Kuna ombwe juu ya chanzo chetu na ulimwengu!

Kuna ombwe juu ya chanzo chetu na ulimwengu!

Ila sio special
Bado tunategemea nature kwenye vitu vingi.
Bado ni wanyama na primates Kama walivyo bonobo
Binadamu ni special sana,.. hii inaweza kuwa proved 100%+mark-up Binadamu ndiyo viumbe VIONGOZI kwa viumbe vingine,...

Sijajua ni kitu gani kinachofanya mpinge ukweli huu ulio wazi,..
 
Ukisema hivi bila kusema chanzo argument yako inakuwa mfu, pia kwamba Mubgu ndio chanzo umeitoa wapi na kwanini upinge kwa ujasiri kana kwamba unajua chanzo kingine.
Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na chanzo, Hata chanzo cha kila kitu kitahitaji kuwa na chanzo chake kingine.

Pasiwepo kitu chochote kile kilicho exist chenyewe tu, pasipo chanzo.

Hivyo kutakuwa na msururu mrefu wa vyanzo vingi visivyo na mwisho.
 
Andiko kubwa sana hilo mkuu😅😅 na kwakifupi kwa hizi akili zetu za past hatuwezi solve hiyo puzzle.

Akili yetu inaamini kwenye references zaidi so hii inafanya wasomi wengi washindwe kujifunza vitu vipya, kwamfano tafiti nyingi huwa zimekaa zaidi kwenye kurelate na past kisha kutoa conclusion so inapotokea kitu kipya hakuna ambae atakitolea conclusion badala yake wataendelea kukifuatilia huku wakiwa wanaendelea kurelate na tabia ya kitu au vitu fulani fulani ambavyo vilikuwepo hapo past.

Kwahiyo hata procedure ambazo hufanyika kwenye uchunguzi wa vitu vingi ni history ambayo ilikua proved kwa asilimia fulani katika kutoa matokeo chanya ya jambo hilo, so jambo likiwa ni jipya na halina historia yoyote ya kuwahi kuwepo duniani hakuna akili ya kawaida ya mtu yeyote duniani itakayoweza kulitolea ufumbuzi.

Kwahiyo ujanja wetu wote inategemea kale na pasipo na kale hakuna chochote ambacho kinaweza kufanyika na mwanadamu.

Kale hutumika ili kuitabiri future but universe ikibadili tabia zake kidogo watu wote duniani wataanza kulalamika... Chukulia mfano wakulima walivyokariri majira ya Kila mwaka, so wanaenda shamba kwa kufuata ratiba zile zile ila ikitokea universe ikabadilika kidogo au ikakataa kutabirika kwa angalau miaka mitano tu, wote mtakufa njaa😂😂😂.

Listen, kitendo cha kushindwa kuvuta na kutoa hewa wote tunaamini kwamba ni kifo kwakua historia tuliyoikuta imetuamunisha hivyo, na haujawahi kuwa na historia ya tofauti na hapo lakini what if hii historia iko wrong na haikufanyiwa utafiti wowote?...

Unajua wanyama wakali na ambao sio wakali kwa experience ya past ambayo kuna watu wameipata kwa maumivu makali na wakaamua kurithisha historia hiyo kizazi na kizazi.

Mtoto anavyokua huwa anajaribu kila kitu kwakua Hana experience na chochote na hapo watu wanasema bado Hana akili ndio maana anafanya hivyo, lakini kadri anavyokua anapata uzoefu kwa kujifunza kwa maumivu au kuhadithiwa na wale waliomtangulia nae ndio anatofautisha kipi ni kipi... So everything in your brain ni history and once ukaja na kitu kipya kabisa ambacho hakijawahi kuwepo duniani na ukashindwa kuprove basi wasomi wote watakuona wewe ni mwehu, so hakuna namna mnaweza kuyajua mambo hayo kwa akili hizi za past.

Na the bad thing ni kwamba ili universe ikucontrol vizuri ikakuwekea mipaka miwili sayansi na dini.

