Kutoka uwanja wa Uhuru: Tamasha la CCM linalojumuisha wasanii Tanzania

Moto uliwashwa hapo noma sana.
Wapinzani wanatetemeka
IMG_20200815_222819_822.jpg
IMG_20200815_223542_892.jpg
IMG_20200815_223546_287.jpg
 
CCM imetufanya wananchi wa nchi hii tuonekane kuwa Ni wajinga kwa kudhani kuwa tunaweza kubabaishwa na nyimbo za wasanii.

Sisi tunataka mje mtuambie Ni kwanini mmetuingiza kwenye Lindi kubwa la umaskini kwa kiwango hiki.

Tunataka mje na majibu mazuri ya kutuelewesha kwanini kwa miaka mitano hamkuongeza mishahara ya watumishi wa umma.

Tunataka mje mtuambie Ni kwa nini hamkuwapandisha madaraja watumishi.

Tunataka mje na majibu ya kwanini hamkutoa ajira.

Tunataka mtujulishe Ni kwanini hamku panua masoko kwa ajili ya mazao ya wakulima.

Tunataka mje mtueleze ni kwanini mliamua kununua ndege badala ya kutuchimbia visima vya maji ili watu wa vijijini nasi tufaidi angalau hako ka keki ka taifa letu.

Tunataka mtueleze ni kwanini katika awamu hii kipato Cha mwananchi kimeshuka kwa kiwango kikubwa hivi.

Tunataka mtuambie Ni kwanini mnatumia gharama kubwa kuwalipa wasanii kwenye kampeni zenu. Nk

Ukweli Ni kwamba kwa sasa wananchi hatuna muda wa kusikiliza ngonjera na mapambio ya wasanii kuliko kusikiliza sera zitakazo tuondoa kwenye unyonge huu ambao ni dhahiri kwamba kwa kiwango kikubwa umasababishwa na utawala huu wa CCM.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
YEYOTE ALIYEWEZESHA HII ' IDEA ' NAMPA HESHIMA YAKE

Magoiga SN

Rafiki yangu mmoja ambaye ni kijana wa upinzani amenifuata inbox akiwa na lengo la kuniambia kuwa wananchi wote waliohudhuria tamasha la CCM uwanja wa Taifa jana walienda kwa sababu ya wasanii na siyo CCM, kwahiyo nisishangilie uwanja kujaa

Nilichomjibu:

Ni kweli, wapo walikwenda pale kwasababu ya wasanii na wapo waliokwenda pale kwasababu ni tamasha linaloihusu CCM ndiyo maana uliona wengi wamevaa nguo za chama, lakini kitu cha muhimu cha kukumbuka ni kwamba tamasha la jana lilihusu uzinduzi wa nyimbo 500 za kampeni za CCM zilizoimbwa na wasanii zaidi ya 200 nchini.

Nyimbo zilizokuwa zikitumbuizwa ni nyimbo zinazoihusu CCM , Rais Magufuli na utekelezaji wa ahadi na ilani ya uchaguzi tu, hakukuwa na Bedroom ya harmonize wala money money ya 20 Percent, yaani kwa lugha rahisi sana ni kwamba wananchi kwa hiyari yao wenyewe walikaa uwanjani kuanzia saa kumi na mbili asubuhi mpaka saa saba usiku wakisikiliza na kucheza nyimbo zinazoisifia CCM, kumpongeza Rais Magufuli na serikali anayoiongoza, what a milestone

Wasanii wote walipanda jukwaani wakiwa wamevalia mavazi au sehemu ya vazi yenye nembo ya CCM nk, wasanii waliwaimbisha watazamaji, kuwachezesha na kuwashirikisha ktk uimbaji wa nyimbo za CCM. Yaani kuanzia saa moja asubuhi mpaka usiku wa maneno neno CCM, neno Magufuli, neno utekelezaji wa miradi ya maendeleo, neno amani na utulivu yalikuwa yakijirudia kila baada ya sekunde kadhaa. Ukumbi mzima ulitapakaa alama za CCM, rangi ya vazi la CCM, screen kubwa jukwaani haikukauka kauli mbiu za CCM, yaani ni sawa na kusema uwanja mzima influenced kwa kijani na njano kuanzia mazingira mpaka maudhui ya nyimbo zote

Kwa lugha nyingine ni kwamba, wananchi walikuwa wakicheza nyimbo ambazo ujumbe mkubwa ulihusu ubora na uimara wa CCMkaka chama cha siasa, Rais Magufuli kaka kiongozi makini na mafanikio makubwa yaliyopatikana ktk miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa

Watu wakiwa wanawasikiliza wasanii ambao wanawakubali na kuwapenda kuanzia saa moja asubuhi mpaka usiku wa manane wakiwa wanatumbuiza ujumbe wa aina moja kuhusu CCM, Rais Magufuli na miradi ya maendeleo iliyoelekezwa huku wakicheza na kufurahia ina faida kubwa sana ktk ushawishi na afya ya akili.

