SoC03 Kutokana na Stori ya kweli: Maisha Yangu yalivyobadilika ndani ya dakika moja

Stories of Change - 2023 Competition

2018

JF-Expert Member
Jan 1, 2018
546
778
Salaam
(Namfahamu Mama nijasiri, anaondoa Utando unapodandia kuta,anatoa nyoka makatili,anapambana na majangiri wanapovamia nyumba,anaweka paa juu ya vichwa,sikuogopa njaa -nilishiba,Niliona wengine nguo za kuvaa zimechanika,wakati kwetu nyuso ziling'aa migongo ilifunikwa,Radi ilipiga wala sikujali Maana Mama alikua Simba Kwenye msitu mkali,Wapo waliozijua sifa zake japo mtaani halikuwika jina lake halikuandikwa bali. Edited from dizasta Vina Hatia V)

Nimetoka katika familia ya kawaida sana,nikilelewa na Mama pekeyake baada ya Baba yangu kufariki nikiwa na umri wa Mwaka mmoja na miezi minne kiasi cha kutokua na kumbukumbu yoyote inayohusu uhusiano wowote baina yangu na Baba.

Mama amepambana sana kama akina Mama wengi duniani kote kuhakikisha nakuja kuishi maisha ya kujitegemea na yasiyo na mateso hasa katika usomaji na aliamini elimu pekee ndio nyenzo ya kutimizia icho alichokiota muda wote.

Hivyo alipambana kwa kuanza kunipeleka twisheni kabla hata ya kuanza chekechea kwa mwalimu ambaye tulikua tumepanga nae kwenye nyumba moja (ticha Neema). Alifanikiwa ku-unlock my math-talent, pia alinisaidia niweze kujua kusoma mapema kabla hata ya kuanza chekechea na io ikawa msingi mzuri na uliokuja kuleta mafanikio makubwa sana kwenye elimu yangu ya msingi, sekondari mpaka chuo kikuu.

Baada ya kufika chuo kikuu ndipo kona kona, milima na mabonde kwenye maisha yalianza na taabu nyingi zikaibuka na kuziibua zingine ambazo pia ziliibua zingine.Kabla ya kujiunga chuo kikuu nilikua na tabia ya kujiwekea akiba ya fedha jambo ambalo nilijizoesha tangu nikiwa shule ya msingi nakumbuka nikiwa chekechea mpaka darasa la kwanza nilikua nikipata hela Kwa kupewa na ndugu au nimeuza mchanga nampa Mama anitunzie yote au sehemu ya io hela. Lengo kuu ni kwaajili ya kwenda kumpelekea bibi zawadi kipindi tunaenda kusalimia kijijini mimi na Mama au kwaajili ya matumizi yangu siku za sikukuu. Nilipofika darasa la tano mpaka darasa la saba hapo nilikua natunza hela zangu kwa ajili ya kwenda kufanyia mitihani ya jumamosi.

...............................................................................
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom