Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,999
- 1,187
According to the dataz ni kwamba ilifikia mahali wajumbe walitaka kushikana mashati, by kesho Mungu akijalia nitakuwa na exactly nini hasa Mbunge Sendeka alichosema.
Lakini pia aligusia kitendo cha mtoto wa Lowassa, ambaye sio kiongozi wa taifa letu in any capacity, alivyohusishwa na mkataba wa Richimonduli na kufikia kufaidika na hela zetu walipa kodi ambazo sasa amefungua kampuni moja ya Card za Simu, ambayo inampatia hela nyingi sana as a profit, biashara ambayo wananchi wengi walijaribu sana kuiomba kibali serikali wakakataliwa lakini huyu kijana akapewa bila matatizo, biashara ambayo hata mtoto wa Mengi ambaye ni marehemu sasa aliwahi kuiomba serikali akakataliwa.
Kama nilivyoahidi kuwa tunaendelea ku-monitor yanayojiri Dodoma, kwa karibu sana na tutaendelea tu kuhabarishana hapa kwenye uwanja mtukufu wa JF!
Pole na hongera sana Mkuu ESFM, tupo pamoja, tunakuombea Mungu aendelee kukuweka mbali na mikono ya mafisadi