Mr.Toyo
JF-Expert Member
- Feb 9, 2007
- 433
- 117
Wangwe agoma kufuta kauli yake bungeni
MBUNGE wa Tarime Chacha Wangwe amekataa kufuta kauli yake ya Julai 10, mwaka jana kwamba kulikuwepo na vitendo vya vurugu na mauaji wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa wa Rais na wabunge katika Jimbo la Tarime, Desemba,2005.
Mbunge huyo alisema hayo katika waraka aliomwandikia Spika wa Bunge Samuel Sitta, akisema yeye mwenyewe na wanachama, wananchi na wapiga kura wa Jimbo hilo waliathirika moja kwa moja na vurugu, majeraha na mauaji hayo na kwamba hakutoa kauli hiyo kwa urahisi au kwa kuifurahia au bila kufikiria uzito wake.
Nilitoa kauli hiyo kwa kuelewa fika uzito wake lakini kwa kutegemea kwamba ingefanyiwa kazi na vyombo vinavyohusika ili hatua za kinidhamu au kisheria kuchukuliwa dhidi ya waliohusika na vitendo hivyo vya kihalifu.
Suala la tafsiri ya ya kauli yangu halikuwa na haliwezi kuwa ni hoja ya msingi. Kwa hiyo, sidhani kama ni sahihi au halili kwa mimi kuadhibiwa kwa kusema ukweli ambao hata hivyo umetafsiriwa na Mheshimiwa Spika, alisema Wangwe.
Mbunge huyo katika waraka wake aliomwandikia Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano alisema hawezi kufuta kauli yake kwa kuwa Kamati ya Bunge imethibitisha ukweli wa kauli yake.
Katika waraka huo alisema kuwa anafahamu fika kwa msimamao huo anaweza kuadhibiwa na Bunge na kwamba hata kama ataadhibiwa itakuwa ni kwa sababu ya kusema ukweli uliothibitishwa na Kamati iliyoundwa na Spika.
Nilitegemea baada ya Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama kuthibitisha ukweli wa kauli yangu, Mheshimiwa Spika ungevielekeza vyombo husika kuifanyia kazi kauli hiyo na ripoti ya Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, alisema Wangwe katika sehemu ya waraka huo.
Mbunge huyo alisema kwa kuwa aliitoa kauli hiyo ndani ya Bunge na alitakiwa kuithibitisha mbele ya Bunge, alitegemea kwamba ripoti ya kamati hiyo ingetolewa hadharani kwa Wabungeni ili nao wafahamu ukweli au uongo wa kauli yake.
Alisema alitegemea kuwa angepatiwa nakala ya ripoti ya Kamati hiyo ili ajue ni uongo upi hasa anaotakiwa kuufuta kusudi asiadhibiwe na Bunge.
Yote haya hayajafanyika kwa sababu ambazo ni wewe mwenyewe unayaweza kuzifahamu au kuzielezea. Kwa maana hiyo, siko tayari kufuta kauli ya kweli na ambayo ukweli wake umethibitishwa na Kamati ya Bunge. Alisema Wangwe.
Mbunge huyo alisema kuwa haoni sabuabu ya kufuta kauli yake kwa kuwa Kanuni za Bunge haziruhusu wala kuunga mkono tafsiri ya kauli ya Spika juu ya kauli yake (Wangwe) na kwamba hadhani kama ni sahihi au halali kwa yeye kuadhibiwa kwa kusema ukweli.