Kusema ukweli nchi ya Rwanda ni nzuri sana

Wakili wa shetani

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2022
Posts
1,976
Reaction score
3,738
Nimekuwa nafuatilia video za nchi ya Rwanda, hata za huko vijijini. Kwa kweli hii ni nchi nzuri sana. Baada ya miaka kumi ikiendelea hivi itakuwa muonekano wa nchi za Ulaya hata kuzidi.

Kila kitu unaona kimepangwa na wapangaji wanaojali watu wao. Mambo yote yanaonyesha kuwa kuna order.
Nimejifunza kuwa ukidhibiti rushwa kila mtu ndani ya nchi anaamka na kufanya mambo kwa manufaa ya wote. Rushwa inavunja moyo wenye nia ya kuendeleza nchi.

Fatilia na pato la kila raia..Nchi ipo vizuri kimiundombinu lakin raia ni masikini wakutupwa..halafu Rwanda ni nchi ndogo sana ni sawa na Mkoa mmoja wapo wa Tz.
Rwanda siyo nchi ndogo. Kieneo sawa ni ndogo. Lakini ina watu milioni 14. Imepita nchi nyingi kubwa kwa eneo kama Namibia na Botswana. Pia makazi ya wananchi na muonekano wao hawaonyeshi huo umasikini wa kutupwa. Hata kwenye slums na vijijini watu wanaonekana wana sura za 'matumaini'. Na hata kipato hatujapishana sana. Wao wana pato la mtu wastani dola 1,000 na sisi dola 1,300.
 
Fatilia na pato la kila raia..Nchi ipo vizuri kimiundombinu lakin raia ni masikini wakutupwa..halafu Rwanda ni nchi ndogo sana ni sawa na Mkoa mmoja wapo wa Tz.
Ishu sio umaskiini Wala pato, ishu ni discipline na accountability, TZ chukulia mfano ripot ya CAG japo imepikwa madudu still yapo lakini hakuna anayejali, kosa kubwa LA dunia ambalo limefanyika TZ ni kuvuruga mahakama na bunge wallah hayo ni majuto makubwa kabisa Kwa watu wenyewe akili wanaofikiria mbali, hatuwezi kutoboa kamwe Kwa namna hii
 
Tanzania asilimia kubwa ni vichaka na nusu jangwa
Ndio usisahahu vilima vya hapa na pale, mabonde, miinuko, maporomoko, vijito vya hapa na pale, tambarale angavu, vumbi la kufa mnyama mpaka unajiuliza hiki nini, ardhi ngumu kipindi cha ukame na jua kali haipitishi jembe wala sululu (hii niikuta huko kijiji fulani kabla mvua haijanyesha), imebarikiwa kila aina ya muonekano wa mazingira
 
Kweli
 
Fatilia na pato la kila raia..Nchi ipo vizuri kimiundombinu lakin raia ni masikini wakutupwa..halafu Rwanda ni nchi ndogo sana ni sawa na Mkoa mmoja wapo wa Tz.
Hii hoja ya kwamba ni nchi ndogo mi wala sijawahi elewa mantiki yake ni nini?kwani hata kama wewe una nchi kubwa basi si hata resources ulizokua nazo zinalingana na eneo lako sasa kama vyote ni direct proportional kwanini usifanye maendeleo according to your resources?
 
Nimekuwa nafuatilia video za nchi ya Rwanda, hata za huko vijijini. Kwa kweli hii ni nchi nzuri sana. Baada ya miaka kumi ikiendelea hivi itakuwa muonekano wa nchi za Ulaya hata kuzidi.

Kila kitu unaona kimepangwa na wapangaji wanaojali watu wao. Mambo yote yanaonyesha kuwa kuna order.
Nimejifunza kuwa ukidhibiti rushwa kila mtu ndani ya nchi anaamka na kufanya mambo kwa manufaa ya wote. Rushwa inavunja moyo wenye nia ya kuendeleza nchi.

Kumbe umekuwa ukifuatilia lakini hujawaahi kufika rwanda .........

Mi nilijua umefika kumbe tuu umeangaliia video za ai
 
Hii hoja ya kwamba ni nchi ndogo mi wala sijawahi elewa mantiki yake ni nini?kwani hata kama wewe una nchi kubwa basi si hata resources ulizokua nazo zinalingana na eneo lako sasa kama vyote ni direct proportional kwanini usifanye maendeleo according to your resources?
Nchi kubwa ndio ulitakiwa iwe rahisi zaidi kuendelea kuliko nchi ndogo kama vile US, China, Russia, Canada, Brazil, Australia n.k.
 
Nimekuwa nafuatilia video za nchi ya Rwanda, hata za huko vijijini. Kwa kweli hii ni nchi nzuri sana. Baada ya miaka kumi ikiendelea hivi itakuwa muonekano wa nchi za Ulaya hata kuzidi.

Kila kitu unaona kimepangwa na wapangaji wanaojali watu wao. Mambo yote yanaonyesha kuwa kuna order.
Nimejifunza kuwa ukidhibiti rushwa kila mtu ndani ya nchi anaamka na kufanya mambo kwa manufaa ya wote. Rushwa inavunja moyo wenye nia ya kuendeleza nchi.

Hiyo Nchi ni ya mafukara
 
kuna mtaa umefanana na makambako kabisa
 
Hii hoja ya kwamba ni nchi ndogo mi wala sijawahi elewa mantiki yake ni nini?kwani hata kama wewe una nchi kubwa basi si hata resources ulizokua nazo zinalingana na eneo lako sasa kama vyote ni direct proportional kwanini usifanye maendeleo according to your resources?
Hoja yako ingekuwa na nguvu kama Rwanda tungelingana kwenye maeneo au Rwanda ingekuwa inaeneo kubwa kuliko Tz halafu inamiundombinu mizuri kila eneo..uchumi na pato zuri la kila raia na kukua kwa kasi ya 4G kuliko Tz..hapo sasa tungejitizama marambili mbili kwanini Rwanda wametuzidi kila kitu? ukubwa wa nchi hata maendeleo hali sisi tuna eneo dogo halafu tupo nyuma...
 
Back
Top Bottom