Kutoka Bungeni: 2006 - 2010

Kutoka Bungeni: 2006 - 2010

Asha hao walikuwa wanachangia as Chadema au Serikali kivuli ya Wapinzani?....

Kama nimekukera na UCCM wako kameze chupa! Wasemaji wa upinzani wanasema kupitia hotuba. Michango hiyo ya kina Dr Slaa, Zitto, Cheyo nk wamezungumza kama wabunge wakiwakilisha majimbo yao ya uchaguzi kwa tiketi ya vyama vyao. Lakini soma hitimisho langu, nimesema wapinzani endeleeni kukandamiza kibara mpaka kieleweke. Hii sasa ni kwa ujumla wao!

Asha
 
Kazi Nzuri kijana.
Naona unafanya uliyotumwa kufanya. Keep up the good work
 
Mimi nashindwa kuelewa kabisa, inakuwa akina Zitto wanaona haya mambo lakini akina CCM hawaoni? Wao wamesoma shule gani hasa?

CCM wanakuwa bungeni kivuli tu. Wao ni wale ambao tunasema wanaomba ubunge ili kutimiza haja za binafsi. Hawana lolote na hata hivyo vitabu hawasomi hata kidogo. Wapinzani endeleeni kuwapa hard time akina Kikwete na wanazi wenzake.
 
Asha Conclusion yako haimake sense wakati ushatoa Credits ktk utangulizi wako...kama wanajeshi wanakwenda Vitani, then credits goes for few...nafikiri tutashindwa vita...

Utangulizi wako ni wa Ushabiki unaonesha upungufu wako ktk kufikiri mambo Wide...na Ktk national interest...the bad image ulionayo ktk akili yako kila anae kuchallenge the opposite ni CCM...the same Image wabunge wa CCM ndio walionayo kuwa kule bungeni...wao watapinga anything as long kitatoka upinzani...
 
Asha Conclusion yako haimake sense wakati ushatoa Credits ktk utangulizi wako...kama wanajeshi wanakwenda Vitani, then credits goes for few...nafikiri tutashindwa vita...

Utangulizi wako ni wa Ushabiki unaonesha upungufu wako ktk kufikiri mambo Wide...na Ktk national interest...the bad image ulionayo ktk akili yako kila anae kuchallenge the opposite ni CCM...the same Image wabunge wa CCM ndio walionayo kuwa kule bungeni...wao watapinga anything as long kitatoka upinzani...

Chuma, mimi na wewe tuko humu siku nyingi hivyo naujua msimamo wako katika masuala ya kitaifa. Kama umekereka shusha pumzi tusonge mbele. Yani kusema kwamba Dr Slaa na Zitto ni wabunge wa CHADEMA imekuwa nongwa. Ulitaka nisemeje? Angekuwa Dr Slaa amezungumza kama waziri kivuli nisingesema hayo. Lakini amezungumza kama mbunge binafsi yakhe!. Au unapenda tu CCM ndio isifiwe? Kwa taarifa yako, kama watanzania hatutafikiria udhaifu wa CCM na kufikiria chama mbadala wake hatutaweza kubadili huu mfumo wetu wa kifisadi. Upinzani oyeeeeeeeee oyeeeee. Bajeti mbadala juuuuuuuuu juuuuu. CCM chiniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Mwanajeshi asiyejua jeshi lake hafai vitani kwa kweli, askari wenzake ni heri wampige risasi manake anaweza kuwauza kwa adui

Asha
 
Bunge hili lilitunga sheria ambayo ilitoa unafuu usio na lazima kwa makampuni ya madini kwa kiasi cha asilimia 15 unafuua mbao umeifanya Taifa lipoteze shilingi bilioni 883 katika kipindi cha miaka 10 toka sekta ya madini ianze kukua katika Taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tulitegemea kwamba katika finance bill ya mwaka huu Waziri wa Fedha angefuta kabisa sheria hiyo kwa sababu sheria hiyo bado iko kwenye vitabu vyetu vya sheria na inafanya makampuni ya madini ambayo yana mikataba yasiweze kulipa kodi hiyo,...Kwa hiyo unaweza ukaona ni jinsi gani ambayo Taifa linapoteza na mabilioni ya fedha kwa sababu ya sheria ambazo tumezitunga sisi wenyewe na tunao uwezo wa kuweza kuzirekebisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, na msamaha huu ungefutwa ungeweza hata kusaidia kupunguza zile kodi ambazo tulizipandisha mwaka jana kupelekea mfumuko wa bei uweze kutokea.

Waziri anaweza kufuta sheria ya Bunge?

Mheshimiwa Zitto, tafadhali naomba unisaidie hapo.
 
Waziri anaweza kufuta sheria ya Bunge?

Mheshimiwa Zitto, tafadhali naomba unisaidie hapo.

Kuhani Mkuu

Finnance Bill ambayo huwa Act baada ya kupitishwa na sheria inayosimamia utekelezaji wa bajeti.

Alichotegemea zitto hapo ni kuwa katika mjadala wa bajeti wa sasa katika vile vitabu vinne kile cha nne ambacho ni finnance bill kingekuwa na hoja ya serikali ya kufuta hiyo misamaha ili iwe finance act itayaosimamia bajeti ya mwaka huu!

Lakini Mkullo na wenzake hawayakuyaona hayo......wanafikiria kuhusu uchawi tu

Asha
 
Hansard ya leo bado haijatoka. Ikitoka tu wana JF mtapata nini alisema Cheyo na ni nini alisema Dr. Slaa

Mchango wangu ni wa jana jioni ndio maana hansard yake tumepata

Uendelee hivyo hivyo Zitto, kujiweka na kujichanganya na Watanzania wenzako ili kuwafahamisha mambo mbali mbali muhimu yanayojiri katika nchi yetu. Ukiendelea hivi na kujiepusha, kuukemea na kupambana na mafisadi kwa nguvu na uwezo wako wote basi siku zote utakuwa kipenzi cha Watanzania bila kujali itikadi zao maana utakuwa umeweka maslahi ya nchi na Watanzania mbele kuliko maslahi ya chombo chochote kile ndani au nje nchi. Mungu akujalie ili ututumikie Watanzania kwa kipindi kirefu kijacho.

Kuna wengine wanadhani kwamba JF ni kundi la wasaliti ambalo kila kukicha ni kusema mabaya tu ndani ya nchi yetu na kusahau mazuri yanayofanyika. Ukweli ni kwamba asilimia 99.9 ya wana JF wana mapenzi ya kweli na Tanzania na wanataka kuona nchi yetu inapiga hatua kubwa ya maendeleo na kuweza kuinua viwango vya maisha vya Watanzania walio wengi, bali tunayoyaona kila kukicha ni maamuzi ambayo hayaheshimu matakwa na maoni ya Watanzania hivyo kutokuwa na maslahi yoyote kwa Watanzania bali kwa wageni na kundi la mafisadi wachache.

Wengi wetu tulidhani burden kubwa waliyobebeshwa Watanzania ya kulipa kodi itapunguzwa ili 'wawezekaji' hasa katika sekta ya madini walipie asilimia kubwa ya makusanyo ya kodi ndani ya nchi yetu, lakini si hivyo 'wawezekaji' pamoja na kuwa wanapata faida kubwa sana kutoka kwenye rasimali zetu kama dhahabu, gesi, Tanzanite n.k. bado wanalipa asilimia ndogo sana ya kodi au hawalipi kabisa kitu mabcho Watanzania wengi hatukielewi. Kuna faida gani basi ya kuwakaribisha 'wawekezaji' kama nchi hainufaiki kwa chochote kutoka kwao?
 
Kuhani Mkuu

Finnance Bill ambayo huwa Act baada ya kupitishwa na sheria inayosimamia utekelezaji wa bajeti.

Alichotegemea zitto hapo ni kuwa katika mjadala wa bajeti wa sasa katika vile vitabu vinne kile cha nne ambacho ni finnance bill kingekuwa na hoja ya serikali ya kufuta hiyo misamaha ili iwe finance act itayaosimamia bajeti ya mwaka huu!

Ahsante.

Kwa hiyo Bunge liliitungia Serikali sheria mbaya halafu Wabunge hapa walalamika kwa nini Serikali haijaleta pendekezo la kufuta sheria mbovu.

Kama Wabunge wanajua sheria waliyotunga ni mbovu, kwa nini wasubiri pendekezo kutoka kwa waliowatwika hiyo sheria mbovu ili kuifuta? Kazi yao nini kama sio kutunga na kufuta sheria mbovu bila kusubiri kuombwa?
 
Asante sana mheshimiwa Zitto kwa mchango maridhawa.....

Ndugu zangu nadhani siku ambayo watanzania tutakuwa kitu kimoja katika kupambana na adui yetu, nadhani huo utakuwa mwanzo na mwisho wa matatizo yote. Hakika hatuwezi kuwa na approach moja, lakini kweli tujiulize kwa nini hata maswala ya msingi ya kitaifa tunaweka itikadi mbele?

Tujiulize makampuni yanasamehewa kodi..billions and billions...wakati wananchi hata mafuta ya taa hawana...na sasa tunaanza kugundua wenye hisa kwenye hayo makampuni ndo hao viongozi wetu...Inasikitisha sana. Na mtu bila mshipa wa aibu..yuko busy anatetea unazi kama huu..

Naamini CCM ni chama kama vyama vingine, hata supporters wa CCM naamini siyo wote ni mafisadi au wanafaidika na ufisadi, jamani tuweke itikadi nyuma linapokuja swala la kujadili whats good for our country! Tanzania ikipata maendeleo hata ndugu zako watafaidika..no one here hates CCM, as CCM zelouts may want us to believe......we hate what they do! Simple.

CCM mnatulostisha kikweli na tumechoka kuwa laughing stock ya dunia..kila kigezo cha umasikini tunachukuliwa sisi (iwe UN, WB, DONORS etc)..haki ya nani iko siku mtajuta kuzaliwa..we are tired!
 
Mkuu Zitto,

Hongera kwa kazi nzuri mnayoifanya. Umadhubuti wenu umeanza kufanya wingi wa wabunge wa CCM isiwe hoja. Jana jioni nilipomwona mbunge wa mvomero akiwataka wabunge kuachana na mambo ya EPA nilishtuka na kuhisi kuwa tayari kuna kitu kimeshapangwa na hawa wana CCM ambacho chaweza kuwa kama kile alichofanya Mdhihiri mwaka jana.
Matumaini ya wapenda maendeleo ya nchi ni kuwa hakuna kitakachowafanya mrudi nyuma. Umma wa watanzania uko nyuma yenu mpaka kilichotokea EPA na Richmond kieleweke !
 
Bunge hili lilitunga sheria ambayo ilitoa unafuu usio na lazima kwa makampuni ya madini kwa kiasi cha asilimia 15 unafuua mbao umeifanya Taifa lipoteze shilingi bilioni 883 katika kipindi cha miaka 10 toka sekta ya madini ianze kukua katika Taifa letu.


...kweli hapa tuna serikali,na msisahau holiday in , Sheraton,kempsink na makampuni ya Rostam aziz wamepewa msamaha kiasi gani ukichanganya na incompetency ya TRA sitashangaa tunapoteza zaidi ya 50% ya pesa zote...JK kweli upupu bora aondoke tuu lakini atashinda kwa 80% ya Jf votes,itabidi muendelee kula jeuri yenu
 
Jumatatu, Juni 16, 2008
Mheshimiwa Naibu Spika, tulitegemea kwamba katika finance bill ya mwaka huu Waziri wa Fedha angefuta kabisa sheria hiyo kwa sababu sheria hiyo bado iko kwenye vitabu vyetu vya sheria na inafanya makampuni ya madini ambayo yana mikataba yasiweze kulipa kodi hiyo, kuna mashauriano ambayo Serikali imefanya na baadhi ya makampuni ya madini lakini kama suala hili hatutalitoa kwenye sheria halitaweza kusaidia na mfano mmoja tu wa madhara ya sheria hiyo ni kwamba kampuni ya Bulyanhulu Gold Mine ambayo inangepaswa kuwa imeanza kulipa kodi ya mapato haitalipa kodi ya mapato kutokana na faida yake mpaka mwaka 2019 yaani haitaanza kulipa corporate tax mpaka mwaka wa mwisho wa Rais wa awamu ya tano na hawa wameanza na Rais wa awamu ya tatu. Kwa hiyo unaweza ukaona ni jinsi gani ambayo Taifa linapoteza na mabilioni ya fedha kwa sababu ya sheria ambazo tumezitunga sisi wenyewe na tunao uwezo wa kuweza kuzirekebisha..

Mheshimiwa Zitto asante sana kwa kuona mengi ambayo wabunge wetu wengi hawana muda wa kuliangalia. Ninangojea kwa hamu sana kujua jibu litalotolewa na Mhe Mkullo....huwa najiuliza,hivi waandaaji hawa wa bajeti ni wasomi kweli au ndo wanakwamishwa na viongozi?

Bulyahulu!!!!!!!nikisikia tu hili jina, moyo unaenda mbio nakumbuka maafa 1996 sijui imefikia wapi ile kesi. Mhe Zitto,mbona hatuambiwi hawa Barrick wanachota kiasi gani cha dhahabu na ni thamani gani? Tuna haki ya kujua hilo
.

