Kutoka Bungeni: 2006 - 2010

Kutoka Bungeni: 2006 - 2010

Mushi

Are you in your mind? Wabunge 11 wa CHADEMA watavunja vipi bunge mbele ya Wabunge zaidi ya 200 wa CCM?

Zitto alipeleka hoja ya Karamagi matokeo yake CCM wakamsimamisha.

Dr Slaa alipeleka hoja ya BOT wakaipiga dana dana.

Wapinzani wakaenda kwa umma. Matokeo yake, Waziri Mkuu akajiuzulu na Baraza kuvunjwa kutokana na Richmond baada ya Kamati tuele iliyoundwa baada ya mawaziri kuzomewa zomewa.

Kikwete baada ya kuzomewa akaunda Kamati ya Bomani na kujipendekeza kumchukua Zitto.

Sasa subiri uone mambo yanayokuja.

Wakati mwenzako Masaka anapata uongofu wewe ndio unapata upofu?

Aiiiii weewe Mushi, mbona unanisikitisha?

Au huko ulipojificha kwa muda na kurejea walikupeleka kwenye vitisho?

Asha

Sasa hizi kelele zitawasaidia nini nyie CHADEMA AMA WANANCHI?
AMA MNATAKA KAMATI NYINGINE YA RAIS?
KELELE ZENU AMBAZO MNAKIRI ZINAFUNIKWA NA UMAFIA WA CCM zina thamani gani kama mnakula CHUNGU KIMOJA NA MAFIOSO MAFISADI?
Nyie mnataka mpewe NCHI?
Mnaota!
Kama kweli mna uhusiano mzuri na hao CCM mafioso mnaofanya nao kazi bungeni na kamatini...Then mimi si msukule!
 
Sio hatari da Asha, nimelituliza dongo hilo.

Kuunga mkono upinzani ni pamoja na kujaribu kuchuja hoja zetu za upinzani na kuleta zile zilizo bora zaidi. Angalia jinsi CCM wanavyotupiga bao kila siku Asha. Tukija bungeni na hoja zilizopikwa nusu nusu CCM wataendelea kuzi filibuster na "kushika Utamu" mpaka jehanamu ya moto igande barafu.

Kwa hiyo nadhani Mbunge wa upinzani akisema kitu ambacho kinahitaji maelezo, ni wajibu wangu kama mwana upinzani mwenye kuwajibika, na mwenye mawazo huria, kumuomba maelezo zaidi.

Bahati mbaya huu mvutano wa mawazo ndani ya ukoo wa upinzani hauruhusiwi. Unageuka kuwa ushabiki wa Pan Afrika na Cosmo FC, na kuchanana kama hilo jiwe ulilolirusha baada ya kupungukiwa na majibu.

Wapinzani wa kweli hatutakubali upinzani hafifu.

Poa kaka,

Nimekulewa sana tu. Hebu muandalie basi Zitto huo muswada binafsi ausukume mbele. Unajua wabunge wetu wa upinzani ni woman/man alone. Hawana watendaji wanawazunguka kwa wingi kama ilivyo kwa wabunge wa nje wenye ma-researchers nk. Utajisikiaje ukikaa kwenye luninga halafu ukaona muswada ambao umeandika mwenyewe unasomwa? Utajisikiaje zaidi ukiona mabadiliko ya mfumo wa misamaha ya kodi yakiwa yametokea kutokana na mchango wako tu wa kukaa mbele ya kompyuta kwa masaa kadhaa na kumwandikia muswada mbunge mbadala? kama umevutiwa na wazo hili hebu tuwasiliane basi kwenye ashabdala@yahoo.com.

Tusikubali upinzani uwe na kasoro bwana. Lazima tuwe best of the best!

Asha
 
Sasa hizi kelele zitawasaidia nini nyie CHADEMA AMA WANANCHI?
AMA MNATAKA KAMATI NYINGINE YA RAIS?
KELELE ZENU AMBAZO MNAKIRI ZINAFUNIKWA NA UMAFIA WA CCM zina thamani gani kama mnakula CHUNGU KIMOJA NA MAFIOSO MAFISADI?
Nyie mnataka mpewe NCHI?
Mnaota!
Kama kweli mna uhusiano mzuri na hao CCM mafioso mnaofanya nao kazi bungeni na kamatini...Then mimi si msukule!

CHADEMA wanauhusiano vipi na mafioso? Au umekukuwa risasi isiyemfahamu adui?

Nilidhani ni wachawi tu ndio wenye kuroga watoto wao wenyewe!

Asha
 
Wote hawa ni MAFIOSO NDUGU ZANGU!
Kikwete alijikuta mtegoni baada ya mpango mahususi wa kuzitumia pesa za EPA kwenye kampeni yake ya USHINDI WA TSUNAMI!
Alipogundua hilo....Ikawa kama enzi UKIMWI ulipokuja ambapo watu walianza kuambukizana makusudi ili wasife wenyewe ama kutajana tena!
Kikwete kafanikiwa sana...Keshawaambukizia VIRUSI VYA UMAFIA NA UFISADI...
Sasa mnatufanya sisi PUMBAVU?
ZITTO HAKUJUA KUWA JOHNSON MWANYIKA NI MTUHUMIWA WA RICHMOND AMBAYE ALIWEKWA NA SWAHIBA WAKE DON KIKWETE KWENYE KAMATI YA MADINI YEYE PAMOJA NA MAFIOSO WENGINE?
Atawapiga vita kivipi?
Ama VIRUSI TAYARI DHIDI YA KINGA ZA FIKRA ZA KIZALENDO?
 
Wote hawa ni MAFIOSO NDUGU ZANGU!
Kikwete alijikuta mtegoni baada ya mpango mahususi wa kuzitumia pesa za EPA kwenye kampeni yake ya USHINDI WA TSUNAMI!
Alipogundua hilo....Ikawa kama enzi UKIMWI ulipokuja ambapo watu walianza kuambukizana makusudi ili wasife wenyewe ama kutajana tena!
Kikwete kafanikiwa sana...Keshawaambukizia VIRUSI VYA UMAFIA NA UFISADI...
Sasa mnatufanya sisi PUMBAVU?
ZITTO HAKUJUA KUWA JOHNSON MWANYIKA NI MTUHUMIWA WA RICHMOND AMBAYE ALIWEKWA NA SWAHIBA WAKE DON KIKWETE KWENYE KAMATI YA MADINI YEYE PAMOJA NA MAFIOSO WENGINE?
Atawapiga vita kivipi?
Ama VIRUSI TAYARI DHIDI YA KINGA ZA FIKRA ZA KIZALENDO?

BTW: Hivi jmushi1 unamfahamu Joseph Mushi wa CCM yule kinara wa ufisadi? Maana kuna Mushi aliyekaribu sana na mafioso. Ni jamaa yako?

Asha
 
BTW: Hivi jmushi1 unamfahamu Joseph Mushi wa CCM yule kinara wa ufisadi? Maana kuna Mushi aliyekaribu sana na mafioso. Ni jamaa yako?

Asha

Dada Asha sina uhusiano wowote na Mushi huyo...Ila kweli haya ninayozungumza hapa ni ya KIFISADI?
AMA NI SPIN INAANZA?
 
Kikwete Aliambukizwa Virusi Vya Ufisadi Na Umafia Na Yeye Kavi Spread...dawa Ni Kuchoma Wote Moto!
 
Pundit,
Mkonge ni biashara iliyokwisha siku nyingi sana. Unajua yapo mazao ambayo hayawezi kuwa replaced kirahisi lakini sio Mkonge, navyofahamu mimi Miwa imerudi tena kwa kasi kubwa sana. Wenzetu Kenya hivi sasa ndio zao lao kubwa hasa mikoa ya kusini magharibi.
Wanachokifanya Kenya nadhani ni mfano mzuri sana kwetu na tunaweza kuiga tukiyatumia mashirika hayo hayo wanayotumia Kenya. Wenzetu kwa sababu nchi yao ina wakulima wadogo wadogo kama sisi wakishika maeneo makubwa.
Sasa basi shirika linalonunua miwa kwa wananchi ndilo linakodisha hizo ardhi kwa wananchi na kuwalipa kwa kila msimu wa mavuno kulingana na hetka ulizokuwa nazo. Shirika hilo ndilo huleta matrekta yake na kulima, kupanda na hata kuvuna lakini mshiko wanaochukua wananchi kwa ardhi tu ni tosha kabisa hasa ukizingatia kwamba hukwenda shambani kulima wewe..Ardhi yako ni mtaji tosha kabisa.
Hivyo Kenya unaweza kuwa na shamba kubwa ukaingiza fedha safi huku wewe mwenyewe ukifanya kazi kiwandani, ofisini ama biashara nyingine na hata siku moja hujaingia shambani kulima...
Kwa hiyo utaona kwamba badala ya kuwa na kundi la wakulima asilimia 60 au 80 hizi kampuni zinakuja na vifaa vyao... na pengine yanaweza kuwa mashirika 15 tu ambayo yanaajiri labda asilimia 10 ya wananchi wote!..hivyo wamekata kabisa asilimia kubwa ya kundi la wananchi wanaowekwa fungu la wakulima, na ukija tazama uvuvi utaona pia makampuni makubwa yanayonunua samaki kwa wananchi (sangara) wamewapa wananchi vifaa vya uvuvi wakishirikiana na vyombo vya serikali ili kulinda both wawekeshaji na wananchi wasije lipwa kitumwa..

Ni aibu kubwa sana kwa Tanzania pamoja na wasomi wetu kuona kwamba utajiri wa nchi hii unawekwa ktk sinia la pilau bila nyama na kuwapa wananchi ambao hawafahamu kabisa kuwa pilau hilo ni mabaki (ukoko), Pilau lenye nyama linaliwa chumbani na Masheikh (viongozi) wavaa suti jua kali!
Bajeti hii ni matayarisho la sherehe nyingine kwa hawa viongozi ambao wamemtupa kabisa mwananchi na kutazama wanaweza kuvuna nini zaidi toka kwa mwananchi.
 
Shukrani Sana bwana Zitto Kwa mchango wako huo kuhusu bajeti ya mwaka huu... nanimependa sana ulivyo hitimisha kwa kugusia suala la magunia na mkonge..

hicho ni kilio na ni aibu sana kwa hii nchi yetu kutupa raslimali zake ambazo hazipatikani nchi zote duniani na kukimbilia ku import substitute ya rasilimali izo...je mnataka kuacha izo raslimali zichukuliwe na wazungu wanyonyaji ( Wawekezaji ) wauze wapeleke hela kwao..na baadae wananchi waanze tena kuwalalamikia mmeuza raslimali zao???? huu ni ujinga usiovumilika..mnaacha mazao ya msingi kabisa ambayo tunaweza tuka take a comperative advantage agaisnt other contries yafe halafu mnaleta wawekezaji wayafufue!!!!!!!!!!! hivi ivi vitu vinahitaji akili ya kwenda kusoma Havard University??????

Sinzungumzii hayo mashamba ya mkonge mnayomiliki nyinyi kama serikali ( na sidhani kama yapo tena)..ila ni bora upromote bidhaa za nchini kwako kwanza kabla ya kwenda nje...huo ndio msingi mkubwa sana wa kukua kiuchumi hasa kwa nchi yetu kama hii.


Huu ni mtazamo tu wananchi msijenge chuki
 
Mimi nitatoa mfano mmoja na nilitoa taarifa hii toka mwaka jana kwamba leo India wameweka compulsory usage ya magunia yao ya jute kwa ajili ya mazao yote ya India. Sisi hatujaweka compulsory usage ya maguni yetu ya katani, matokeo yake ni kwamba tunakuwa tuna-export jobs kwenda Bangladeshi na India kwa sababu hatulindi sisal yetu, katani yetu wala hatulindi viwanda matokeo yake ni kwamba baadhi ya wawekezaji wamenunua viwanda havifanyi kazi kwa sababu ya mazingira hayo ya kikodi.


Heshima ya Upiganaji Kaka Zitto,
Ningependa usipapase bali ukune suala la magunia kwa mapana yake ambayo kwa upeo wa maelezo hapo juu yadhihirisha UNAFAHAMU.

Kwa ushokozi:

Tueleze unalolifahamu juu ya MeTL inanufaika vipi na mwanya wa uagizaji magunia?

Tueleze MeTL inafaidika vipi na kumiliki mashamba ya mkonge, godown na viwanda vya mkonge vilivyobinafsishwa (sasa havifanyi kazi) wakati magunia yanaagizwa toka nje?

Mwisho katika mazingira hayo hapo juu, mfanyabiashara mh. Mohamed (MB) anachangia vipi mada kama hii?

KUNA WATU NA MAKAMPUNI HAYAJADILIKI TANZANIA SI KWA SABABU YA HESHIMA WALIYOJIJENGEA KWA JAMII BALI UMAFIA ULIOKITHIRI KWA TAIFA
 
Zitto, jamaa wengi wanasema hujibu email je tatizo ni nini? muda au umuhimu? Mimi nafikiri ni vizuri kujibu emails.
 
MHE. DR. WILBROD P. SLAA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, niungane na wenzangu kuchangia bajeti hii. Nianze kwanza kwa kusema kwamba nimeshtushwa sana na maandalizi ya bajeti ya mwaka huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa bahati mbaya, Watanzania wengi na tukiwemo baadhi yetu sisi Wabunge, tunafikiria bajeti ni hotuba ya Waziri. Bajeti ni vitabu vinne, hotuba ya Waziri, ni ufafanuzi tu wa maeneo. Vitabu vinne visipooana hasa mapato na matumizi, bajeti ile haipo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Watanzania wengi wakiwemo hata wa barabarani, Waandishi wa Habari labda hawajatusaidia sana hapa, baada ya kusikia hotuba ya Waziri, hawajaona takwimu, hawajaona vitabu, wanaisifu bajeti lakini kumbe ni sawa na mtu asiyejua barua iliyowekwa ndani ya bahasha ina nini kumbe imeandikwa unaenda kunyongwa, ndivyo Watanzania tulivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nianze kuchangia kama ifuatavyo:-

Kwanza sina sababu ya kurudia tofauti ambayo iko kwenye vitabu hivi hasa Kitabu cha Mapato, Kitabu cha Kwanza, tofauti katika ujumla wake imeorodheshwa na Mheshimiwa Zitto na Mheshimiwa Cheyo, mimi sitarudia eneo hilo, ni zaidi ya bilioni karibu 120, kama hesabu yangu ni sahihi, nikikosea, Waziri aniambie baadaye.

Mheshimiwa Naibu Spika, nasahihishwa, naambiwa wala siyo 120 ni 136 bilioni. Tofauti ya zaidi ya bilioni 130, ni hesabu kubwa mno.

Waheshimiwa Wabunge, kazi tunayofanya ni kazi ya Kikatiba, Ibara 63(3)(c) inasema:-

“Kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu na wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano, na kutunga Sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huu”.

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi hiyo ya kutunga Sheria, tunaikamilisha kwa kupitisha Finance Bill siku za mwisho. Ndiyo maana kuna Finance Bill na Appropriation Bill. Kwa utaratibu huo, kazi tunayofanya, ni kazi ya kutunga Sheria, ni kazi ya Kikatiba, siyo ya ushabiki wala ya kuona tu kwamba hapa tunaweza kuisifia. Tusifie tunachokijua, tulichokisoma, tulichokiona na kilicho sahihi chenye maslahi kwa Watanzania wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tofauti ya bilioni 130, haikubaliki popote kwamba haiko kwenye vitabu. Naomba kwa hilo, nitangaze siungi mkono bajeti hii na Waziri akitaka ana njia moja tu, kwenda kurekebisha hivi vitabu na siku ya kupiga kura, hivi vitabu ambavyo ndiyo tunavipitisha viwe vimerekebishwa na viletwe Bungeni tuweze kuvipigia kura. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, nimeangalia vile vile kwenye Finance Bill, nimekuta kuna upungufu mwingi. Waheshimiwa Wabunge, tusipokuwa waangalifu, kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, tunaweza tukacheza mchezo mbaya sana. Huu ni mchezo wa hatari hasa Wabunge tukiwa na ushabiki tu kwa kupongeza hotuba badala ya kuangalia vitu vilivyoko ndani ya bajeti. Sitaki kwenda zaidi ya hapo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, unapokuta kwenye bajeti unaletewa kwenye Finance Bill maeneo karibu matano, sita yanasema “the Minister may determine” hapo tuko kwenye hali ya hatari sana katika nchi hii. Imefika mahali Bunge linaacha kazi ya kupitisha bajeti, linampa sasa Waziri, ukisema “the Minister may determine” kiwango atakachochukua EWURA, maana yake Waziri ataenda kuchukua kile kiwango, lakini EWURA nao watapitisha kwa watumiaji wa maji au kwa wasafirishaji kwenye nauli au sijui kwenye kitu gani. Huu ndio utaratibu wa kodi. Kodi hailipwi na yule anayeitoa, yule anaitoa ni chombo cha Serikali cha kuweza kukusanyia kodi mlipa kodi ni mtumia huduma. Sasa mtumia huduma wa EWURA, mtumia huduma wa Civil Aviation, wa Port Authority, wale wote ni watumiaji Watanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kwa maana nyingine tumefanya double taxation bila kuelewa yaani tumemlipisha Mtanzania kodi mara mbili, actually mara tatu. Ile anayolipa ya indirect kwenye huduma mbalimbali kama soda, bia na kadhalika na nguo ya pili ni ile ambayo anadaiwa alipe kwa Regulatory Authority, ile mamlaka yenyewe na ya tatu ile ambayo inachukuliwa sasa kwa mamlaka ambayo na yenyewe itaihamisha baadaye. Hii ni hali ya hatari sana Wabunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda Wabunge tuelewe kabisa kwamba maamuzi yetu yanaweza kuwa kitanzi kwa Watanzania. Bunge linaweza kuwa kitanzi kwa Watanzania tusipokuwa makini na tusipokemea matendo ya aina hii. Sasa Waziri atuambie anaposema anaenda ku-determine, sisi katika Bunge hili kwenye Finance Bill tunapitisha nini? Tunapitisha ku-determine? Tunapitisha viwango vilivyokubalika au tunapitisha…




MHE. DR. WILBROD P. SLAA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakubali lakini unapounganisha vitabu vinne, huwezi kujadili kitu kimoja kwa sababu ni saa hizi ndiyo wanaenda kufanyia kazi. Kwa uzoefu wetu, Finance Bill inajadiliwa kwa nusu saa. Kwa hiyo, sibishani na wewe, nakubali hilo lakini ukweli ni kwamba ni lazima tuangalie mtiririko katika yote kwa sababu yaliyoko kwenye Finance Bill ndiyo yaliyoko kwenye kitabu cha kwanza, kitabu cha pili na kitabu cha tatu. Sasa huwezi kuacha kujadili kwa sababu tu tutajadili mwishoni, mtiririko unaweza kuwa mgumu na yale yote ninayoyasema yako katika kitabu cha kwanza, yamekuwa reflected humo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani niseme tu jambo lingine la mwisho katika hilo. Nimeshtushwa sana na kipengele kimoja hapa. Juzi Waziri alijibu ndani ya Bunge hili kuhusu kodi inayotozwa kampuni moja kule Kilimanjaro Airport kwamba inalipa nini? Sasa ninashangaa hii kampuni inatulipa hela kidogo sana. Nadhani Waziri alisema haizidi milioni tatu. Leo naishangaa kampuni hii tunaenda kuikopa sisi Serikali, hivi unapokopa kampuni ambayo inakulipa kidogo sana halafu wewe unatakiwa kuisimamia, hivi utawezaje kuisimamia hiyo kampuni? Mimi mantiki ya aina hii, nimeshindwa kuielewa, nitaomba Waziri anithibitishie baadaye maana yake ni nini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la mwisho, vitabu vyenyewe pia vina vitu ambavyo havieleweki. Hivi ukituambia Mheshimiwa Waziri Tanzania Harbours Corporation, ni kitu gani katika Tanzania ya leo? Iko kwa Sheria ipi? Ukiniambia kwamba kuna Tanzania Harbours, ipo kwa Sheria ipi? Hivi ni kweli Serikali haijui vyombo vyake? Tukifikia hapa tumefika wapi katika nchi hii?

Mheshimiwa Naibu Spika, namalizia, hayo yako mengi, yasinichukulie muda bure, kwa sababu nataka kusema mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini maana yake ni kwamba vitabu hivi vinatakiwa vitupwe na tena haraka iwezekanavyo, tupate vingine, tuwe na muda wa kusoma vitabu hivi ili tupitishe bajeti.

Mheshimiwa Naibu Spika, niseme mambo mawili tena. La kwanza, bajeti ni lazima imguse mwananchi wa kawaida. Kwa bahati mbaya, kwenye vitabu hivi, mwaka huu na hata kwenye hotuba ya Waziri, amefumbafumba, hotuba haionekani hasa mapato, jumla yake yote ni wapi na kutoka kwenye kifungu kipi?

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tumeshtushwa, tukirudi kwenye vitabu hivi, unapokuta sukari inakuja kuwekewa VAT maana yake ni kwamba, mwananchi ambaye tayari saa hizi amezidiwa, unamwondoa kwenye listi ya watu watakaokunywa chai Tanzania. Kwa hiyo, tujue kwa bajeti hii, tumepunguza wanywa chai, hii ndiyo maana yake hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunapokuta kwamba katika hali ya sasa pembejeo, japo hatukuiongezea kodi lakini kodi za nyuma zilikuwepo na kwa bajeti hii, hatujaifanyia adjustment na mbolea leo ni shilingi 75,000 kule Kusini, shilingi 50,000 kule kwangu Karatu, maana yake ni kwamba mwananchi wa kawaida hawezi kutumia mbolea. Kwa hiyo, bajeti haija-reflect, tumekwenda kugusa maeneo ya kodi madogo sana. Motopoa ni kitu gani kwa Mtanzania wa kijijini, hivi anaielewa? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukisema unaondoa kodi kwenye magunia, kiwanda chenyewe sijui kiko wapi, sijui kama kiko hai, cha Moshi kimefungwa siku nyingi. Hivi effect yake kwa mwananchi wa kawaida iko wapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, Mtanzania alitegemea kwenye bajeti hii, bei ya cement itashuka, bei ya bati itashuka, lakini kwa jinsi ilivyo, kwa kuwa umepandisha vitu vingine, kwa mfano magari ya CC5000, maana yake bei ya vitu hivyo nayo itapanda. Kwa sababu magari ya CC5000, ni malori na mabasi, ukishayagusa hayo, umegusa nauli, utagusa vitu vyote ambavyo vinaendana navyo na vyenyewe vitapandisha bei ya vitu vingine vyote. Kwa hiyo, nilidhani hapa tuna wajibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kilichonishtua katika ukurasa wa 86, Vote 50, nimeona kodi moja ambayo ni ya ajabu na ninaomba Waziri baadaye anisaidie. Tunapotoza kodi kwa mfano kwenye magari, kwenye kipengele kidogo cha 050903, Motor Vehicle Registration Fee, halafu pale chini unarudi tena unasema Motor Vehicle Number Plate, hivi uli-register nini kama hakuna number plate kwenye hiyo gari? Una-register nini kama siyo number plate? Sasa unapokuja kufanya hivyo maana yake ni nini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika nchi zote ninazozifahamu, ukiacha hii ya kwetu, number plate inakuwa control measure, haiwi ni revenue measure, sisi tunageuza kuwa revenue measure. Hili ni jambo ambalo linaongeza gharama bila sababu na tunafikiri haya magari ni ya watu wakubwa, anayepanda taxi siyo mtu mkubwa. Kule vijijini, wala tusifikirie msongamano wa Dar es Salaam kwamba tunaweka hii ili tupunguze msongamano wa magari kule Dar es Salaam, inaweza, lakini kwenye miji yote siku hizi Watanzania wanatumia kama usafiri, kama ambulance kupeleka mgonjwa hospitali kwa sababu magari madogo (taxi) zimejaa kwenye miji yote, nani hajui hili? Anayepanda ni yule mtu wa kawaida. Kwa hiyo, ukiongeza hizi maana yake unamwongezea nauli na taxi sasa hivi hazipandiki tena, nadhani wote tunafahamu hiyo. Kwa hiyo, tunaongeza gharama bila sababu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie kwa kuwa muda si mrefu, nina mambo mawili madogo. La kwanza, nimempelekea Mheshimiwa Waziri hoja zangu nyingine kwa madokezo madogo madogo kwa utaratibu wa kawaida wa Bunge zaidi ya matatu au manne. Nitapenda nipate ufanunuzi wa kina wa masuala hayo. Mengine mwisho wa yote, nadhani ninaweza nikaomba kuunda Kamati Teule ya Bunge tena kama sitapata majibu, sasa namwachia hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ningependa nipate ufafanuzi katika maeneo ya ubadhirifu hasa TANGOLD na MEREMETA. Ninaomba kitu kimoja kikubwa hapa. Tunafahamu sasa na tuna kumbukumbu, tuna nyaraka za Serikali kwamba TANGOLD na MEREMETA zote mbili zimeandikishwa nje ya nchi kama makampuni ya kigeni. TANGOLD imeandikishwa Mauritius nyingine imeandikishwa Uingereza na nimeomba details huko kwako. Naomba zile details zijibiwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwa hapa ninachoomba, ninahitaji kujua accounts zao za nje zinakaguliwa na nani? Tungependa kupata hizo fedha tangu walipoanza mpaka leo walipofunga kama ni MEREMETA na kama ni TANGOLD najua bado ipo, kwa hiyo tungependa kujua wanakaguliwa na nani na kwa nini hizi hela hazionekani na kwa nini kwa mfano account ya TANGOLD iliyoko Dar es Salaam ambayo iko hapa hapa nchini kwetu haikuwa imekaguliwa labda kama imekaguliwa, ni mwaka huu kwa mara ya kwanza. Kwa nini miaka yote haijakaguliwa na sasa ina fedha kiasi gani lakini kwa nini haikuwa inakaguliwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho nimempelekea Mheshimiwa Waziri. Vile vile tumeipongeza TRA na mimi naipongeza lakini Kambi ya Upinzani tulisema kuna unyanyasaji, nimempelekea ushahidi wa aina ya unyanyasaji uliokuwa umetokea. Hatujui ni wangapi wamenyanyaswa kwa kiwango hiki. Haiwezekani kampuni ya Kitanzania tunayotakiwa kui-promote tunainyanyasa halafu tunasema hakuna rushwa, wakati mwingine inaweza kuleta mashaka kumbe mapato, makusanyo yanaongezeka. Kwa matukio ya aina hii, nitapenda nipate maelezo ya kina kuhusu suala la aina hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili nisigongewe kengele kwa kuwa mimi ni wa mwisho, naomba kurudia kusema kwamba mimi sitaunga mkono hoja hii ya bejeti na ninaomba Waziri anipe taarifa ya kina ni kwa nini vitabu hivi vinatofautiana. Kama atakubaliana, aende kutengeneza vingine ili budget debate iende vizuri kwa sababu Wabunge tunatakiwa kuwa na information sahihi ili tunapopitisha tuwe tunapitisha kitu ambacho tuna uhakika nacho.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. (Makofi)
 
Adai hao watu wakamatwe sasa maana hayo mambo ya meremeta tushajua na EPA na kila kitu...Ripoti zipo na watuhumiwa wameruhusiwa kwenda kuchangia bajeti...Mi naona tuanze kamata kamata.
 
Huu ndio umemfanya hata Spika kuahirisha kutoa mwongozo juu ya Bajeti tunasubiri hiyo kesho kama waziri atasema kitu gani baada ya jana kukubali makosa.
 
Sasa, Mkuu Dr. Slaa kanionyesha ukali wake.... yani huyu namkubali sana maanake kagusa sehemu ambazo mimi binafsi zilinishtua sana.
Yes.. mkuu Geeque, namkubali Dr. Slaa ameiva kisawasawa na hotuba zake, maswali yake yote yanalenga manufaa ya mwananchi!
 
MHE. DR. WILBROD P. SLAA:

Mheshimiwa Naibu Spika, Watanzania wengi wakiwemo hata wa barabarani, Waandishi wa Habari labda hawajatusaidia sana hapa, baada ya kusikia hotuba ya Waziri, hawajaona takwimu, hawajaona vitabu, wanaisifu bajeti lakini kumbe ni sawa na mtu asiyejua barua iliyowekwa ndani ya bahasha ina nini kumbe imeandikwa unaenda kunyongwa, ndivyo Watanzania tulivyo. (Makofi)
Jiongelee mwenyewe na hao wengi, Dr. Slaa!

Usituchanganye wote kwenye kapu la dhihaka!

Na hata hao wengi unawakejeli bure tu. Mwanachi wa kawaida atapataje access ya kupitia vitabu vinne vya bajeti kama hotuba ya Waziri ime fudge the data, Bunge lenu lenu rubber stamp "vitabu vya kutupa" vya Mkulo, na Tanzania hakuna Press?

Kuna siku Watanzania wataanza kuheshimiwa na Viongozi wao.

No, sipigi makofi!
 
Jiongelee mwenyewe na hao wengi, Dr. Slaa!

Usituchanganye wote kwenye kapu la dhihaka!

Na hata hao wengi unawakejeli bure tu. Mwanachi wa kawaida atapataje access ya kupitia vitabu vinne vya bajeti kama hotuba ya Waziri ime fudge the data, Bunge lenu lenu rubber stamp "vitabu vya kutupa" vya Mkulo, na Tanzania hakuna Press?

Kuna siku Watanzania wataanza kuheshimiwa na Viongozi wao.

No, sipigi makofi!

PR na communication kazi bongo, Dr. Slaa ana point za nguvu sana lakini kujieleza shida.I have the feeling kwamba hili swala halijawa exposed kwa maximum effect.Halafu hilo la ku-belittle Watanzania unnecessarily nililiona.Inaonekana ana imani kama za Nyani Ngabu.

Marekani Obama kasema watu wako "bitter" tu cha mtema kuni kakiona !

Slaa inaonekana ameibuka na jazba sana, kwa kukerwa sana bila shaka.Lakini huwezi kuanza kuikosoa serikali kwa kukosa umakini kwa kuja na data zilizokosa makini.Amesimama kuzikosoa figures za serikali bila ya yeye mwenyewe kuwa na uhakika

Mheshimiwa Naibu Spika, nasahihishwa, naambiwa wala siyo 120 ni 136 bilioni. Tofauti ya zaidi ya bilioni 130, ni hesabu kubwa mno.

Inaonekana kama mheshimiwa alikuwa anatoa an impromptu speech, kitu hakijaandaliwa wala kuandikwa chini, is that so?


For what it takes amefanya kazi nzuri sana ku expose uozo, lakini angeweza kuwa organized zaidi.
 
Kuhani,
Mkuu umeyasoma vizuri maneno ya Dr. Slaa?...
Alichosema ni kwamba wapo watu wanashangilia kuona bahasha iliyokuja (hotuba ya Waziri wa fedha) bila kufahamu yaliyomo ndani ya parcel hiyo!...
Na ikiwa wewe umeshangilia ujio wa bahasha hiyo then umo katika fungu la kufikiria upya makofi ulopiga mwanzoni!.. na kaeleza vizuri yaliyokuwemo ktk bahasha hiyo ambayo kayafananisha na hukumu ya kunyongwa!
Kifupi hata yeye mwenyewe hakupiga makofi kama unavyosema wewe....bali kalifungua kwanza hilo pakacha na kusoma yaliyomo, jambo ambalo watu wengi hawakufanya.
 
PR kazi bongo, Dr. Slaa ana point za nguvu sana lakini kujieleza shida.

Ya, hajui kujieleza. Lakini kwa Bongo, ni creme de la creme.

Sasa yeye hawezi, nani ataweza kujieleza Bongo?
 
Back
Top Bottom