Kuwa introvert ni tabu sana!

Kuwa introvert ni tabu sana!

Introvert tuko wengi sana! Na jamii zetu za kiafrika sio rahisi kutuelewa!

Mimi nilikuwa napenda kukaa ndani mpaka nagombana na wazazi, eti toka nje dunia ikujue?! Unakaa ndani kama vile msukule au ndondocha! Ha ha haaa!

Bahati nzuri shuleni nilikuwa na akili sana! Yaani kipanga haswa! Nilikuwa nakamata number moja tu kuanzia primary mpaka advance! Hivyo nilipata marafiki wengi sana wakawa wananiheshimu sana, hata walimu pia walinipenda na kunizoe sana!

Maana bila kuwa na iq kubwa ya akili darasani, sijui kama ningekuwa hata na marafiki jamani, mpaka leo wale marafiki tuliosoma nao wakiniona wananisifiaga sana kwa akili zangu darasani.

Sasa kasheshe inakuja huku mtaani ambao hawakujui uwezo wako wa akili shuleni. Unaonekana unajisikia, unajitenga, mtu wa kujiona! Maana wao wanataka uwazoee na kuwafuata makwao kama wao walivyo ukienda kinyume basi wewe unajiona sana au unaringa! Kumbe ni hulka yako tu ya kutokutaka kuchanganyika sana!

Hatupendi kuongea sana lakini tukiamua kuongea tuna points sana sio poa
 
Hapana darsani mpk chuo nimekaa siti za mbele, kanisani labda nyuma kujae ila napenda kukaa siti ya pili kutoka mwisho,

Msosi nikiamua kurudia narudia,

Kuomba maji naomba Ila naangalia mazingira km yanaruhusu
Ukiona huwezi kukaa siti za mbele kanisani😊 ama safu ya mbele msikitini..

Au kuwa wa kwanza kupiga paper two kwenye misosi kwenye tafrija au sherehe..

Wengine hawawezi kukaa siti za mbele shuleni ama chuoni..usitufiche wewe ni introvert
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom