo hakikisha akiwa bado mdogo mpe kazi ambazo zitaongeza ujasiri wake, sanasana hakikisha anakuwa anafanya zile kazi ngumu kiasi na pia uwe unampa maneno ya kumtia moyo ya kwamba anaweza!. jitahidi kumsoma hali zake maana ni mabingwa wa kuficha!, hivi ndo viumbe vinaweza kutunza siri mpaka kufa!.

Mwisho kuwa makini na namna unavyoenenda nae maana anaweza akawa anakushinda hata utafakari!, usimtake ajielezee sana bali kama ni kitu cha kufanya muache afanye!, maana huwa si wazuri sana kwenye kujieleza ila kutenda wapo smart sana!.
HAKUNA SIRI TENA!!
 
Mimi naweza kukaa wiki bila kutoka kabisa mfano Toka niliporudi Toka ibadani jmapili mpaka Leo sijatoka hata hapo nje, kazi zangu nafanyia nyumbani
 
Kijana wangu ni introvert, nilipata kazi sana kumuelewa huko nyuma, nimekuja kuelewa kua ni intovert akiwa secondary school, yani ulivuoongea vyote kuhusu intovert ni kama unamjua mwanangu, yani umemsema yeye kila kitu, hadi nikahisi au ana tatizo anaficha. Now hua namuacha tu na mambo yake japo sometimes anakera sana, mtoto gani anapenda kua peke ake mala nyingi, busy na cm au computer au chumbani kwake anaangalia tv, but is not good kiukweli, hata akiwa na tatizo huezi jua
introvert huko majuu wengi wao ni huckers na data analytics
 
nilipanga nyumba nzima peke angu, kwa pembeni kuna wapangaji wengine ila wote tuko ndani ya kiwanja kimoja na father houce yuko mbali na sisi na sikuwai kumuona zaidi kuongea kwa phone,

nikitoka asubuhi narudi night, kwa kifupi nlikuwa sipiki kabisa nakula magengeni tu nikirudi home nimeshiba😁,, jirani zangu walikuwa hawanielewi kama nimeoa au bachela,,

weekend ndio wananiona nikifua nguo, unahisi kabisa watu wanataka story na mimi lakini sasa mtu mwenyewe sina mda 😁,,

natamani niendelee kuandika lakini naona ivivu 😁
 
Na kuna wengine wanakuogopa mpk akiwa anajambo anataka kulifikisha kwako anajiuliza aanzie wapi...🤣
Yaani, ilichukuwa muda mrefu wakwe zangu kunielewa. Nashukuru sijawahi kuwa fake au kulazimisha uchangamfu, wanaona poa tu na imenisaidia kuepuka lawama. Kusema kweli michanganyiko ya watu ipo very draining. Unahitaji muda mreeeeefu kukusanya nguvu tena kufanya shughuli inayohusisha kuchanganyika na watu
 
Sisi ndo wale tunahairisha appointments, Bora tulale nyumbani.

Sisi ndo wale tunabore ile mbaya tukikutana physical kama hatujakuzoea

Sisi ndo wale long distance relationship zetu zinalast kuliko kuishi wawili pamoja.

Sisi ndo wale mimea na wanyama inatuelewa zaidi kuliko binadamu

Sisi ndo gallery zetu zimejaa picha za mawe, milima, miti, wadudu, majengo, vyakula.

Sisi ndonwale tunajua mashairi ya nyimbo zote.

Sisi ndo wale tunasoma vitabu vingi kwa walati mmoja.

Sisi ndo wale tunaweza sana kazi za kibunifu na za mifumo.
KENZY ongeza na hizi
 
Sisi ndo wale tunahairisha appointments, Bora tulale nyumbani.

Sisi ndo wale tunabore ile mbaya tukikutana physical kama hatujakuzoea

Sisi ndo wale long distance relationship zetu zinalast kuliko kuishi wawili pamoja.

Sisi ndo wale mimea na wanyama inatuelewa zaidi kuliko binadamu

Sisi ndo gallery zetu zimejaa picha za mawe, milima, miti, wadudu, majengo, vyakula.

Sisi ndonwale tunajua mashairi ya nyimbo zote.

Sisi ndo wale tunasoma vitabu vingi kwa walati mmoja.

Sisi ndo wale tunaweza sana kazi za kibunifu na za mifumo.
KENZY ongeza na hizi
mulemule...
 
Kwahiyo JF wote ni introvert, maana mmetaja tabia zangu zote.
inawezekana!
Introverts huweza cyber connections, mambo ya physical sio kabisa! So asilimia kubwa swali lako ni kweli
Extrovert na mambo ya kuchekea na hamuonani wapi na wapi. Ni intorvet tu mnaweza kudate, kuzaa watoto, kuachana na kupeana companyi mkiwa hamuonani na wakawa tu sawa!
 
Mnajipa labels za kijinga na kuona sifa. Kila mtu siku hizi ni introvert. Mna upumbavu endelevu.

Binadamu yeyote anaweza badilika tokana na mazingira.
Anaweza kuwa mpole au mchangamfu.
Kuwa katili au na huruma.
Kuwa boring au mcheshi.
Etc etc.

Hizi ni traits na binadamu yeyote yule wa kawaida has nothing to do with those stupid labels ili kujiona special. Mna upumbavu endelevu nyie vitoto.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom