Kuna ombwe juu ya chanzo chetu na ulimwengu!

Kuna ombwe juu ya chanzo chetu na ulimwengu!

Kwa sababu Mungu/Miungu/Miungu/Mungu sio chanzo Cha maisha.

Kuna mtu mmoja humu JF aliwahi sema kama square root ya 2 huijui haifanyi jibu kuwa 3.

Kitu hicho ndio kinachokataa kuwa huyo ndiye.
Hukutakiwa kutaja kabisa kwasababu hakipo, ulipotaja kwa kukataa maana yake umelinganisha na ukafikia tamati kwa kuwa na chanzo sahihi.

Huwezi sema 1*1 sio 1 kama hauna jibu lingine kuoinga argument ya kwanza.
 
Daaah we jamaa naona umerudi yule wa zamani sasa....
Maana hapo kati naona ulijichanganya kwa nyuzi za chitchat ahahah

Mkuu umeongelea space.... Sasa ukiondoa nafasi manayake vtu si vitabanana kutakua na tufe la vitu au .😂😂😂😂🫵🫵🫵🫵
Vitabanana wapi sasa mkuu....??
ukiondoa space hakuna chakubanana maana yake ni kwamba hakuna uwezekano wa kuwepo kwa kitu maana vitu vinategemea space ku exist ni kama useme uondoe siti ya kukaa maana yake hakuna kukaa!.
sasa shida inakuja hapa je kukiwa hakuna space kunakuwaje..?
nani anaejua utupu/vacuum wa asilimia mia..?
can you even imagine that..?
 
T

Tutazamaje nje ya box,wakati umesema huwa tunawaza tunachokiona!?
Tunawaza tunachokijua sio kukiona lakini sijasema kwamba hiyo inatufanya tusiyajue tusiyoyajua maana kabla binadamu hakujua kama kuna galaxy, hakujua kama kuna gravity n.k lakini alipofanya tafiti akayajua hayo!, hivyo maana yake tukifanya tafiti ulimwengu basi kuna uwezekano wakujua vitu ambavyo hatujawahi hata kuviwaza ama kuvijua itakuwa ni kama surprise kubwa mno!.

Naweza kukupa huu mfano watu wengi ukiwauliza kuwa mwanga unatokana na nini watakujibu kwasababu wanajua lakini waulize giza linatokana na nini wengi wao watakujibu ni kukosekana kwa mwanga!, ndio ni kukosekana kwa mwanga lakini unaweza kunielezea giza linazalishwa na nini pasipo kugusia mwanga..?
yani nielezee giza linakuwaje kuwaje na katika hilo jibu lako usigusie mwanga!.

kwenye hilo swali kinaweza kikaumana sana maana mpaka sasa binadamu hatujui nini chanzo cha giza ulimwenguni!, hatujui kama linazalishwa na nguvu fulani ama ni kama natural space colour!.
sasa ili kujua inatakiwa tufanye tafiti maana kitu kama hichi hata utumie background ya kumbukumbu zako bado haupati jibu!, so tafiti ndio zitakazofuta ombwe la majibu tusiyoyajua.
 
Anaweza kuwa special(ingawaje kila kiumbe kina u special wake)............Lakini sio MUHIMU kwenye hii Dunia kuliko wengine.
Huo umuhimu tumejipa kwasababu tupo more intelligent PENGINE kuliko viumbe wengine.

Hata tukitoweka Duniani na hakika Dunia itakua BORA zaidi kuliko tukiwepo

Umuhimu tunaojipa ni DHANA za KIIMANI kwamba hii Dunia "tumeumbiwa" sisi Binadamu, na vingine vyote tumepewa ili tuvitawale
Kila kiumbe ni muhimu,.. ila Binadamu ndiyo the most Intelligent creature hapa Duniani na hilo ndiyo linamfanya Binadamu awe na mamlaka juu ya viumbe wengine,..

Binadamu hajipi umuhimu kwa sababu za kiimani bali ni kitu ambacho kinathibitishika kwenye maisha ya kila siku kwamba Binadamu ana tawala viumbe wengine kutokana na kuwa na akili zaidi,...

Au unataka useme isingeandikwa kwenye vitabu vya Kiimani,.. ungeshindwa kugundua fact hii iliyo wazi👀?
 
Vitabanana wapi sasa mkuu....??
ukiondoa space hakuna chakubanana maana yake ni kwamba hakuna uwezekano wa kuwepo kwa kitu maana vitu vinategemea space ku exist ni kama useme uondoe siti ya kukaa maana yake hakuna kukaa!.
sasa shida inakuja hapa je kukiwa hakuna space kunakuwaje..?
nani anaejua utupu/vacuum wa asilimia mia..?
can you even imagine that..?
Matter... anything that can ... Space,
Sasa space ni matter au sio matter...?
 
Mimi naweza sema hivi, Mungu muumba wa mbigu na nchi yupo, lakini elimu tuliyofundishwa kumuhusu yeye haina ukweli!! mfano biblia inasema Kristo alifanyika maskini, Ili kwa umasikini huo.wa mwaminio wapate kuwa matajiri!! 2Wakorinto 8:9.
Sasa kama elimu hii ni kweli, au kama kanuni tunazofundishwa makanisani zingekuwa kweli.basi Wakristo wote tungekuwa matajiri!! pia Kuna andiko linasema "sisi tu Warithi walithio pamoja na Kristo, Warumi 8:16-17
Pia biblia inasema " Mbingu na vyote vijazavyo ni Mali ya Bwana Zaburi 24.
Sasa kama sisi tu Warithi,tunarithi nn? Maana yake tunarithi vitu vyote vizilivyo umbwa na Mungu.kama mafundisho ya Biblia yangekuwa yanajitoshereza, Walokole wote tungekuwa mabillionea!!! mbona haiko hivo?? maana yake mafundisho ya Biblia hayajitosherezi, au ??
 
Matter... anything that can ... Space,
Sasa space ni matter au sio matter...?
Sio matter maana ukiangalia definition ya matter na Space ni tofauti na matter ndio ina exist kwenye space so kama hakutakuwa na space maana yake hata matter haitakuwepo!, so unaweza ku imagine kivipi kutokuwepo kwa space kunavyokuwa...?
 
Hili swali walianza kujiuliza tangu enzi na enzi mpaka leo hakuna majibu na bado tutaendelea kujiuliza na majibu hatutopata hata ifanyike tafiti ya namna gani mambo mengine ni miujiza miujiza tu hayaeleweki katika akili ya kawaida haya thibitiki
 
Mimi naweza sema hivi, Mungu muumba wa mbigu na nchi yupo, lakini elimu tuliyofundishwa kumuhusu yeye haina ukweli!! mfano biblia inasema Kristo alifanyika maskini, Ili kwa umasikini huo.wa mwaminio wapate kuwa matajiri!! 2Wakorinto 8:9.
Sasa kama elimu hii ni kweli, au kama kanuni tinazofindishwa makanisa zingekuwa kweli.basi Wakristo wote tungekuwa matajiri!! pia Kuna andiko linasema "sisi tu Warithi walithio pamoja na Kristo, Warumi 8:16-17
Pia biblia inasema " Mbingu na vyote vijazavyo ni Mali ya Bwana Zaburi 24.
Sasa kama sisi tu Warithi,tunarithi nn? Maana yake tunarithi vitu vyote vizilivyo umbwa na Mungu.kama mafundisho ya Biblia yangekuwa yanajitoshereza, Walokole wote tungekuwa mabillionea!!! mbona haiko hivo?? maana yake mafundisho ya Biblia hayajitosherezi, au ??
Ndio hayajitoshelezi haswa ukipeleka nadharia za Mungu wa biblia na quran kuhoji ki uhalisia ama ki sayansi!.

Mfano Hizi imani zimekuwa zikiaminisha kuwa Mungu ni muweza wa yote!, hii kanuni ya uweza wa yote unajitafuna ikiwa utaipa changamoto katika namna hii!.
Ikiwa Mungu ni muweza wa yote basi aweze kutengeneza jiwe asiloweza kulibeba!, sasa akiweza ni ameweza lakini ikitokea akashindwa kulibeba pia atakuwa hana hiyo sifa ya uweza wa yote na akiahindwa kulitengeneza pia sio muweza wa yote!.

Chengine kitendo cha Mungu kumuumba shetani na kuwatupia viumbe wake anaowapenda ni ujinga wa karne ambayo haifai hata kusikilizwa wewe huwezi kuwa na kuku unaowapenda halafu ukawafungia na nyoka bandami mwao!. ikiwa wewe ni unaweza kuamua kila kitu hivyo hakuna kinachokufunga so hata kama hao kuku ukiamua kuwasamehe huna hasara, ukiamua kuwaua pia huna hasara sasa ukishasema unaupendo basi inatakiwa uonekane huo upendo kimatendo!. ni mantiki ndogondogo tu ambazo binafsi naona hata hazihitaji mjadala mrefu!.
kusema kweli sikuhizi hata kulumbana na watu wanaoamini hivyo vitabu naona kama ni ujinga na kujichosha!...😅
 
Kila kiumbe ni muhimu,.. ila Binadamu ndiyo the most Intelligent creature hapa Duniani na hilo ndiyo linamfanya Binadamu awe na mamlaka juu ya viumbe wengine,..

Binadamu hajipi umuhimu kwa sababu za kiimani bali ni kitu ambacho kinathibitishika kwenye maisha ya kila siku kwamba Binadamu ana tawala viumbe wengine kutokana na kuwa na akili zaidi,...

Au unataka useme isingeandikwa kwenye vitabu vya Kiimani,.. ungeshindwa kugundua fact hii iliyo wazi👀?
Mkuu umuhimu wa binadamu dhidi ya viumbe wengine kwenye hii Dunia yetu ni upi?.... Kuwa ua?

Hiyo more intelligent imeisaidia nini Dunia hii (sio maisha yetu) Dunia kwa ujumla wake umuhimu wetu ni upi?
Tumeiboresha Dunia kwenye nyanja ipi zaidi ya KUIHARIBU?

Umuhimu wa Binadamu ungekua pale Dunia inapokua haijiwezi bila Sisi....... Lakini ukweli ni kwamba Dunia ni SALAMA na BORA zaidi bila sisi.

Kuwa more intelligent haimaanisha kuwa sisi ni MUHIMU kuliko wengine wakati intelligence hiyo INAHARIBU Dunia
Sisi ndio viumbe wa HOVYO kabisa katika kuiharibu Dunia.
 
Hukutakiwa kutaja kabisa kwasababu hakipo, ulipotaja kwa kukataa maana yake umelinganisha na ukafikia tamati kwa kuwa na chanzo sahihi.

Huwezi sema 1*1 sio 1 kama hauna jibu lingine kuoinga argument ya kwanza.
What is asserted without evidence can be dismissed without evidence.

Any claim lacking supporting evidence can be rejected without evidence.

Wanaodai na walioeleza kwamba Mungu ni chanzo cha ulimwengu, Kwanza Hawana uthibitisho wowote ule.

Hawawezi kuthibitisha uwepo wa Mungu huyo.

Kwa hivyo huyo Mungu, can be dismissed and rejected without evidence.
 
Ndio hayajitoshelezi haswa ukipeleka nadharia za Mungu wa biblia na quran kuhoji ki uhalisia ama ki sayansi!.

Mfano Hizi imani zimekuwa zikiaminisha kuwa Mungu ni muweza wa yote!, hii kanuni ya uweza wa yote unajitafuna ikiwa utaipa changamoto katika namna hii!.
Ikiwa Mungu ni muweza wa yote basi aweze kutengeneza jiwe asiloweza kulibeba!, sasa akiweza ni ameweza lakini ikitokea akashindwa kulibeba pia atakuwa hana hiyo sifa ya uweza wa yote na akiahindwa kulitengeneza pia sio muweza wa yote!.

Chengine kitendo cha Mungu kumuumba shetani na kuwatupia viumbe wake anaowapenda ni ujinga wa karne ambayo haifai hata kusikilizwa wewe huwezi kuwa na kuku unaowapenda halafu ukawafungia na nyoka bandami mwao!. ikiwa wewe ni unaweza kuamua kila kitu hivyo hakuna kinachokufunga so hata kama hao kuku ukiamua kuwasamehe huna hasara, ukiamua kuwaua pia huna hasara sasa ukishasema unaupendo basi inatakiwa uonekane huo upendo kimatendo!. ni mantiki ndogondogo tu ambazo binafsi naona hata hazihitaji mjadala mrefu!.
kusema kweli sikuhizi hata kulumbana na watu wanaoamini hivyo vitabu naona kama ni ujinga na kujichosha!...😅
Mi Naona kwenye Dini tulipgwa kama tulivyopigwa kwenye Mitaala ya Elimu!! Vilivyomo humo ndani, havina uhalisia kabisa!!!
 
Mkuu umuhimu wa binadamu dhidi ya viumbe wengine kwenye hii Dunia yetu ni upi?.... Kuwa ua?

Hiyo more intelligent imeisaidia nini Dunia hii (sio maisha yetu) Dunia kwa ujumla wake umuhimu wetu ni upi?
Tumeiboresha Dunia kwenye nyanja ipi zaidi ya KUIHARIBU?

Umuhimu wa Binadamu ungekua pale Dunia inapokua haijiwezi bila Sisi....... Lakini ukweli ni kwamba Dunia ni SALAMA na BORA zaidi bila sisi.

Kuwa more intelligent haimaanisha kuwa sisi ni MUHIMU kuliko wengine wakati intelligence hiyo INAHARIBU Dunia
Sisi ndio viumbe wa HOVYO kabisa katika kuiharibu Dunia.
Kwamba Binadamu hatujaiboresha Dunia kwenye nyanja yoyote?,.. nadhani kwasababu umeamua kuwa upande wa negative tu,. ila Binadamu tunasaidia kwenye survival ya viumbe wengine kwa njia tofauti tofauti kwa mfano ikitokea maradhi ya mlipuko au mabadiliko ya asili (volcanoes, ukame n.k) Binadamu ndiyo viumbe pekee ambao wanapambana kuhakikisha changamoto kama hizo zinapatiwa suluhisho kwa kutumia tiba na teknolojia tofauti tofauti....

So, kimsingi akili zetu ni sehemu ya ulinzi wa Dunia hata kama ni kwa asilimia ndogo, sio tu kuharibu.
 
Kaka upo sahihi,.. Ila ukweli ni kwamba Binadamu tumepewa sehem ndogo kwenye elimu na kama elimu juu ya chanzo cha ulimwengu (Jinsi ilivyoumbwa) ingekua ndani ya uwezo wetu kufahamu basi mpaka leo naamini kwa jinsi binadamu tulivyopewa uwezo wa kudadisi na kutafuta majibu ya maswali basi huenda mpaka leo tungekua tumepata jibu la swali hilo ambalo naamini kila binadamu aliyezaliwa akiwa na utimamu wa akili anajiuliza,.... so kimsingi mimi nadhani kuna baadhi ya elimu Mwenyezi Mungu aliamua zibaki kwake tu kwa mfano hakutaka kutupa uwezo wa kujua kwamba kwa nini Yeye ana uwezo wa kuwepo pasipo kutegemea uwepo wa kitu kingine chochote (Ilhali Binadamu sisi kutokana na kiwango cha ufahamu wetu ni kwamba ili kitu chochote kiwepo kinahitaji kufanywa au kutengenezwa uwepo wake).

Ndiyo maana hata Qur'an inasema kwamba Binadamu tumepewa sehemu ndogo kwenye ujuzi " وَمَا أُوتِيتُم مِّنَ الْعِلْمِ إِلَّا قَلِيلًا......" hivyo kuna vitu kuvijua ni ngumu sana maana inaonekana vipo nje ya uwezo wetu na kadri tunavyojiuliza maswali tunaibua maswali mengine yasiyo na mwisho,.. na ndiyo maana inapaswa tuamini na tukubali (surrender) kwamba baadhi ya vitu vipo nje ya uwezo wetu wa kufikiri...,
WAchina 90% ni atheist

Mbona wanafanya maelfu ya tafiti Kila siku na ukute 90% ya vitu ilivyo navyo unanunua kutoka china kwanini huyo Mungu wenu asiwape huo uwezo ninyi mnaomuamini
 
Huu mjadala nitahitaji ukae hivi mapema kabisa ili niweze kueleweka kabla sijagusia kitu chochote!.

Maswali mengi tunayojiuliza na hatujapata majibu mpaka sasa juu ya chanzo cha ulimwengu na chanzo chetu!, ni kwasababu kuna kitu ama vitu hatujavijua bado!.
Sina hakika sana kama tutakuja kuvijua ama tusivijue hivyo mijadala ya mabishano juu ya imani za Uungu itaendelea kuwa pambe siku hata siku mpaka pale kanuni kadhaa zitakapokuja kugundulika!.

Nimeamua nianze na hitimisho ili nieleweke kwa wepesi sana!.

Nikianza na nadharia ya uumbaji inakosa majibu maana haionyeshi nani ni wamwisho ambae ameanza kuumba kila kitu!, kwani kanuni hii itamtaka nae alieumba kuumbwa! so haileti tamati ila tu italeta tamati kama kutakuwa na muingiliano wa kanuni yoyote tusiyoifahamu ambayo itakuwa na majibu!.

Mtazamo wa Uungu kwangu mimi binafsi unazidi kudidimia siku baada ya siku haswa nikiangazia mambo kadhaa ambayo yanaleta mkanganyiko aidha juu ya uwepo wake ama nadharia hii inabaki kwenye ombwe lilelile lisiloleta majibu stahiki!.

Nikitazama kati ya hivi vitu vitatu ndio naona ombwe kubwa zaidi na naona imeshinda akili yetu kwasasa (sijui kwa baadae), vitu hivyo ni muda, space (nafasi), nguvu(energy) na akili!.

Ukianza kuzungumzia mwanzo wa ulimwengu ni ngumu sana kuvitenganisha hivyo vitu maana kila kitu kinamuhitaji mwenzake naweza kusema kama ni sarafu basi hiyo ni sarafu yenye pande zote hizo!!!.
Inaonyesha kabisa mpangilio hapa ulimwenguni umekaa ki intelligent yani kunalazimika kuwe na akili ili vitu vienende kama vilivyo!, hapohapo nguvu inaingia kwani akili bila nguvu haiwezi kufanya kazi na nguvu bila akili haiwezi kuenenda ama kukaa kwenye mpangilio na hivi vyote haviwezi kupata muda wakufanya hivyo kama hakuna nafasi(space).

Mpaka hapo inakuwa ni ngumu sana kujua nini kilianza na kilianzaje na hata kama vilianza kwa pamoja basi vilianzaje anzaje sehemu isiyokuwa sehemu na vilitokea wapi sehemu ambapo hakuna sehemu!.
Ama naweza kuiweka hivi "Ni kivipi kitu kitokee sehemu ambapo hakuna sehemu na kwanini..?"

Moja kati ya kitu nilichokuja kugundua kwenye ufahamu wetu ni kuwa "Binadamu mara nyingi huwa tunawaza kile tunachokijua na ndio mara nyingi tunatolea bunifu zetu kwenye hivyohivyo vitu tunavyovijua!, Hivyo kutokana na ugumu huo ndio maana bado tupo kwenye ombwe lakushindwa kuelewa nini chanzo cha ulimwengu!.

Kwasababu gani..?
kwasababu hii hatujui hata kama tunauliza swali sahihi ama sio sahihi (chanzo cha ulimwengu ni nini..?) kwa tafsiri yetu inaweza ikawa ni sahihi maana kwa mazingira tuliyopo yametupelekea kuwaza kuwa kila kitu kuwa na chanzo lakini usikute kwenye kanuni za ulimwengu si lazima kila kitu kiwe na chanzo!, na sasa je kama hakina chanzo basi kina nini..? sasa hili ndio ombwe lenyewe ambalo hatulijui tunabaki tunagaagaa kama kidudu kilichopotea tundu lake!.

Najua ni ngumu kuwaza kitu kisichokuwa na chanzo ama kanuni ambayo haileti chanzo!, kama nilivyoandika hapo juu kuwa akili zetu mara nyingi haziwazi vitu tusivyovijua yani ni ngumu sana kuwaza kitu ambacho huna past nacho!. hata nikikuambia uwaze kuhusu kiumbe hai mpya mwenye kanuni nje na hizi tunazofahamu utajikuta unawaza kiumbe mwenye macho, pua, mdomo n.k yani bado yale mazingira yatakuandama maana ndicho unachokijua!.

Sasa tunafikaje huko tusipopajua..?
Sioni njia nyengine isipokuwa njia ni moja tu "tafiti!". ulimwengu ni kama kitabu ukiamua ukifunue na ukiamua ukifunike!, ila akili ya binadamu huwa haina chakufunika huwa inafunua basi kufunua kitabu huwa ni asili yetu shida ipo kwenye kusoma na kuelewa tu!.

Najua kwa miaka nenda rudi vitu vingi vimegundulika vimezua mijadala na kuibua fikra nyingi na mpya!, na vilevile vimezua imani ila bado havijaleta majibu makuu ya yale tunayoyataka kuyafahamu!, bado kiu hakijakatwa hakuna Mungu ama nadharia yoyote ya Uungu iliyoleta majibu yakujitosheleza juu ya kinagaubaga wa nini chanzo cha ulimwengu...?

Hivyo basi mpaka hapo sitakuwa nachakuongeza ama kupunguza!, ombwe hili ni lilelile isipokuwa nimeona majibu sehemu ambapo hakuna jibu maana penye majibu hapana majibu nafikiri ni wakati wakutazama nje ya box, ahsanteni.
Ukijadili haya, usisahau kuwa kuna suala la dimensions, na kuna mengine tuu kuyaelewa ni shughuli kwa sababu yanatuzidi.

Mpaka sasa mwanadamu aliepo duniani hawezi kufahamu yote ya 4th dimension, as well as higher ones...so ni ngumu kujua kuhusu origin.

Zaidi zaidi tunadanganyana tuu
 
WAchina 90% ni atheist

Mbona wanafanya maelfu ya tafiti Kila siku na ukute 90% ya vitu ilivyo navyo unanunua kutoka china kwanini huyo Mungu wenu asiwape huo uwezo ninyi mnaomuamini
Unajua unaowaita atheist wa kichina nyuma yake kuna nani?

Unajua maana ya dragon wanaemtumia kwenye tamaduni zao?

Nenda kamsome kwanza dragon wanaemtumia kwa undani, chimba zaidi ujue foundation yake na jinsi alivyossmbaa kisha kasome Ayubu 41 yote...then linganisha...uone utapata nini..

Mnatajaga - tajaga tuu mambo alafu hamchimbi taarifa kwa undani...sio sawa.

Na mnapokebehi imani pasipo kuijua kwa undani ni sawa na kuwa mtu asiye na maarifa...na kujidanganya...kisa hajui.
 
Back
Top Bottom