jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,375
- 25,453
Jumatatu, Juni 16, 2008
MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kunipa nafasi ya kuchangia hotuba hizi mbili hotuba ya bajeti na hotuba ya hali ya uchumi. Ninafahamu ya kwamba sisi kama Kambi ya Upinzani ni Serikali kivuli. Jukumu letu la kidemokrasia ni kuonyesha pale ambapo wenzetu wa Serikali inayoongoza hawapaoni na tumeonyesha katika bajeti yetu kivuli, maeneo ambayo wenzetu hawakuyaona katika bajeti iliyopita, wameyaona katika bajeti ya mwaka huu na wakawa wamepelekea Serikali kuweza kuongeza mapato. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa Waheshimiwa Wabunge wanapozungumza na kudhihaki bajeti kivuli ambayo Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed ameitoa kwamba ni alfu lela ulela nashindwa kuelewa sifa zilizowafanya Wabunge hao kuja katika Bunge hili. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nitaanza na hali ya uchumi.
NAIBU SPIKA: Naibu Spika husikiliza yote tu, alfu lela ulela na mengineyo. (Makofi/Kicheko)
MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nitaanza na hali ya uchumi. Tuna changamoto kubwa sana kama nchi, kwamba hivi sasa tunaishi katika uchumi unaokuwa lakini umaskini haupungui na hii ndio changamoto ambayo bajeti inapaswa kuijibu na haiwezi kujibiwa kwa bajeti ya mwaka mmoja inajibiwa kwa utaratibu maalumu. Toka tumeingia katika Bunge hili, hii ni bajeti ya tatu, kumekuwa na rekodi za uchumi kukua lakini taarifa mbalimbali za Serikali, kwa mfano Taarifa za hali ya umaskini. Toka tumekuwa Wabunge kumekuwa na taarifa mbili za hali ya umaskini (P&HDR 2005 na 2007), zote zinaonyesha kwamba umaskini kwa wananchi bado ni mkubwa na katika bajeti iliyopita tulizungumzia suala zima la madhara ya kupandisha kodi za baadhi ya vitu kwa maisha ya wananchi na wenzetu (CCM) wakakataa kata kata lakini athari zinaonekana hivi sasa na leo tunaiita bajeti ambayo Mheshimiwa Waziri Mkulo ameitoa kwamba ni bajeti ya wananchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, haiwezi kuwa bajeti ya mwananchi kwa sababu kodi ambazo zilipandishwa mwaka jana hazijashushwa kurudishwa katika viwango vya mwaka 2006/2007, itakuwa ni bajeti ya mwananchi iwapo tu kodi hizo zitakuwa zimeshushwa lakini kitendo cha kuziacha kodi hizo kama zilivyo bado kitaendelea kufanya mfumuko wa bei uweze kuendelea na hili nitaeleza nitaelezea huko chini.
Uchumi wetu umebadilika, tumetoka katika uchumi unaotegemea kilimo tumeenda katika uchumi unaotegemea huduma. Asilimia 47.3 sasa ya uchumi wetu ni huduma na asilimia 28.2 tu ndio kilimo.
Lakini mipango yetu bado ni kana kwamba uchumi unategemea kilimo na tumeonyesha baadhi ya wasiwasi wetu kutokana na takwimu ambazo zimetolewa lakini mipango ya nchi ambayo uchumi wake ambao takriban nusu unategemea huduma ni tofauti na mipango ya nchi ambayo takriban zaidi ya nusu inategemea kilimo. Bajeti hii ni mwendelezo wa bajeti zilizopita ambapo huduma ilikuwa ina mchango mdogo sana katika uchumi, kwa hiyo kwa vyovyote vile kutokana na bajeti hii ni vigumu sana changamoto za sasa za nchi kuweza kujibiwa.
[MHE. KABWE Z. ZITTO]
Mheshimiwa Naibu Spika, sekta ya madini ambayo ndio ilikuwa sekta inayoongoza kwa ukuaji, hivi sasa imekuwa ni sekta ya pili au ya tatu kwa ukuaji, ukuaji wa uchumi sasa unategemea sekta ya mawasiliano na kwa kiasi kikubwa sekta hii bado haichangii vya kutosha katika mapato ya Serikali, kuna baadhi ya maeneo ambayo Waziri wa Fedha ameonyesha ili Serikali iweze kukusanya pesa zaidi lakini wakati anaangalia maeneo hayo bado eneo lenyewe la sekta ya madini bado halikuangaliwa hata kidogo na huwa tunapata wasiwasi mkubwa sana kwamba baadhi ya mapendekezo ambayo Kamati ya Rais ya kuangalia sekta ya madini iliyotoa na si baadhi mapendekezo, yote hayajachukuliwa, matokeo yake ni kwamba bajeti imeangalia zaidi kupandisha kodi za walaji yaani consumption tax na kuacha kabisa kupandisha kodi kwa watu ambao ni wale wazalishaji kwa maana ya wawekezaji na wawekezaji wa ndani na wa nje ya nchi siyo wawekezaji wa nje peke yake.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo tumejikuta tuna chumi mbili ndani ya nchi moja uchumi wa matajiri na uchumi wa maskini, uchumi wa maskini wanauita ni rural economy ambapo ndiko wanakoishi na matokeo yake ni kwamba maskini either bidhaa ambazo yeye analima, (anazozalisha) hazikui lakini bei za bidhaa ambazo yeye anatumia zinakuwa, kwa hiyo maskini anauza kwa bei za vijijini na ananunua kwa bei za mjini. Kwa hiyo hali yake ya kipato ni lazima iendelee kuwa chini, ni tegemeo la bajeti yeyote ile katika nchi yeyote ile iwapo bajeti ikitumika kama sera ya kuangalia ni jinsi gani ambavyo uchumi wa nchi unakwenda wataweza kuangalia ni jinsi gani ya kupunguza gharama hii ambayo mkulima anapata kwa ajili ya kuhakikisha kwamba anabakia na fedha ya kutosha.
Mheshimiwa Naibu Spika, tumeelezwa kwamba Serikali imeweka vipaumbele na vipaumbele vimetajwa na pesa zimetajwa kwa ajili ya vipaumbele lakini napata wasiwasi sana kwamba inawezekana kuna ukosefu wa uratibu ndani ya Serikali, taarifa ya hali ya umaskini ya mwaka 2007 ambayo imetolewa mwaka huu imeonyesha changamoto ambazo nchi inazo na ni maeneo gani ambayo yakitiliwa mkazo tutaweza kwenda mbele kiuchumi. Wenyewe wanaita drivers of growth na wameweka maeneo manne ambayo yanapaswa kuangaliwa na kuwekewa mikakati maalum - transport services ambayo ndani yake kuna miundombinu na huduma zingine za usafiri, madini, horticulture kwa Kiswahili nadhani ni masula ya maua ukulima wa maua na kadhalika na utalii.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ukiangalia bajeti jinsi ilivyokaa jinsi gani ambavyo tumegawa rasilimali zetu kidogo ambazo tunazipata haikuangalia kabisa vipaumbele hivi ambavyo taarifa ya Serikali imezitoa taarifa ambayo ndio inafanya tathmini ni wapi ambapo tunakwenda kuhusiana na suala zima la kupunguza umaskini.
Nadhani Wizara ya Fedha na Uchumi inabidi iangalie kwa sababu taarifa ya hali ya umaskini inatolewa na idara ndani ya Wizara ya Fedha na Uchumi kwa hiyo ni rahisi sana kwa idara hiyo ya kuondoa umaskini kuwasiliana na Idara ya Sera ya Wizara ya Fedha, kuwasiliana na Idara ya Bajeti ya Wizara ya Fedha ili kuweza kuangalia ni vipi ambavyo tunavyofanya vipaumbele vyetu, tukiamua kuweka vipaumbele kufurahisha wananchi kwa sasa huko tunakokwenda kutakuwa ni kugumu sana kwa sababu utagawa pesa kwa kila sekta lakini zile sekta hazitachochea sekta nyingine. Kwa hiyo kuna umuhimu mkubwa sana wa kuweza kuangalia vitu kama hivyo katika hali ya juu na ni suala lile lile la kubadili mindsett.
[MHE. KABWE Z. ZITTO]
Mheshimiwa Naibu Spika, ni vipi ambavyo bajeti yetu inaendana na changamoto ambazo tunazo hivi sasa? Kwanza bajeti imeshindwa kabisa kukusanya kodi zinazostahili kwenye madini na ninashindwa kuelewa ni kwa sababau gani, kwa sababu inafahamika wazi kabisa kwamba mwaka 1997 na Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed ameielezea hapa, Bunge hili lilitunga sheria ambayo ilitoa unafuu usio na lazima kwa makampuni ya madini kwa kiasi cha asilimia 15 unafuua mbao umeifanya Taifa lipoteze shilingi bilioni 883 katika kipindi cha miaka 10 toka sekta ya madini ianze kukua katika Taifa letu.
Mheshimiwa Naibu Spika, tulitegemea kwamba katika finance bill ya mwaka huu Waziri wa Fedha angefuta kabisa sheria hiyo kwa sababu sheria hiyo bado iko kwenye vitabu vyetu vya sheria na inafanya makampuni ya madini ambayo yana mikataba yasiweze kulipa kodi hiyo, kuna mashauriano ambayo Serikali imefanya na baadhi ya makampuni ya madini lakini kama suala hili hatutalitoa kwenye sheria halitaweza kusaidia na mfano mmoja tu wa madhara ya sheria hiyo ni kwamba kampuni ya Bulyanhulu Gold Mine ambayo inangepaswa kuwa imeanza kulipa kodi ya mapato haitalipa kodi ya mapato kutokana na faida yake mpaka mwaka 2019 yaani haitaanza kulipa corporate tax mpaka mwaka wa mwisho wa Rais wa awamu ya tano na hawa wameanza na Rais wa awamu ya tatu. Kwa hiyo unaweza ukaona ni jinsi gani ambayo Taifa linapoteza na mabilioni ya fedha kwa sababu ya sheria ambazo tumezitunga sisi wenyewe na tunao uwezo wa kuweza kuzirekebisha.
Mheshimiwa Naibu Spika, misamaha, mwaka 2005 wakati tuko kwenye kampeni za uchaguzi Serikali ilitoa misamaha ya kodi miwili wa kwanza ya mafuta kwamba makampuni ya madini hayatalipa kodi ya mafuta mpaka watakapomaliza kama ni dhahabu wanayochimba, kama ni almasi wanayochimba, kama ni Tanzanite wanayochimba na tulishauri kwamba msamaha huo ufutwe kwa sababu ni msamaha ambao hausaidii chochote.
Mheshimiwa Naibu Spika, na msamaha huu ungefutwa ungeweza hata kusaidia kupunguza zile kodi ambazo tulizipandisha mwaka jana kupelekea mfumuko wa bei uweze kutokea. Sisi kama Tanzania hatuna uwezo hata kidogo wa ku-control bei ya mafuta katika soko la Dunia lakini tunao uwezo wa ku-deal na kodi zetu ili kuweza kuhakikisha kwamba tunapunguza ukali wa upandaji wa bei katika soko la Dunia. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ilipaswa kuangalia hizo kodi zetu ili ziweze kupunguza huo ukali wa maisha. Mwaka 2007/2008 aliyekuwa Waziri wa Fedha Mheshimiwa Zakia Meghji alionyesha katika sura ya bajeti kwamba Serikali itakusanya kiasi fulani cha mapato shilingi bilioni 239 kutokana na marekebisho mbalimbali ya kodi, katika bajeti ya mwaka huu Waziri wa Fedha hakuonyesha viwango mbalimbali vya mabadiliko ya kodi vitaifanya Serikali ikusanye kiasi gani? Kwa hiyo ninadhani ni muhimu sana kuwa na mtiririko ulio sawa au consistency ili kuhakikisha kwamba kunakuwa na hali ambayo ni nzuri zaidi.
[MHE. KABWE Z. ZITTO]
Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa, bajeti ni vitabu vinne, volume one mpaka volume four, volume one ndio inayo-dill na mapato ya Serikali na ninasikitika kwamba mara nyingi hatuiangali hii volume. Ukiangalia kitabu cha kwanza cha bajeti utagundua mambo mawili la kwanza tunategemea sana kodi za biashara kwa maana ya import, import duties. Mabadiliko ya kodi ambayo Serikal imeyatangaza sasa asilimia 50 itatokana na import duties, hii ni hatari sana katika uchumi wa sasa, tunaokwenda, tuna East African Customs Union tunaenda kwenye common market, tunasaini EPA ambayo itaondoa kodi mbalimbali dhidi ya European Union tutapata tatizo kubwa sana kurekebisha kodi hizi tutajikuta kwamba tunakuja kuumia sana huko baadaye.
Katika revenue book, wakati Waziri wa Fedha anasema kwamba tutakusanya shilingi bilioni 58 kwa mauzo ya hisa za NMB, kwenye revenue book zinaonekana shilingi bilioni 42. Tunapopitisha bajeti tunachoangalia ni revenue book, ni nini ambacho tunakichukua? Ni hotuba ya bilioni 58 au ni revenue book ya bilioni 42, nilikuwa ninaomba Waziri wa Fedha aweze kuliangalia hilo.
Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho kabisa, kama tunataka kuongeza uzalishaji wa kutosha kwenye baadhi ya mazao ambayo tunayo ni lazima tuangalie jinsi gani ya kutoa incentives kwa baadhi ya mazao. Mimi nitatoa mfano mmoja na nilitoa taarifa hii toka mwaka jana kwamba leo India wameweka compulsory usage ya magunia yao ya jute kwa ajili ya mazao yote ya India. Sisi hatujaweka compulsory usage ya maguni yetu ya katani, matokeo yake ni kwamba tunakuwa tuna-export jobs kwenda Bangladeshi na India kwa sababu hatulindi sisal yetu, katani yetu wala hatulindi viwanda matokeo yake ni kwamba baadhi ya wawekezaji wamenunua viwanda havifanyi kazi kwa sababu ya mazingira hayo ya kikodi.
Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa ninaomba Waziri wa Fedha ajaribu kuangalia uwezekano wa angalau mazao mawili, mahindi na korosho ziwe ni compulsory kutumia maguni ya katani ili ku-stimulate uzalishaji wa katani na kufanya viwanda vya katani ambavyo vimekufa hivi sasa viweze kuzalisha magunia ya katani na yaweze kutumika katika nchi, vinginevyo itakuwa ni tatizo ambalo tutaendelea nalo tutaendelea kutegemea kodi kutokana na imports ambazo madhara yake ni makubwa sana kutokana na Dunia ya sasa ya globalization.
Ni lazima kuangalia Serikali isikwepe kazi yake ya distributive role. Ni kazi ya Serikali yeyote Duniani kukusanya kutoka matajiri kuwapeleka maskini ili kuweza kupunguza gharama za maisha yao na ndio kazi ya bajeti kama sera na siyo bajeti kama urari wa mapato na matumizi.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru sana. (Makofi)
Mh Zitto haya mambo uliyoyazungumzia ni muhimu.Lakini yanajulikana na ulishawahi kuyapigania huko bungeni na wakaku suspend na baadae kamati ikaundwa ya madini ambayo KUNA MAFISADI WALIKUWA NDANI.... Johnson Mwanyika....Mtuhumiwa mkuu wa RICHMOND alikuwepo kwenye kamati EPA.Mafisadi waliwekwa pamoja na wewe ambaye ulinyimwa nafasi ya kupata muafaka utakaotokea kwenye kamati teule ya bunge ili kuweza kuona ni kwa jinsi gani haki huru ya watu huru itapatikana.Tukasema usiingie kwenye kamati!Kuingia kwako kamatini kulisaidia sana kumsafisha kiaina mfisadi na hivyo kupelekea kuyumba kwa haki.Mh Zitto....Kama hutaweza kuja na udhibitisho kuwa wabunge wa CCM hawatakupa tena umaarufu kwa kukufukuza BUNGENI na Kukuundia kamati nyingine zenye mishahara minono...Basi utakuwa umetuweka kwenye njia panda!