Sunday, 22 July, 2001, 08:36 GMT 09:36 UK
Tanzania's pot of gold
The Bulyanhulu complex has Tanzania's deepest mine
By Roger Dean in Dar es Salaam
A huge new gold mine has been opened in Tanzania, making the country Africa's third largest producer of gold.
Bulyanhulu mine near the northern town of Mwanza, which now employs more than 900 people, is the biggest underground gold mine in the country.
It is owned by the Canadian company Barrick Gold Corporation and, after an investment of $280m, is forecast to produce about 400,000 ounces of gold a year
This will take Tanzania's annual gold output to more than a million ounces, bettered in Africa only by Ghana and South Africa.

Je sisi wananchi tumefaidika nini?

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho kabisa, kama tunataka kuongeza uzalishaji wa kutosha kwenye baadhi ya mazao ambayo tunayo ni lazima tuangalie jinsi gani ya kutoa incentives kwa baadhi ya mazao. Mimi nitatoa mfano mmoja na nilitoa taarifa hii toka mwaka jana kwamba leo India wameweka compulsory usage ya magunia yao ya jute kwa ajili ya mazao yote ya India. Sisi hatujaweka compulsory usage ya maguni yetu ya katani, matokeo yake ni kwamba tunakuwa tuna-export jobs kwenda Bangladeshi na India kwa sababu hatulindi sisal yetu, katani yetu wala hatulindi viwanda matokeo yake ni kwamba baadhi ya wawekezaji wamenunua viwanda havifanyi kazi kwa sababu ya mazingira hayo ya kikodi.

Mhe ZITTO....spot on...ukipata nafasi soma hii http://www.fundinguniverse.com/company-histories/Barrick-Gold-Corporation-Company-History.html inawezekana sababu mojawapo ya hawa kutolipa kodi siyo nguvu za Sinclair tu bali kuna wazito wengine.......
 
Sasa huko Bungeni kama hakuna mabadiliko ya kweli basi hata hizi kauli za Zitto zitaishia kutungiwa kamati na Kikwete kama ilivyotokea before!Hakuna jipya hapa!Jipya ni pale tutakapoona kuwa ni kweli kuna wabunge wa kutosha wa CCM ambao wataungana na wapinzani...Other than that ni kweli naibu spika aliposema kuwa anasikiliza Alfa lela ulela
 
Mkuu zitto heshima yako bro,

Halafu huyo Naibu Spika nae akili fupi sana,hivi hayo maneno yake yanalisaidia vipi taifa?

Kamanda zitto na Dr. Slaa msikate tamaa hata sisi wananchi tupo nanyi.Maneno ya mchango wako yatatumika in future for reference tutakapokua tunatoa hukumu na kiama kwa walioko madarakani sasa.

Kuna hata maprofesa wa uchumi,finance etc huko bungeni lakini empty! Muda wote watu wamekaa bungeni leo hii wanaaibishwa na bwana mdogo kabisa Zitto?

Shame on them!
 
Oops safari zimezidi sasa ndiyo naona ngoma yako Mkuu Zitto .Umenikuna mkishenzi .Kwa nini hao CCM wasije kwako na wapinzani kwa ujumla wakaazima akili zenu hata kwa nusu siku wakatutendea haki na kuwapa akili zenu?
 
Oops safari zimezidi sasa ndiyo naona ngoma yako Mkuu Zitto .Umenikuna mkishenzi .Kwa nini hao CCM wasije kwako na wapinzani kwa ujumla wakaazima akili zenu hata kwa nusu siku wakatutendea haki na kuwapa akili zenu?

...dawa sio kuwaazima akili ni kuwa vote out tuu...anzia na jimboni kwako kuwanyima kura na kuhakikisha wengine nao wanafanya kama wewe na wengine tutafanya panapohusika...block by block change is coming!
 
Halafu nina swali langu kwa mkuu Zitto....Huyo mwanyika ni muhusika wa RICHMOND?
 
Mkuu zitto heshima yako bro,

Halafu huyo Naibu Spika nae akili fupi sana,hivi hayo maneno yake yanalisaidia vipi taifa?

Kamanda zitto na Dr. Slaa msikate tamaa hata sisi wananchi tupo nanyi.Maneno ya mchango wako yatatumika in future for reference tutakapokua tunatoa hukumu na kiama kwa walioko madarakani sasa.

Kuna hata maprofesa wa uchumi,finance etc huko bungeni lakini empty! Muda wote watu wamekaa bungeni leo hii wanaaibishwa na bwana mdogo kabisa Zitto?

Shame on them!

Naibu Spika anajifanya yupo katika "House of Commons"

Tatizo hatuna "House of Lords" au ndiyo NEC?
 
Back
Top Bottom