Kuna ombwe juu ya chanzo chetu na ulimwengu!

Unajua ishu ipo kwenye kuthibitisha,.. mimi nikikuomba unipe uthibitisho kwamba dunia ni duara na inazunguka huwezi ukaleta au inawezekana?

Kabla big brains hawajagundua kwamba dunia ni duara,.. Jamii iliamini dunia ina umbo gani?,.. na Big brains ni uthibitisho gani walitoa kwa jamii juu ya ugunduzi huo? huenda kweli Dunia ni duara linalozunguka ila sidhani kama kuna uthibitisho ambao hata layman ukimuuliza atajibu kwa usahihi.
Ndo maana nikasema, wewe na mimi na wengine wengi tunafanya hitimisho la umbile la dunia kwa mambo ma2 tu,

1. Tunachoona/Kuhisi.
2. Tunachoambiwa/Kusoma.

Sasa, ukiwafuta wanasansi waliotuambia dunia ni kama tufe wakatupa na sababu huenda tungekubaliana kuwa sio tufe sababu tunachokiona si tufe.

Ila kwa sababu wanasema dunia ni tufe na wakatoa sababu, za kuambiwa tukichanganya na zetu ndo tunafanya hitimisho.

Wewe umehitimisha kuwa huo ushahidi hautoshi kufikiri dunia ni tufe, mimi nimehitimisha kuwa huu ushahidi unatosha kufikiri dunia ni tufe. Za kuambiwa tumechanganya na zetu.

Kwani ikiwa dunia sio flat wala tufe bali ni pembe tatu wewe unapoteza lolote?
 
Niliona unajadiliana na mtu kuhusu Huruma,.. kwamba kwanini matatizo yapo ikiwa Mungu ana huruma?

Mimi naona tunashindwa kuelewa kwasababu hatutaki kusoma na ku push akili zetu kuelewa zaidi,.... ngoja nijaribu kuelezea kama utanielewa:

Kwa mfano ishu ya huruma & kwanini mabaya yanatokea wakati Mungu ana huruma,.... Mfano kwenye Qur'an kuna aya inasema "....Mungu habadilishi hali za Jamii/watu husika mpaka wao watakapoamua kubadilika......" sasa hapa tumepewa nyenzo kubwa ambayo ni "Akili" kupitia akili ndiyo utajua kwamba Mungu ametuhurumia sana.,, akili inatufanya tujue kipi kina madhara tuepuke na kipi kina faida tukifanye,.. ukiangalia kuna mateso mengi binadamu tunapitia kutokana na jinsi sisi wenyewe tulivyoamua kuendesha maisha yetu,. tukiamua kubadilisha tabia zetu tukaishi kwa kuthaminiana na kujaliana kwenye hali tofauti regardless ya rangi wala mitazamo asilimia kubwa ya mateso hayatokuepo,..

Lakini pia kwenye kusoma kuhusu Mungu anavyofanya huruma zake kuna sehem anasema...." Wala usidhani Mwenyezi Mungu amepuuzia wanayoyatenda madhalimu. Anawaakhirishia tu mpaka siku ambayo macho yatakodoka yakibaki yametazama kwa kutetemeka.”

Hiyo inajibu kwamba Kuna mambo Mungu anayaachia yatokee haijalishi sisi tutayaona ni mabaya kiasi gani, Yeye ameshayapangia muda wa kuyahukumia,.....

Pia miongoni mwa changamoto ninayoiona kwa atheist ni mtazamo wao juu ya kifo& uhai,.. atheist wengi wanaona Uhai ni kitu bora na kifo ni kitu kibaya au kuangamia, (Sasa huo mtazamo kwa uelewa wangu sio sahihi,.. What if kwa Mungu uhai na kifo ni vitu vya kawaida sana kwake? huenda sisi tunathamini uhai kwakuwa hatujui kuna nini nyuma ya kifo,. what if kifo ni utulivu usio na purukushani za uhai... kuna uwezekano ukijua yaliyo nyuma ya kifo ukabadili mtazamo).

Nimejaribu kufafanua sikulazimishi kukubaliana na mimi ila nadhani kuna concept umepata..., kama kuna sehem hujaelewa unaweza kuuliza.
naam mkuu, kimtazamo wa kiimani upo sawa tu sidhani kama kuna shaka.

ila kimtazamo wa "mtazamo huru" hapo kuna mgogoro mkubwa sana --- maana kutakua na kiunzi cha kuthibitisha
 
Ndo maana nikasema, wewe na mimi na wengine wengi tunafanya hitimisho la umbile la dunia kwa mambo ma2 tu,

1. Tunachoona/Kuhisi.
2. Tunachoambiwa/Kusoma.

Sasa, ukiwafuta wanasansi waliotuambia dunia ni kama tufe wakatupa na sababu huenda tungekubaliana kuwa sio tufe sababu tunachokiona si tufe.

Ila kwa sababu wanasema dunia ni tufe na wakatoa sababu, za kuambiwa tukichanganya na zetu ndo tunafanya hitimisho.

Wewe umehitimisha kuwa huo ushahidi hautoshi kufikiri dunia ni tufe, mimi nimehitimisha kuwa huu ushahidi unatosha kufikiri dunia ni tufe. Za kuambiwa tumechanganya na zetu.

Kwani ikiwa dunia sio flat wala tufe bali ni pembe tatu wewe unapoteza lolote?
Nimekupata vizuri,..
 
Hakuna Ombwe lolote mkuu...... Fikra kama hizi zinatokana na ATHARI za KIDINI ambazo zime brainwashed akili zetu kwa muda mrefu kuhusu UUMBAJI

Binadamu anazaliwa, anapambana kuishi then anakufa(kama viumbe wengine wote)...... Binadamu huwa tunajikuta tu tumezaliwa na tunatakiwa kupambana kubakia hai as long as tutakavyoweza the tunakufa.

Itoshe kusema HAKUNA aliye UMBA hii Dunia wala hakuna anayejua Dunia ilikuaje hata miaka milioni moja huko nyuma achilia mbali miaka laki moja tu
Na HAKUNA namna tunaweza kurudi nyuma hadi wakati tunaodhani Dunia "iliumbwa" kujua ilikuaje.
Kitu ambacho angalau tuna uhakika nacho ni kwamba Dunia imepitia mabadiliko(evolution) hadi kuwa kama ilivyo sasa

Udadisi wa binadamu na ustadi wa ulimwengu kwa miaka mingi umekua ukimsukuma Binadamu kutaka kujua ulimwengu wenye ustadi mkubwa ulifanyikaje......? Matokeo yake Binadamu "wakamtengeneza" MUNGU ambaye unatakiwa to blindly believe Him na Sayansi ikaja na NADHARIA ambazo zipo open to be challenged

Don't forget this..... Umezaliwa ili uje kupambana kuishi kwa kadiri utakavyo weza kisha utakufa.

Huu mjadala nitahitaji ukae hivi mapema kabisa ili niweze kueleweka kabla sijagusia kitu chochote!.

Maswali mengi tunayojiuliza na hatujapata majibu mpaka sasa juu ya chanzo cha ulimwengu na chanzo chetu!, ni kwasababu kuna kitu ama vitu hatujavijua bado!.
Sina hakika sana kama tutakuja kuvijua ama tusivijue hivyo mijadala ya mabishano juu ya imani za Uungu itaendelea kuwa pambe siku hata siku mpaka pale kanuni kadhaa zitakapokuja kugundulika!.

Nimeamua nianze na hitimisho ili nieleweke kwa wepesi sana!.

Nikianza na nadharia ya uumbaji inakosa majibu maana haionyeshi nani ni wamwisho ambae ameanza kuumba kila kitu!, kwani kanuni hii itamtaka nae alieumba kuumbwa! so haileti tamati ila tu italeta tamati kama kutakuwa na muingiliano wa kanuni yoyote tusiyoifahamu ambayo itakuwa na majibu!.

Mtazamo wa Uungu kwangu mimi binafsi unazidi kudidimia siku baada ya siku haswa nikiangazia mambo kadhaa ambayo yanaleta mkanganyiko aidha juu ya uwepo wake ama nadharia hii inabaki kwenye ombwe lilelile lisiloleta majibu stahiki!.