Sayansi inataka uamini kitu kwa kuthibitisha na kale while dini inakutaka ubaki kwenye upast wako na wala usianze kuacha ubongo wako uelee kwenye hoja nzito za future😅😅😅 mnajikuta mpo mpo tu na ulimwengu unaendelea kuwaamulia Kila kitu mnachotakiwa kufanya na hata mnavyotakiwa kuishi over and over again.
We jamaa wewe daaah hatareee sana
 
Hii ni kweli kwasababu ni kitu kipo wazi kuanzia hapa na kuendelea sisi ndio tunatengeneza huu ulimwengu but sisi tulitengenezwa na nani na tumetokea wapi? Kwasababu ukisema tumetokea bila chanzo probability ya vyanzo vingi vya aina hii kutokea bila chanzo ingekua kubwa na ukisema kuna chanzo ambacho tumetokea lazima na hiko chanzo kiwe na chanzo so hii inakua ni infinity loop.

Labda tukubali kwamba universe huwa inajianzisha upya Kila baada ya muda fulani kwamba inafuta kizazi hiki na kuanzisha kizazi kingine kwa namna yake yenyewe.😅😅😅.

Kwasababu history inaonesha kwamba kuna uwezekano mkubwa ustaarabu wa kale ulikua more advanced kuliko huu ambao sisi tupo.

So labda Dunia kuna level fulani ya ustaarabu viumbe wakifikia ni labda wanajipoteza wao wenyewe kwa shinikizo la universe kisha viumbe vipya vinaanzishwa na kuanza tena moja.😂😂.

Au inawezekana hii sio universe pekee ambayo ipo ila labda kuna universe nyingine ambayo iko na viumbe walio more powerful than us and labda kinamna fulani wao ndio walianzisha huu ustaarabu kisha wakarudi kwenye universe yao then wanaendelea kutucontrol (something like hizo story za Aliens and blah blah kama hizo).

But vyovyote vile itakavyokua ila Mimi naamini kuna namna universe inatamani sisi tubehave ila kutokana na kelele za dunia tunashindwa that's why kuna nyakati unaweza kupata picha ya mbele ya maisha yako ukiwa umelala (wakati ambao ubongo unakua haukabiliani na kelele yoyote).
Nyie majamaa huwa mnakula nini mbona mna waza hvo aiseeeeee...

Hivi ni hii hii astronomy nayosoma mimi au kuna zaidi na zaidi aiseee mbona mpo advanced sana kwa kufikilia mambo wakuuu 🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌
 
Ukisema hivi bila kusema chanzo argument yako inakuwa mfu, pia kwamba Mubgu ndio chanzo umeitoa wapi na kwanini upinge kwa ujasiri kana kwamba unajua chanzo kingine.
Kwa sababu Mungu/Miungu/Miungu/Mungu sio chanzo Cha maisha.

Kuna mtu mmoja humu JF aliwahi sema kama square root ya 2 huijui haifanyi jibu kuwa 3.

Kitu hicho ndio kinachokataa kuwa huyo ndiye.
 
Kwanini unasema Binadamu tunajipa u-special? Binadamu hatujipi u-special bali ndiyo tumeumbwa hivi tupo na akili kubwa kuliko viumbe wengine,..

Sisi tuna uwezo wa kuvifanya viumbe vingine vile tunataka,.. hata Dunia tukiamua kuiharibu tunaweza hiyo inatosha kukuonyesha jinsi gani Binadamu ni viumbe special wenye akili kubwa na hatari!


