Kutangaza nafasi za ajira kwa watu "Wa ndani ya NSSF" ni Ubaguzi, Rais Samia ingilia kati, unachonganishwa na wananchi!

zeuman

JF-Expert Member
Aug 2, 2023
261
480
Haiingii akilini NSSF wamepata wapi huu ujeuri wa kuamua kuwatenga na kuwabagua watanzania wengine wote ili kuajiri wateule wao tu waliopewa nafasi kinyemela ya mikataba na kwa gia ya "kujitolea". Lazima nyuma yake kuna vigogo vinasukuma hii agenda nyuma ya pazia!

Haishangazi yalishaanza makelele ya baadhi ya vigogo kuishambulia PSRS kwa kutumia kisingizio cha mapungufu yake ili kupenyeza agenda ya taasisi kuajiri wenyewe!

Tayari baadhi ya mawaziri na wabunge walishaanza kuandaa mazingira kwa kutaka waliojitolea kupewa kipaumbele!! Lakini mbaya zaidi si tu hizi taasisi zinaridhika kwa kuajiri zenyewe, lakini zimeenda mbali zaidi na kuamua kuwatenga na kuwabagua watanzania wengine wote kwenye ajira. Tayari walishaweka watu wao bila ushindani na kuwapa mikataba na sasa wanataka kuwathibitisha.

Hii haikubaliki. Ndio maana tunamwomba Rais Samia alikemee hili kwa nguvu zote, vinginevyo Watanzania wataamini kuwa UBAGUZI HUU UNA BARAKA ZA RAIS!

Ninaamini NSSF huenda wanazo nyingi zaidi, na hizi nafasi 392 za mwanzo ni za kupimia kina cha maji tu. Wakifanikiwa hapo huenda hata matangazo ya kazi kwenye tovuti yao wakaacha kuyatoa, wakawa wanatangaziana tu kwenye magroup yao ya Whatsaap. Sehemu ya tangazo lao hilo hapo chini:

INTERNAL VACANCY ANNOUNCEMENT
National Social Security Fund (NSSF) as part of our commitment to encourage growth anddevelopment within the Fund, we are excited to announce 392 internal job opportunities available for all Fund’s employees with specific task contracts. Only candidates who are inspecific task contract term within the Fund should apply.

Naomba watanzania tulipinge jambo hili kwa nguvu zetu zote, vinginevyo hii nchi itakuwa na matabaka ya WATWANA na WATAWALA. Kama huna mtu huko juu hutakuwa na nafasi ya kupenya hata kama uwezo na sifa unazo.

Wakigoma kubadili msimamo niwaombe mawakili kuomba COURT INJUCTION kusimamisha mchakato huu wa ajira za ubaguzi, huku mkifungua kesi mahakamani kuwatetea watanzania walio wengi ambao hawana "Connection" na wanategemea kupata ajira kupitia ushindani wa wazi na wa haki kwa watanzania wote!
 
Hilo ni chaka ipo Taasisi moja HR antokea kanda fulani, mbaya zaidi alichukua vijana 10 wa internship wote wanatokea sehemu moja bila aibu na watu waliomba internship kinoma .

Baada ya ajira wakaanza kuajiriwa wale wa intership kwa kuandika barua kwend utumishi na interview walifanya geresha, kazi zilipoanza wale 10 maana nafasi zilikuwa kama 40 kwa hiyo palikuwa na wapya 30.

Wala 10 wakawa masnitch dhidi ya wenzao kwa maana wamepenyezwa.
 
Haiingii akilini NSSF wamepata wapi huu ujeuri wa kuamua kuwatenga na kuwabagua watanzania wengine wote ili kuajiri wateule wao tu waliopewa nafasi kinyemela ya mikataba na kwa gia ya "kujitolea". Lazima nyuma yake kuna vigogo vinasukuma hii agenda nyuma ya pazia!!

Haishangazi yalishaanza makelele ya baadhi ya vigogo kuishambulia PSRS kwa kutumia kisingizio cha mapungufu yake ili kupenyeza agenda ya taasisi kuajiri wenyewe!!

Tayari baadhi ya mawaziri na wabunge walishaanza kuandaa mazingira kwa kutaka waliojitolea kupewa kipaumbele!! Lakini mbaya zaidi si tu hizi taasisi zinaridhika kwa kuajiri zenyewe, lakini zimeenda mbali zaidi na kuamua kuwatenga na kuwabagua watanzania wengine wote kwenye ajira. Tayari walishaweka watu wao bila ushindani na kuwapa mikataba na sasa wanataka kuwathibitisha.

HII HAIKUBALIKI. Ndio maana tunamwomba Rais Samia alikemee hili kwa nguvu zote, vinginevyo watanzania wataamini kuwa UBAGUZI HUU UNA BARAKA ZA RAIS!! Ninaamini NSSF huenda wanazo nyingi zaidi, na hizi nafasi 392 za mwanzo ni za kupimia kina cha maji tu. Wakifanikiwa hapo huenda hata matangazo ya kazi kwenye tovuti yao wakaacha kuyatoa, wakawa wanatangaziana tu kwenye magroup yao ya Whatsaap. Sehemu ya tangazo lao hilo hapo chini:
INTERNAL VACANCY ANNOUNCEMENT
National Social Security Fund (NSSF) as part of our commitment to encourage growth anddevelopment within the Fund, we are excited to announce 392 internal job opportunities available for all Fund’s employees with specific task contracts. Only candidates who are inspecific task contract term within the Fund should apply.

Naomba watanzania tulipinge jambo hili kwa nguvu zetu zote, vinginevyo hii nchi itakuwa na matabaka ya WATWANA NA WATAWALA. Kama huna mtu huko juu hutakuwa na nafasi ya kupenya hata kama uwezo na sifa unazo.

Wakigoma kubadili msimamo niwaombe mawakili kuomba COURT INJUCTION kusimamisha mchakato huu wa ajira za ubaguzi, huku mkifungua kesi mahakamani kuwatetea watanzania walio wengi ambao hawana "connection" na wanategemea kupata ajira kupitia ushindani wa wazi na wa haki kwa watanzania wote!!
Mtu kajitolea kifanya kazi muda mwingine anapewa hela ya nauli tu leo ajira zimetoka akose dah inaumiza bora wawe kipaumbele nao wasuuzike nafsi. Mtu kajitolea zaidi ya mwaka anasugua tu hajui lininataajiriwa na bado anapiga kazi leo kashaizoea kazi na bahatinimekuja mnataka kuziba rizikinyake.
 
Shida hujui kama hata kujitolea nayo inahitaji connection ni vigumu kupata nafasi ya kujitolea sehemu bila connection labda kama hiyo sehemu hawakupi chochote ndo maana tunataka fair competition
 
Mtu kajitolea kifanya kazi muda mwingine anapewa hela ya nauli tu leo ajira zimetoka akose dah inaumiza bora wawe kipaumbele nao wasuuzike nafsi. Mtu kajitolea zaidi ya mwaka anasugua tu hajui lininataajiriwa na bado anapiga kazi leo kashaizoea kazi na bahatinimekuja mnataka kuziba rizikinyake.
Wanachuo wangapi wanataka kujitolea wanakosa kaangalie ule mfuko TAES walivyojaa na nafasi hawapi.

A fair competition kama waliofanya TAA ni nafasi za mda ila tangazo lipo kila mtu aombe .....Wapo watu wamejitolea wanafanya kazi hata majibu ya chuo hajatoka yaani baada ya kumaliza UE ...Niliona watu kibao wakifanya hivyo mwaka wetu tuliomaliza na wamepata kwa connection tena Taasisi za serikali hata field walifanyiw humo.

Usichokijua na wengi hawajui , Taasisi za serikali kama zote zinatoa intership ila inakuwa ni ishu ya internal recruiting ndio maana haiko fair ,leo unaenda kuomba unakuta tangazo kwa HR hakuna nafasi za kujitolea ,ila wengine wanakuja baada yako na wanapiga fresh kisa ndugu au connection.
 
Katk recruitment processes kuna INTERNAL AND External sources za kupata hao wanaowataka.

Mie sioni shida hapo. Na navyofikiri.. hao NSSF wanamamlaka ya kuajiri Kwa MKATABA wa muda fulani na sio ule mkataba wa PERMANENT.

hivyo kuna aina nyingi za mikataba ikiwemo huo wa Specific TASK ambao ukimaliza hiyo shughuli ndio basi unasepa na kuna mkataba wa Muda yaan mwaka/miaka.

Naona wanataka kuwabadirisha mkataba wale wanaowataka. Na sio kama ni PERMANENT (Kwa navyoona).

Ni zoez la kuhuisha mikataba hapo.

Serikal inapoelekea inatoa AJIRA sawa ila AJIRA nyingi zitakuwa za MIKATABA mifupi mifupi na sio zile za PERMANENT.
 
Pamoja na mapungufu ya PSRS, lakini hii taasisi imejitahidi sana kutenda haki kwenye suala zima la ajira!! Ni vyema mapungufu yake yakashughulikiwa na siyo kuyatumia mapungufu hayo kama kisingizio cha kuruhusu taasisi ziajiri zenyewe!! Unaona sasa NSSF walivyoanza mapema tu ku-abuse/kutumia vibaya nafasi hiyo ya taasisi kuruhusiwa kuajiri zenyewe!! MCHECHU (yule mtendaji mkuu wa hazina) katika hili amechemsha sana!! Amedhihirisha kuwa na mentality ya kibeberu yenye misingi katika msemo usemao "mwenye nguvu mpishe".
 
Back
Top Bottom