Nikitazama kati ya hivi vitu vitatu ndio naona ombwe kubwa zaidi na naona imeshinda akili yetu kwasasa (sijui kwa baadae), vitu hivyo ni muda, space (nafasi), nguvu(energy) na akili!.

Ukianza kuzungumzia mwanzo wa ulimwengu ni ngumu sana kuvitenganisha hivyo vitu maana kila kitu kinamuhitaji mwenzake naweza kusema kama ni sarafu basi hiyo ni sarafu yenye pande zote hizo!!!.
Inaonyesha kabisa mpangilio hapa ulimwenguni umekaa ki intelligent yani kunalazimika kuwe na akili ili vitu vienende kama vilivyo!, hapohapo nguvu inaingia kwani akili bila nguvu haiwezi kufanya kazi na nguvu bila akili haiwezi kuenenda ama kukaa kwenye mpangilio na hivi vyote haviwezi kupata muda wakufanya hivyo kama hakuna nafasi(space).

Mpaka hapo inakuwa ni ngumu sana kujua nini kilianza na kilianzaje na hata kama vilianza kwa pamoja basi vilianzaje anzaje sehemu isiyokuwa sehemu na vilitokea wapi sehemu ambapo hakuna sehemu!.
Ama naweza kuiweka hivi "Ni kivipi kitu kitokee sehemu ambapo hakuna sehemu na kwanini..?"

Moja kati ya kitu nilichokuja kugundua kwenye ufahamu wetu ni kuwa "Binadamu mara nyingi huwa tunawaza kile tunachokijua na ndio mara nyingi tunatolea bunifu zetu kwenye hivyohivyo vitu tunavyovijua!, Hivyo kutokana na ugumu huo ndio maana bado tupo kwenye ombwe lakushindwa kuelewa nini chanzo cha ulimwengu!.

Kwasababu gani..?
kwasababu hii hatujui hata kama tunauliza swali sahihi ama sio sahihi (chanzo cha ulimwengu ni nini..?) kwa tafsiri yetu inaweza ikawa ni sahihi maana kwa mazingira tuliyopo yametupelekea kuwaza kuwa kila kitu kuwa na chanzo lakini usikute kwenye kanuni za ulimwengu si lazima kila kitu kiwe na chanzo!, na sasa je kama hakina chanzo basi kina nini..? sasa hili ndio ombwe lenyewe ambalo hatulijui tunabaki tunagaagaa kama kidudu kilichopotea tundu lake!.

Najua ni ngumu kuwaza kitu kisichokuwa na chanzo ama kanuni ambayo haileti chanzo!, kama nilivyoandika hapo juu kuwa akili zetu mara nyingi haziwazi vitu tusivyovijua yani ni ngumu sana kuwaza kitu ambacho huna past nacho!. hata nikikuambia uwaze kuhusu kiumbe hai mpya mwenye kanuni nje na hizi tunazofahamu utajikuta unawaza kiumbe mwenye macho, pua, mdomo n.k yani bado yale mazingira yatakuandama maana ndicho unachokijua!.

Sasa tunafikaje huko tusipopajua..?
Sioni njia nyengine isipokuwa njia ni moja tu "tafiti!". ulimwengu ni kama kitabu ukiamua ukifunue na ukiamua ukifunike!, ila akili ya binadamu huwa haina chakufunika huwa inafunua basi kufunua kitabu huwa ni asili yetu shida ipo kwenye kusoma na kuelewa tu!.

Najua kwa miaka nenda rudi vitu vingi vimegundulika vimezua mijadala na kuibua fikra nyingi na mpya!, na vilevile vimezua imani ila bado havijaleta majibu makuu ya yale tunayoyataka kuyafahamu!, bado kiu hakijakatwa hakuna Mungu ama nadharia yoyote ya Uungu iliyoleta majibu yakujitosheleza juu ya kinagaubaga wa nini chanzo cha ulimwengu...?

Hivyo basi mpaka hapo sitakuwa nachakuongeza ama kupunguza!, ombwe hili ni lilelile isipokuwa nimeona majibu sehemu ambapo hakuna jibu maana penye majibu hapana majibu nafikiri ni wakati wakutazama nje ya box, ahsanteni.
 
mkuu kwenye maelezo yako yale yana what if nyingi mkuu, ndo maana nikakwambia kwa mtazamo wa kiimani.
Ndiyo natumia what if kwasababu mimi na wewe hatuna uthibitisho wa nini kipo mbele baada ya uhai huu tulionao hivi sasa,.. na kutumia "What if" ni kawaida kwa mambo yote yaliyofichikana na yaliyo mbele yetu cause hatuna uhakika yatatokea kwa namna gani,.. kwa mfano wewe ukisema kesho saa 6:30 utapiga chafya,. nikikuomba uthibitishe sasa hivi utaweza?

Kuna vitu vipo nje ya uwezo wetu kuthibitisha,.. na kushindwa kuthibitisha haimaanishi havipo au havijawahi kuwepo,.. Miaka mingi nyuma ukiwaambia watu kwamba kuna viumbe vidogo sana 'bakteria' wanaweza kuwa kwenye sehemu na wao wasione wangekuona kichaa na kuomba uwathibitishie,. usingeweza kuthibitisha,.. Lakini Bacteria wapo/hawapo?

mifano ipo mingi sana mikubwa kwa midogo.. au chukulia kwenye maisha tu mtu amefanyiwa uhalifu ameenda kushtaki Mahakamani ila kwa bahati mbaya hana uthibitisho wa kumtia hatiani mhalifu,.. mhalifu atashinda kesi,.. lakini hiyo haimaanishi kwamba uhalifu haujafanyika......
 
mkuu upo sahihi nakubaliana na wewe, ila tutakuwa kumeshift mjadala ndo maana inakua tunavutana,

mimi nilijaribu kuelezea hoja ya
Watu ni vyepesi kuamini kwamba tupo kwenye simulation kuliko kuamini uwepo wa mungu, Elon musk alishawahi kukili kwamba kuna chance kubwa sana ya ulimwengu wetu kuwa kwenye simulation tena sio base simulation, Neil degrase tyson kasema odds ya ulimwengu wetu kuwa kwenye simulation ni 50/50, hivyo kama kuna uwezakano wa kuwa kwenye simulation basi kuna intelligence inayohusika na kutengeneza ile simulation, watasema labda ni advance cillivization au powerful quantum computer ila ukiingiza tu neno Mungu mjadala unaanza

kwamba mgogoro mkubwa wa kisayansi ndo unakuja.

ule mjadala mwingine wa huruma na hoja zingine ndo tutakesha sana , kwa sababu unagusa sana imani
 
Hakuna Ombwe lolote mkuu...... Fikra kama hizi zinatokana na ATHARI za KIDINI ambazo zime brainwashed akili zetu kwa muda mrefu kuhusu UUMBAJI

Binadamu anazaliwa, anapambana kuishi then anakufa(kama viumbe wengine wote)...... Binadamu huwa tunajikuta tu tumezaliwa na tunatakiwa kupambana kubakia hai as long as tutakavyoweza the tunakufa.

Itoshe kusema HAKUNA aliye UMBA hii Dunia wala hakuna anayejua Dunia ilikuaje hata miaka milioni moja huko nyuma achilia mbali miaka laki moja tu
Na HAKUNA namna tunaweza kurudi nyuma hadi wakati tunaodhani Dunia "iliumbwa" kujua ilikuaje.
Kitu ambacho angalau tuna uhakika nacho ni kwamba Dunia imepitia mabadiliko(evolution) hadi kuwa kama ilivyo sasa

Udadisi wa binadamu na ustadi wa ulimwengu kwa miaka mingi umekua ukimsukuma Binadamu kutaka kujua ulimwengu wenye ustadi mkubwa ulifanyikaje......? Matokeo yake Binadamu "wakamtengeneza" MUNGU ambaye unatakiwa to blindly believe Him na Sayansi ikaja na NADHARIA ambazo zipo open to be challenged

Don't forget this..... Umezaliwa ili uje kupambana kuishi kwa kadiri utakavyo weza kisha utakufa.
Hakuna ombwe? kwanini umezaliwa? lengo ni nini? kwanini upo Duniani na si sehemu nyingine yoyote?

NB: Dini haimfungi mtu yoyote akili,. hakuna namna dini ikuzuie kufikiria beyond,.. na kuhusu kuwa brainwashed hata wewe upo hivyo na ndiyo maana unaamini kwenye Evolution uliyofundishwa ila ukiambiwa utaje hata kiumbe kimoja ulichoona kiki- evolve hujui.
 
mkuu upo sahihi nakubaliana na wewe, ila tutakuwa kumeshift mjadala ndo maana inakua tunavutana,

mimi nilijaribu kuelezea hoja ya

kwamba mgogoro mkubwa wa kisayansi ndo unakuja.

ule mjadala mwingine wa huruma na hoja zingine ndo tutakesha sana , kwa sababu unagusa sana imani
Sawa,.
 
Ndo maana nikasema, wewe na mimi na wengine wengi tunafanya hitimisho la umbile la dunia kwa mambo ma2 tu,

1. Tunachoona/Kuhisi.
2. Tunachoambiwa/Kusoma.

Sasa, ukiwafuta wanasansi waliotuambia dunia ni kama tufe wakatupa na sababu huenda tungekubaliana kuwa sio tufe sababu tunachokiona si tufe.

Ila kwa sababu wanasema dunia ni tufe na wakatoa sababu, za kuambiwa tukichanganya na zetu ndo tunafanya hitimisho.

Wewe umehitimisha kuwa huo ushahidi hautoshi kufikiri dunia ni tufe, mimi nimehitimisha kuwa huu ushahidi unatosha kufikiri dunia ni tufe. Za kuambiwa tumechanganya na zetu.

Kwani ikiwa dunia sio flat wala tufe bali ni pembe tatu wewe unapoteza lolote?
Au basi tuseme Dunia Haina umbo maalumu 🤣🤣 Dunia ni Shapeless 🤣🤣
 
Hakuna Ombwe lolote mkuu...... Fikra kama hizi zinatokana na ATHARI za KIDINI ambazo zime brainwashed akili zetu kwa muda mrefu kuhusu UUMBAJI

Binadamu anazaliwa, anapambana kuishi then anakufa(kama viumbe wengine wote)...... Binadamu huwa tunajikuta tu tumezaliwa na tunatakiwa kupambana kubakia hai as long as tutakavyoweza the tunakufa.

Itoshe kusema HAKUNA aliye UMBA hii Dunia wala hakuna anayejua Dunia ilikuaje hata miaka milioni moja huko nyuma achilia mbali miaka laki moja tu
Na HAKUNA namna tunaweza kurudi nyuma hadi wakati tunaodhani Dunia "iliumbwa" kujua ilikuaje.
Kitu ambacho angalau tuna uhakika nacho ni kwamba Dunia imepitia mabadiliko(evolution) hadi kuwa kama ilivyo sasa

Udadisi wa binadamu na ustadi wa ulimwengu kwa miaka mingi umekua ukimsukuma Binadamu kutaka kujua ulimwengu wenye ustadi mkubwa ulifanyikaje......? Matokeo yake Binadamu "wakamtengeneza" MUNGU ambaye unatakiwa to blindly believe Him na Sayansi ikaja na NADHARIA ambazo zipo open to be challenged

Don't forget this..... Umezaliwa ili uje kupambana kuishi kwa kadiri utakavyo weza kisha utakufa.
Kunywa bia mbili mkuu nakulipia Kwa namba ya nida hapa
,👍
 
Kwa hyo mkuu unataka kusema ni coincidence tu dunia ikawa na hewa nzuri, maji safi ,jua kutoa nishati inayotosha binadamu kuishi sio kidogo wala sio nyingi, kila kitu kimewekwa vizuri kabisa ku suistain maisha kwa viumbe, ila vyote hivyo iwe ni coincidence sidhani "too much coincidence is not a coincidence"
 
Hakuna ombwe? kwanini umezaliwa? lengo ni nini? kwanini upo Duniani na si sehemu nyingine yoyote?

NB: Dini haimfungi mtu yoyote akili,. hakuna namna dini ikuzuie kufikiria beyond,.. na kuhusu kuwa brainwashed hata wewe upo hivyo na ndiyo maana unaamini kwenye Evolution uliyofundishwa ila ukiambiwa utaje hata kiumbe kimoja ulichoona kiki- evolve hujui.
Yes hata mimi athari za dini au sayansi zimeniathiri pia

Hakuna OBWE............ tumelitengeneza kwasababu ya athari za imani na sayansi pia
Zinatulazimisha kuona LAZIMA kuna CHANZO na kina MADHUMUNI ya sisi kuwepo

Wewe na kuku na panzi na samaki na miti hamna tofauti yoyote ya sababu ya kuzaliwa.
Tumezaliwa ili tuje kupambana kubaki hai as long as tutakavyo weza ili tuzaliane............ existence ya viumbe hai vyote ni KUZALIANA

HAKUNA uhitaji wowote wa kujua hayo maswali yako wala hayata kusaidia chochote.
Binadamu HAWEZI kujua kila kitu na wala HALAZIMIKI kujua kila kitu...... Kwasababu amejikuta tu kazaliwa na atatakiwa kupambania kuwa hai kisha atakufa
Hayo mengine ni MBWEMBWE TU
 
Ukweli mtupu huu mkuu 🤣
Sisi binadamu na wanyama wengine hatuna utofauti.

Tunazaliwa, tunaishi, tunaumwa na tunakufa.
Kama wanyama wengine tu.
Mengine yote ni mbwembwe zetu binadamu
 
Inaonekana umekata tamaa ya kufikiria zaidi,.. ila ombwe lipo na sababu ya ombwe kuwepo si athari ya Dini wala Sayansi bali ni akili zetu,... Akili zetu zinapenda kudadisi hakuna namna utaizuia akili ya binadamu kujiuliza maswali juu ya ulimwengu kwa ujumla,.. hata maendeleo ya kiteknolojia unayoyaona ni matokeo ya akili ya binadamu,.. Binadamu sio sawa na Panzi, Kuku na viumbe wengine kama ulivyosema.
 
Ukweli mtupu huu mkuu 🤣
Sisi binadamu na wanyama wengine hatuna utofauti.

Tunazaliwa, tunaishi, tunaumwa na tunakufa.
Kama wanyama wengine tu.
Mengine yote ni mbwembwe zetu binadamu
Hahh kwahiyo Wewe na Panzi akili zenu zipo sawa,..? Hamna tofauti?😅

Binadamu ana uwezo mkubwa mno Binadamu tumeweza mpaka ku manipulate mifumo ya viumbe hai mpaka leo tuna Kuku wa maabara,. watoto wa maabara na mambo mengi makubwa,... Panzi anaweza??

Dah hivi Jamii forum si ni home of Great Thinkers?
 
Kwa hyo mkuu unataka kusema ni coincidence tu dunia ikawa na hewa nzuri, maji safi ,jua kutoa nishati inayotosha binadamu kuishi sio kidogo wala sio nyingi, kila kitu kimewekwa vizuri kabisa ku suistain maisha kwa viumbe, ila vyote hivyo iwe ni coincidence sidhani "too much coincidence is not a coincidence"
Mkuu mimi ninacho maanisha ni kwamba wote tumejikuta tumezaliwa na kuikuta hii Dunia kwenye huu USTADI wa hali ya juu kabisa.
Na JUKUMU LETU MAMA ni kuhakikisha tunapambana tuishi ili tuzaliane kadri tutakavyoweza the same as Funza, Tumbili, Samaki, Nyoka, nk nk

Tofauti yetu kubwa na viumbe wengine ni kwamba sisi tupo more intelligent PENGINE kuliko viumbe wengine na ndio maana tunajipa UMAALUMU na tuna hangaika kutafuta MUUMBA na sababu za kutuumba jambo ambalo HALINA MAANA YOYOTE

Kula, kunywa, kupambana na changamoto zako zinazo hatarisha maisha yako HAKUNA maana yoyote zaidi ya hiyo........ Failed to do so u die
 
Back
Top Bottom