Just Imagine Binadamu ameweza kugundua Bunduki, atomic bombs na vitu vingi vya hatari,... kuna kiumbe kinaweza kunusurika iwapo Binadamu tutaamua kuharibu? Binadamu ndiyo viumbe ambao tunakaa vikao na mikutano mbalimbali kujadili jinsi ya kulinda uwepo wa viumbe wengine wasitoweke Duniani.....
Mkuu kwa muktadha wako huu binadamu ni muhimu katika KUIHARIBU Dunia

Mimi sio mtaalamu wa kiikolojia lakini nina hakika Dunia hii ni salama zaidi kwa viumbe wengine wanaoitegemea na uasili wa dunia ikiwa bila ya sisi Binadamu

Dunia ipo HATARINI zaidi kuendela na kanuni zake za kiasili kwasababu ya Binadamu
 
Binadamu ni special sana,.. hii inaweza kuwa proved 100%+mark-up Binadamu ndiyo viumbe VIONGOZI kwa viumbe vingine,...

Sijajua ni kitu gani kinachofanya mpinge ukweli huu ulio wazi,..
Viongozi kwenye lipi?
Kwamba anaongoza Samaki kwenye bahari au minyoo ardhini?
Special haumwi au kushambuliwa na magonjwa, au ana efficient ya asilimia 100 kwenye kutunzwa nishati?
Kama sio huo uspecial anautoa wapi?
 
Mkuu kwa muktadha wako huu binadamu ni muhimu katika KUIHARIBU Dunia

Mimi sio mtaalamu wa kiikolojia lakini nina hakika Dunia hii ni salama zaidi kwa viumbe wengine wanaoitegemea na uasili wa dunia ikiwa bila ya sisi Binadamu

Dunia ipo HATARINI zaidi kuendela na kanuni zake za kiasili kwasababu ya Binadamu
Ni invasive species moja ya ajabu.
Ina abudu Mungu wa uongo asiye onekana na inaharibu nature inayo onekana.
 
Nyie majamaa huwa mnakula nini mbona mna waza hvo aiseeeeee...

Hivi ni hii hii astronomy nayosoma mimi au kuna zaidi na zaidi aiseee mbona mpo advanced sana kwa kufikilia mambo wakuuu 🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌
Mkuu wote tunaotea otea tu hakuna mwenye jibu kamili na kama yupo basi ameamua kujiaminisha kwenye kile anachokiamini ila kiukweli haya mambo ni ya juu sana ukilinganisha na uelewa wetu huu tulio nao.
 
Watu hudharau vitu vidogo nakuona havina majibu lakini ukija ukakaa chini ukafikiria unaweza kushangaa sana!, moja kati ya kitu ambacho tumekizoea na tuankichukulia easy lakini kwangu mimi naonaga kama ni kitu cha ajabu ni "space!" nashangaa jinsi ilivyo inavyoweza kupitisha mawimbi ya kila namna halafu kitu kinachoniwazisha zaidi ni ukitoa space unabaki na nini..?😅
Hichi kitu huwa kinanifanya muda mwengine niwaze huenda tunauliza maswali ambayo si sahihi!.. lakini bado hatujui kama ni sahihi ama si sahihi na ndio maana nikahitimisha kuwa lazima tujikite kwenye tafiti binadamu hatuna asili ya kukaa nakutulia tu lazima tujue kwenye hichi chungu kuna nini...???

Ni watu wachache tu hawajabadili mitazamo wanaweza kuona unahoji mambo yakipuuzi!, lakini hakuja ujuzi unakuja bila kuhoji na tafiti!. Maisha/uhai ni sanaa na ni sayansi pia itategemea utajivika vazi lipi kati ya hayo!.

By the way mfano nawashangaa sana watu wanaoshangaa namna gravity inavyofanya kazi kwenye dunia yetu nakuona ni kama longolongo nakuanza kusema dunia ni flat..!!! ila hivyo viumbe sikuhizi sitaki kubishana navyo ila wanatakiwa wajifunze kuhusu space ilivyo inavyo behave n.k basi hawatakuja kuona tabu kuelewa kuwa dunia ni duara!.
Daaah we jamaa naona umerudi yule wa zamani sasa....
Maana hapo kati naona ulijichanganya kwa nyuzi za chitchat ahahah

Mkuu umeongelea space.... Sasa ukiondoa nafasi manayake vtu si vitabanana kutakua na tufe la vitu au .😂😂😂😂🫵🫵🫵🫵
 
Moja kati ya vitu vinavyodumaza kufikiri kwetu na kuvumbua mambo ni dini, tunafikiri kwamba majibu yote ya kweli lazima tuyapate kwenye vitabu vya Mungu tu, au kuwa majibu yaliyo sahihi ni yale yaliyoko kwenye hivyo vitabu tu. Kumbe tunapaswa kufikiri na kutafiti zaidi juu ya muhustakabiri wetu.
Kanuni ya uumbaji ni fumbo kubwa sana, ni jinsi gani dunia imeumbwa?! Ni jinsi gani vitu halisi vimeumbwa tokana na vitu visivyoonekana na visivyo halisi? Tuna safari ndefu ya kutafuta majibu ya kweli na hasa tukienda mbali ya majibu ya dhambi!!
Kuna logic kubwa sana hapa.
 
Mkuu kwa muktadha wako huu binadamu ni muhimu katika KUIHARIBU Dunia

Mimi sio mtaalamu wa kiikolojia lakini nina hakika Dunia hii ni salama zaidi kwa viumbe wengine wanaoitegemea na uasili wa dunia ikiwa bila ya sisi Binadamu

Dunia ipo HATARINI zaidi kuendela na kanuni zake za kiasili kwasababu ya Binadamu
Yes sahihi kama tunaweza kuiharibu Dunia maana yake tunaweza kuifanya ikawa bora pia,... Ni maamuzi tu.

Binadamu ni kiumbe special na hilo lipo wazi,.
 
shida sio hiyo mkuu shida ni life style!, wapo watu manguli sana wakuwaza kushinda hata hao unaowaona ma genius!, isipokuwa watu hawapo focus na vitu kama hivyo, hivyo wanajikuta wachache wanaoweza kuwaza vitu kama hivyo na kufocus wanafaulu!.
jifikirie mtu anazaliwa system anayokitana nayo ni kuabudu nakuaminishwa maswala ya Mungu wa kwenye vitabu na hapohapo bado anakutana na aina ya maisha ambayo yanamtaka aishi kwa kutafuta fedha nakuwaza mambo yakwawaida tu ya kila siku!.

Angalia hata vyakula tunavyokula ni junk food kila siku kwasababu ya biashara na ndoto za watu zakujipatia fedha!, wala si kula chakula huku ukimakinika nini unatakiwa ule kuongeza nini chenye manufaa kwenye mwili wako!.
Kama ni safari basi bado ni ndefu mno!, kuna vitu unatakiwa uvitoe kichwani mwa watu na hapo utakutana na vita kubwa mno yani binadamu mpaka aje kufikia ustaarabu wa angalau asilimia 50 basi kazi ni kubwa mno!..😅
we mpaka leo watu wanaishi kwa kumpigania Mungu yani kiumbe kilichoumba ulimwengu na kina kila aina ya uwezo nguvu n.k ati kikitukanwa we unakipigania...!! halafu wewe ukivamiwa tu hata na kibaka hakikupiganii unakabwa na unatoa vitu bila tabu!.. sasa hii akili uje uibadili ifikie uelewa na ustaarabu wa walau asilimia 50 basi utakuwa umepiga hatua kubwa mno!. kifupi safari bado ni ndefu maana wanao wa brain wash watu hawataki kuwaachia maana wanapata faida na hao waliokuwa brain washed hawataki kuwaza nje ya box watoke humo!.
Kenzy your genius noted
 
Viongozi kwenye lipi?
Kwamba anaongoza Samaki kwenye bahari au minyoo ardhini?
Special haumwi au kushambuliwa na magonjwa, au ana efficient ya asilimia 100 kwenye kutunzwa nishati?
Kama sio huo uspecial anautoa wapi?
Binadamu ndiyo the most Intelligent creature,. Unabisha?


Kitendo cha binadamu kuwazidi viumbe wengine wote akili huo ni uthibitisho tosha kwamba Ndiyo mwenye mamlaka (power) kuliko viumbe wote,.. Sasa hizo nguvu za kubisha sijui unazitoa wapi😅
 
Binadamu ndiyo the most Intelligent creature,. Unabisha?


Kitendo cha binadamu kuwazidi viumbe wengine wote akili huo ni uthibitisho tosha kwamba Ndiyo mwenye mamlaka (power) kuliko viumbe wote,.. Sasa hizo nguvu za kubisha sijui unazitoa wapi😅
Viumbe wenye akili kuliko watu wapo, we need more research.

Kwa hapa duniani akili hazipo kwa binadamu tu.

Hivyo sio special
 
Viumbe wenye akili kuliko watu wapo, we need more research.

Kwa hapa duniani akili hazipo kwa binadamu tu.

Hivyo sio special
Sawa,. Nitajie kiumbe mmoja aliyemzidi akili binadamu.

Sijasema viumbe wengine hawana akili bali wamezidiwa mbali mno.
 
T
Huu mjadala nitahitaji ukae hivi mapema kabisa ili niweze kueleweka kabla sijagusia kitu chochote!.

Maswali mengi tunayojiuliza na hatujapata majibu mpaka sasa juu ya chanzo cha ulimwengu na chanzo chetu!, ni kwasababu kuna kitu ama vitu hatujavijua bado!.
Sina hakika sana kama tutakuja kuvijua ama tusivijue hivyo mijadala ya mabishano juu ya imani za Uungu itaendelea kuwa pambe siku hata siku mpaka pale kanuni kadhaa zitakapokuja kugundulika!.

Nimeamua nianze na hitimisho ili nieleweke kwa wepesi sana!.

Nikianza na nadharia ya uumbaji inakosa majibu maana haionyeshi nani ni wamwisho ambae ameanza kuumba kila kitu!, kwani kanuni hii itamtaka nae alieumba kuumbwa! so haileti tamati ila tu italeta tamati kama kutakuwa na muingiliano wa kanuni yoyote tusiyoifahamu ambayo itakuwa na majibu!.

Mtazamo wa Uungu kwangu mimi binafsi unazidi kudidimia siku baada ya siku haswa nikiangazia mambo kadhaa ambayo yanaleta mkanganyiko aidha juu ya uwepo wake ama nadharia hii inabaki kwenye ombwe lilelile lisiloleta majibu stahiki!.

Nikitazama kati ya hivi vitu vitatu ndio naona ombwe kubwa zaidi na naona imeshinda akili yetu kwasasa (sijui kwa baadae), vitu hivyo ni muda, space (nafasi), nguvu(energy) na akili!.

Ukianza kuzungumzia mwanzo wa ulimwengu ni ngumu sana kuvitenganisha hivyo vitu maana kila kitu kinamuhitaji mwenzake naweza kusema kama ni sarafu basi hiyo ni sarafu yenye pande zote hizo!!!.
Inaonyesha kabisa mpangilio hapa ulimwenguni umekaa ki intelligent yani kunalazimika kuwe na akili ili vitu vienende kama vilivyo!, hapohapo nguvu inaingia kwani akili bila nguvu haiwezi kufanya kazi na nguvu bila akili haiwezi kuenenda ama kukaa kwenye mpangilio na hivi vyote haviwezi kupata muda wakufanya hivyo kama hakuna nafasi(space).

Mpaka hapo inakuwa ni ngumu sana kujua nini kilianza na kilianzaje na hata kama vilianza kwa pamoja basi vilianzaje anzaje sehemu isiyokuwa sehemu na vilitokea wapi sehemu ambapo hakuna sehemu!.
Ama naweza kuiweka hivi "Ni kivipi kitu kitokee sehemu ambapo hakuna sehemu na kwanini..?"

Moja kati ya kitu nilichokuja kugundua kwenye ufahamu wetu ni kuwa "Binadamu mara nyingi huwa tunawaza kile tunachokijua na ndio mara nyingi tunatolea bunifu zetu kwenye hivyohivyo vitu tunavyovijua!, Hivyo kutokana na ugumu huo ndio maana bado tupo kwenye ombwe lakushindwa kuelewa nini chanzo cha ulimwengu!.

Kwasababu gani..?
kwasababu hii hatujui hata kama tunauliza swali sahihi ama sio sahihi (chanzo cha ulimwengu ni nini..?) kwa tafsiri yetu inaweza ikawa ni sahihi maana kwa mazingira tuliyopo yametupelekea kuwaza kuwa kila kitu kuwa na chanzo lakini usikute kwenye kanuni za ulimwengu si lazima kila kitu kiwe na chanzo!, na sasa je kama hakina chanzo basi kina nini..? sasa hili ndio ombwe lenyewe ambalo hatulijui tunabaki tunagaagaa kama kidudu kilichopotea tundu lake!.

Najua ni ngumu kuwaza kitu kisichokuwa na chanzo ama kanuni ambayo haileti chanzo!, kama nilivyoandika hapo juu kuwa akili zetu mara nyingi haziwazi vitu tusivyovijua yani ni ngumu sana kuwaza kitu ambacho huna past nacho!. hata nikikuambia uwaze kuhusu kiumbe hai mpya mwenye kanuni nje na hizi tunazofahamu utajikuta unawaza kiumbe mwenye macho, pua, mdomo n.k yani bado yale mazingira yatakuandama maana ndicho unachokijua!.

Sasa tunafikaje huko tusipopajua..?
Sioni njia nyengine isipokuwa njia ni moja tu "tafiti!". ulimwengu ni kama kitabu ukiamua ukifunue na ukiamua ukifunike!, ila akili ya binadamu huwa haina chakufunika huwa inafunua basi kufunua kitabu huwa ni asili yetu shida ipo kwenye kusoma na kuelewa tu!.

Najua kwa miaka nenda rudi vitu vingi vimegundulika vimezua mijadala na kuibua fikra nyingi na mpya!, na vilevile vimezua imani ila bado havijaleta majibu makuu ya yale tunayoyataka kuyafahamu!, bado kiu hakijakatwa hakuna Mungu ama nadharia yoyote ya Uungu iliyoleta majibu yakujitosheleza juu ya kinagaubaga wa nini chanzo cha ulimwengu...?

Hivyo basi mpaka hapo sitakuwa nachakuongeza ama kupunguza!, ombwe hili ni lilelile isipokuwa nimeona majibu sehemu ambapo hakuna jibu maana penye majibu hapana majibu nafikiri ni wakati wakutazama nje ya box, ahsanteni.
Tutazamaje nje ya box,wakati umesema huwa tunawaza tunachokiona!?
 
Hili linawezekana mkuu.
Lakini mimi naona kadiri tunavyokwenda hali inazidi kuwa mbaya zaidi

Tunaacha hata kutumia vitu vya asili na tunahamia zaidi kwenye artificial zaidi
Nahisi kama binadamu wajao watakua na maisha mafupi sana
watakuta miti yote ishaisha, samaki wapungua sana baharini, ardhi imeishiwa rutuba na mengi mno
 
Yes sahihi kama tunaweza kuiharibu Dunia maana yake tunaweza kuifanya ikawa bora pia,... Ni maamuzi tu.

Binadamu ni kiumbe special na hilo lipo wazi,.
Anaweza kuwa special(ingawaje kila kiumbe kina u special wake)............Lakini sio MUHIMU kwenye hii Dunia kuliko wengine.
Huo umuhimu tumejipa kwasababu tupo more intelligent PENGINE kuliko viumbe wengine.

Hata tukitoweka Duniani na hakika Dunia itakua BORA zaidi kuliko tukiwepo

Umuhimu tunaojipa ni DHANA za KIIMANI kwamba hii Dunia "tumeumbiwa" sisi Binadamu, na vingine vyote tumepewa ili tuvitawale
 
Back
Top Bottom