Mimi siyo mwanasaikolojia lakini wataalamu wa masuala ya 'marketing and branding' wanajua vyema hii mbinu, wataalamu wa masuala ya saikolojia wanajua vyema hiki kitu, kwahiyo ukweli ni kwamba hili tamasha la CCM kuzindua nyimbo za kampeni zilizoimbwa na asilimia 99 ya wasanii wote nchini siyo kitu kidogo

Akili ya kawaida ya kibinadamu inapenda kuunga mkono upande ambao unaonekana kuwa smart, upande ambao hata wale unaowapenda na kuwaamini wanauunga mkono, upande ambao una uhakika na kile ambacho unaakifanya.

Ndiyo maana hata ambao hawakuweza kufika uwanjani walikaa kwenye TV zao kufuatilia nini kinafanyika uwanja wa uhuru, ninachoweza kusema ni kwamba tamasha hili limefuatiliwa na watu wengi sana bila kujali itikadi zao, na nyimbo zilizokuwa zikitumbuizwa jukwaani ni nyimbo za CCM, na bado waliendelea kufurahia.

Aliyewaza na kusimamia utekelezaji wa hiki kitu (hii idea) nampa heshima yake, kama ni wewe Ndugu Hamphrey Polepole BIG UP sana.

Sasa chama kitazame namna ya kuifanya hii idea iwe ya kila mwaka, angalau mara moja kwa mwaka wasanii wawe wanafanya kitu kama hiki, kama mwaka huu kinefanyika Dar es Salaam, mwaka kesho inaweza kufanyika Mtwara, au Mwanza au Arusha nk nk, burudani ni tiba, na burudani ya nyimbo za CCM ni tiba ya uzalendo.

Magoiga SN
IMG_20200816_090322_576.jpg
IMG_20200816_083108_002.jpg
IMG_20200816_090309_637.jpg
 
Bado sijamuona msanii anayeiimbia CCM kutoka moyoni kama alivyokuwa kapiteni John Komba.

Ngoja tuone labda atatokea.

Maendeleo hayana vyama!
Komba alikuwa next level. Hakuna atakae weza kum replace. Hata TOT bado wanaangaika mpaka lro lakin wapi.
 
Kuna wanaodai kuna wagombea wameanza kampeni kabla ya muda
Naomba kuuliza..lile tamasha ambalo wasaanii walizindua nyimbo ..zilikuwa nyimbo za nini?..
polepole alihusikaje?
Magufuli alipiga simu ili iweje?.

Wasaanii waliokuwa wanasema mitano tena na kuimba nyimbo za Mgombea wa CCM..yote Yale sio kampeni kabla?..
 
Hawajielewi wale jamaa, wale wasanii wote walikuwa wanaipamba CCM lakini sikumsikia mtu yeyote akikemea lile jambo, tena na kwa kunogesha tukio na Magufuli nae akawapigia simu kuwapongeza wale wasanii, kwamba nae alikubali kufanyiwa kampeni kabla ya wakati.

Ndio maana Lissu anawaambia waache kumtisha kwa vitu vya kitoto.
 
Kuna wanaodai kuna wagombea wameanza kampeni kabla ya muda
Naomba kuuliza..lile tamasha ambalo wasaanii walizindua nyimbo ..zilikuwa nyimbo za nini?..
polepole alihusikaje?
Magufuli alipiga simu ili iweje?.

Wasaanii waliokuwa wanasema mitano tena na kuimba nyimbo za Mgombea wa CCM..yote Yale sio kampeni kabla?..
Hilo tamasha lilikuwa la siku moja lakini kampeni tunaziona kwenye TBC na Chanel 10 kila uchao
 
Kuna wanaodai kuna wagombea wameanza kampeni kabla ya muda
Naomba kuuliza..lile tamasha ambalo wasaanii walizindua nyimbo ..zilikuwa nyimbo za nini?..
polepole alihusikaje?
Magufuli alipiga simu ili iweje?.

Wasaanii waliokuwa wanasema mitano tena na kuimba nyimbo za Mgombea wa CCM..yote Yale sio kampeni kabla?..
nishaulizaga hili swali kwenye uzi mmoja hivi but bado nasubiri jibu hadi leo.
 
Kuna wanaodai kuna wagombea wameanza kampeni kabla ya muda
Naomba kuuliza..lile tamasha ambalo wasaanii walizindua nyimbo ..zilikuwa nyimbo za nini?..
polepole alihusikaje?
Magufuli alipiga simu ili iweje?.

Wasaanii waliokuwa wanasema mitano tena na kuimba nyimbo za Mgombea wa CCM..yote Yale sio kampeni kabla?..
Waambieni wagombea wengine wa Urais walikatie rufaa NEC hapo tutajua mbivu na mbichi
 
Back
Top Bottom