Kuwa introvert ni tabu sana!

Kuwa introvert ni tabu sana!

Nilikuwa introvert mzee, naishukuru pombe imenitoa huko. Hiyo hali ni kama uchizi, unawezajikuta psycho kimasikhara, introvert ni kama ufala na udomozege. Kitu pekee positive introvert chakujivunia ni akili(ubunifu)

Mbali na hapo ni hali mbaya sana kuwa anti social. Kuna mstari mwembamba sana wa kuwa introvert na tabia za ajabu ajabu kama kujiua(kuwa kwenye nafasi kubwa ya kupata sonona),kuua,umasikini(introvert na self confidence ni sawa na left and right)...

Mi naishukuru lifestyle ya kiafrika angalau kwa kiasi kikubwa inaepusha hiyo hali, ila huko mbeleni hawa wakina junior nawaonea huruma sana.
True pombe husaidia kutibu hiyo Hali forever...Mimi mpaka na maliza ELIMU ya juu sikuwai kunywa Wala kutumia kilevi chochote..baada ya kuingia ULIMWENGUNI ndio Nika anza ku boost kidogo konyagi ndogo kila weekend ilisaidia Sana kuupunguza u INTROVERT WANGU up to now NAWEZA NIKA HUBIRI HATA KWENYE DALADALA 🤣😂
 
Ukubwani huku my introvency naona ndo inazidi
Mimi ni maua, pets , kupika na social media
Naweza kumaliza likizo ya siku 28 nikiwa nimetoka nje mara 4 tu, nazo ni kanisani paap(napo nitatafuta kona nitakayokaa mostly mwenyewe.
Sipendi kwenda harusini wala kwenye watu wengi popote.
Nikifika vituoni, sokoni kuna namna nasikia kubanwa pumzi.
The only place ninajiona niko happy, full and peace ni nyumbani kwangu.
Inanipa peace ya kutizama mimea yangu, wanyama ninaofuga, nachora sometimes, nafuma occasionally yani kwa ujumla mimi najiona kabisa Ulimwengu unajikamilisha ndani ya nyumba.
Kipindi cha working from home was my best working moment.
Watu tuongee ila muwe huko huko mliko like this, sending email, kuchat(sipendi pia simu , iwe kupiga na kupigiwa)
Sipendi video calls(kama wewe sio mwenzi wangu usinipigie video call, sitaki kukuona sitaki unione while talking, just send a text nitakujibu, maana sipendi hata mlio wa simu. Hata yeye anajua sipendi video calls, na simu ni vile tu ndiyo mawasiliano.
Ninaweza kuwasiliana kwa maandishi zaidi(nina uwezo wa kuchat hata na watu 10 kwa muda mmoja na hakuna atakayefeel siko makini nae!)

Weird i know, but with my age sijioni nikibadilika.
Sina opportunity yoyote ninakosa, links zangu zinajikamilisha kunifanya niishi , as sina tu ndoto ya utajiri, ninataka tu kumudu maisha yangu binafsi na ya familia, which nimeweza hizo zingine sioni ni my cup if tea.
 
True pombe husaidia kutibu hiyo Hali forever...Mimi mpaka na maliza ELIMU ya juu sikuwai kunywa Wala kutumia kilevi chochote..baada ya kuingia ULIMWENGUNI ndio Nika anza ku boost kidogo konyagi ndogo kila weekend ilisaidia Sana kuupunguza u INTROVERT WANGU up to now NAWEZA NIKA HUBIRI HATA KWENYE DALADALA 🤣😂
😂 ukitwanga nyagi ndio unakuja gundua ukiwa na akili timamu uwezi furahia hali ya uintrovert. O level mwanzoni hiyo hali imenitesa sana kuona mademu ninaowakubali mashkaji waliochangamka wanajizagamulia tu, napenda mpira ila siwezi changamana na watu kwenye kuuchambua...

Ila siku nimepiga kiroba ndio nikajua nastahili mengi zaidi ya haya, kuanzia hapo naishi fresh tu bila hata tungi. Kwakweli sitamani mtoto wangu aje pitia hali niliyopitia kwenye huo ufala. Kwangu mwanamme haifai kabisa kuwa introvert
 
We haukua introvert ila ulikua Domo zege
 
Ukitumia pombe kidogo kidogo inasaidia kuondoa na kutibu na ku unlock 🔓 hizo codes za kua introvert hatare Sanaa.
 
Unaweza kushinda ndani kama jini nani sijui!, Halafu ukitoka nje dakika mbili tu unatamani tena kurudi ndani.. mbaya mbovu introvert tunaujinga huu.

Naweza nikawa nataka kutoka na wewe umekaa sehemu nayotaka kupita naweza nikasubiri mpaka utoke ndo namimi nipite!, mitabia myengine sijui ya wapi tu!..

Huku mitandaoni tumejazana maana ndo sehemu tunaweza hata kumtishia mtu kumdunda!, ila huku ana kwa ana hata kutukana tu ni kasheshe!.

Ndo viumbe pekee vinakaa mji fulani ila vinajua mitaa michache sana maana kutembeatembea sio pendeleo sana kwao!.

Mzazi mwenye mtoto wa aina hii usimsokote sana mwanao kumlazimisha achanganyikane na watu!, wakati wake ukifika atachanganyika na atachagua wakuchanganyika nao!.

Pili mfatilie ila usimfatilie sana mpaka ukaziba uhuru wake ambao ni amani yake!, utamkosesha kujiamini hata akiwa peke yako atakuwa anaona kama unamuangalia 24/7.
Usiruhusu mtu mwengine ambae hazijui hulka za mwanao amsumbue hovyohovyo bila sababu za msingi.

Jua vitu anavyovipenda ukiweza mpatie kadri uwezavyo kwa vipimo vya wastani, usimzidishie.
Introvert wengi wana hulka ya uoga na akikuwa hiyo hulka ikakomaa ndo inamvaa na kumsababishia "anxiety".

Hivyo hakikisha akiwa bado mdogo mpe kazi ambazo zitaongeza ujasiri wake, sanasana hakikisha anakuwa anafanya zile kazi ngumu kiasi na pia uwe unampa maneno ya kumtia moyo ya kwamba anaweza!. jitahidi kumsoma hali zake maana ni mabingwa wa kuficha!, hivi ndo viumbe vinaweza kutunza siri mpaka kufa!.

Mwisho kuwa makini na namna unavyoenenda nae maana anaweza akawa anakushinda hata utafakari!, usimtake ajielezee sana bali kama ni kitu cha kufanya muache afanye!, maana huwa si wazuri sana kwenye kujieleza ila kutenda wapo smart sana!.
Unatishia kudunda watu mtandaon au co
 
True pombe husaidia kutibu hiyo Hali forever...Mimi mpaka na maliza ELIMU ya juu sikuwai kunywa Wala kutumia kilevi chochote..baada ya kuingia ULIMWENGUNI ndio Nika anza ku boost kidogo konyagi ndogo kila weekend ilisaidia Sana kuupunguza u INTROVERT WANGU up to now NAWEZA NIKA HUBIRI HATA KWENYE DALADALA 🤣😂
lakini kwenda hata kuifata hiyo pombe unaona aibu kinyama...🤣
 
Tangu kwenye uzi wa Da'Vinci miaka ile, hili nilishazungumzia introvert ni ugonjwa wa akili. Nazungumza kwa uzoefu sababu nilishakuwa huko.

Kuna mstari mwembamba sana wa uintrovert na uchizi
Sahihi kabisa. Hivi Hilo kundi wanawezaga kuwa wanasiasa?! If yes, wanawezaje kujichanganya wakati wa uhitaji wa kura?!
 
Mie bado sijijui km ni introvert au ndo nn, maana nina tabia za introvert, ila nikipata wasaa wa kuchangamana na watu wangu wa karibu, basi nachachuka kuliko wao.

Na wao huwa hawaelewi nini hiki, 😂😂😂😂
Ni introvert na ndio maana unachachuka mbele ya unaowajua!, huwezi kufanya hivyo kwa ambao hujawazoea!.
umaweza kucharuka mpk akija ambae hajakuzoea anamvuta rafiki yako pembeni anamuuliza "Mh! huyu ndo fulani..?"🤣
 
We haukua introvert ila ulikua Domo zege
Domo zege mpaka kwa wanaume wenzangu? 😂 mzee kuna mstari mwembamba sana wa udomo zege na introvert. Kuongea ni mara chache sana tena mpaka kwa watu uliozoeana nao hasa. Ajabu ni kwamba haka katabia kana bahati sana kutongozwa na mademu 😀. Introvert wengi hufuatwa na mademu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom