Kutoka Bungeni: 2006 - 2010

Kutoka Bungeni: 2006 - 2010

Wabunge sasa hivi komaeni watu wakamatwe na si kulia lia mambo ya uchawi na kukibimbia bungeni halafu kurudi na yale yale!Kama mlikuwa mkijali maisha yenu dhidi ya mauwaji na ushirikina ni kwanini hamkuwakamata MAFISADI?Nilishawahi kusema itageuka kuwa Dog catch your ass instead of you catchin the dog's ass!Sasa badala ya mafisadi kuogopa...Ni wananchi na wawakilishi wao wana unya unya!
 
Kama nimekukera na UCCM wako kameze chupa! Wasemaji wa upinzani wanasema kupitia hotuba. Michango hiyo ya kina Dr Slaa, Zitto, Cheyo nk wamezungumza kama wabunge wakiwakilisha majimbo yao ya uchaguzi kwa tiketi ya vyama vyao. Lakini soma hitimisho langu, nimesema wapinzani endeleeni kukandamiza kibara mpaka kieleweke. Hii sasa ni kwa ujumla wao!

Asha

acha upambe wako wa vyama vya siasa hapa ! alaaa !
 
Ilibidi atueleze tofauti ya huu msamaha na ule wa wawekezaji wa migodi. Halafu pia tuelewe kama ni busara kwa Serikali kujaribu kufufua sekta ambayo hata wafanya biashara wameiona haina faida. Kama wafanyabiashara wanadhani hii biashara haistahili hata kuilipia kodi, tungependa kujua kwa nini Serikali iione kwamba ni biashara yenye faida, kama anavyopendekeza Mh. Zitto.

Yaani hata cha kuongeza sina
 
Zitto, Shukran sana kwa mchango wako ambao umegusia mambo mengi muhimu.
Isipokuwa mkuu wangu kama kwaida yangu nina shindwa kuelewa pale uliposema TUMETOka katika uchumi unaotegemea kilimo tumeenda katika uchumi unaotegemea huduma!..
Mmetoka na nani?... maanake navyoelewa hizi ni sera za CCM, sera ambazo mimi mpiganaji wa JF sikubaliani nazo wala sioni unafuu wake kwa sababu KILIMO ndicho uti wa mgongo wa nchi yetu.. Tutake tusitake!...
kwa nini kumekuwepo na matokeo ya kukua kwa Uchumi wakati wananchi wanaendelea kuwa maskini ni kwa sababu hiyo kwani ni asilimia zaidi ya 80 wanategemea kilimo na ndicho pekee kinachowagusa wengi wetu moja kwa moja.
Hizi huduma ambazo mnakimbilia ni mali za nje malia ambazo uwezo wa kuwekesha hatuna ihivyo vyombo vya nje ndivyo vimejikita na kupewa hizo nafuu za kodi ambazo bila mahesabu ya kina Mkuu Augustine utaona kwamba pato la taifa haliwezi kuongezeka kwa kiwango sawa na ukuaji wa uchumi.
Kisha ikiwa wananchi wakulima, iwe kilimo ufugaji ama uvuvi wataweza kuwa na kipato kizuri kwa mwaka ni rahisi kwao kununua hizo huduma na mali zinazoagizwa toka nje..

Kifupi ni kwamba navyoitazama mimi Tanzania ya leo, mfumo wake ni ule unaogawa wananchi na kuweka makundi mawili kama alivyofanya mkoloni..Tunatazama fungu fulani wa watu hivyo vipaumbele vyetu vinapangwa kuwatazama wao.. Mwananchi ni mtumwa tu atapata ajira ya utumwa na bajeti haiwezi kumtazama hata kidogo..
Hata hayo madini, Utalii na kadhalika hayawezi kumwokoa mwananchi wa kawaida unless mikataba yote ifutwe na mfumo mpya uundwe laa sivyo maombi yenu ama niseme mchango wenu wa hiyo bajiti kivuli hauna maana kabisa kwani hamuwezi kubadilisha MIKATABA haramu iliyokwisha kubaliwa na kuwekewa sahihi..
In all mkuu bajeti yetu inazidi kumkandamiza mwananchi kama bajeti ya Mkoloni Muingereza ambaye naweza kumpa points juu ya serikali hii kwa sababu aliweza kukipa kilimo kipaumbele zaidi..
Nafahamui sana kuwa wakati umebadilika na kwamba sasa hivi huduma ni muhimu lakini hizi huduma haziwezi kabisa kuinua maisha ya mwananchi kjutokana na sisi wenyewe kutokuwa na uwezo wa kifedha na techonologia kiasi kwamba tutategemea sana wawekeshaji toka nje ambao ni lazima watatufunga ktk mikataba migumu...
Ushauri wangu ni kurudi kwenye basics ambako maendeleo ya Tanzania yatakuja tukianza kutoka chini - kutazama nguvu ya wananchi wako na ardhi bora uliyopewa na Mwenyezi ambayo chochote kinaweza kulimwa na kustawi vizuri!... Kupuuza kilimo, ufugaji na uvuvi ni hatua moja nyuma..Hii ndio sera ya CCM na ndio sababu kubwa ya mimi kutokukubali kujiunga ktk kundi hilo!
 
Jumatatu, Juni 16, 2008

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kunipa nafasi ya kuchangia hotuba hizi mbili hotuba ya bajeti na hotuba ya hali ya uchumi. Ninafahamu ya kwamba sisi kama Kambi ya Upinzani ni Serikali kivuli. Jukumu letu la kidemokrasia ni kuonyesha pale ambapo wenzetu wa Serikali inayoongoza hawapaoni na tumeonyesha katika bajeti yetu kivuli, maeneo ambayo wenzetu hawakuyaona katika bajeti iliyopita, wameyaona katika bajeti ya mwaka huu na wakawa wamepelekea Serikali kuweza kuongeza mapato. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa Waheshimiwa Wabunge wanapozungumza na kudhihaki bajeti kivuli ambayo Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed ameitoa kwamba ni alfu lela ulela nashindwa kuelewa sifa zilizowafanya Wabunge hao kuja katika Bunge hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaanza na hali ya uchumi.

NAIBU SPIKA: Naibu Spika husikiliza yote tu, alfu lela ulela na mengineyo. (Makofi/Kicheko)

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nitaanza na hali ya uchumi. Tuna changamoto kubwa sana kama nchi, kwamba hivi sasa tunaishi katika uchumi unaokuwa lakini umaskini haupungui na hii ndio changamoto ambayo bajeti inapaswa kuijibu na haiwezi kujibiwa kwa bajeti ya mwaka mmoja inajibiwa kwa utaratibu maalumu. Toka tumeingia katika Bunge hili, hii ni bajeti ya tatu, kumekuwa na rekodi za uchumi kukua lakini taarifa mbalimbali za Serikali, kwa mfano Taarifa za hali ya umaskini. Toka tumekuwa Wabunge kumekuwa na taarifa mbili za hali ya umaskini (P&HDR 2005 na 2007), zote zinaonyesha kwamba umaskini kwa wananchi bado ni mkubwa na katika bajeti iliyopita tulizungumzia suala zima la madhara ya kupandisha kodi za baadhi ya vitu kwa maisha ya wananchi na wenzetu (CCM) wakakataa kata kata lakini athari zinaonekana hivi sasa na leo tunaiita bajeti ambayo Mheshimiwa Waziri Mkulo ameitoa kwamba ni bajeti ya wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, haiwezi kuwa bajeti ya mwananchi kwa sababu kodi ambazo zilipandishwa mwaka jana hazijashushwa kurudishwa katika viwango vya mwaka 2006/2007, itakuwa ni bajeti ya mwananchi iwapo tu kodi hizo zitakuwa zimeshushwa lakini kitendo cha kuziacha kodi hizo kama zilivyo bado kitaendelea kufanya mfumuko wa bei uweze kuendelea na hili nitaeleza nitaelezea huko chini.
Uchumi wetu umebadilika, tumetoka katika uchumi unaotegemea kilimo tumeenda katika uchumi unaotegemea huduma. Asilimia 47.3 sasa ya uchumi wetu ni huduma na asilimia 28.2 tu ndio kilimo.
Lakini mipango yetu bado ni kana kwamba uchumi unategemea kilimo na tumeonyesha baadhi ya wasiwasi wetu kutokana na takwimu ambazo zimetolewa lakini mipango ya nchi ambayo uchumi wake ambao takriban nusu unategemea huduma ni tofauti na mipango ya nchi ambayo takriban zaidi ya nusu inategemea kilimo. Bajeti hii ni mwendelezo wa bajeti zilizopita ambapo huduma ilikuwa ina mchango mdogo sana katika uchumi, kwa hiyo kwa vyovyote vile kutokana na bajeti hii ni vigumu sana changamoto za sasa za nchi kuweza kujibiwa.


[MHE. KABWE Z. ZITTO]

Mheshimiwa Naibu Spika, sekta ya madini ambayo ndio ilikuwa sekta inayoongoza kwa ukuaji, hivi sasa imekuwa ni sekta ya pili au ya tatu kwa ukuaji, ukuaji wa uchumi sasa unategemea sekta ya mawasiliano na kwa kiasi kikubwa sekta hii bado haichangii vya kutosha katika mapato ya Serikali, kuna baadhi ya maeneo ambayo Waziri wa Fedha ameonyesha ili Serikali iweze kukusanya pesa zaidi lakini wakati anaangalia maeneo hayo bado eneo lenyewe la sekta ya madini bado halikuangaliwa hata kidogo na huwa tunapata wasiwasi mkubwa sana kwamba baadhi ya mapendekezo ambayo Kamati ya Rais ya kuangalia sekta ya madini iliyotoa na si baadhi mapendekezo, yote hayajachukuliwa, matokeo yake ni kwamba bajeti imeangalia zaidi kupandisha kodi za walaji yaani consumption tax na kuacha kabisa kupandisha kodi kwa watu ambao ni wale wazalishaji kwa maana ya wawekezaji na wawekezaji wa ndani na wa nje ya nchi siyo wawekezaji wa nje peke yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo tumejikuta tuna chumi mbili ndani ya nchi moja uchumi wa matajiri na uchumi wa maskini, uchumi wa maskini wanauita ni rural economy ambapo ndiko wanakoishi na matokeo yake ni kwamba maskini either bidhaa ambazo yeye analima, (anazozalisha) hazikui lakini bei za bidhaa ambazo yeye anatumia zinakuwa, kwa hiyo maskini anauza kwa bei za vijijini na ananunua kwa bei za mjini. Kwa hiyo hali yake ya kipato ni lazima iendelee kuwa chini, ni tegemeo la bajeti yeyote ile katika nchi yeyote ile iwapo bajeti ikitumika kama sera ya kuangalia ni jinsi gani ambavyo uchumi wa nchi unakwenda wataweza kuangalia ni jinsi gani ya kupunguza gharama hii ambayo mkulima anapata kwa ajili ya kuhakikisha kwamba anabakia na fedha ya kutosha.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeelezwa kwamba Serikali imeweka vipaumbele na vipaumbele vimetajwa na pesa zimetajwa kwa ajili ya vipaumbele lakini napata wasiwasi sana kwamba inawezekana kuna ukosefu wa uratibu ndani ya Serikali, taarifa ya hali ya umaskini ya mwaka 2007 ambayo imetolewa mwaka huu imeonyesha changamoto ambazo nchi inazo na ni maeneo gani ambayo yakitiliwa mkazo tutaweza kwenda mbele kiuchumi. Wenyewe wanaita drivers of growth na wameweka maeneo manne ambayo yanapaswa kuangaliwa na kuwekewa mikakati maalum - transport services ambayo ndani yake kuna miundombinu na huduma zingine za usafiri, madini, horticulture kwa Kiswahili nadhani ni masula ya maua ukulima wa maua na kadhalika na utalii.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ukiangalia bajeti jinsi ilivyokaa jinsi gani ambavyo tumegawa rasilimali zetu kidogo ambazo tunazipata haikuangalia kabisa vipaumbele hivi ambavyo taarifa ya Serikali imezitoa taarifa ambayo ndio inafanya tathmini ni wapi ambapo tunakwenda kuhusiana na suala zima la kupunguza umaskini.
Nadhani Wizara ya Fedha na Uchumi inabidi iangalie kwa sababu taarifa ya hali ya umaskini inatolewa na idara ndani ya Wizara ya Fedha na Uchumi kwa hiyo ni rahisi sana kwa idara hiyo ya kuondoa umaskini kuwasiliana na Idara ya Sera ya Wizara ya Fedha, kuwasiliana na Idara ya Bajeti ya Wizara ya Fedha ili kuweza kuangalia ni vipi ambavyo tunavyofanya vipaumbele vyetu, tukiamua kuweka vipaumbele kufurahisha wananchi kwa sasa huko tunakokwenda kutakuwa ni kugumu sana kwa sababu utagawa pesa kwa kila sekta lakini zile sekta hazitachochea sekta nyingine. Kwa hiyo kuna umuhimu mkubwa sana wa kuweza kuangalia vitu kama hivyo katika hali ya juu na ni suala lile lile la kubadili mindsett.


[MHE. KABWE Z. ZITTO]

Mheshimiwa Naibu Spika, ni vipi ambavyo bajeti yetu inaendana na changamoto ambazo tunazo hivi sasa? Kwanza bajeti imeshindwa kabisa kukusanya kodi zinazostahili kwenye madini na ninashindwa kuelewa ni kwa sababau gani, kwa sababu inafahamika wazi kabisa kwamba mwaka 1997 na Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed ameielezea hapa, Bunge hili lilitunga sheria ambayo ilitoa unafuu usio na lazima kwa makampuni ya madini kwa kiasi cha asilimia 15 unafuua mbao umeifanya Taifa lipoteze shilingi bilioni 883 katika kipindi cha miaka 10 toka sekta ya madini ianze kukua katika Taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tulitegemea kwamba katika finance bill ya mwaka huu Waziri wa Fedha angefuta kabisa sheria hiyo kwa sababu sheria hiyo bado iko kwenye vitabu vyetu vya sheria na inafanya makampuni ya madini ambayo yana mikataba yasiweze kulipa kodi hiyo, kuna mashauriano ambayo Serikali imefanya na baadhi ya makampuni ya madini lakini kama suala hili hatutalitoa kwenye sheria halitaweza kusaidia na mfano mmoja tu wa madhara ya sheria hiyo ni kwamba kampuni ya Bulyanhulu Gold Mine ambayo inangepaswa kuwa imeanza kulipa kodi ya mapato haitalipa kodi ya mapato kutokana na faida yake mpaka mwaka 2019 yaani haitaanza kulipa corporate tax mpaka mwaka wa mwisho wa Rais wa awamu ya tano na hawa wameanza na Rais wa awamu ya tatu. Kwa hiyo unaweza ukaona ni jinsi gani ambayo Taifa linapoteza na mabilioni ya fedha kwa sababu ya sheria ambazo tumezitunga sisi wenyewe na tunao uwezo wa kuweza kuzirekebisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, misamaha, mwaka 2005 wakati tuko kwenye kampeni za uchaguzi Serikali ilitoa misamaha ya kodi miwili wa kwanza ya mafuta kwamba makampuni ya madini hayatalipa kodi ya mafuta mpaka watakapomaliza kama ni dhahabu wanayochimba, kama ni almasi wanayochimba, kama ni Tanzanite wanayochimba na tulishauri kwamba msamaha huo ufutwe kwa sababu ni msamaha ambao hausaidii chochote.

Mheshimiwa Naibu Spika, na msamaha huu ungefutwa ungeweza hata kusaidia kupunguza zile kodi ambazo tulizipandisha mwaka jana kupelekea mfumuko wa bei uweze kutokea. Sisi kama Tanzania hatuna uwezo hata kidogo wa ku-control bei ya mafuta katika soko la Dunia lakini tunao uwezo wa ku-deal na kodi zetu ili kuweza kuhakikisha kwamba tunapunguza ukali wa upandaji wa bei katika soko la Dunia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ilipaswa kuangalia hizo kodi zetu ili ziweze kupunguza huo ukali wa maisha. Mwaka 2007/2008 aliyekuwa Waziri wa Fedha Mheshimiwa Zakia Meghji alionyesha katika sura ya bajeti kwamba Serikali itakusanya kiasi fulani cha mapato shilingi bilioni 239 kutokana na marekebisho mbalimbali ya kodi, katika bajeti ya mwaka huu Waziri wa Fedha hakuonyesha viwango mbalimbali vya mabadiliko ya kodi vitaifanya Serikali ikusanye kiasi gani? Kwa hiyo ninadhani ni muhimu sana kuwa na mtiririko ulio sawa au consistency ili kuhakikisha kwamba kunakuwa na hali ambayo ni nzuri zaidi.


[MHE. KABWE Z. ZITTO]

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa, bajeti ni vitabu vinne, volume one mpaka volume four, volume one ndio inayo-dill na mapato ya Serikali na ninasikitika kwamba mara nyingi hatuiangali hii volume. Ukiangalia kitabu cha kwanza cha bajeti utagundua mambo mawili la kwanza tunategemea sana kodi za biashara kwa maana ya import, import duties. Mabadiliko ya kodi ambayo Serikal imeyatangaza sasa asilimia 50 itatokana na import duties, hii ni hatari sana katika uchumi wa sasa, tunaokwenda, tuna East African Customs Union tunaenda kwenye common market, tunasaini EPA ambayo itaondoa kodi mbalimbali dhidi ya European Union tutapata tatizo kubwa sana kurekebisha kodi hizi tutajikuta kwamba tunakuja kuumia sana huko baadaye.
Katika revenue book, wakati Waziri wa Fedha anasema kwamba tutakusanya shilingi bilioni 58 kwa mauzo ya hisa za NMB, kwenye revenue book zinaonekana shilingi bilioni 42. Tunapopitisha bajeti tunachoangalia ni revenue book, ni nini ambacho tunakichukua? Ni hotuba ya bilioni 58 au ni revenue book ya bilioni 42, nilikuwa ninaomba Waziri wa Fedha aweze kuliangalia hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho kabisa, kama tunataka kuongeza uzalishaji wa kutosha kwenye baadhi ya mazao ambayo tunayo ni lazima tuangalie jinsi gani ya kutoa incentives kwa baadhi ya mazao. Mimi nitatoa mfano mmoja na nilitoa taarifa hii toka mwaka jana kwamba leo India wameweka compulsory usage ya magunia yao ya jute kwa ajili ya mazao yote ya India. Sisi hatujaweka compulsory usage ya maguni yetu ya katani, matokeo yake ni kwamba tunakuwa tuna-export jobs kwenda Bangladeshi na India kwa sababu hatulindi sisal yetu, katani yetu wala hatulindi viwanda matokeo yake ni kwamba baadhi ya wawekezaji wamenunua viwanda havifanyi kazi kwa sababu ya mazingira hayo ya kikodi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa ninaomba Waziri wa Fedha ajaribu kuangalia uwezekano wa angalau mazao mawili, mahindi na korosho ziwe ni compulsory kutumia maguni ya katani ili ku-stimulate uzalishaji wa katani na kufanya viwanda vya katani ambavyo vimekufa hivi sasa viweze kuzalisha magunia ya katani na yaweze kutumika katika nchi, vinginevyo itakuwa ni tatizo ambalo tutaendelea nalo tutaendelea kutegemea kodi kutokana na imports ambazo madhara yake ni makubwa sana kutokana na Dunia ya sasa ya globalization.
Ni lazima kuangalia Serikali isikwepe kazi yake ya distributive role. Ni kazi ya Serikali yeyote Duniani kukusanya kutoka matajiri kuwapeleka maskini ili kuweza kupunguza gharama za maisha yao na ndio kazi ya bajeti kama sera na siyo bajeti kama urari wa mapato na matumizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru sana. (Makofi)

Kwa hiyo hii ndiyo lugha rasmi mnayotumia bungeni? Wananchi wasipowaelewa mnasema wamehongwa T-shirt. Mh. naomba ufafanuzi hapa ulikuwa unamaanisha nini?
Kwa hiyo kuna umuhimu mkubwa sana wa kuweza kuangalia vitu kama hivyo katika hali ya juu na ni suala lile lile la kubadili mindsett.
 
Hansard ya leo bado haijatoka. Ikitoka tu wana JF mtapata nini alisema Cheyo na ni nini alisema Dr. Slaa

Mchango wangu ni wa jana jioni ndio maana hansard yake tumepata

NInavyojua mimi JF ipo hapa kwa manufaa ya taifa siyo chama fulani cha siasa. Tungependa kujua kila mtu amesema nini na tuchambue pumba zipi na mchele ni upi au mtutangazie rasmi kwamba JF ipo kwa manufaa ya chama fulani cha siasa sisi wengine tutafute makao mapya.
 
Is sisal making a comeback? Most people had thought it to be on the verge of being replaced by synthetics.

mzee pundit,
mara yako ya mwisho kwenda maeneo ya tanga ilikuwa lini ?? mbona kuna mashamba mengi tu huko !
 
..Najaribu ku-imagine hivi hata humo bungeni kusingekuwa na mbunge hata mmoja wa chama cha upinzani haya mauchafu yanayoibuliwa yangejulikana kweli?? Maana wabunge wa CCM kwa jinsi walivyo na nidhamu ya unafiki lazima wangenyuti kimya mambo yanaenda " funika kombe mwanaharamu apite" anaenda kusaini anavuta chake siku zinaenda...

Inauma sana.. Kwa kweli wa-tz kuna haja 2010 kuangalia upya huu upepo wa kimaruhani wa CCM vinginevyo nchi itapotea kabisa licha ya kuwa na utajiri pomoni...Lakini umasikini ndio unanzidi kuongezeka.
 
..Najaribu ku-imagine hivi hata humo bungeni kusingekuwa na mbunge hata mmoja wa chama cha upinzani haya mauchafu yanayoibuliwa yangejulikana kweli?? Maana wabunge wa CCM kwa jinsi walivyo na nidhamu ya unafiki lazima wangenyuti kimya mambo yanaenda " funika kombe mwanaharamu apite" anaenda kusaini anavuta chake siku zinaenda...

Inauma sana.. Kwa kweli wa-tz kuna haja 2010 kuangalia upya huu upepo wa kimaruhani wa CCM vinginevyo nchi itapotea kabisa licha ya kuwa na utajiri pomoni...Lakini umasikini ndio unanzidi kuongezeka.

Samahani naomba uliza.
Hivi ni kweli kwamba wabunge wa CCM huwa wanayaona haya madude mfano kama jana hii ya karne aliyo itoa jana Dr Slaa ya tofauti ya biln 130 kwa bajeti ya Mkulo, huwa wanasoma na kuamua kunyamaza kwa nidhamu ya chama? ama kwa vile mzizi wa ufisadi umeshamiri katika chaguzi/teuzi zao basi wabunge wengi wa CCM ni wale ambao japo hutazama hayo makabrasha uwezo wa kuyachambua huwa hawana? yaani nina maana kwamba walio wengi CCM ni Chitarilo type?

Ama kuwa mbunge wa CCM ni kuwa 'Yes man' kwa lolote lile hata kama liko wazi kwamba ni fyongo?
 
Hii serikali mnaoitetea hivi hamuoni aibu jamani au mnaubia katika serikali hii???Tujibuni jamani kuna watu humu JF wapo mstari wa mbele kuitetea sana serikali kila kukicha....watueleze wanaubia na serikali??
 
Well said,ila hao walio kuwa wanacheka bajeti wa wapinzani kweli wehu mbona hawakucheka iliyosomwa na CCM!!! utani umezidi mmle ndani na NS naye eti anasikiliza hata hizo za halfu lela ulela sijui!!!!
Bwana Zitto we kandamiza tu mpaka wajione wako kwenye njozi za mabadiliko..cheers
 
Well said,ila hao walio kuwa wanacheka bajeti wa wapinzani kweli wehu mbona hawakucheka iliyosomwa na CCM!!! utani umezidi mmle ndani na NS naye eti anasikiliza hata hizo za halfu lela ulela sijui!!!!
Bwana Zitto we kandamiza tu mpaka wajione wako kwenye njozi za mabadiliko..cheers

Alafu mbunge mwenyewe aliye ongea hayupo kabisa katika medali za siasa alidandia tu...atuambie ameisadiaje serikali ya CCM katika ubunge wake kama si kusinzia tu bungeni...ndo maana alikurupuka akasema lela ulela kasoma ngumbaru tu huyu...sijui tumhurumie?au tumfanyaje maana maneno mengine watu wanalopoka tu hawajui athari zake.Sasa hata wananchi walio mtuma awawakilishe wakisikia hivyo si aibu jamani>?Ameacha kupigania maendeleo kusini huko ambako kila mtu anakimbia kufanya kazi yeye anaongea utumbo tu bungeni.Wabunge wengine wanaudhi sana itakuwa ilikuwa njia ya kujipatia umaarufu sijui?
 
CCM ilishajisiku nyingi, tunachelewasha maziko tu.Mpaka lini tudanganywe wadanganyika?
 
Zitto nakupa Heko! Kazi nzuri inayofanywa na kambi ya upinzani bungeni inaonekana dhahili kwa watanzania. Nami naipongeza kambi hii.

Serikali ya ccm inabidi ijifunze kubadilika na ianze sasa kufanya kazi kwa manufaa ya watanzania. Kitendo cha kutotoza kodi makampuni ya madini ni ufisadi wa hali ya juu. Kwanini serikali inasita kuyatoza ushuru hayo makampuni ya migodi wakati huohuo inaendelea kutoza ushuru mafuta yote ya petrol na diesel yanayotumiwa na DALADALA zitoazo huduma kwa walala hoi wa nchi hii pamoja na viwanda vinavyozalisha bidhaa mbalambali zitumiwazo na walala hoi watanzania??!! Naishangaa sana hii serikali ya ccm!

Kwa maoni yangu, Serikali yetu inabidi ipunguze kodi kwa mafuta yote ya diesel na petrol ambayo huingizwa nchini kwa ajili ya matumizi ya sector ya transport na viwanda vinavyozalisha bidhaa mbalimbali hapa nchini. Kodi hii kwa sasa ni Tsh 539/liter kwa petrol na Tsh. 514/liter kwa diesel ambayo mwisho wake hulipwa na mlala hoi wa tanzania kila anapolipa nauli na kila anunuapo bidhaa yoyote ile amboyo ni pamoja na chakula chake cha kila siku. Isitoshe, serikali bado inatoza tena ushuru mwingine kwa mafuta hayohayo wa 1.2%FOB kwa mafuta yote yanayotumiwa na viwanda vyetu pamoja na gari zote hapa nchini zikiwemo daladala ambazo ni mkombozi wa huduma ya usafiri kwa wanyonge na masikini wa nchi hii. Anayebebeshwa gharama zote hizi ni mwananchi mlalahoi wa tanzania. Kwanini serikali isipunguze hizi kodi na kuzihamishia migodini??

Serikali yetu inabidi ianze sasa kutoza kodi kwa mafuta ya diesel yanayotumika migodini ili hawa wawekezaji nao waanze kuchangia uchumi wa nchi yetu na wawapunguzie mzigo walala hoi wa nchi hii waliobebeshwa kodi hii ya mafuta wakati mafisadi wenye migodi wakiendelea kutumia mafuta bila kuyalipia kodi yoyote. Hadi lili tutaendelea kuwaruhusu hawa mafisadi wa nje na wa ndani wabebe madini yetu bure???
 
Ahsante sana Zito kwa maelezo yenye uelewa na yaliyojitosheleza.Lakini ....,baada ya yote haya mwisho wake ni nini?????Tatizo langu siku zote ni kuwa hawa wanazi'CCM' wanajua yote haya mabaya lakini wanakanyagia vilevile.....wakati wa kampeni ukifika tutabembelezwa kidogo then watarudi madarakani,full stop!!..waliomo humuhumu na wadanganyika wengine ndio watasimama kutwa nzima kuwapa kula!!!!...
 
Last edited:
mzee pundit,
mara yako ya mwisho kwenda maeneo ya tanga ilikuwa lini ?? mbona kuna mashamba mengi tu huko !

Swali si kwamba kuna mashamba au hamna, sijauliza comeback ya kulimwa.Niko interested kujua kama mkonge unalipa katika soko la dunia.Kuna kipindi hapa kati watu walikuwa wanatumia sana synthetic products ikawa kama mkonge hauna deal, je tunatumia resources zetu vizuri kwa kulima mkonge au tunshindwa tu kuyabadili haya mashamba ya mkonge na kulima mazao mengine yenye faida kubwa zaidi?

Hilo ndilo swali.
 
Mimi nashindwa kuelewa kabisa, inakuwa akina Zitto wanaona haya mambo lakini akina CCM hawaoni? Wao wamesoma shule gani hasa?

Hili nalo unauliza? hawakusoma lakini kwa ile wanaita takrima wako mujengo! Sasa watasema nini? wachache walio na uelewa ndiyo hao tunawafahamu kwa jina la mafisadi! Wewe fuatilia tu utasikia michango yao inavyosikitisha. "Oh mh Spika kwetu hakuna barabara.....Naunga hoja asilimia mia moja"😕
 
Kikwete kama ni chakula anapika basi kishakuwa sumu kutokana na hiyo michanganyiko!

Sitta ni shujaa kwasababu alipigania kuwepo uchunguzi wa RICHMOND.
Johnson Mwanyika akawa ni mmoja wapo wa watuhumiwa wa RICHOMD...MKATABA AMBAO HATA LOWASSA ALISHAMWAMBIA YEYE NA MWANYIKA PAMOJA NA DON MAFIOSO TOP MWENYEWE KUWA NI MBOVU NA HAUFAI!

Kikwete akaona ataumbuka hivyo akamuweka Mwanyika kwenye kamati haraka haraka ya kuwachunguza mafisadi wengine ili sasa waje pamoja na kunegotiate namna ya kuua noma pande zote za EPA na RICHMOND...Na huku akimwambia LOWASSA KUWA BADO ANAWEZA KUJITETEA NA KUBAKI KAZINI...

Akageuka upande wa PILI akam TAP Zitto ambaye naye alikuwa akiwaumiza huko Bungeni....Wakamweka kapu moja na MAFISADI kwenye kamati ya MADINI.

Walichozungumza humo ndani ya kamati anayejua ni MKUU MAFIOSO NA SINCLAIR pamoja na Hao kina ZITTO na wanakamati wengine.

Sasa wakaanza kuwazuga wananchi kuwa tusubiri BUNGE likianza kwani watayazungumzia yale ambayo wananchi wanayoyapigia kelele kuwa SASA MAFIA WAWEKWE NDANI...

Kumbe Mafioso ni WOTE na sasa woga ni UCHAWI BUNGENI NA HAKUNA ANAYETAKA KUKAA BUNGENI NA KUJADILI ISSUES ZA WANANCHI.
Baada a kurudi BUNGENI...

Wameanza upya eti wanazungumzia mambo ya ufisadi na namna rasimali za Taifa zitakavyoendelea kutumika ili kuwanufaisha wananchi!?

KUNA MWANANCHI ASIYEJUA KUWA MAFIOSO NI CCM NA SERIKALI YAKE NA KWAMBA HAWAWEZI KUJIKAMATA AMA KUJICHUNGUZA?

Kuna asiyejua kuwa hata wale tunaowaona kama ni wakombozi wetu bado wana maswali ya kutujibu?
 
Back
Top Bottom