William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
- Thread starter
-
- #601
Wakuu heshima mbele, kama tulivyoahidi kuwa tutahitimisha dataz za nec,
1. Kulikuwa na wazungumzaji wengi siku hiyo, kutoka makundi mawili yaisyokubaliana na kupendana kabisaa kama ilivyojionyesha kwenye mjadala huu wa siku ya mwisho, ingawa kati ya wote waliooongea, ni watatu ndio hoja zao ni worhty kuziweka hapa, nao ni muungwana, sendeka, na selukamba.
2. Sendeka, alianza kwa kumshambulia muungwana kwa nguvu sana kuwa anawalinda mafisadi, ndio maana wanakuwa na kichwa cha kuweza kwenda kwenye majimbo yao ya uchaguzi na kutengeneza sherehe zao kubwa za mapokezi na kulidhihaki taifa na hotuba zao chafu.
3. muuungwana alismama kujibu tena kwa hasira sana kuwa maneno ya sendeka hayana ukweli kwa sababu, kama sio yeye muungwana, el bado nagekuwa na madaraka mpaka leo, ".....ninasema kuwa siku nne kabla ya kwenda Dodoma kwenye kikao cha ile ripoti, edward alikuja kwangu na kuniomba kuwa nimpe nafasi ili ajieleze kuhusiana na ripoti, lakini nikamkatalia kata kata na kumtaka aende mbele ya wananchi kule bungeni akajieleze na kujitetea kwa sababu mimi siwezi kumsaidia....", " .....lakini kwa mshangao mkubwa akaniletea barua ya kujiuzulu, badala ya kujitetea bungeni......"
4. Ikaja zamu ya selukamba, aliyemshambulia sana sendeka kuwa ni kibaraka wa mama kilango, na kusema kuwa choko choko zote za kina sendeka na wenziwe zinaanzia kwa mama kilango, alismea kuwa "........kuna watu ambao hawaonekani kuelewa kuwa uchaguzi wa urais uliiisha zamani bado wanataka urais mpaka leo, hivi hawajui kuwa Tanzania tuna rais tayari?...."
selukamba aliwashangaza wajumbe wote kwa kauli nzito aliyoitoa kuwa anaomba kulindwa maana mama kilango (ambaye hakuhudhuria kiako siku hiyo), amemtishia sana kuwa anaweza kumpiga au kumfanyia ubaya.
5. sendeka alirudi tena na kumjibu selukamba kuwa ni kibaraka wa mafisadi na hasa el na akamuonya muungwana na njama kubwa wanaozizfanya za kutaka el awe rais mwaka 2010, "....tunajua kuwa mnajitayarisha kugombea urais mwaka 2010 sio siri sasa kama sio unafiki ni nini mwambieni tu rais yupo hapa?....", ilibidi muuungwana aingilie kati maana sasa wajumbe walikuwa karibu washkane mashati, alianza kwa kujaribu kumsafisha el lakini wajumbe wakaguna sana kwa mshangao, ndipo alipoanza kunawa mikono kama nilivyozileta jana.
6. Ishu ya Mkamba kuondolewa ukatibu ilisemwa wazi pamoja na juhudi zote za baadhi ya mafisadi kuitoa kwenye agenda na ilikubaliwa kuwa itapelekwa kwenye kikao cha karibuni cha cc kwa uamuzi wa mwisho. Na pia wanachama wote watakaobainika kuwa ni mafisadi watafukuzwa chama.
7. Mbunge wetu shujaa Mwakyembe bado hajarudi Dodoma, mpaka sasa hivi ninapoandika, akiendelea na uchunguzi wa madikatari bingwa DAr, naye Spika amewapa masaa 72 wale wote kuanzia polisi mpaka uwt waliokuwa wakichunguza ile soo ya bunge, kumpa matokeo mara moja. Sasa the showdown ya makundi haya mawili kati ya mafisadi na wengine inahamia bungeni, ambako the dataz ni kwamba kati ya siku mbili zajazo kutakuwa na mashambuliano ya kukata na shoka, kwenye mjadala wa bajeti.
Kwa haya wakuu naomba kusema ndio mwisho wa dataz kutoka kikao cha nec kilichoisha hivi karibuni, heshima mbele kwa wote waliochangia hii mada, na wale waliopitisha angalau macho yao tu, nia na madhumuni yetu ni moja tu nayo ni kuelimishana na kuhbarishana habari muhimu za taifa letu na kumuachia mwananchi aaamue mwenyewe cha kufanya, au kutokufanya. Ni muhimu kupeana za ndani kabla hazijafika kwenye media na kuwa spinned na kina Chiligati, maana sasa hata waki-spin tunawangalia kwa macho mawili maana we know the truth.
Ahsante Wakuu! tuendelee kukata ishus maana taifa liko njia panda!
Kwa hiyo data za Lunyungu kuhusu Lowassa wewe huna!
Field Marshall ES said:Wakuu heshima mbele, kama tulivyoahidi kuwa tutahitimisha dataz za nec,
1. Kulikuwa na wazungumzaji wengi siku hiyo, kutoka makundi mawili yaisyokubaliana na kupendana kabisaa kama ilivyojionyesha kwenye mjadala huu wa siku ya mwisho, ingawa kati ya wote waliooongea, ni watatu ndio hoja zao ni worhty kuziweka hapa, nao ni muungwana, sendeka, na selukamba.
HATA HIVYO...Aliyasema haya alipokuwa akimjibu Ole Sendeka...Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza zaidi kuwa yaliibuka mabishano makali kutokana na mjadala wa hoja ya Richmond,baada ya Lowassa kusimama na kujitetea kuwa alishatoa ushauri mara mbili mkataba huo uvunjwe lakini alikataliwa.
Baada ya mabishano makali, inadaiwa kuwa Rais Kikwete alilazimika kusimama na kutoa ufafanuzi na kueleza kuwa Lowassa alikuwa na nafasi ya kutoa maelezo na kutojiuzulu nafasi yake, lakini mwenye aliona kujiuzulu ndio uamuzi wa busara.
Talking about USANII ama lack of LEADERSHIP?3. muuungwana alismama kujibu tena kwa hasira sana kuwa maneno ya sendeka hayana ukweli kwa sababu, kama sio yeye muungwana, el bado nagekuwa na madaraka mpaka leo, ".....ninasema kuwa siku nne kabla ya kwenda Dodoma kwenye kikao cha ile ripoti, edward alikuja kwangu na kuniomba kuwa nimpe nafasi ili ajieleze kuhusiana na ripoti, lakini nikamkatalia kata kata na kumtaka aende mbele ya wananchi kule bungeni akajieleze na kujitetea kwa sababu mimi siwezi kumsaidia....", " .....lakini kwa mshangao mkubwa akaniletea barua ya kujiuzulu, badala ya kujitetea bungeni......"
Mkuu Fundi hatuwezi kukwepa kujadili yanayojiri kwenye tifa letu kwa kuogopa aibu, yaliyotokea na tunayo yajadili ndio hasa uwezo wetu wa-Tanzania kiakili ulipo, kwa sababu look watu waliosoma Harvad kina Obama sasa wako wapi na hawa wenzetu waliosoma Harvad kina Chenge na Mungai walipo?
Hatuwezi ku-denial uwezo wetu wa kufikiri na kuona mambo kitaifa, mkuu Fundi haya tunayoayajadili yana-reflect us as a nation, kuyakwepa kwa sababu ni aibu ni kujaribu kuyafukia sio solution yatakuja kurudi tu mbele ya safari!
.....................Tunaingia gharama kubwa (mheshimiwa lazima ataenda ulaya kuangaliwa afya yake kama vile alivyoenda Pombe) kwa imani hizi zisizo na msingi. ...............
Nchi inayumba sana. ama kweli tuko kwenye auto pilot hadi 2010
Asante MwikimbiANDREA!mwana wa chenge! nimekukosea nini mimi taifa lako? nimekusomesha hadi ndani na nje, nikakupa kiti cha enzi uweze kuwahukumu wenye haki na wakosefu, ukaamua kujilimbikizia mali za yatima na wajane! nimekukosea nini mimi taifa lako?
nikakupa wadhifa mkubwa kuwatetea hawa maskini wangu, ukaamua kuchukua chakula chao ukajilisha mwenyewe na kingine ukawatupia mbwa, nimekokosea nini mimi taifa lako?
ukaamua kuasi na kuuma mkono wako wa kulia! ukaamua kuungana na beel-zebul, ukaniasi mimi niliyekulisha ukanawiri.
tazama sasa nimekuacha! beel zebul ameamua kukuumbua, tazama sasa nimekuacha, nimekuacha uabike!
beel-zebul=shetani mkuu
Mzee wewe Nuksi....Nimekukubali.Kumbe unajua hata siri ya vile VILIO siku ile...!!!!!!!Jamaa according to the dataz ni uwt, kumbe na yeye kuna deal nyingi ndogo ndogo ambazo amewahi kukatiwa mpango hata kabla hajawa ag, na pia kwenye hili deal inasemekana kuwa amekatiwa, kwa sababu kisheria yeye ndiye aliyetakiwa kuwa mstari wa mbele sasa hivi kudai sheria imevunjwa, lakini ndio kwanza najivuta vuta,
Sasa subiri tuone majibu ya Pinda, maana nasikia huko ndani kunawaka moto, waliokula wote wanahaha, kinachosikitisha hapa ni how sisi as a nation tuliweza kuwa na Waziri Mkuu mjinga mjinga kama Lowassa? The man is so arrogant nasikia ilifikia mahali alikuwa ani-run serikali kama Kingdom yake vile, yaaani nasikia viongozi wetu watu wazima na akili zao wenye wake nyumbani na watoto walikuwa wakimsujudia huyu fisadi, how? na WHY?
Wakuu kwa kweli inasikitisha sana kusikia ambayo hayajasemwa hadharani kuhusiana na huyu mkuu, yaani ndani ya bunge mkuu alikuwa akibadili wabunge kina mama kama nguo, ambao wote walilia sana ile siku, halafu eti anasema kuwa hakutegemea kuwa hawa wabunge wajinga wajinga wangeweza kumuondoa? Unajua wakuu ninaomba mzitafute dataz za huyu mkuu yaaani ni aibu hata kuitwa m-Tanzania!
Kasheshe;
Wasiwasi wangu ni kinachotokea nyuma ya pazia yaani kundi A na kundi B ndani sisiem. Inaonyesha kuna mpasuko mkubwa/ombwe katika uongozi wa nchi yetu. Hivi kama tuko katika auto pilot, je mafisadi wakimdhibiti rubani itakuwaje? Pia ndugu yangu zingatia kwamba demokrasia ya kuua nchi sio demokarasia ifaayo kwani kadri mkuu FM alivyodokeza inaonekana sio demokrasia bali domokrasia ndani ya chama tawala.
For the sake of Mjadala uliopo mbele yetu.Aboh! Hollow Brain?how does it look like?kwi kwi a question is a question!u're an idiot kabisa!
Kwa hiyo data za Lunyungu kuhusu Lowassa wewe huna!
Wewe si upo Dodoma mbona huna dataz hata moja? Mijitu mingine bwana mbona hueleweki na majina yako 100 humu, huku unasema one thing halafu unageuka na kusema another ndio maana mkuu sipendi kuwatse my ku-debate na watu kama wewe,
Wazee msiokuwa na dataz hakuna mashindano hapa, wewe kama ulikuwa nazo za lowassa kilichokushinda kuziweka hapa ni nini hasa? Ningekuelewa kuwa wewe unanilipa mimi kuleta dataz na unanipa hizo dataz, then ni kweli una the rights kuniuliza kwa nini sikuleta za lowassa, mkuuu kula dataz hapa au waachie wenye vichwa wazichambue!
Na ninawaahidi kuwa tutaendelea kuleta dataz hapa JF kama kawa, halafu pole sana mkuu nasikia majuzi ulimpigia simu mama ukala mawe haijawahi kutokea pole sana!
Mimi siko kwenye denial. Najua jamii yangu ndivyo inavyoamini. Lakini kujua huku hakuniondolei hisia za aibu. Ni kama vile ambavyo ningependa majadiliano zaidi kwenye yale ambayo naona ni substantive lakini najua wengi wetu interest zao ni kwingine. Hii ni www, hatuwezi wote kuwa na interest zinazofanana.